Haya wapendwa wa mimi ile siku yetu yakuadhimisha upendo iliendaje??? mwenzenu kwanza niliisahau kabisa sasa sijui ndo kuchuja kwa penzi au??? Ha! ha! ha! cha ajabu tulikuwa tumepanga quality time zetu bila hiyo siku kuiweka kwenye ratiba ,nilikuja kustukia mared kopa kwenye mitandao few days before ya wapendanao, heee!! nikajikausha nikijua nitamsuprise Baba watoto in a day.... mara nyingi huwa napenda kufanya kitu tofauti nyumbani kwangu, mfano mwaka jana nilitandaza red roses kila kona in our bed room mpaka bathroom, mwanga wafujo fujo kureflect mazingira, kubadilisha dizaini ya muonekano na candle fulani, na vikorombwezo fulani mnyalu mie, bora mradi siku iwe yakitofauti...... (Kwa mama wawili chakitofauti maana huwa sifanyi mara kwa mara wandugu Khaa na haya mabox ya ulaya!!!!! mmh!)then hayo mengine ya kwenda sijui Dinner na vizawadi yalifuata, so nikiwa tayari nimeshapata idea nifanye nini in a very limited time na ubusy huu, sinikasahau tena a night before maana ilikuwa busy mnoo........ gafla nikiwa kwenye usingizi mzito alfajiri na mapemaaaa, i got a soft, warm kiss from my Huby,iliyonitoa usingizini huku sauti ikininon'goneza Happy Valentine. Hee nilikurupukaje??? maana niliona kama naota ........mtu niliyetaka kumsuprise yeye ndo kanisuprise kwi! kwi! kwi! sikumbuki kama niliijibu zaidi yakushout No! sio leo Ha! ha! ha!lakini nikajipa moyo atanikoma akirudi kazini leo maana ni full maujuzi mwee!!!! ile nimefika tuu na mimi ofisini kwangu nikijua ntachomoka nikafanye nilichotaka kufanya duu!!! one of my team ananipigia simu haji anaumwa, ikimaanisha nina short staff, kulingana na mzigo uliopo boss sina ujanja lazima niingie mzigoni kusuport team.............. mwisho wa siku hakukuwa na maujuzi wala masuprise, zaidi ya muhusika kurudi kazini kwake nakuja kunisaidia kazi zangu maana ilikuwa ni balaa akili aykuwa mengine kwa kweli haikuwepo........ huyu ni mama wawili na wale wenzangu wote iliyowapita in either way msinyongeke sana, hiyo ni siku tuu na haitupi asilimia mia kwamba ndo kupeeendaaa au Kupeeendwaaaa.... upendo wa kweli haupimwi kwa hiyo siku japo ni nzuri kuona mtu anaijari kwa namna fulani........
Na wale wenzetu mlioisherekea ipasavyo hongereni mno.... nimefurahi kuona watu mitandaoni walivyoisherekea tofauti tofauti yaani hadi raha...... kuna hii moja hapa ya my girlfriend kweli nimeipenda mno, kaujuzi tuu kale alikowaza kufanya fanya nimependa...........
hakuhitaji kutoka aliona afanyie kwenye moja ya kajisehemu ya nyumba yake.......( je kunahitaji mabillion kufanya hivi? NO! ukishindwa kununua hizo red red tumia hata khanga unayovaa, maua jipitishe kwa jirani hapo vuta viwili yaani ni ubunifu tuu
nimeona aibu tuu kumuuliza wifi yetu.....ila nahisi alipofika tuu baba watoto kutoka kazini alimpeleka bafuni kwanza na kumvalishwa ( Nimewaza tuu) ( Je inashindikana???)
hivi kweli kuna haja ya kwenda Dinner hapo??? hata kama uwezo wa samaki haukuwepo hata dona na mlenda wako we dizaini kitofati tuu na alivyozoea kuifanya siku.....
usiulize kwa nini kaka yenu katulia kwa wifi yetu, mipicha tuu inatueleza jinsi alivyo happy
haya sasa( sio kwamba hatutandiki vitanda vyetu ni maubunifu tuu yakufanya siku iendee hata kama aliondoka asubuhi amenuna kwa maujuzi haya mmmh!!!
The End......
Mwisho wa siku tusikariri nimeona watu wengi wakilalamika siku haikwenda kwani wenzi wao wengi walisema hawa pesa, mara walikuwa wamenuna, mara yaani ni lawama mwanzo mwisho. jamani watu tunakariri sana hizi style mi kunasiku huwa nalaumu kwa nini hii mitandao ilikuwepo yaani tumekaa kimaigizo igizo hata na vitu ambavyo hata they dont real matter ila kwa sababu mtu kafanya basi hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa, hujui tunaigiza au la tena na sisi wenye uwezo wa kurushia vipicha ndo tunawamalizaje sasa. ( bahati mbaya hayo ndo yaliyonikuta mbona picha lazima mngeziona) Na wengine mlikuwa mmekaa mkao wakusubiri kuona mapicha ya Mama wawili.....
Ni kweli sa nyingine huwa tunabomoa na kungine tunajenga cha msingi ni wewe mhusika unayepokea uwe na ufahamu nini kinakufaa na nini hakikufai.
hi mama wawili
ReplyDeleteumejisemea ukweli mwaya.Naona tuache kusubiri kutendewa.Its time wake tutende tu.Japo kidogo kwa uwezo wetu
mama wa3
naomba nikurekebishe kiswahili kwa upendo tu , ni YALIYOJIRI, na pia neno kwa AJILI sio ri!! naona unaweka R kwenye haya maneno mara kwa mara. kiroho safi tu ukipenda pokea.
ReplyDeletesorry i mean sometimes unaweka L, or R pasipostahili.
ReplyDeleteusijari mdau wangu mwenzio hili ni janga inapofikaga kutofautisha L na R nimtafaruku kuanzia kutamka mpaka kuandika .... tena bora nikiwa naandika halafu narudi tena nakurekebishika muda mwingine na google inahusika sana ila kwenye kuongea utanihurumia........ahsante
ReplyDeletewe mama wawili umenichekesha, katika kumjibu umechapia tena hahahah
ReplyDelete