Pages

Ads 468x60px

Saturday, December 14, 2013

HAYA WAKE WEMA MPOO??????

PLEASE PLEASE TUSIPITE KIMYA KIMYA....... HATA WAUME WEMA MNAOPITA HUMU MTUSAIDIE, HUYU NI MKE FANYA KAMA NI WAKO,  UBAVU WAKO UNATARAJIA NINI AFANYE ILI NDOA ZETU ZIWE KATIKA KUSUDI LA MUNGU????  BABA WATOTO UKINISOMA PLEASE SEMA NENO NA MIMI NIPONE............WAPI WATUMISHI WA MUNGU TUMEAMBIWA MWANAMKE MPUMBAVU HUBOMOA NYUMBA KWA MIKONO YAKE MWENYEWE LAKINI HATA NYIE MMEAMBIWE MUISHI KWA AKILI NA WAKE ZETU..................... Tufunguke wandugu lugha za hekima zitumike hata mtoto mdogo akisoma  ajifunze hekima ya ndoa .........yangu ntafunguka mwisho baada ya wadau. MBARIKIWE

Rose dada yangu,

sijui nianzie wapi lakini huwa napita bloguni kwako nikaona umesema kama tuna issue tuitupie wadau wasaidie.Naomba na wewe mwenyewe pia unijibu.

Mimi nina shida jamani mwenzenu, wanawake wacha Mungu nisaidieni mnakuwaje wake wema kwa waume zenu?Ndoa yangu inakaribia five years imebarikiwa watoto.Mume wangu ni mtu mzuri sana.Tatizo tunapogombana ananiambia mimi nina kiburi am too proud na nina dharau.Eti hakuna mwanaume anayeweza vumilia dharau zangu.

 Hayo yote yanaanzia wapi sasa uliza,Kweli tkikorofishana yeye anaamua kunichunia kama vile kunikomesha sijui sasa na mimi huwa siwezi kwenda kuanza kubembeleza.Wandugu yaani siwezi njiona kama najichoresha.Kama juzi na hairstyle nilibadilishawatu wakanisifia sana Mume hakusema hata neon kama hajaniona.Iliniuma sana.basi na mimi huwa nakaa kimya naendelea na maish kama kazini naenda kama mahitaji ya nyumbani yan=mepungua eg nyama maziwa nanunua bila kusema neon. Hapo ndo ntaambiwa najifanya superwoman etc.Yaanimwenzenu sielewi nauo=mia mnoo hata tukiwa tumechuniana nalia mno kimya kimya nikiwa peke yangu.Mbele yake hata machi=ozi hayatoki maana najifeel kujicchoresha.

Jingine ambalo naadmit mimi ni mkali kwa maana y a sauti yangu.Iko juu..kwahiyo huwa naepeuka discussions nae anponikwaza maana ansema namgombeza wakati mm ndivo nilivo.Maongezi yetu inabidi yafanyike usiku wa ma manane maana ni majibizano hasa.

Kwakifupi nifanyeje mwenzenu naaombiwa siko humble am too proud.Wenzangu mnafanyaje jamani. Hapa nilipo  karibu mashtaka yanapelekwa kwa wazazi wangu eti nikakae nyumbni nijifunze kuwa mke.I am so offended mwenzenu..Hata nikinunua vitu tu vya watototo naambiwa najifanya nna hela.Kamamkuna hata wakaka wa imani mnasoma huku hebu nisaidieni .Au sikuumbwa kuwa mke?

Asante
Mke mwema mtarajiwa

17 comments:

  1. Hii imenigusa Mammy maana hata mimi nilishawahi kui~face kwa mume wangu. Ila ninachomshauri kwa experience yangu atulie na kunyamaza kama anavyofanya tena hata hayo majibizano ya usiku wa manane aachane nayo ajifunze kumyamazia mume wake. Nahisi mume wake atakuwa mbabe ndio maumbile yake sasa ni kuishi nae kwa akili tu. Ukimyamazia mwanzoni ataona unamdharau ila baadae atakuelewa tu maana ukiona amezidisha unamwambia ninanyamaza ili kuleta maelewano. Kumbuka naongea kwa experience yangu na ilinisaidia kwa kiasi kikubwa sana. Ila la kukupeleka kwa wazazi it is o.k nionavyo mimi maana wote mtafunguka ya moyoni na ni muda mzuri wa kusema na yako uliyonayo kwa upole ili usije ukaonekana huwa unamfokea mume wako. Kama Unaongea kwa nguvu (Kwa hasira ) ni maumbile yako pia na unaweza kujirekebisha kwa kuongea kwa uangalifu muda wote unapoongea na huyo mume wako. Haya waume zetu wa kibongo bongo mwenzangu wanapenda sana mwanamke anaekuwa chini always hivyo jitahidi yeye aonekane yuko juu hata kama ni wewe unafanya shopping n.k just mshirikishe tu atakuelewa tu na umuombe sana Mungu awapatie amani ya familia. Nawasilisha

    Mdau kutoka Kilimanjaro

    ReplyDelete
  2. Pole zake, huyu dada atakuwa na sauti kali kama yangu yani hata kama sigombi waweza sema nagomba ila kwa mume wangu naiwezea sanaaa soln ni kukaa kimyaaaa nikisema nibishane nae lazima nishinde! Sasa pia huyo mumeo cha kwanza yupo inferior kwako sijui kwa nini lakini nyie mwajuana, kuna wanaume anaoa kwa nyumba yenye status like mtoto wa ....... nk sasa mkifika huko kila usemacho anajua kimetoka kwa sauti ya mamlaka ya ukoo wenu la hashaaaa kaa nae mweleze, kama labda mumeo hana pesa ama kazi kama yako navyo huchangia, au hiyo ya wewe kuona vyakula flani vimeisha umwambie anaona ohhhhh mtoto wa tajiri huyu nk nk so ni wasiwasi wake tu kaoa kusiko, ila pia kama kweli wewe mke una dharau na kuji proud acha mara moja kwenye ndoa hatuendi hivyo, kama pesa kwenu zipo umeolewa iweje? Kwa mume ni kunyenyekea, heshima, utii, adabu na kujitoa kwa moyo.

    ReplyDelete
  3. Mimi ni binti,Sijaolewa illa ndoa ni kujishusha,kukubaliana,kujinyenyekeza,kuchukuliana na kusameheana. Kutoka ndani ya moyo wako.
    Kama una haya hata sauti yako iweje mtaelewana tuu!
    Icho ulichosema chakutokubembeleza icho..hmm ndo kasheshe maana uelewe wanaume ni kama watoto, wengi hata kama amekosea anataka wewe ndo uombe msamaha.. Sasa aunt,kwa muda ule we jifanye mjinga jishushe,weka mambo sawa,ila siku mkiwa mmekaa hata usiku mueleze kwa upole huku unacheka na kumgusagusa kuwa hukupenda,au ukiona utayatibua basi we jishushe af mpotezee mchambe kimoyomoyo hasira zijuishe af ucheke ndo imetoka ipo siku atajiona mjinga!
    Pia uwe unamwa;bia Mungu kuwa hupendi nini na unapenda nini umwombe arekebishe.
    Ukirudishwa kwenu tayari cv yako ishaingia doa mama.

    Nb.. Sijaolewa mie binti tuu.. Ila nmejaliwa upeo wa saikoloji na huwa nasoma sana habari za ndoa na mambo yake. Na kwa uelewa wangu ndo uo

    ReplyDelete
  4. Mimi nadhani mume kuna wakati anaboreka tu, kuna mambo mengi, pengine anapitia wakati mgumu ofisini, lakini sidhani kama hapo ni kuita wazazi mnaweza kukaa wenyewe muende hata out muongee kwa upole umuulize, je anataka hela zako uwe unazibank tu for future use na yeye aprovide ? Yaani akueleze anataka huko ndani mkaeje kimatumizi, mkikubaliana kuwa labda unawalipa mahousegirls, unanunua vyakula, labda analipia magari maintenance na school fees etc
    Kitu kingine je kipato chako ni kikubwa zaidi yake au ni kidogo ? Inabidi uende taratibu ujue anachokitaka haswa kimatumizi ili msikwazane, na wewe hapo hapo ni muda wako, unaweza kumwambia naomba kama umechelewa ninunue kisha unirudishie, yaani if that's what he wants,

    Mimi na mume hatujaandikiana nani anunue nini ila ikitokea niko mjini ananiambia nunua hichi na hichi, ikiwa yeye katoka pia namwambia, ni nyama tu ndio ananunuaga exclusively pamoja na matengenezo ya magari, mengine yote kuanzia ada mpaka housekeeping inategemea who has the money.
    Lakini december wakati wa likizo we take turns to pay for holiday, this year its my turn so I pay for holiday trip...kwakweli kipato tunalingana and we are very open on how we spend our money, wote wawili tunakatwa sawa kwenye account ya watoto

    Muite tu sehemu make mdiscuss kiishe mkishawekeana boundaries, stick to them, don't escalate it to others

    ReplyDelete
  5. Maombi tu yatakusaidia mama. Omba sana, mllie Mungu sana na atakubadilisha.

    Mimi nilikuwa kama wewe. Attitude, pride na mke mwenye maneno makali. Ningegombama ma mume wangu nilikuwa naongea maneno mabaya sana kwake. Matokeo yake ni ndoa ambayo haikuwa na furaha.

    Ila nikamjua Mungu na nikaamua kubadilika. Of cos, haijawa rahisi, lakini kwa uwezo wa Mungu nimeweza. Nina kama mwaka tangu nibadilike, ndoa yetu ni ya amani na upendo. Wala sikumbuki mara ya mwisho tumegombana au mara ya mwisho mimi kulia. Before that nilikuwa nalia karibia kila siku.

    Nimewezaje kubadilika?
    Bibilia na maombi kwanza. Ukisoma Bibilia utajua maana ya mke mwema.
    Pili, niliamua kuwa sitagombana na mume wangu kuhusu vitu vya kijinga. Cos apo ndipo arguments zetu zilikuwa zinaanzia. Yaani nimekuwa pro. Mume wangu akisema shati ni ya black wakati naona kabisa ni ya navy blue, sibishani nae. Ndo namkubalia kabisa, ndio mume wangu ni ya black. Akivaa zake huko afu aone kuwa sio black, akisema sasa mbona ni ya navy blue, nitakubaliana naye vile vile. Unaweza kuniona mjinga but hii approach imetuepusha kutokana na maugomvi ya kijinga sana.
    Tatu, kukaa kimya. Nikiona kama mume anatafuta ugomvi, au kuna kitu tumepishana, sijibizani nae. Nakaa zangu kimya. Of cos sio rahisi, lakini kwa uwezo wa Mungu nimeweza. Nne, mume wangu pia aliamua kubadilika. Sasa hapa ndo maombi yanahusika sana. Cos hauwezi ukamwambia badilika akabadilika, lakini kwa uwezo wa Mungu inawezekana. Mume wangu alipoona navyojitahidi kubadilika niwe mke mwema, alinitoa out, akaniambia na yeye anataka abadilike ili tu enjoy ndoa. Nikasema amen.
    Tano, nimeacha kufuata ushauri wa marafiki. Yaani nikiwa na tatizo kwenye ndoa, nimejua Mungu hujibu maombi, yaani kabisa nimeachana na ushauri wa wanawake wenzangu.
    Sita, kama naweza kunyenyekea mbele ya Mungu, basi naweza kunyenyekea mume wangu.
    Of cos, tumaweza tukakupa ushauri, ila kama haujaamua kubadilika, yote ni bure. Nimeolewa miaka sita, ila sasa ndo tuna enjoy ndoa. Namshukuru Mungu kuwa nimebadilika sana, mume wangu mwenyewe kila siku anasema he loves the new me even more. Namshukuru Mungu pia kutokana na changes nilizofanya, ndoa tamu, mume amepunguza kutoka kwenda out. Anaambiaga marafiki zake na enjoy mke wangu, nyie nendeni.
    Sio kwa uwezo wangu, ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
    Nakutakia kila la heri!

    ReplyDelete
  6. Nimesahau kuongelea mambo ya hela. Wanaume wana mambo yao jamani.
    Mume wangu ana kazi nzuri tu, na mimi namshukuru Mungu biashara inaenda vizuri. Mambo ya shopping ya vitu vya nyumbani wala hanaga shida, mimi ndo huwa nafanya.
    Ila kuna kitu pia nimejifundisha. Naomba nikupe mfano: kuna siku tukapita sehemu kuna nguo kadhaa nilipenda. Mume kasema chukua mke wangu, nitakununulia. Nilikuwa na hela mfukoni, ningeweza kujilipia, but wala hata sikutaja nina hela. Nilisema asante mume wangu na mabusu juu.
    Au tukiwa nyumbani, kama taa imeungua inahitaji kubadilishwa. Of cos naweza kubadilisha, but huwa nasubiri hadi mume arudi home namwambia nisaidie kubadilisha taa mume wangu. Men love to be needed. Let him be a man. Let him be your man. Fine, unaweza ukafanya hiki au kile, but involve him. Unataka twende wote kwenye shopping ya watoto mume wangu? Anaweza akasema hapana sitaweza lakini shika hela ukanunua wanachotaka. Au akasema ndio. Problem is, kama hayuko interested at all. And if so, basi unaweza kwenda zako na kufanya shopping. Akikuita superwoman, remind him that you tried to involve him first.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dada umeongea vizuri sana..mi cjaolewa na by nature ni mbishi na kiukwel nasoma sana vitabu so nauelewa mkubwa kuliko mpenz wangu...kuna wakati nikiwa mimi yani uwa namuona anakuwa mdogo sana..kuna shoga angu akanipa kitabu cha fascinating womanhood..yani nilijifunza mambo mengi sana wanaume wanapenda kuhitajiwa.yani umuone na kumuonesha unautambua na unajua kwamba yeye ndo mwenye nyumba au yupo responsible kwako..wanapenda kudekewa bt usimpelekeshe..tangu nimeanza kuprictise nliyosoma kwenye hiki kitabu yani naona mabadiliko makubwa sana kwenye mahusiano yangu..yani atakama unaela yakujihudumia smtmz muombe tu kimapenzi akatae yeye..kama ni msomaji wa vitabu jaribu kutafuta icho kitabu usome

      Delete
  7. Mmmmmmh tena ukiwa mtoto wa wenyewe bora uoane na family friend ukija kujipatia mume uswaz kwetu utajuta mana kila utakachofanya mume atawaza nyumban kwenu tu

    ReplyDelete
  8. Mmmh mume wa huyu dada anapenda mke asiye independent halaf kaoa independent ndio maana ila mi sioni kosa la huyu dada hata kidogo ukikosana na mwanaume mnabishana then maisha yanaenda sasa huyu anaetaka mwenzie awe chini km si kutaka kuabudiwa n nn!?

    ReplyDelete
  9. kwa mtizamo wangu huyo mume insecurity issues!! nakuna sababu nyingi sana ambazo zina mfanya awe hivyo, turidi kwenye maandiko mwanzo 2:15&18 hiyo mistari miwili ina state role ya mwanaume ni nini na role ya mwanamke ni nini!! acha ni fafanue zaidi ili twende sawa!! mandiko yametufundisha kua mume,ni provider, protector &leader wakati mke ni msaidizi!! na hata leo tuona jamii nyingi inakuza wanaume kwa mtizamo huo!! sasa basi inapofikia anaona ananyang 'anywa asili yake hiyo "ego " (sijui kiswahili chake) inajeruhika sasa basi anairudisha vipi his ego kwanza kwa kua mkali, pili hasiikilizi tatu anajitakasa nafsi yake kwa kuwapa wengine makosa!! wajibu wa mke hali hiyo ikitokea ni kua mvumilivu,na kutumia hekima mf. mkiwa mnafanya argument na wote mkaghafirika hata kama wewe mwanamke uko sawa, ukimyamazia hautasaidia chochote bali utaongeza majeraha badala yake hebu mwambie mf . "naona wote tume ghafirika na hatuwezi kujadili hili swala kwa hekima hebu tutulie tulitafakari tutalijadili kila mtu akiwa mwenye utulivu " huo ni mfano tu!! au unaweza kukubaliana na anacho kisema afu ukaingia kwenye maombi mungu wetu hashindwi jambo kama swala sio sahihi hakika hatalipa kibali he he he he he! (msinipige mawe hapo) ila ndo ukweli wenyewe huo! .....turudi kwa mdau mleta mada!! kuhusu lile swala la kufanya jambo unapoona upungufu, mfano unapoona chakula ndani kimeisha badala ya kununua hebu jadiliana nae kupata opinion yake,akitoa go ahead ndo uendelee na jukumu hilo!! kwa namna hiyo ataona una muheshimu!! huo ndo mtizamo wangu bandugu!!

    ReplyDelete
  10. (Mume wangu akisema shati ni ya black wakati naona kabisa ni ya navy blue, sibishani nae. Ndo namkubalia kabisa, ndio mume wangu ni ya black. Akivaa zake huko afu aone kuwa sio black, akisema sasa mbona ni ya navy blue, nitakubaliana naye vile vile. Unaweza kuniona mjinga but hii approach imetuepusha kutokana na maugomvi ya kijinga sana). Hii nimeipenda bure. Hawa wanaume wetu jamani kumbe ndio wanataka hivyo.... mmmh too much inahitaji uvumilivu. Nilihudhuria kitchen party moja hivi karibuni tukawa tunafundishwa kung'ata ulimi yaani maana yake ni kunyamaza tu mwanamke kuepusha majibizano kwa waume zetu. Inasaidia sana hata siku moja mume wako akija anahasira zake na kugomba ukimnyamazia tu ugomvi hauwezi kuwa mkubwa kama utakavyoamua kujibizana nae. Hata wale wanamama wanaopigwa ndani ya ndoa zao huwa mara nyingi chanzo ni yeye kujibizana na mume wake. USHAURI: Unamnyamazia wakati anahasira au anakugombeza kwa wakati huo ila usinyamaze daima unamtafutia muda au siku ana furaha unamuelewesha na kumuelezea jinsi ulivyoumia wakati anakugombeza au hasira zake zilikuumiza lazima atakuomba msamaha ila ni kujitahidi kujua tu jinsi ya kuwasilisha suala hilo kwake ili usije ukamtibua tena.


    ReplyDelete
  11. Pole sana dada. Mimi niko kwenye ndoa miaka 5 na nusu sasa. Kwa kweli na mshukuru Mungu sijawahi juta kuwa kwenye ndoa hii. Ni kwa neena na rehema zake. Katika kipindi hicho kutofautia kupo kama binadamu wa kawaida. Cha kuzingatia ni kusoma sana neno la Mungu na kulifanya ndiyo dira ya maisha (standard of your life). Kabla ya kufanya chochote jiulize neno la Mungu linasemaje katika hicho unachotaka kufanya ndipo uchukue hatua. Mfano kumnyamazia siyo suluhisho ndo kuchochea ugovi na shetani anafurahia hapo. Tulia kidogo ongea na mwenzako myamalize. Neno linasema kusikuchwe ungslipo na hasira. Kama inatojea imeshindikanika ongea na Mungu wako yaani Mungu aliye hai, Mungu anayesikia na kusema. Mwambie ukiamini na kutokuwa na shaka hata kidogo utapo jawabu la maombi yako. Wazazi, ndugu na marafiki si wakupelekewa tofauti zetu. YESU alikuja kwa ajii ya mizigo yeto kwa hiyo tumtwike yeye. Naye anafanya. Mimi huwa nafanya hivyo na nimeona matokeo yake. Baada ya maombi anakuja kukubaliana na mimi na nikamwambia nilichofanya na sasa anafahamu huwa naenda wapi tukishindwa kukubaliana jambo.
    Pia kumbuka kushuka kubali kuwa mjinga ili werevu wako ukaonekane. Kuwa mpole hata kama yeye ndo kakosea. Mimi nami nasauti kali nakuws jama nagombeza ninapokuwa natoa msisitizo wa jambo. Amekuwa akiniambia na nimjifunza kuwa makini nalo na nimemwomba Mungu anisaidie katika hilo. Na tumekubaliana pia kuniambia kama sauti itapanda na imetusaidia sana. Vyote hivyo si rahisi ila kwa msaada waYesu yote yanawezekana kwake yeye aaminie. Soma zab 32.8 ubarikiwe

    ReplyDelete
  12. sifa 20 za mwanamke mwema hupatikana katika kitabu cha Methali 31:10------ mke mwema ni nani awezae kumwona ? maana kima chake chapita marijani.(1) chunga sana kinywa chako wakati ukiongea na mwenzako, maneno mazuri nyama ya ulimi kaktika ndoa ndio kitu kikubwa sana .moyo wa mumewe humwamini(2) uaminifu siyo tu wa kutoka njee ya ndoa hata kwenye mambo mengine ya fedha mfano na kuwa mkweli kwa mwenzako.humtendea mema wala si mabaya ssiku zote za maisha yake(3) kuna wanawake wengine muda wote wanawaza mabaya kwa weume zao kutwa kucha kupenda ugomvi kuwaona waume zao hawana furaha wao ndio furaha yao.hutafuta sufu na kitani hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.anafanna na merkebu za biashara huleta chakula chake toka mbali .............................................. naomba nisiwamalizie zama humo kwa biblia yako utazikuta zote sifa z a mwanamke aliye mwema nimejribu kuelezea kwa uchache msichoke kusoma wapendwa wangu nawapenda sana na wengine mzidi kutujuza .

    ReplyDelete
  13. Dahh hii story mama wawili naona kama umenisema na mimi vile.
    Mimi sijaolewa na sababu inayonifanya niwe hivyo ni kwamba huwa they tell me am bossy, nina sauti ya ukali, i look serious, proud and i have an ego. sijui kama ni kweli maana they are the ones who see it, lakini pia naogopa kuingia kwenye mahusiano kwa sababu naona kama nitamuumiza au kujiumiza mwenyewe maana nina hicho kitu cha kukaa kimya mtu akinikosea wanasema ninadharau. Naomba Mungu sana anitengenezee njia ya kuwa mke mwema.
    Asanteni wadau pia kwa mawazo yenu,mnatusaidia sana

    ReplyDelete
  14. AnonymousDecember 15, 2013 at 4:50 PM umenikosha,yaani umebarikiwa na ni ushauri mzuri kwa mtoa mada. Ubarikiwe zaidi na zaidi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amina! Ubarikiwe na wewe pia.
      Ndoa nyingi hazina furaha siku hizi cos tunataka tuwe level moja na waume zetu. Haiwezekani. Na ikiwezekana, hapakaliki. Even the Bible instructs wives to be submissive to their husbands. Wanawake tumeumbwa na pride, lakini tunaweza kunyenyekea.
      Nawatakieni ndoa zenye upendo na baraka!!
      Mungu atuwezeshe kuwa wake wema!

      Delete
  15. Mara nyingine omba msamaha hata kama unajua hauna kosa kufanya yeye alidhike na mambo yaende sawa kwa wakati huo...tafuta siku nyingine mkiwa hakuna ugomvi,mwambie unavyojisikia...mimi naona bora ulie mbele yake ajue unajiskiaje. Halafu apply hii mimi imenisaidia"kama huwezi kumwambia face to face kwamba kununiana kunakuumiza, send him a text msg ukiwa job,mwambie kila kitu unavyojisikia na ungependa hiyo hali iishe,huwezi amini mimi huwa namtumia msg na inawork maana kama atakuwa positive mtachat for a while na mtaend na romantic msgs na jioni kila mtua atakuwa na ham ya kuonana na mwenzie..ha aha mimi hufanya hayo yote na imenisaidia sana..hatugombani mara kwa mara na no mnuno wa mda mrefu and my hubby is very short tempered hata ndugu zake wanamjua lakini wanashangaa kuona silalamiki coz nishamjulia. And u know what huwa anawaamba ndugu zake "hakikisheni mnapatana na mke wangu maana mkishindwana na huyo mimi hutaweza kumaliza masaa 2 tumeshakosana,maana ni MVUMILIVU sana" nina miaka 5 kwenye ndoa na ninaona kama miezi miwili#teamhappymarriage#

    ReplyDelete