Pages

Ads 468x60px

Friday, October 11, 2013

NIMESHINDWA KUJIZUIA



 Naamini kuna Mtu mmoja katika hii Dunia yani kama ni Rose  ( mama wawili)  ni huyo huyo  akitokea mwingine watafanana kwa mambo fulani fulani lakini ukichunguza kiundani utaona tofauti kati yao, nikimanisha hata utendaji wao wa jambo,ndoto zao,  nini wakipendacho na nini asichokipenda............ ingawa, mara nyingine twafanana kwa sababu fulani fulani kama vile, nataka kuwa kama fulani, kumpenda zaidi muhusika,au inaweza kuwa moja ya misingi yakukamilisha uhalisia wako, lakini si moja ya misingi mikuu au mashindano kutaka kuoneshana mimi ni zaidi ya............. mengi ya haya hutupelekea kupoteza muda na kufanya ukamilifu wetu usikamilika  na zaidi kupoteza lengo lakujua wewe ni nani na umebeba nini ndani yako................



 nakazia kwa mfano mdogo kwa mablogger ili twende sawa ukitaka habari za utoaji, ujasiriamali na mashauzi yamjini mtafute  (Muke ya Muzungu,M.K), Ukitaka kujua Habari za maharusi na nini kinatrend muone  ( team hawachovi,Muke ya A), kwa habari za mujini nani kapigwa,kasutwa, kwa ujumla nini kinaendelea mujini muone (Dada yetu S. unstop...) kwa habari za ujumla  lifestle,serikali,mujini,............ muone (J.G muke ya D) hii ni baadhi tu yamifano tukazie mazungumzo yetu na hao ni watu ambao wengi wetu tunawafahamu wapo wengi mno mno................ukija kwa Mama wawili hapa utanipata kwa habari zakipendwa kutiana moyo we njoo tu tutafundishana kushika jembe,kulima, mpaka mavuno kigezo uwe na uvumilivu tu....... ukiona nafanya mengine mengine ujue labda niko inspired au ndo vile na mimi nataka nionekane kwi! kwi!kwi! ( mwenye uelewa na aelewe)

Sasa basi pamoja na kwamba tumeumbwa hivyo kuna watu amabao pia wameweka ili kukamilisha uhalisia wetu bila hata sisi au wao kujitambua mara nyingine...... nazidi kumtukuza Mungu kwa ajili ya hili fumbo..... natafakari tu kwa uelewa wangu huu mdogo kama lisingekuwa fumbo mbona humu duniani tungedaiana fadhila mpaka basi......... kitu kidogo tuu  tunalaumu bila mimi usingepata,nilikuombea wewe, na vitu kama hivyo lakini!!! huo ni ubinadam na ni kweli kiroho safi wandugu, Mfano kama mimi nilikuchukulia mtu muhimu sana kwenye maisha yangu na kufanya kila niwezalo siku utakayokuja kunijeruhi ntakumbuka tuu ile jeraha uliyoiacha ndani ya moyo wangu  siku zinavyozidi kwenda ndo naweza kujisahaulisha na kutafuta nafsi ya moyo wangu( human nature....) na hii ni sababu kubwa ambayo naamini kwa nini Mungu alifumba hili kwa baadhi ya watu na pia kuepuka kujitukuza mwenyewe bila kujiuliza uweza umepata wapi??? ( huo ni mtazamo tu wa Mama Wawili)


Leo katika pitapita zangu nimekutana na hii picha........ nimejikuta natokwa na machozi ya furaha huku nikiwaza mengi mno hasa katika safari yangu ya maisha................. ndipo nilipojikuta nikiandika haya yote......
Huyu Mama alipewa kipaza sauti siku ya graduation party yangu aombe, nakumbuka sikuwa kihivyooooo kiima lakini kulikuwa kuna connection moja ya hatari kati yangu na yale maombi sijui km yeye alilitambua hilo au ukimuliza nini aliomba siku ile atakumbuka mmmh!! mpaka apewe mkanda ajisikilize ki ukweli alitumika mnoo, alibomoa, aliharibu, alipanda, akabariki akaachilia mamlaka za kunifanya Huyu Rose anayeandika hapa............... kuna vitu naviona leo hii ninachoona ni list ya yale maombi aliyotamka siku ile huku kukiwa na tick kuubwaaa ikimaanisha IMEKUWA!!!!  Kwa kweli amekuwa ni mmoja wa watu walioifanya safari yangu nakukubali kutumika kwa uaminifu..........

NAMSHUKURU MUNGU MNO KWA AJILI YAKE NA PIA NA HESHIMU ILE NAFASI ALIYOKUBALI KUTUMIKA.......... JINA LA BWANA LIBARIKIWE


No comments:

Post a Comment