Pages

Ads 468x60px

Tuesday, February 4, 2014

THE DAY.............


Haya ile siku yetu yakuvaa nguo za shule ndo ishaanza........... ni full shangwe ndani ya nyumba ninavyosaidiwa kuhang na kuziweka vizuri sasa mwee...... ila kuna haka jambo mwenzenu mnisaidia naumia wandugu wala sio masihara nafikiri sijajua njia mbadala yakutumia kina mama wakibongo popote mlipo..........

 nimeamka asubuhi naimba ule wimbo, HALELUYA TUMSHANGILIE HALELUYA, SIKU TULIYOINGOJEA IMEWADIA...... nikijua ntapata suport from them maana huwa tunapenda kuimba pamoja,  ikiwa kama mbinu yakuwaamsha nimeingia room kwa Christabell kastuka natabasamu kubwaaa (GOOD MORNING MUMY) in her Voice nikamjibu tukapeana ma hug na makiss kama kawaida yetu tunaelekea kwa Careen sasa mi naendelea kuimba huku Christabell anatabasamu, Careen anastuka MUMY WHAT ARE YOU SINGING???? WHAT IS TUNKUSHANKILIYE MEANS??? in her voice...... Heee Mama mtu naumbuka kumbe hapa hatuelewani nimekuwa kituko??? Hii hali mwenzenu huwa inanitesa, hasa pale wanapoongea na Bibi zao bongo wanapofikia mahali hawaelewani..... Bibi hawezi kujiongeza wala mjukuu hajiongezi, nabaki kurudishiwa simu na lawama juu..... Jamani wenzangu mnafanyaje wapenzi najitahidi sana lakini naona siku zinavyozidi kwenda bado hakieleweki na hii inachangia sana maisha yao ya daycare mimi ninapokuwa mzigoni..... nimewaza labda nitafute vitabu labda tuwe tunawasomea tukiwa na muda ila nawaza haviwezi kuwachanganya??? hasa sasa hivi walivyoanza shule wanatakiwa kutokuchanganywa ili akili yao itulie sana na kile wanachofundishwa?....... maana bado kuna maneno huwa wanachanganya na kiswahili ila wao hawaelewi kama ni kiswangish ... siku moja nilienda daycare nikaambiwa Christabell amemwambia mwenzake MY MUMY IS GONNA CHAPA YOU, sasa walimu wanataka kujua chapa maana yake nini.... yaani wako hivyo wapendwa, walilojua neno la kiswahili wenyewe wanajua ndivyo hivyo wanavyotakiwa kuzungumza . 

KINA MAMA OUT THERE MNANIELEWA PLEASE SAIDIA MIMI 
day one toto za mimi hizi


my life
kamkono kamenyooka ka mama wawili jamani kusuka zakuendea shule sio mbaya eti???

 i cant wait kuwaona wanavaa vi skirt na vigauni shule yao pre primary wanavaa hivi  year one ndo mwendo wa vigauni na skirt.kindy ni option avae au avae nguo ya kawaida ... i thought kwa siku ya kwanza ngoja na kenyewe kajisikie kako shule. 


Siku hazigandi wandugu AHSANTE BWANA YESU

3 comments:

  1. Hongereni saana dogo , mabinti wako vema na wamependeza....Nawatakia shule njema,neno la kwenda nalo shule " tutakuwa vichwa na wala sio mkia".

    ReplyDelete
  2. Mwenyezi Mungu akukuzie..wawe vichwa na sio mkia. AmEN

    ReplyDelete
  3. Wala usiwe na wasiwasi kuwa watachanganyikiwa kujua lugha mbili tofauti. Nilikuwa na wasiwasi pia kuhusu wanangu nikamuuliza pediatrician akaniambia ikifikia wakati watajua wenyewe! At home tunaongea both swahili &english...ninapoongea na baba yao swahili ninapoongea na wao nachanganya...tena hiyo " I will chapa you" ndio yenyewe.
    KUHUSU nyumbani TZ wala usiwe na wasiwasi najua huwa wanalaumu sana kwanini hawajui kiswahili but remember they live abroad...na kutwa wapo na watu wanaotumia kiingereza.
    BUT uwe unawatupia neno moja moja wakiwa wanaongea na watu wa nyumbani example "shikamoo" na mengine ambayo atakumbuka kuongea nao next time.
    Yrs. mama J&S

    ReplyDelete