Pages

Ads 468x60px

Sunday, March 13, 2016

TUZUNGUMZE

Wapenzi wangu  kumekuwa kimya sana......  kikubwa kwa sababu ya mda ambao nimejiona km ikitokea kupost basi cha haraka ni  mapicha  kitu ambacho sina uhakika km ndio kusudi kubwa la blog yetu.......

 Lengo kubwa la blog yetu ilikuwa nikumrudishia Mungu utukufu kwa yale aliyotenda anayotenda na atakayoendelea kutenda,  nikimaanisha kimwili na kiroho, uelewa wa mambo na jinsi unavyoweza kukabiliana nayo.........Hivyo utakubaliana na mimi topic za Tuzungumze ndo kubwa zinazobeba ujumbe wa blog. Mapicha ilikuwa ni kajisehemu tuu kakuchangamshia genge.

 Kutokana na kubanwa kidogo (jina la Bwana libadilikiwe ananiinua viwango kwenda viwango) lakini bado kuna hii kalama ambayo naamini nisiiache ikapotea...... naamini kuna wengi mnabarikiwa  ha!ha!ha!   badala yakukaa masaa matatu mpaka manne chini kuandika kufuta yaani too much  nimejikuta  nimekaa baada ya kutoka kanisani nawaza hayo masaa yakuandika yaani naweza sema huu ndo muda wangu mwenyewe hasa baba wawili akiwa hayupo nawatoto wako busy na movie zao baada ya kanisani............nikajikuta nimewaza kumuita mtoto anichukue video ya dk 10 kusave masaa yakuandika nilichotaka kuandika ha!ha!ha! yaani nizungumza kwa sauti hahaha!! nianze kujirekodi  halafu niwarushie kitu ambacho naamini hakita chukua  muda na labda kwenye kuzungumza sitatumia nguvu mnoo na akili ya kuchambua ili ujumbe ufike ha!ha!ha! 
 halafu ndo tuendelee na mapicha....

 nimejikuta nasutwa sana kurusha mapicha tuu bila kusimamia kusudi ambalo hapo mwanzo lilikuwa kiukweli nimejikuta nateseka tuu  km mkinisoma nimekuwa mvivu sana kuyapost huku ila ukinifuata facebook na instagram narusha rusha tuu.......


haya kwa udhamini wa Careen ingia kwenye link 


ukajue nimezungumza nini.... hatukujipanga jamani imetokea tuu   kiswangishi kiko humo ni noumaaa ha!ha!ha! na dogo kweli kunichukua kwa dakika 8-9 aisee...... nilimuahidi chocolate ha!ha!ha! wanaruhusiwa chocolate moja kwa siku so nimemwambia akitulia ya pili anapata ha!ha!ha! utaona mikono mara sijui kafanyaje lakini kwa ujumla ujumbe umefika...... 




Nawapenda

1 comments:

  1. Hiyo mama wawili inaitwa kuishi maisha yako...
    Mimi sipendi sana ku interact na watu sababu nimegundua nina differ na wengi...na mazungumzo yangu yanaishia kuwa kikwazo...
    Ila kuna ambao nimeshawasoma na sina shida nao...
    Unaweza ukaongea kitu mtu akaona unaringa, una dharau kumbe wewe hauko huko...
    Ningekupa mfano lakini naogopa labda niliozungumza nao wamo humu...
    Lakini nimekuelewa...ni ngumu sana ku share your dreams, na successes na watu afu wakachukulia pouwa...ni bora uishie kuongea na baba wawili baas...

    Watu wengi confidence zero...niliwai ongea kitu kwa office mate wangu basi kila siku akawa ana rewind kwa watu wengine...sikumuelewa maana yeye mumewe yuko vizuri saaana kuliko sie lakini kakwazika kuona nina big dreams...
    Mama wawili mwenzio

    ReplyDelete