Pages

Ads 468x60px

Tuesday, October 15, 2013

NIKUTIE MOYO



Nimejifunza kitu, japo niliwahi kusoma na kukisikia lakini leo nimekishika mwenyewe na kukithibitisha................MUNGU WETU NI MUNGU ATUWAZIAYE YALIYO MEMA
wakati wewe unajiuliza imekuwaje Mungu hakujibu au amekaa kimya hasa pale unaposugua goti,unapolia, unapojeruhiwa na hata kujikuta umepoteza tumaini........ ninachoweza kukwambia Mungu anatambua na kuthamini maumivu,machozi,na kila kigumu unachopitia................ISIPOKUWA hivyo vyote haviwezi kuvuruga mpango wake ulio mwema kuliko kiwango cha vile ulivyokihitaji.................

na wakati mwingine huwa kuna mambo fulani fulani yanayoendelea ndani  kuhusiana na hilo jambo ambalo kama ungefunuliwa mwanzo ungeweza hata kubadili maombi kuhairisha  hasa ukiangalia ugumu na usumbufu wa wakibinadam....... hivyo kwa mtazamo wangu naona  ameamua kuruhusu tuuu hayo maumivu na machozi maana ndio kiwango chetu huku akiachilia ufanye kwa nafasi yako na Yeye amalizie kwa muda sahihi na kwa jinsi iliyo sahihi...................


 na pia nilichojifunza unapokuwa kwenye maandalizi yakupokea unahitaji hekima sana....  kama tujuavyo Baba wa uovu naye hajalala anatafuta mlango wa kuingia na kuvuruga na usipokuwa makini unaweza kupoteza kusudi zima  kwa wakati huo.......  ninachoweza kushauri ni kwamba hakikisha umekabidhiwa funguo yaani muujiza tayari unao ndio uruhusu mdomo wako kufunguka................japokuwa Mungu wetu halali wala hasizii kwa ajili yetu bado atafanya njia yakutokea...... aiseee!!!!! anavyokutoa sasa!!!!!!! ( ha!ha!haaa!! nimejisikia kumcheka Shetani wandugu maana kwa hili hajanipata............ anasoma namba)

 Mwisho nilichojifunza ndani ya  hili Mungu hafungi mkataba juu ya jambo fulani alilokupa, atakufungua tuu ujue ni kwa nini hakukupa lile amekupa hili, wapi ulipo kosea , na kwa nini amekupa muda huu na sio muda ule, ni kwa nini aliruhusu upitie yale uliyoona kuwa ni mazito na magumu kumbe kilikuwa kiwango chako, kiwango cha uhitaji wako ulikiweka chini sana nakujisahau kuwa wewe ni kichwa na wala sio mkia,na mengineyo mengi yatakayopelekea kujitathimini na kujitambua  HUKUHITAJI MUUJIZA ULE BALI HUU ULIOUPATA SASA UNAKUSTAHILI NA UMEKUJA  KWA MUDA ULIO SAHIHI............

HUYU NDIO MUNGU WETU BWANA!!!!!?????

kesho nitafunguka kidooogo kwa mifano halisi ILA maliza kwa matumaini makubwa INAWEZEKENA... NA MUNGU HASHINDWI NA  WALA USIMPE MIPAKA YA UKUBWA WA JAMBO...... UWEZA WAKE NI ZAIDI YA HIVYO UNAVYOFIKIRI........

( mnaochukia maandishi wiki hii mnisamehe kidogo niko kihisia zaidi....)

No comments:

Post a Comment