Pages

Ads 468x60px

Monday, December 8, 2014

NAWAMISO.................



 Wapendwa wangu huku mafichoni hakuna jipya, Habari ya mjini ni maproject tuu Ha!ha!ha!  

 Hivi ndugu zangu hii project iliishaje?? maana naona kama hii video ilitoka kama miezi miwili mitatu iliyopita au ilirekodiwa miaka hiyo???? Imekuwaje sasa wameitoa kipindi hichi ?? mbona kama naona uhalisia na video vinanichanganya???? Au mimi ndo sielewe maproject huwa yanakaaje?? kweli ushamba mzigo yaani kama ,maproject ya pande ile ndo yamenimalisa kabisa mwenzenu khaaa!! 

Vinginevyo wimbo mzuri, umebeba ujumbe mzuri,Tatizo ile project yao sijajua ilikuwaje japo hainihusu............. mzigo unakuja pale ninapousikiliza huu wimbo mapokeo yanagoma kabisa.

Hapa ndipo unapokuwaga mtihani kwa watu fulani fulani ,kwa pande hii naweza sema Watumishi,  muimbaji, mchungaji,  ni kweli huwa kuna uvumi, au mara jingine kama wanadamu huwa tunakosea lakini huwa kuna namna fulani huwa tunatakiwa tuifanye.
Ngoja nijisemee kwa mfano Mimi sihitaji kujua ilikuwaje au imeishaje, ili niupate huu ujumbe vizuri labda ningepata suprise moja kali kwenye moja ya media kama nilivyozoea kuwaona na mabig smile yao hata kwenye video wenyewe mjionee............... then ndo ningekuja sasa kuiona hii video duu!! yaani ningemtukuza Mungu mnoo kwa ajili yao, Ningemcheka shetani mpaka angeshangaa kwa ajili yao(Angalizo,Namtukuza MUNGU na Nakumcheka shetani kila siku hapa nazungumzia kwa hili).
 Mbona hii CD kwenye gari isingetoka  ningeisikiliza mchana na jioni.....maana natembea na ushuhuda ulio hai.(After maproject)

Yaani, hili limenifanya nijiwazie mwenyewe hivi YESU alivyofufuka angeamua   aunge zake mbinguni bila kuwatokea wanafunzi wake ili kuthibitisha ufufuo wake kama neno lilivyoandikwaingekuwaje??? hivi sipangetokea kamvurugano fulani japo bado kuna wale ambao ,mpaka kesho hawakuamini kwa maana tangu kabla haijawa walishajipa majibu kuwa ni uvumi................ Nielewe niliposema hapo juu kuna namna fulani yatupasa kufanya...... kwangu mimi achana tuu na ule uthibitisho naamini wanafunzi hapa walifarijiwa, walitiwa moyo,na pia walipata nguvu zaidi yakusonga mbele .

Nimejiuliza tuu kama asingefanya vile mbona tungekuwa namaswali mengi sana hivi leo........... na pengine kuamini kwetu kungekuwa kwa mashaka,  labda ndo maana na mimi nimeshindwa kuisikiliza kwa hisia nakutaka kuelewa zaidi (Nawaza tuu wapenzi). Na vipi sasa kwa yule ambaye yupo mlangoni anataka kuingia???? Anaanzaje sasa kutuelewa????Asikwambie mtu wapendwa kuna mahusiano makubwa mnoo kati ya ujumbe na mtoa ujumbe.

 Hee nimeanza sasa.... mtajiju si mmenimiss wenyewe???? ndo nimekuja sasa ha!ha!ha!ha! haya ndo mnijibu na ahsante woooote kwa mainbox yakunikumbuka...........


Penda nyie sanaaaaa

1 comments: