Pages

Ads 468x60px

Tuesday, February 2, 2016

NYUMA YA PAZIA 2

Siniliwaambia tukaenda kijijiniiiii.......... Basi huko tulimfuata huyu bi mkubwa aliyemzaa Mama mkwe wangu, Kwa upande wangu hichi kizazi hakipo tena.........Hivyo tuliona kuna haja ya watoto kwenda wakaelewe na vile vile Mume wangu kalelewa na huyu Bibi wakati wazazi wamehamia kwenye miji yao.......... kwa kweli nilijifunza mengi mnoo hapa kijijini aisee, watoto walienjoy mnooo............. 
mzee anamaneno huyu hatari anakwambia vita vya Hitra  mi nilikuwa binti mkubwa sana..........(nyoo mi mnafikiri mi mwenzenu?? pumbavu zenu in her voice ha!ha!ha!).
ana mipasho ya hatari 

Anakwambia hao ndo mabest wake yaani usipomkuta kwake mtafute kwao ...........

Aisee jiko ndo nilikabidhiwa ha!ha!ha! nilikoka moto aisee, nilipuliza kuni ha!ha!ha! sio msosi wa watu wawili yaani ilikuwa ukitenga sufuria kama hakuna wageni basi idadi ndogo watu ishirini hivi kikikikiiii 


Team matembezi tulikuwa tunazunguka tuu kijijini huyo mtoto mdogo, mtoto wa mdogo wangu  watu walikuwa wanafikiri nae wangu ha!ha!ha!

spotted


Team no stress tulikuwa tunajizungukia tuu. Excuse nywele za Careen zilitakiwa ziwe za kubana alivyoona mwenzake bob basi akagoma kufunga......

 spotted

tukapelekwa shule aliyosoma Dad ake......ha!ha!ha! i wish mngesikia hayo maswali yaliyokuwa yanaulizwa na watoto wake kikikikiii!!
kuna picha moja Baba yao alipiga enzi hizo kwa pozi hilo la Careen na eneo hilo hilo , Sasa Baba yao anawakumbusha hiyo picha  basi ikawa kosa wakaanza kumtania eti na wao wanaiga pozi ha!ha!h!

my wawili my life!

 nimezipenda tuu picha nimeshindwa nitoe ipi niache ipi nikikumbuka namazungumzo ya hapo basiii!!


 Tukapelekwa na Darasani aisee wanangu wanahistoria kichwani........ Nafurahi kile nilichotegemea wakajifunze hapo kijijini walikipata na zaidi..........

Tunawapenda

2 comments:

  1. Bibi amejua kunichekesha. Furaha ilimzidi bibi jamani. ila huko kwa green hadi raha. Ndo mlienjoyije?? Wa kina careen wangu watalilia kurudi tena.

    ReplyDelete
  2. Nice photos, nice family...mama wawili mwenzio

    ReplyDelete