Pages

Ads 468x60px

Thursday, January 1, 2015

JIKONI NA MAMA WAWILI.............

Ahsante Mungu tumeuona wandugu........Sio kwamba tu bora kuliko waliotangulia bali ni kwa neema tuuu................Kaa mkao wa matarajio maana UTUKUFU WA PILI NI MKUU KULIKO ULE WA KWANZA...... Tegemea kuongezeka katika  kila eneo la maisha yako.Mwaka 2014 tulikuwa na mengi tuliyoyapitia,Tulianguka na kujikwaa, tulishindwa na kukata tamaa, Tulishindwa kuleta ndoto zetu kwenye uhalisia na mpaka sasa hatuna matumaini.Ninachotaka kukwambia TUMAINI LIPO.......Bwana hajakuacha wala kukupungukia, aliruhusu maana ndivyo ilivyotakiwa iwe katika kukuleta  pale alipo kukusudia. Kumbuka Mungu wetu anatuwazia yaliyo mema. kwa macho ya kibinadamu unaweza usilielewe ruhusu Roho mtakatifu akusaidie kuelewa..........Naongea kwa ushahidi wapenzi 2014 kuna jaribu moja nilipitia, kiukweli ndani ya wiki niliteseka sana, maana nilishindwa kumuelewa Mungu, Nakumbuka kujisemea kwa namna hii ntawezaje kumtia mtu moyo??? Duuu!!! Pale nilipotulia na kuruhusu utendaji wa kiroho aisee!!! nakumbuka nilikuwa naoga bafuni nilipewa jibu ambalo mpaka sasa huwa nalikumbuka nakuogopa jinsi Mungu anavyo Shughulika na maisha yetu .......... 

Bwana alivyotutoa kwenye lile eneo Wapendwa leo hii tunamshukuru Mungu mnooo kwa ajili ua lile jaribu!! Sijui niwaambiaje mnielewe wapenzi wangu kwa mfano!!!!!!! zaidi ninatubu kwa ajili ya ile wiki tuliojipa mawazo, nakujipa maumivu ambayo bwana tayari alikuwa kazini...................Ninachotaka kusema ni hivi, Unamamlaka yakufufua mifupa mikavu, Haijalishi umezungukwa na nini, na nani? acha kusumbukia kwa habari ya kibali maana hapo ndipo wengi tunashikwa na adui........ Tambua uliyenaye wewe ni mkuu kuliko wakuu woooote wa dunia.Wewe ni mshindi,Tena ni kichwa wala sio mkia,wanasema,........ MAJARIBU NI MTAJI....................HAPPY NEW YEAR


out of topic: Hahaaa! jamani hatuja panda mbegu mwaka huu  because tuna madeni mengi khaaa!!! ile mbegu iliyopita bado hatujamaliza deni ngoja tumalize kwanza ha!ha!ha!ha!

haya mwenzenu ndo sikuu yangu jikoni duuu!!! siku kama hizi unakumbuka majiko ya chini yakukaa halafu mabinti wamekuzunguka unaita tuu fulani niletee, fulani osha.... fulani njoo nisogezeee ha!ha!ha1ha!
 nimesimama leo mwanamke masaa karibu sita!!!!kiuno hakina kazi aiseee!!!

 ndo nimeanza hapo... ee bwana hilo dude linavalia kwa vile tuu nimeamua kuwa kikazi mara chache sana kuniona nalo ha!ha!ha!ha!

 hii nimewaletea tuu haina uhusiano na mapishi muone mmalizio wa mti na taa wanangu walivyoupamba.

hapo zimetoka Sambusa,Vitumbua,Egg chop na Sparkling fruit punch
Kuku lazima sikukuu eti???

Egg Chop  zimegoma kidogo muonekano lakini zimelikaje??

Chezea mother house weyeeeeee.......
 nilihisi left over zitabaki wiki nzima tunaangaika nazo mmmmh!!! leo siku ya pili naona sahani nyeupeeeee ha!ha!ha!


midomo inajieleza ha!ha!ha!

Mama tomboa a.k.a vitumbua ndo anavyoviita mwenyewe..........

mapozi ya ya kushiba hayo.......

my life........Thank God!
Furaha yao furaha yangu. Ahsante LAMOUR kwa kuwapendezesha wanangu go follow her @akailatailors.

Nawapendeni na nyinyi wooooote wadau wangu.

Mbarikiwe

3 comments:

  1. Yaani!! Nafikiri Kuna muda Mungu anakutumia kunipa majibu ya maswali yangu! It cant be a shear coincedence!!

    ReplyDelete
  2. Hongera mama wawili sichoki kuangalia kwako pazuri sana! bila kusahau picha ya mwisho iko poa

    ReplyDelete