Pages

Ads 468x60px

Wednesday, December 4, 2013

TUZUNGUMZE



Kwa uelewa wangu huu mdogo nyumba ya Mungu ni sehemu pekee tunapokuwa na Muda mzuri  wakutafakari, kujifunza, kujikumbusha, neno la Mungu  na pia kusifu na kuabudu kwa habari ya Matendo makuu ya Mungu. kwa mfano unapokuwa kazini akili yako nyingi unaitumia masuala yanayohusu hiyo kazi, na unapokuwa shuleni  muda mwingi uko bize na masuala ya shule japo kuna muda wakuvusha bado hauchukui muda  mwingi, ndivyo ilivyo pia harusini,msibani,na shughuli yeyote ile wanadamu tumekuwa tukiwajibika sawa sawa ........... nazungumza na yule anaenielewa japo kuwa ,bado tuna watu wako kinyume kwa kila kitu yupo darasani anawaza makumbi ya starehe,kanisani anawaza biashara yaani yeye ni Z-A sio A-Z huyu tumuache kwanza...........................


Kinachonishangaza inapofika kwenye suala la nyumba ya Mungu, wandugu tumekuwa wazito  mnoo, tunatafuta sababu sana ,sijui hili pepo limetokea wapi?????? wengi wetu  tunaamini lakini ikifika suala la nyumba ya Mungu linapewa nafasi ya mwisho kabisa. imefikia hatua tunakwenda nyumba ya Mungu kwa bahati mbaya na sio bahati mbaya kukosa kuingia nyumbani mwa  Mungu.Nijuavyo mimi ile tuu kwenda kwenye nyumba ya Mungu ni ishara ya Shukrani, unyenyekevu,kuthamini ile nafasi aliyokupa Mungu hapa Duniani bila kujari unapitia nini na una hali gani ile pumzi tu, inatosha kupondeka na kumrudishia Mungu utukufu.


Wengi wetu tumenyoosheana sana vidole kupata sababu tusiende kanisani tunadai kwa sasa hakuna kanisa la kweli sijui unasoma kitabu gani basi hata kama ndo hivyo nenda basi ukabadilishe hali ya hewa ( siumesoma Mungu anajibu maombi ya mwenye haki?? kupitia wewe kanisa la kweli litapatikana kama ukisimama kwa nafasi yako) wengine wamedai wanakwazika kupitia waumini wengine( kwani huja soma tuchukuliane sisi kwa sisi mbona ukialikwa maharusini,na shughuli zozote zinazofanana ukifika unawakuta wenyewe wamekuandalia na taarabu na miili yao sasa, we mwenzangu na mimi mwili kama wa Mama wawili hapa na hata hizo nyimbo zenyewe huzijui lakini bado utachukuliana nao tena utahudhuria mpaka mataa yazimwe, sasa kwenye nyumba ya Mungu kinakushinda nini tena unadeal na watu wa imani moja?????? asikwambie mtu hakuna kitu kizuri kama kudeal na mtu wa imani moja na hofu ya Mungu ikiwa ndani yenu.

wengi wetu tumedai makanisa ni Biashara  kila ukienda kinachozungumzia ni sadaka ,kwani we mwenzangu unasoma kitabu kipi  ambacho hujakutana na  fungu la kumi,sadaka za shukrani, ahadi,malimbuko,kawaida,mavuno,upatanisho, dhambi na zinginezo??? huyo unaesema mfanya biashara yeye anakufundisha kweli ikupasayo kufanya huku anajilia taratibu fungu la kumi na kulijenga kanisa,hata hivyo  ni haki yake wandugu msimchungulie sana!!! na hata kama haitendei sawa sawa wewe haikuhusu fanya kama neno linavyokwambia hayo mengine atajuana na Mungu wake........ tufikie hatua tukomae wandugu .......... ninachosikitika sana hapa hata madhabahuni hofu imeingia kulisemea hili tumekuwa tukiambiwa habari za kupokea  bila kuhusianisha na kutoa, kwa akili zangu hizi ndogo somo la kupokea linamahusiano makubwa  nakutoa, kupokea  bila kutoa ni danganya toto wandugu...............

Nawengine tumejiwekea kautaratibu kabisa eti badala yakutoa fungu la kumi kanisani bora nikampe muhitaji, ndugu kila sadaka inautaratibu wake sadaka ya muhitaji na fungu la kumi ni sadaka mbili tofauti labda mimi ndo sielewi lakini kama wote tunasoma kitabu kimoja turudi tena darasani na roho wa Mungu akatuongoze kulipambanua hili (watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa)
 na hizi zote  ni mbinu za muovu kutaka kutuchanganya KWELI ITABAKI KUWA KWELI.

Na wakati mwingine mi naona roho za ubinafsi umetuingia tunakwepa majukumu, kanisani hebu tutafakari utawajibika wapi kufanya kazi ya Mungu????? kama tupo bize mitaani??? nikisoma wenzetu waliweka manukato kwenye madhabahu, wakina Suleimani walijenga kanisa kwa Dhahabu,wakina Daudi walibeba sanduku kucheza mpaka nguo kutoka leo hii hata kwenda kushiriki  kupanga meza,kusafisha kanisani hatuwezi  na bado tunalalamika hatumuoni Mungu maishani mwetu ...... tujiulize wewe na mimi tumefanya nini nyumbani mwa Mungu hata tukatikisa madhabahu ya moto ikashuka kujibu maombi yetu.tufanye kwa nafasi zetu na yeye Mungu wetu atafanya nafasi yake tusitegeane wapendwa.

wanadamu tumekuwa na sababu mnoo wandugu, haya kwa sisi watafutaji sasa utakuta jumapili pesa inakuchungulia mnoo ,wenye shift nao za double pay, na mimi mama wawili hapa jumapili utakuta na magari kama matatu yakuosha yenye thamani si chini ya $800, hapo mimi na Baba wawili kama sio kanisani mbona tunakomaa tunapiga bila garama zakumlipa mfanyakazi......... wakunielewa na anielewe mwisho wa siku pesa ni makaratasi mpango nikujiongeza kwa huyu yeye anayeweza kukupa hayo makaratasi.....................



Wandugu sijakamilika hata mimi bado sana nahitaji neema ya Mungu kumjua zaidi ila kwa hili la kwenda kwenye Nyumba ya Mungu lisitafutiwe sababu tena litufanye kuwa na shauku ......yaani kama mimi Mama wawili hunipangui kabisa kwenye Muda wa kwenda kanisani wanaonifahamu wanalijua hilo na wengine wameniita mnafiki naenda kufichia maovu yangu huko ( waache wajinga na ujinga wao kasome mithali 14:7-9) ukizingatia naupata kwa masaa mawili asubuhi na jioni mawili hapo nimesifu,nimeabudu, nimepata neno na kunyweshwa chai,  tofauti na hapo milango imefungwa kama unaingia lazima uaminike kupewa funguo yakuingia mara  kwa mara  hata hivyo hairuhusiwi(chezea nchi za watu) nawaonea wivu sana mnaopata muda masaa 24 nyumbani kwa Bwana aisee.


NIMEMALIZA NA MBARIKIWE




Yohana 15:18-20

18 “Kama ulimwengu ukiwachukia, fahamuni kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa watu wa ulim wengu huu, ulimwengu ungeliwapenda. Ulimwengu unawachukia kwa sababu ninyi si wa ulimwengu huu na mimi nimewachagua kutoka katika ulimwengu.

3 comments:

  1. umesema kweli, yatupasa kumpa mungu yalio yake kwenda kwenye nyumba za ibada na kusali kwa pamoja tunapata baraka nyingi sana kwani alisema walipokusanyika wawili watatu nami nipo.

    ReplyDelete
  2. nakupenda bure mama wawili

    ReplyDelete
  3. umenigusa haswaa!! Mwenyezi Mungu anitie nguvu!

    ReplyDelete