Pages

Ads 468x60px

Thursday, December 13, 2012

MTAZAMO


Duniani kila mtu anahitaji  second chance, siongei kwa sababu ya kitu ila nimeguswa na picha nzima ya bidadaa nimejiuliza mengi sana km kusingelikuwa na second chance sijui leo ningekuwa wapi...... wakati huu ni wakati ambao mtu hujitambua na kujirekebisha na wakati huu pia unategemeana  sana umekukuta katika mazingira yapi.......na kwa habari nani anisaidie ili niwe sawa Mungu mwenyewe ndo atajua atumie daraja lipi ili nipite..... kuna wakati huwa naona ni vema mtu apite mazingira fulani ambayo badae akatengenezea ushuhuda kwa maana nyingine asivuke stage fulani ya maisha ili asijekuwa limbukeni..... sio stage zote ni nzuri inategemea na mazingira mfano isingekuwa rahisi kumkuta mama wawili nimedondokea kwenye madawa km bidada lakini ilikuwa rahisi kunikuta kwenye ulevi NA AHIMIDIWE HUYU MUNGU ALIYENITOA HUKO LEO NASHUHUDIA......NI  mengi sana niliyoyapitia ambayo yananipelekea ni heshimu nafasi ya pili na pia na furahia kwani naamini kulikuwa na sababu iliyonipelekea leo niwe hivi nilivyo.....

nani atatumika kuwa daraja...... jamani hivi hujawahi kuona unamatatizo mengi lakini unajikuta unasacrifice kila kitu unamsaidia mtu mwingine???? huu ni ubinadam wa kawaida tu haijalishi we ni nani, na pia huo ndio wakati tunaouita unatumika kwa ajili ya maisha ya mtu fulani ili avuke kwenye daraja.....sioni ajabu kwa Muheshimiwa anaweza hata yeye mwenyewe hajielewi kwa nini amefanya Wakati ulioandikwa ukifika umefika.........

Mi namtakia kila namna yakushinda hayo aliyopitia huyu bidada.... 

ni mtazamo wa Mama wawili......

No comments:

Post a Comment