Pages

Ads 468x60px

Thursday, February 13, 2014

SEMA NENO................



Habari  mama wawil,natumaini mu wazima mpenzi.nimefurahi kushare na sisi wadau wako jinsi Mungu anavyokukutanisha na watu ambao wala kwa akili zako hukutegemea lakini kwa Mungu imekuwa hapo ndio ninaposema akili zetu zikifika mwisho Mungu ndo anaanzia hapohapo,Sasa mama wawil kuna hili  tatizo jingine sijui ni mimi tu mama wawili mwenzio au ni wamama wote bado sijajua.Jinsi ya kupanga burget yani mimi sijielewi kabisa na kwenye hili eneo nahitaji ushauri kwa kweli,yan mimi nikiwa na elfu tano inatosha,elfu kumi inatosha na kuendelea kwangu mimi naona ni tatizo.Kama elfu tano inatosha kwa nini nitumie elfu kumi?hapa naongelea kwa mahitaji ya nyumbani madogomadogo au ni kutokuwa na maarifa?Mda mwingine ndo namkumbuka yule mtumishi wa Mungu aliyeulizwa apewe nini akaomba Hekima,na kweli baada ya kupewa hekima kila kitu kilikuja na aliweza kukimeneji,Mama wawili hekima ni kitu kizuri sana.Hata kwako inakuwa hivyo hivyo au ni kwangu tu?barikiwa mamy.

Kwi! kwi! kwi! mdau hapa kwa kweli hata mimi ni janga kwa jina jingine naitwa vulu vulu, sina uwezo mkubwa wa kipesa ila namshukuru Mungu kwa hichi anachonibariki....... sijui kuihurumia pesa when it comes to myself na familia yangu.  wanaonijua wananielewa hilo,Tena kwenye swala la kula!!!!1 kuna mda huwa hatasijui nimenunua nini na ni sh. ngapi , ninachojua ni jumla ya shopping yangu, kama ni mapungufu basi hilo ni moja ya pungufu langu..........kuna kipindi nikaaza kuigiza kujibana  nataka kujua kwa wiki imeenda sh. ngapi, nimekulaje weee!!! i wasnt happy wandugu nikajikuta sio mimi kabisa........ yaani unakutana na mtu anakwambia kabisa leo kitunguu shop fulani bei  hii,Nyama iko kwenye discount duuu!!  nisikudanaganye huwa  naona wamebarikiwa kwa hilo lakini, mwisho wa siku  wao ni wao na mimi ni mimi. cha msingi  ni kujitambua.
Sisi tuna hiyo acc. ambayo ndo mama vuluvulu najiachiaga na kikiisha ndo najua kujibana mpaka muda wa kujazilizia ufike. then kuna hiyo acc. ndo dont touch lazima kuwe na signature za watu( kwi! kwi! kwi!) kuthibitisha, sasa ngoja kitoke na kwa nini kitoke??na mara nyingi kunakuwa kuna target ya kitu kwa muda wa kutoka  huwa ni muda wa ile Target umefika.

 Labda hii ndo inanisaidia maana sijaona kama mipango inaharibika kwa sababu ya uvulu vulu wangu,  hii ni kibinadamu labda niseme. N a pia  kumkabidhi Mungu kila pesa yako, bila kusahau fungu lake maana ni lazima. hatashindwa kujaza kapu lako (andiko hilo) kile kidogo kikibarikiwa utajikuta kinatumika kwa namna ya ajabu mnoo. unaweza ukajikuta unapokea kiasi fulani na mwenzio  na wewe unamahitaji mengi kuliko ya mwenzio lakini mwisho wa siku wewe umesogea kuliko mwenzio , hii ni siri ya kiimani, ambayo wengi wetu hatujaijua na hata kama tunaijua tunaitafutia namna yakuikimbia ni NEEMA!!!!

SIDHANI KAMA NIMEKUWA MSAADA KWA HILI MY DEAR.
  

6 comments:

  1. praise the Lorn Jesus ! yani kwenye swala la kutunza oesa mimi linanishinda kabisa saa nyingine mpka najiuliza nina nini mbona nakuwa na matumizi mabaya ya pesa hivi naweza nikatoka nikaenda supermarket labda kununua vitu vya kula ndani nitanunua na nikikuta na kitu kingine kama nimekipenda hata kama hakikuwa kwenye hiyo bar get nitanunua tu najitahidi sana kubana matumizi nashindwa. najitahidi sana na ninamwomba sana Mungu hata nikiwa natoa fungu la kumi sala yangu inakuwa ni hiyo Yesu aniponye hili eneo kwa kweli.

    ReplyDelete
  2. nakumbuka mtumishi mmoja alikuwa anatoa ushuhuda hapo mwanzo alikuwa anahesabu vichwa vya dagaa yaani, hatupi ni mlo uliokamilika na watoto lakini Mungu amemuinua sasa hata huwa akumbuki lini alikula dagaa, mavyakula yamejaa kwenye friji anafanya kuchagua.......... kupitia hili unaweza ukawa una 10,000 yamatumizi ya kawaida lakini hapo hapo unahitaji la 100,000 , huwezi ukalala njaa eti kwa sababu unataka 100,000 ambayo hata hujui itajijazilizia lini.... kikubwa ni hekima yakujua kama unaenjoy baraka zako au ndo chuma ulete...... utajua tuu kama huna amani na kile unachotumia kinakuhukumu hapo mpendwa kazana maombi kuna kajiroho ndani yake, lakini kama una amani na kila kitu na kukupa furaha na hakuna kinachoharibika kwenye mipango, mpenda we endelea kula bata hizo ndo baraka zenyewe tunasema.

    ReplyDelete
  3. Amen dada. Umeleta mada ya janga la watu wengi kwenye maisha yao(including me).
    Ninawezaje kuwasiliana na wewe kama topic, either ya Tuzungumze au kupata ushauri?

    ReplyDelete

  4. kwa

    kwakweli kwa hili tuko wengi nilidhani ni mimi tu, nimetokea katika maisha magumu sana, lakini sasa namshukuru Mungu napata riziki kidogo inasaidia siyo sawa na zamani maisha niyopitia shida moja kubwa ni hiyo ya barget siwesi kabisa kubarget nika mwenzangu aliyechangia hapo juu hata nikienda shopping nikiona kitu kinanipendeza lazima ninunue nina matumizi mabaya sana nainavyotumia wala roho haimi utafikiri hela nimeokota kumbe naitolea jasho yaani kujinyima siwezi sijui ndio wanaitaga roho tajiri jamani hii mada imenitouch sana



    ReplyDelete
  5. Hehee mama watatu hili ndo gonjwa langu sugu. Yaani niko mbaya upande huu hadi aibu. Marafiki zangu huwa wananishangaa ila ndo nilishachemka hapa. Leteni ma ushauri wadau naimani kuna watakao pona.

    ReplyDelete