NAHESABU MASAA TUU NIUONE MWAKA 2013....... nina kila sababu yakumshukuru Mungu kwa yale yote tangu nilipokuwa tumboni mpaka hivi leo........ nimeona, nimeshuhudia, nimepitia, na bado nangoja......Mbali na miangaiko ya dunia ile tu kupumua na kuwa na afya sina sababu yakutokukushukuru.........Umenibariki siku hadi siku,umeniinua kutoka katika kiwango kimoja kwenda kingine, umeniweka mbali na mikono ya waharibifu, nimekuona ukinitetea na kunisimamia hukumu ya wale walionipiga vita............ooh! nikijikagua, nakiri kwa akili zangu timamu mimi si mkamilifu mpaka nikastahili haya.! bali ni neema na upendo wako kwangu unaonifanya nijivunie kuwa wa thamani mbele zako.............Ahsante kwa damu ya Mwanao ambayo imemwagika nakufanyika ukombozi wa maisha yangu..........Nisaidie Bwana kutokukumbuka majeraha niliopigwa na adui yangu mtesi ambayo yaliniinua kiwango kikubwa cha imani kwa maana uliruhusu kwa sababu, na wewe ni Mungu utuwaziaye yaliyo mema........ ukanipe kibali niingiako na nitokako, ukanifanye mkuu ktk kila ardhi niikanyagayo, neno lako likafanyike dira ya maisha yangu, nikakamilishe yale uliokusudia bila kuruhusu mkono wa muovu ulionia mabaya juu yangu..................ukanipe heshima ya kuwa Mtoto,Mke,Mama,mchapa kazi,rafiki kila kitu kwa nafasi yake.....zaidi ya yote ukainue kiwangu changu cha maombi,usomaji wa neno na kulitendea kazi, maana ndipo palipo uzima..............
binti mlokole akitoka kanisani
kila la kheri wadau wangu.........
msikate Tamaa ng'ang'ania muujiza wako mpaka kieleweke
songa mbele.........
angalia kwa umbali ulikotoka na mshukuru Mungu kwa hapo ulipo..........jipe moyo hata hapo palipo baki panawezekana.......
tarajia mwaka wa ushindi, panga mikakati iliyo sahihi mkabidhi Mungu.........
anza Mwaka kwa kutafakari..... jipe muda wa kutosha ikiwezekana usijichanganye sanaaa...... maana mwaka utaanza bila kujijua umeanzaje...... kwa mfano ukianzia kilabuni hivyo ndivyo mwaka wako utakavyomaliza hahahaaaaa!! mtazamo tuu.......
muke ya Slay......