Pages

Ads 468x60px

Wednesday, November 18, 2015

NYUMA YA PAZIA NO1.............

Haya bila shaka mnashauku yakujua kulikoni....... Ngoja leo tuanze na magauni hayo ilikuwaje??

Kiukweli sikuwa na wazo kabisa la kufanya chochote kwa habari ya birthday yangu........ hadi hapa wiki 3 kabla ya siku, ambayo nilienda kwenye shughuli moja nikamuona mdada kavaa gauni la dizaini hizi. sio kwamba ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana nalo, nimeliona sana ila nilikuwa naamini sio kwa mwili huu wangu ha!ha!ha!  lakini nilikuwa nayapenda mnoo, nakumbuka mpaka nilikuwa najisemea moyoni hili gauni likimpata mtu fulani atapendeza mnooo........ Basi nilivyomuona yule Dada nikajikuta tuu nawaza, Vipi km nimekaa mezani nimezungukwa na wadada wenye miili yao wamevaa hivyo ha!ha!ha!ha! yote mawazo lakini...

Ndipo wazo la kufanya kitu kupitia birthday yangu likaja, Nikawaza vipi nipate wanawake 7-10 wamevalia haya magauni?? huku nikijua mimi muhusika  ntakuwa kituko yaani  ha!ha!ha! ila kwa sababu natamani kuona nimezungukwa na watu wamependeza na maumbo yao. Nikawaza tena hiyo namba nikipata niwafanyie suprise fulani fulani ambazo ziko ndani ya uwezo wangu. Kiukweli uwezo wakuwanunulia nilikuwa sina na hata km nilikuwa nao sidhani km ningenunua  kwa sababu hizi........

Niliamini mualikwa hana shida na visenti vyangu ila utu  wakufaana ndio unaohitajika.........Niliamini nisingekosa watu 5-7 wakukubali ombi langu  kwa ajili ya siku yangu yakuzaliwa.

Pia  niliamini kwa hili ninalotaka kulifanya linahitaji utayari wa bila kushurutishwa............nilihitaji ile Yes movement, yakunionyesha kuwa Rose tupo tayari. japo kuwa hatu hang out mara nyingi pamoja, au hatuonani mara kwa mara lakini tupo pamoja  nawewe............

 Basi moja kwa moja nikajikuta nachat na yule Dada anihakikishie km anaweza kuongea na muuzaji tukapata hayo magauni ndani ya mda mfupi......... akarudi na jibu inawezekana nikamwambia naomba nikupe kazi hapo hapo  naomba unisaidie nipate wadada  5-10 ambao wako tayari kujinunulia hayo magauni kwa muda huu kwa ajili ya birthday yangu.

 Nilikuwa na watu ambao ningeweza kuwaface mwenyewe, nawangekubali ila kiukweli nilitaka wale watu ambao sijashibana nao sanaaa, ambao kukubali kwao kutakuwa kama kurudisha fadhira vile,au kunionea aibu kwasababu nimewaomba na pia nilitaka kile ninachotaka kukifanya nisifanye kwa sababu  ya urafiki wakushibana au undugu.( kama unanifatilia humu huwa nasisitiza ,,mara nyingine jisikie tuu kumbariki mtu tofauti yaani sio ndugu, wala yatima,  na mara nyingine sio lazima awe muhitaji ila pia uwe na hekima wengine hawachelewi kukumwagia chai yako unayombariki usoni, kwakuona unataka kumletea dharau ha!ha!ha! rejea kwa nini nisingeweza kuwanunulia magauni)

 Mimi nilichofanya kuna watu km wawili watatu nilihisi labda na wao wangealikwa kwa sababu zangu binafsi labda wangependa, lakini nilihisi mualikaji anaweza asiwafikirie au hana mawasiliano nao au vyovyote vile kwa hiyo nikatuma tuu ujumbe kwao, kuna birthday party yangu inakuja km ungependa kuniunga mkono naomba uwasiliane na mtu fulani (mwalikaji) atakupa utaratibu. Nilimshangaa Mungu ndani ya siku chache sana alinitumia ujumbe amepata watu mara tatu zaidi ya ninayoitaka, ila wengine wameomba wanamagauni yanayofanana na hayo wanataka wasinunue  ha!ha!ha!

 ( ngoja niwambie iko hivi, unapoishi maisha ambayo mtu akikuuliza who is your best friend au friend  huna jibu na bado ukiwa na kitu km hivi ukajikuta unasupport kubwa mnoo, usiichukulie poa aisee Mshukuru Mungu sana (ntarudi hapa tukimaliza hili la birthday  yangu kuwasimlia kitu kilichonifanya  bado hata ninavyoandika hili kina nitoa machozi)  Ila niamini ni Neema kubwa.

Kumbuka hawa watu hawakuwa wanategemea chochote toka kwangu zaidi ya kuambiwa ni birthday ya Rose ......Utaratibu wa  huku kwetu ukialikwa yaani maana yake usafiri, kula na kunywa juu yako we jiandae tuu uwambiwe garama yake itakuwa sh. ngapi kwa usiku huo, itategemea mnaenda wapi..............hicho ndicho ninachoamini walikuwa wanategemea kitafuata baada ya magauni..


Nikiwa nimeletewa hiyo namba bado sikutaka kujua ni nani na nani. ila nilichoweza kumwambia naomba uwambie ticket yakuingia ni kutoa order ya gauni. ili mipango itimie na pia naomba  maxmum namba iwe 16 mtanielewa kwa nini ilikuwa hivi..........( hahahaa nimeanza jeuri sasa mwee!!!)  

Ngoja niwambie,  Kwenye hizi sherehe iwe harusi au vinginevyo nimeona kuna watu wameamua  shughuli ifanyike vyovyote itakavyo kuwa  ili kuwafurahisha watu au labda kutoa lawama lakini hajafanya km vile angependa iwe .......mwisho wa siku  hauna furaha tena.(NIKOSA KUBWA MNOOO) nakubaliana, kuna wakati labda kuna marekebisho, au ushauri wa kuboresha zaidi lakini ikifikia hatua umekasirika umeamua vyovyote itakavyo kuwa  iwe.........BIG NO!!!

 BASI MAMA WAWILI NILIKUWA NA MIPANGO  ambayo labda ilitakiwa kuboreshwa bila kupoteza ile hadhi yake niliyotaka iwe ambayo mtanielewa badaye............  

Tumalizie mambo ya magauni  ha!ha!ha! Bwana siyakafika siku hiyo ya shughuli asubuhi  we!! watu sikupaniki hasa mimi nilihisi walihitaji wayapate mapema ili wajue watatokaje ...... lakini nilikuwa nina ile nguvu yakuamini km walichagua style inayofanana na maumbo yao bado watapendeza by that time tayari nilishajua nani anakuja. kwa upande wangu kama nilivyojua mwanzo yaani mimi hata iwaje sio type yangu..... ila it was about waalikwa hata nilikuwa sijali nilisema ntalivaa hivyo hivyo hata kama kituko ha!ha!ha! Kulifungua  bwana kha!! niliagiza mawili aisee ma Kubwaaa,mareeeefuuuu., hadi kutembea nashindwa yaani   yaani ningesema nikomae hivyo hivyo lazima ningeitwa chizi ninaejielewa ha!ha!ha! ilihitaji fundi haswaaa kumbuka yamebaki masaa tuuu.

 Ningeweza kutafuta moja ya Gauni lakipekee km birthday girl.....  lakini nilijisemea  moja ya lengo nikutokuwa tofauti na waalikwa  i mean yaani nilitaka iwe km ladies night out ........na hayo magold  ila kwa sababu kutembea nilikuwa na shindwa nikaona isiwe tabu nikatafuta mkasi nikakata hayo magold ya mkono na kifuani  kwenye nguo moja, nikaingia kwenye nguo zangu tafuta gauni inayoendana na hayo material ya magauni yao....... nilitaka kubandika mwenyewe na mkono ila kuna vitu nilitakiwa kufatilia  nikamtafuta Dada mmoja nikamwambia sikia chukua sindano ya mkono ninachotaka haya mavitu yakae hapo kifuani na mkononi nikamuachia na hela ya soda yakumtia moyo  ha!ha1ha! mwisho wa siku hilo ndo gauni....... mkiliangalia sana limefungwa fungwa mnoo maana hayo madude yalikuwa mazito kwa hiyo hata shape ya gauni ikapotea....... ha1ha!ha!


Ikumbukwe lengo ilikuwa nifanye kitu kwa ajili ya namba fulani ambayo ilikuwa iko ndani ya uwezo wangu. Haikuwa kufanya ili nionekane nimefanya, ni ile kutimiza hamu niliyonayo ndani ya moyo wangu .................

ITAENDELEA







3 comments:

  1. nimepanda ulivyo hakikisha wazo lako linakua hai kwa vitendo,hongera your night was beautiful!

    ReplyDelete
  2. Hizo gold hapo kifuani kwako zilinogaaa...you cant even tell ziliwekwa at eleventh hour. haya tunasubiri part two. you are truly blessed. happy bthday once again

    ReplyDelete
  3. Hii safi sana yani nimejifunza mengi! asante

    ReplyDelete