Wandugu semeni neno tupone, mwenzenu nimeshindwa kabisa, kila mstari ninausoma najikuta nalia mno mpaka nahisi kama sijaelewa., ( kwa kusema hivi simaanishi HAKUNA SOLUTION, au MUNGU HAWEZI!!!! hapana HAKUNA LINALOSHINDIKANA KWA MUNGU) ILA,nikisema niseme neno kwa mna huu nahisi my emotions inachukua nafasi sana kuliko hekima ya Mungu. sijapitia hili pito lakini kila huwa nikijaribu kujiweka kwenye majaribu ya aina hii., huwa UBINADAM UNACHUKUA NAFASI SANA mpaka nitulie kidogo....... ila naamini MUNGU HAWEZI AKARUHUSU JARIBU AMBALO SI SAIZI YAKO..........
Hongera kwa blog yako nzuri inabariki pia.
Mimi
ni mama wa umri wa miaka 30 sasa tatizo langu ni hili naomba unishauri binafsi,
ikiwezekana na wasomaji wako wa blog waweze kunishauri. Pia naombeni maombi yenu
pia sababu nahisi nakufa taratibu kabla ya siku yangu kufika. Naomba Email yangu
uiweka kapuni.
Nimeolewa
na nimeokoka kwelikweli. Mwaka wa 6 sasa katika ndoa sijapata mtoto, sijawahi
kupata mimba wala kuhisi dalili hizo. Nimezunguka, nimetibiwa, nimepimwa na kila
njia kwa kadri ya uwezo wangu lakini hola. Chakushangaza ni kwamba kila
nitakavyopimwa na kutibiwa vipimo vyangu pamoja na mwanaume vinaonesha ni mzima
ila madaktari wanajaribu kunipa dawa labda za kuharakisha na kadharika.
Nimeshaombewa
dada nimeshajiombea na marafiki ndugu na jamaa lakini wapi tatizo lipo pale
pale. Siku moja nikajipa ujasiri nikasema kwakuwa napenda watoto sina tatizo ila
Mungu hajanifungulia njia nikachukue mtoto mchanga wa kumu-adapt ili awe kama
wangu nimlee kwa mapenzi yote yaani huwezi kuamini mume wangu alinibadilikia
aligomba akaanza kunituhumu kuwa huenda namu-enjoy labda najua tatizo langu au
ni mgumba mimi yaani sikuamini ninachokisikia aisee isitoshe yeye ana watoto
wake wawili amewazaa na mwanamke mwingine kabla sijaolewa nae. Sasa nimekaa
najiuliza hivi huyu shetani ni wa aina gani ambaye asikii maombi au Mungu
anataka kunipa watoto wa uzeeni kama alivyofanya kwa Sara na Elizabeth kwenye
biblia. Ninamawazo yasiyoisha nilikuwa napenda sana watoto hivyo nilikuwa
nakusanya watoto wa majirani nashinda nao kila wikiendi n.k kwa sasa sijui
nimeathirika kisaikolojia sitaki tena hata kuona mtoto wa mtu mbele ya macho
yangu kiufupi nawachukia. Muda wote nipo ndani peke yangu ata nikiwa ofisini ni
peke yangu siwezi kukaa dk tano bila kutoa machozi. Imefika wakati hata rafiki
zangu nikiwa nao wanaongelea stori za watoto wao n.k. ninapochangia nitaambiwa
subiri kwanza uzae wako ili uone uchungu wa mtoto. Ni mtoto wa kwanza katika
familia yetu na nina wadogo wawili wa kike na wa kiume na wote wameshapata
watoto ila mimi sijapata hadi sasa.
Nimekaa hapa na mawazo tele ambapo naona
hayana majibu nikajipangia mwenyewe hadi tarehe 28/2/2014 kama nitaendelea kuwa
hivi na gharama zote hizi za matibabu zilizotumia mpaka nimebaki na - kwenye
akaunti yangu pasipo mafanikio basi nijiuwe tu ili nimalize stori za utasa
zinazonizunguka. Na pia nimewaza wachungaji wote hawa walioniombe pamoja na
Mchungaji wangu kiongozi ambaye yupo bega kwa bega na mimi kwa ushauri na maombi
sifanikiwi Je ni kosa gani kubwa ambalo nilimkosea Mungu mpaka akaweka alama
katika maisha yangu isiyopungua wala kufutika.
Siku
moja mwenyewe umetoa ushuhuda wa maombi ya kujiambatanisha basi siku hizi kila
ninapokaa na mjamzito au ninapohudhuria hospitali kwa ajili ya ushauri wa
kidaktari najiambatanisha na wanawake wajawazito mpaka najiona chizi saa
nyingine. Ila nikiwa peke yangu ndio najikumbushia ahadi yangu ya kujiuwa
ifikapo tarehe hiyo 28/2 nimekaa nalo mpaka naona tarehe hizo zinafika naombeni
mnishauri wapendwa je hayo ndiyo yale majaribu tunayoyasoma kama ya Ayubu au ni
kitu gani ninachokutana nacho katika maisha yangu.
Asante
na Mungu akubariki
Miaka 30 mbona bado sana kwa Ahadi ya Mungu Mpendwa ? Watu wanazaa mpaka miaka 40, Mama yangu wa Kambo aliyenilea alikaa kwenye Ndoa yake kwa Miaka 15 akaja kupata mtoto akiwa na Miaka 38, 40 , 44, na yeye alikuwa anatulea sisi watoto aliyotukuta tulikuwa watatu ...Sidhani sana kama Unapaswa ujisononeshe na kumkufuru Muumba wako kisa Kachelewa kukupa Mtoto ! Maisha ni zaidi ya kuwa na Mtoto Duniani, Hebu watumikie wale wanaokutegemea , hata kama Mumeo hataki uchukue mtoto nenda katoe misaada kimya kimya ,,,, siku yako inakuja ,acha kabisa kukufuru adhabu yake itakuwa Kali zaidi, acha waliojaaliwa watoto wakubeze wewe wasamehe bure, kwa maana hawajui walitendalo
ReplyDeleteWatoto ni zawadi Mungu anakupa na Mungu anaweza kuchukua muda wowote anaotaka yeye , Jiulize wangapi wanazaa watoto wamekufa hata mara nne , wangapi wanalea watoto wao kwa shidaaa then wanakufa wakiwa ndio kwanza wameanza kutembea , Sisi wote ni wa Mungu , anasababu yake ya kuchelewesha uzazi kwako , Tulia , Endelea Kuomba, acha Mawazo hata kama KiBinaadamu unatamani , Tafadhali
Mungu anakupenda Kukuweka hai Mpaka Unafika miaka 30, wangapi uwajuao wameondoka ?
miaka 30 mbona bado sana? hiyo stress uliyokuwa nayo ndio inazidisha wewe kuchelewa kupata mimba,ondoa stress Kabisa pia kumbuka hakuna situation ambayo hipo permanent, namie nimego through same situation kwasasa nakaribia kujifungua.
ReplyDeleteDahh hata sijui niseme nini dada. Sijaolewa wala sina mtoto lakini naweza kkushauri kitu
ReplyDelete1. Mungu anasema akili yako inapofika mwisho, hapo ndipo yeye huanzia. Ingia kwenye toba na tubu kuhusiana na jinsi ulivyojiwekea kwamba mwisho wako wa kuishi ni tarehe 28.2 kwa sababu mipango ya mwanadamu si mipango ya Mungu. Ikiwezakana funga kwa kutubu hata kwa siku moja.
2. Yer.29:11 "Maana naya jua mawazo niliyowawazia ninyi, asema Bwana ni mawazo ya amani wala si ya mabaya", kwahiyo defenitely Mungu hajawai kukuwazia mabaya au kukufanya upitie hayo uliyoyapitia sasa. Ebu fikiria katika wakati wote wa ndoa yako na mpaka sasa ni mangapi ambayo umeyapitia na kusema isingekua kwa neema ya Mungu tu usingefika hapo.
3. Achana na kuumizwa na wanadamu kwa maneno wanayosema au fanya, you are God's child,you deserve to be happy na kubwa kuliko yote muombe Mungu akuonyeshe kusudi lake katika ndoa yako,kazi na maisha yako kwa ujumla. Wanaokudharau siku moja Mungu ataificha aibu yako na watakuheshimu na kumwabudu Mungu huyo alieonekana kwako.
4.Weka agano na Mungu. Kwa jinsi hiyo ya kukata tamaa baada ya toba na kutubu kwa maombi na kufunga, Mungu huwa anajibu kwa haraka ambapo unaweka agano na yeye. Ebu fikiria unahitaji watoto, je hao watoto Mungu atanufaikaje kwenye utukufu wake na watoto hao? Jaribu kufikiria na ukipata jibu weka agano na yeye. NB. Hakikisha hautasahau agano hilo kuanzia unapata ujauzito mpaka mtoto atakapokuwa,maana Mungu akijibu wanadamu huwa tunasahau sana so ni vizuri kuandika sehemu ambayo hutakaa husahau.
Mwisho ya yote mama jipe moyo, Mungu yupo na hakawii wala kuchelewa so usiache kuomba na kumshukuru kila iitwapo leo.
Kwa kweli nashindwa niseme nini, inashangaza, inaumiza lakini kwa nini yupo aliye sirini siyo kwa haoni elewa kuwa Mungu ni Mungu atendae kazi kwa majira na nyakati zake, yamkini ungepata mtoto mapema lingekuwa jaribu. Naomba usijiwazie vibaya wala kujikana mwenye wewe ni kiumbe wa Mungu tena fikiria ulivyo na thamani kubwa sana mbele za Mungu - jamani kweli unatumia nafasi hii mwanangu kutoka kujiua usitamani kitu hicho kabisa ni kibaya kuliko unavyofikiria majuto yake ni makubwa hayana mfano, mbona Mungu hajakuambia ameshindwa hata siku moja ondoa wazo la ubinadamu lina mawazo mabaya sana. Ukweli si rahisi kupata picha halisi la hilo unalopita lakini tunajitahidi kukutazamisha juu ya makosa ya ubinadamu tulio nao, na sitaki niwe kama rafiki za Ayubu waliokwenda kumfariji kumbe walikuwa wanakosea.
ReplyDeleteKifupi ni kwamba hayo mabaya yote unayoyaona hayana mizizi (kwa tafsiri nyingine siyo ya kudumu) hata kama miaka inapita lakini bado hayatadumu vinginevyo leo hii tusinge furahia wokovu kama Yesu angedumu msalabani au kaburini - hayo yatapita na utabaki kusahau lakini usilazimishe vile utakavyo Mungu ni Mungu hupana atakavyo yeye kwa wakati wake.
dah!!pole dada angu ondoa kabisa hilo wazo la kujiua ni dhambi kubwa sana kwa Mungu MWAMINI MUNGU NA MWACHIE YEYE ATATENDA MIUJIZA.Remember
ReplyDeleteNimesoma kwa makini sana maelezo ya huyu dada mwenye matatizo ya kutopata mtoto. Kwanza napenda niungane na wasomaji wengine katika suala la umri. Dada bado uko kijana sana kukata tamaa ya kukosa mtoto.
ReplyDeleteMimi nimeshuhudia kwa macho yangu mama wa miaka 45 akijifungua mtoto wake wa kwanza katika ndoa yake ya pili baada ya miaka kumi na nane ya ndoa ya kwanza kutokufanikiqa kupata mtoto.
Mimi mwenyewe nilikaa kwenye ndoa yangu kwa miaka saba ndipo nilipopata mtoto wa kwanza. Dafa yangu maisha ya ndoa yana mabonde na milima. Jipe moyo utayashinda. Kujiua sio jawabu ya matatizo yanayokukabili. Sijui utakwenda kumjibu nini mungu unayemuamini.
Kwangu mimi naona dada huna tatizo. unasumbuliwa na Psychological problems. hujiamini, hujikubali na wala humpi mungu nafasi ya kufanya miujiza ndio maana unataka kujiua.
Lkn tatizo lingine hapa naliona liko upande qa mume. Ni ushirikiano kiasi gani anautoa kwa Mkewe katika kipindi hiki kigumu kinachowakabili? kuwa na watoto nje si kusema kuwa hao watoto ni wako kibailojia. Wanawake ni wajanja sana. Mtoto wa Issa anapewa Musa. Kinachoangaliwa ni maslahi na jinsi mwanaume unavyopenda watoto.
Dada nafasi bado unayo tena kubwa tu. Endelea kumuomba mungu huku ukijitahidi kutuliza akili yako hasa unapokuwa kwenye harakati za kumtafuta mtoto.
Mungu akupe watoto wema. Aaamiin.
dada acha kujivuruga,kwanza umri wako bado mdogo kabisa.najua inauma sana kutopata motto,ila muamini mungu usikate tama kwa sababu umri wako bado kabisa.nina marafiki zangu 3 wote hawana watoto.mmoja ana miaka 42 huyo Amelia ameomba amekuwa hana furaha ila nazidi kumpa moyo.mume wake alishazaa watoto 2 kabla ya yeye.na mwengine mpaka ivf ameenda hajapata mimba na ana miaka 35.huyu mume wake ana msapoti sana,alipata mara moja uja uzito ulipofika miezi 4 ukatoka.na kuna mwengine yeyey ana 41 mpaka leo hajapata.ushauri wangu hili ni janga la wengi usikate tama kabisa kama una uwezo jaribuni ivf.ila hili suala mume anatakiwa awe supportive aelewe maumivu yako.otherwise utazidi kuumia
ReplyDeleteMama Wawili, kwa kweli upo kwa ajili ya watu ili uwatoe mahali na kuwapeleka mahali kupitia huduma hii yawezekana waweza ona ni kitu kidogo sana lakini unachokifanya ni kikubwa kuliko umri uliona. Mama wawili utumishi si kusimama madhabahuni tu ziko njia nyingi sana ambazo hupangwa na Mungu kwa mtu husika moja wapo ni hii unayotumiwa wewe sikupi hongera ninachoweza kusema endelea kunyenyekea zaidi Mungu atakutumia kwa makubwa zaidi tena sana.
ReplyDeleteSiku haipiti bila kuchungulia humu nione Mama Wawili unaniongezea nini cha kukifanyia kazi. Umekuwa msaada mkubwa sana kwangu ukweli namshukuru sana Mungu Aliye Juu Sana ajuaye nani yupo kwa ajili ya nani au afanye nini ili Mungu YEHOVA ajitwalie utukufu - endelea usichoke na kazi uliyopewa unatusaidia wengi hasa mimi.
Siku njema!
Miaka sita unalalamika na kutaka kujiaua??acha kumkufuru Mungu;unasemaje umeokoka ilhali IMANI yako juu ya Uweza wa MUNgu haipo??na hilo ndo tatzo..Inua kiwango chako cha imani ;kuna watu wana zaidi ya miaka 15;my sisterz matron wake aliolewa 1998 hadi leo hana mtoto;my friends wawil wameolewa 2007;mmoja 2008 hadi leo hawana watoto but hawalalamiki ndo kwanza wako strong na MUngu ..ushaur wangu ni inua kiwango chako cha Imani ;pia uende kwa watumish wenye upako wakiweka mikono tu unapokea;wakati mwingine tunajifunga kwenye makanisa yetu tuuuu;tafuta na uso wa Mungu kwengine..karibu kwenye siku saba za uponyaji kanisa la UKombozi;tegeta skanska kwa Nabii Malisa;yameanza juzi hadi tar 24;karibu uone ukuu wa Mungu kupitia Mtumishi wake Nabii Malisa..Nimeshuhudia kwa macho yangu kijana wa miaka 23 mwenye HIV akitamkiwa uponyaji;na dada amabe alikuja mara ya kwanza akiwa na ripoti zake kuwa yupo HIV positive akawa hana amani;mtumish (bila nhta kuambiwa)akamtakia uponyaji;ilikuwa mwaka jana October..so my dear you r very young kujiua kisa hujapata mtoto...Mungu wetu hachelewi na wala hapangiwi..
ReplyDeleteDear naomba nikutie moyo mimi nina miaka 42 sina mtoto ila bado namtumaini Mungu.
ReplyDeleteNi kweli mara nyingi hujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu
Rohoni mwangu ninaimani juu ya wewe kupata mtoto kwanza u mdogo mnno ilo la tr 28 achana nalo please ucmfurahishe shetani
Usijiue
ReplyDeleteJamani pole usikate miaka 30 bado sana, Mimi nina miaka 32 sijaolewa na sina mtoto,sina mchumba lakini naendelea kumtumainia Mungu atanipa kwa wakati aliopanga.Nakutia moyo mdogo wangu usikate Mungu ni wetu sote. Kuna semina ya Mwakasege inaendelea ungekuja watu wanapokea miujiza yao. Endelea kujiweka karibu na Mungu. Mungu ana kusudi na kila mtu,
ReplyDelete