Pages

Ads 468x60px

Monday, November 23, 2015

TUENDELEEE........


 Poleni kwa kusubiri........ Tatizo Mama wawili  mambo mengi  kha!! mpaka natamani nipotezee ila sema kila nikikumbuka ilivyokuwa najisikia tuu kushare.......... 

haya tuendelee


  Lengo langu la watu wasiozidi kumi  lilikuwa ni hili gari. Nilipenda  nicruise around na waalikwa wote humu ndani, huku tukipiga story na kugonga glass kwa muda wa masaa mawili kabla hatujaenda dinner..............  Nilipenda kuwasuprise tuu hivyo niliwaambia  tunapoenda dinner ni suprise, hivyo tukutane nyumbani kwangu then wote tuelekee huko....... lakini namba ilivyobadilika to 17 tayari nikajua hili lisingewezekana, nikaruhusu akili yangu ikubari mabadiliko, ambayo niliamini lazima yawe yakuboresha  bila kupoteza ile kiu niliyonayo ndani yangu yakufanya nililoona najitendea haki..........



Nikajikuta nawaza  badala ya wao kuja kukusanyika hapa why nisimpitie kila mmoja nyumbani ??? all i wanted for that day..... dizaini kama Queen treat, ( ukitaka kujua hilo red carpet ilikuwaje duu!!! niachieni tuu mwenyewe yaani ha!ha!ha) Nasikupenda iwe kwangu tuu, bali kwa wale waalikwa wangu pia. Niliamini  itakuwa tofauti kidogo lakini pia sikutaka wajue ntawachukuaje??

 Nikatoka na wazo hili lakuwambia, Kwa sababu venue yetu ni surprise, nakusubiriana  mahala pamoja inaweza kutuchelewesha baadhi yetu wamejitolea kutupitia. Hivyo  tunaomba usiulize ulize nani dereva, we jiandae muda fulani nje dakika 5 kabla dereva atakupigia simu  (Hahahahaaa huu uongo hata mimi mwenyewe sikuuelewa aisee...... kikikiii  nakutubu badae nilitubu.....)

 Sasa basi ilinibidi niongeze  muda wakukodi hilo gari, maana trip ilibidi ziwe mbili tena na sio moja ukiongeza na kwenda door to door lazima muda ungeongezwa. Nilipita nilianza kumchukua wa kwanza  kwa hiyo yeye akampigia wapi nakuja kukuchukua, watatu nae...........,.....,......., it was fun humo ndani kwa kweli.........

Thank God hili lilifanikiwa....... Kiukweli mapokeo yake yalikuwa yakipekee mnoo......... Iko hivi wapenzi wangu, hapa  unapofanya sio unatafuta misifa ya Mama wawili, au umaarufu ha!ha!ha! bali inakuwa ile kiu iliyondani ambayo hujui matokeo yake, na uko tayari kukabiliana nayo kwa vyovyote vile yatakavyokuja.... 

Yanavyokuja kwa namna yakupondeka  na maelezo fulani  ambayo wewe binafsi unaona yamekuwa zaidi, wakati wewe lengo lako niku have fun  na waalikwa wako........ aisee ile feeling yake haielezeki zaidi yakumrudishia Mungu utukufu........

 Ikumbukwe haikuwa kumsaidia Mjane,yatima au muhitaji yoyote, ambaye mapokeo yake nikama umesave life..... hawa walikuwa ni watu ambao yawezekana wanauwezo zaidi yako ila labda kutokana na ubusy wa maisha   kuwaza vitu km hivi si rahisi...... Si hivyo tuu 

 Nina rafiki yangu mmoja ( Mteja wangu ila sasa nahisi nimekuwa km best wake eti ha!ha!ha! )
 Huyu Best ukizungumzia $$$ aisee ana mafarasi huko,  Biashara niliyojuana naye yakumuoshea magari  ana Car yard (anauza magari new na used), ana mainvestment balaa yaani............ kajipanga  haswaa, uzee wake anaumaliza pazuri mnoo ila kuoa mke sasa mweee!!! na nyimbo zangu zakumleta kanisani uwiii!!! hapo ndo najionaga sijakaza vyakutosha  ha!ha!ha! haiwezekani ananimwagia misifa weee halafu nikitaka  kumleta  kwenye lengo husika anagoma yaani atabadilisha na topic ha!ha!ha! sasa sijui injili yangu inakuwaga haina upako, au muda bado, au.......... aisee mi ndo maana nawaheshimu sana watumishi aiseee ..............hichi kipawa usiombe uwe nacho aiseee ha!ha!ha! Wapendwa tuu ndo wamenielewa hapa  )

Tuendelee...........

 Sasa siku moja alileta gari yake yakutembelea ifanyiwe kazi, nikajikuta, nimeifanyia mwenyewe kwa mikono yangu na ilivyofika muda wakumkabidhi, nilimkabidhi bila kuandikia invoice  ili anipe check. Aliponiuliza nilimwambia hii ningependa isifanyiwe mahesabu, kama kunilipa bei yake aliyokuwa anategemea $380 nilivyomjibu vile alionyesha hali yakustuka, nakutoamini vile, akaniuliza mara ya pili km  kweli........ kitu ambacho nilijifunza na ambacho labda alikizungumza kwa namna nyingine  ni hichi,

 Watu hawaelewi ni jinsi gani huleta maana kubwa, kwa mtu km yeye kununuliwa  hata chocolate  nakuletewa kwa kunia  kumbariki........... aliongeza,  kwa nafasi aliyonayo amejikuta yeye ndo wakupewa ahsante maana anategemewa kutoa zaidi kuliko kupokea...............Hivyo basi  nyakati km hizi ambazo anajikuta yeye anatakiwa kusema ahsante zinapomkuta huwa anajikuta na yeye ni binadamu. aliongea mengi ambayo nilijifunza sana.......

 Ikumbukwe labda mimi nilivyofanya ilikuwa tuu labda ni mbinu yakumbariki tuu mteja wangu, kwa mahusiano  mazuri yakibiashara tuliyonayo,  Narudia tena kiasi alichotakiwa kutoa kwake ni km hela ya sukari au  labda ya karanga ,hivyo  sikuwaza  yale mapokeo yatakuwa vile alivyo, ( Ila sasa sema amenifanya,  kila ninachomfanyia nijistukie je nafanya ili nipate misifa  tena au?? hata chocolate aliyoizungumzia haipati tena ha!ha!ha!  Misifa isiyo na maana nikupoteza muda mjue)

 Nimeleta huu mfano ili kukazia mazungumzo yetu  lengo  nikujifunza unapofanya kitu unafanyaje, lengo ni nini?? na jinsi gani unaweza ukazalisha kitu chenye uhai kutoka pande zote mbili........


 Mnataka kujua sasa ilikuwaje tena? maana trip zilikuwa mbili, nilijigawaje??

Tutaendelea

No comments:

Post a Comment