Pages

Ads 468x60px

Wednesday, April 25, 2012

TULIWAKUMBUKA KIHIVI




Haya wadau hivi ndivyo mimi na familia yangu tulivyoamua kusherekea birthday ya mtoto wangu Cristabell baada ya kuona tuonanne kwenye topic ya mtazamo juu ya hili ujue kwa nini niliamua hili na nimejifunza nini juu ya hili....................................Picha na maandishi nimecopy na kupast kutoka kwenye blog ya mlezi wa kituo Miriam kuona zaidi ingia gurdianangel blog.

THANKS A LOT!

Tunashukuru sana familia ya Mr & Mrs Mbeyela kwa upendo wa hali ya juu mliouonyesha kwa watoto wetu wa kituo cha Guardian Angels kwa kutuletea zawadi mbalimbali kama magodoro, Simtank, Mkaa, majiko, mchele, unga, sukari , dawa za meno, mafuta, mafuta ya kupaka, majani ya chai, neti mboga, maharage na vitu vingi vingine kama vinavyoonekana kwenye picha.

Zaidi ya yote kwa kuja kusheherekea Birthday ya binti yenu Isabela pampja na watoto wetu kwa kweli tumefurahi sana na ni upendo wa hali ya juu mliotuonyesha, kwani mngeweza kufanya sherehe nyumbani kwenu na kufurahia huko lakini mkaona ni vyema kula na watoto hawa ambao wengine walibaki wanashangaa tuuu maana hawayajui mambho hayooo! Na kesi mmetuachia kila mtoto anataka kufanyiwa Birthday !

Mungu awabariki sana pale mlipotoa awaongezee mara dufu na karibuni sana kututembelea hata kama hamna cha kutuletea watoto wamewapenda sana!

Thanks Once Again & Be Blessed!
















KWA PAMOJA TUNAMSHUKURU SANA MUNGU KWA NEEMA HII HATA YAKUWAKUMBUKA HAWA WAPENDWA WETU KWA KWELI BINAFSI NILISIKIA AMANI YA ROHO MARA BAADA YA HILI TENDO KUISHA JINA LA BWANA LIBARIKIWE 

No comments:

Post a Comment