Pages

Ads 468x60px

Monday, December 30, 2013

HAPPY BIRTHDAY TO MY GORGEOUS FRIEND

GHANIA
you are the most charming,funny,attractive and rocking personality in town....... miss you and have a great day.


TUJITATHIMINI

Haya wandugu  mwaka huoooo tunauaga kama kawaida yetu tujitathimini  nakumrudishia Mungu utukufu kwa kuwa bado ni mwema kwetu ....... haijalishi mwaka ulikuwaje ile tu kuwa mmoja wa kumaliza mwaka ni neema........

 haya tutiririke inbox (slayros@yahoo.com)


1. NINI UMEJIFUNZA NA UNAUSHUDA WA KWELI MBELE ZA MUNGU KUPITIA BEYOU BLOG

2. NINI UNGEPENDA KIWEPO LABDA KILIKUWEPO  AU KIONGEZEKE

3. NINI KAULI YAKO(MOTTO) KWA MWAKA 2014 HASA UKILINGANISHA NA SOMO ULILOPATA 2013

4.MAMA WAWILI ANAJITAMBUA ILA HAJIELEWI WEWE KAMA MDAU UNAMCHUKULIAJE   TUMIA NAFASI KUMWAMBIA UKWELI BILA WOGA IKIWEZEKANA MKOSOE KWA MTAZAMO WAKO.

5. TOA USHAURI NA MAONO YAKO KWA AJILI YA BLOG YETU 2014


ZAWADI YETU KAMA (MBEGU) ITATOLEWA KWA MSHINDI HAIJAJULIKANA BADO ILA ATAPEWA KULINGANA  NA UHITAJI

MWISHO WAKUPOKEA IJUMAA TAR 3 2014.

 MBARIKIWE

Thursday, December 26, 2013

THE LOOK

Wandugu kwa wale mlio bahati kumuona yule mrembo aliyebebeshwa ( wanasema punda) mimi mwenzenu nimejikuta nalia aisee mpaka nashindwa kulileta humu ndani kama topic. sasa??? hivi  urembo wote ule amekubali kuwa punda!!!!! anavyojua kujitupia sasa  hata mama wawili huwa ananifanya kumchungulia mara kwa mara ......kinachonisikitisha ni watu wangapi kwa kumuangalia wamelazimika kuwa kama yeye  na kutafuta mteremko na mwisho wa siku ndio huyo tumemuona halafu alivyopendeza sasa  na pingu yake plus gwanda la yellow duuu!!!

huwa nafikiri kwa mtu kama yeye (mrembo) $100,000 kwake ni hela ndogo, tuu sasa kumbe hapo  ni mtaji wa boss  ye atapata mshahara baada ya boss kujua faida yake aiseee!!!  naelewa kwa nini lugha zake zote zilikuwa ni mabrand karibu kila week... jamani anauchungu gani  na hiyo pesa wakati yeye anachojua kunyweshwa, kupandishwa ndege na kuingia chooni kuzitoa??? na mwisho kuteketeza maisha ya watu???? inauma aisee sana.....ukiona mtu anamfurahia mtu wa dizaini hii mmmh!!!   acha niendelee kupigika juani na hii summer inanipigaje maana kazi yangu ni 10hrs napigika hapo hapo ntakachokipa kilipe tax, super,insurence,wages yaani we acha tu mpaka nikaje kuongea lugha za brand mpaka kiwe kimeeleweka mno tena kwa mawazo, sema tuu unakuwa umekipenda unataka kujipongeza na wewe lakini ukiifikiria hiyo hela unapata na mawazo maana huko nyumbani bongo sasa!!!! lakini bado najivunia aisee ni changu,na hakimuathiri mtu zaidi yakumfaidisha, hakuna kitu ninachojivunia kama kuokoa ajira za watu wakiwemo wazawa na wasio hasa kuokoa ajira ya watanzania washio huku yaani kwa hili huwa najiona mwepesi mnoooo kwanza naringa.

leo nimekubaliana na mdau wangu kweli usililie.................... atamalizia mwenyewe
nimeanza kuyachukia mapicha gafla 

Muwe na weekend njema

Wednesday, December 25, 2013

NIMEMUELEWA MNOO


hebu tusikilize kwanza kwa wale ambao hamjabahatika  kuiona hii video halafu  nisome chini mpendwa...........






Wandugu bila shaka sikuu ziliende vizuri na kama sivyo amini kuna kusudi jema lililo mbele yako........Mungu hawezi akakuacha na wala hajakusahau hiyo ni safari unayotakiwa kuipitia ili muujiza wako ukamilike. Namuelewa mnoo Charles anaposema akili imefika mwisho aisee................ lakini ninavyoamini mimi kipindi kama hicho kama bado tutang'ang'ania  kweli mpaka ushindi upatikane wewe umepanda kiwango cha imani, na kwa uelewa wangu huu mdogo kiwango cha imani kinapimwa kutokana na lile jaribu unalopitia na ukiona wewe kila kitu mteremko mmmh!! labda inawezekana!!!! lakini, tunaomba maombi yako mwenzetu maana hichi kipindi cha kufika mwisho wa akili ni noumaa........... wala usikitamani kikupate kuna watu mnanielewa hapa ........kikubwa ni ule ushindi wake   ambao ni lazima upatikane no matter what!!!!!!

Naomba nikutie moyo tuu, binafsi nimejitambua asilimia 30% ya mimi is very tough, sijui niisemaje  kwa kiswahili fasaha na 70% yangu ni very very soft aisee mpaka kuna mda najichukia............... hii nafasi inaambatana na machozi ambayo wakati mwingine yanakosa mfutaji zaidi ya Mungu pekee, yale maneno ya huruma na kunitia moyo siyapati maana nimechoka na huruma za wanadamu hivyo mara nyingi chozi langu anayeliona ni Mungu tuu,  nimwepesi sana wakufuta chozi langu  hata wakuja kwa kunyata ntamsikia nakufuta chozi langu  haraka ili asibahatike kuliona wanasema nakufa kisabuni mwee!!!  yaani hichi kipindi maumivu yake niliyonayo sidhani hata kama dawa zakutuliza maumivu huwa sinafaa aisee, huwezi kunielewa ila usiombe mpendwa we endelea kusimuliwa kama tunavyosoma habari ya Tajiri na maskini  kama mwanadamu ukisoma mwili huwa unasisimka imagine jiweke mwenyewe kwenye hiyo nafasi..... .......nnachomshukuru Mungu baada yakujua  hiyo 70% ilibidi nifanye maamuzi ya lazima  kutumia hiyo 30% ipasavyo..... nahisi imenisaidia sana imepelekea 90%  ya jamii inajua am a very tough person, kitu ambacho kimesaidi shetani anavyokuja lazima aje amekamilika akija kijinga jinga hapewi hata round ya kwanza nimeshamzika....... lakini  ukweli unabaki pale pale asilimia hiyo 70 ni kubwa kuliko nyingine hivyo kunawakati  ni lazima huwa inashinda pamoja na jitihada zangu zoote.................................AKILI YANGU HUWA INAFIKA MWSHO wandugu........ lakini nichoipendea hii asilimia  huwa inanirudisha na kujua mimi ni mwanadam,inanifundisha kuwa mnyenyekevu,inanipa muda wakutafakari na kujua namna ya kuchukulia jambo, inanikumbusha kuwa hakuna aliye mkamilifu, inanifundisha kuishi maisha yakumtegemea Mungu zaidi na kusahau kabisa peke yangu sitoweza bila neema yake, inanifundisha wakati mwingine ni lazima upondeke na ukubali ili kuruhusu mpango ulio sahihi, hapa ndo huwa nakaa hata kwenye choo changu nakujifungia mlango na kumwambia Mungu sasa ushuke tuhojiane imekwaje??? maana sielewi akili yangu imefika mwisho.........(samehe lugha yangu cha msingi unielewe)

Angalizo:  Tafadhali  dont take advantage ya watu wa dizaini hii aiseee........ maana Mungu huwa anaruhusu lakini hawaachi  YUKO UPANDE WAO... ninaujasiri na hili maana nimeona nakushuhudia.

UBARIKIWE SANA H KWAKUNITUMIA HII LINK.... sijui unapitia nini au imekuwaje ukanitumia  MUNGU ajuaye kweli yako akakutetee na kukupigania

Tuesday, December 24, 2013

MERRY CHRISTMAS WADAUZ


Remember the real  meaning of CHRISTMAS.....................A child is born......... our Lord and Saviour JESUS CHRIST 
Ila bongo ndo nawamiss hasa kipindi kama hichi aisee................mimi mwenzenu huku hata makanisa yamefungwa wamesema ni siku yakifamilia zaidi wakati nijuavyo mie kipindi kama hichi kule kwetu hata asiyelijua kanisa anaenda.................

karibuni kula pilau lakini nyumbani kwangu sitakuwepo  kazi kwako kujua nilipo kwi! kwi! kwi!

Sunday, December 22, 2013

NIMEGUSWA

haya ni maneno ya mtumishi Steven Wambura 
nimefanya kucopy na kupaste maana yamenigusa mnoo............  ushuhuda unajenga, ushuhuda unainua, hasa tukiwa tunapata kwa watuNtofauti tofauti na jinsi walivyopitia..................INAWEZEKANA KIKUBWA NI KUKAA KWENYE MSTARI NAKUJITAMBUA

KUNAKOPINDI WAKATI NAPITA MAPITO MAGUMU,, AMBAYO SINTASAHAU,,, WAKATI NATOKA KARIAKOO NA MIGUU NAKUJA MPAKA MAGOMENI NDIPO NAPANDA DALADALA ZA KUJA SINZA MAANA MFUKONI NINA MIAMBILI TU,,, NA KUANZIA MAGOMENI MPAKA MWENGE ,, WAKATI MWINGINE DALADALA HUWA MIA MBILI KABLA NAULI HAZIJA PANDA... WAKATI MWINGINE NILITEMBEA KUTOKA MORROCO HADI SINZA KWA MIGUU NA JUA KALI LIKINIPIGA,,,,, MARAFIKI WENGI WA KARIBU WALINISEMA VIBAYA SANA MANENO YALIYONIFANYA KILA SIKU NILIKUWA NAOMBA MAOMBI YA UCHUNGU SANA NA KULIA TU... KILA MMOJA ALISEMA LAKE,, OOH WAMBURA CHOKA MBAYA,,, WAMBURA KAFULIA,,,, YULE MWIMBAJI KWISHAA,, NIMEMKUTA ANAOMBA NIMNUNULIE CHAKULA.... NA NIKWELI NILIFIKIA HAPO PA WATU KUNISAIDIA ILA BAADHI WALIONISAIDIA WALINISEMA TENA KWA WATU,,,,,, HUWEZI AMINI WAMBURA KANIOMBA BUKU NAULI WANGU,,,,, HAHAAA,, NI KWELI SIKUWA NA UJANJA,, MAPITO YALIKUWA MAKALI MNO,,,,, NA KUMBUKA MUNGU ALIKUWA AMENIAMBIA NIITOE GARI YANGU NIMPE MTUMISHI FLANI NA NILIKUWA NAYO HIYOHIYO NA NILIFANYA HIVYO KWA MACHOZI MENGI NA ILIKUWA NI BENZI.... KUTOKEA HAPO HALI ILIKUWA NGUMU SANA ,,, NIKAWA NIKIMUULIZA MUNGU KWANINI NIKITOA NDIO MAMBO YANAGEUKA KUWA MAGUMU TENA ISAKA WANGU YAANI GARI LANGU MOJA ,, HILOHILO TU NILIKUWA NALO,,,, NIKAWA MTU WA KUPANDA DALADALA NA MWISHOWE NIKAWA MTU HATA WA KUKOSA NAULI NA KUTEMBEA KWA MIGUU NA MWISHOWE NIKAWA NIKIPEWA CHAKULA NA RAFIKI ZANGU KAMA,,, IMASON MWANA ZAMBE NA CHRIS'S MWASOTA WALIOJITAHIDI KUFICHA SIRI ZANGU MNO ZA MAPITO YANGU,,,, HAWA WALIUSIKA SANA KATIKA MAPITO YANGU NA KUNILIPIA NAULI KILA NIKIALIKWA KUIMBA NA HUKO NILIPOALIKWA NILIKUWA SIPEWI CHOCHOTA HIVYO ILIWALAZIMU KUNILIPIA TENA NAULI KURUDI HOME NA KUNINUNULIA CHAKULA........ NDUGUZANGU ILIFIKIA MAHALI NILIONA BORA NIFE,,, NILIKATA TAMAA YA KUISHI MAANA NILIKUWA MWAMINIFU KATIKA ZAKA NA SADAKA NATENA NILIFANYA NA ZAIDI,,, ILA MUNGU HAKUWA KIMYA BALI ALIKUWA AKINIRANDA........ NAWASHUKURU SANA IMASONI, CHRIS'S NA HATA WALE WALIONISAIDIA WAKANISEMA ,, WOTE ILIKUWA NI MPANGO WA MUNGU ILI LEO NIFIKIE MAHALI NACHAGUA GARI LA KUTOKA NALO ,,,,,,, NI NEEMA TU ,,, NEEEMA,, NDUGU.... LAKINI KWA USHUHUDA HUU NATAKA NIKWAMBIE WEWE ULIYEKATA TAMAA,, AU WEWE ULIYEDHARAULIWA AU WEWE UNAEPITIA MAGUMU NA UNAONA AFADHALI UFE,,, NAKUTABIRIA HUTAKUFA NA UTUKUFU WAKO WA MWISHO UTAKUWA MKUU KULIKO WA KWANZA,,, VUMILIA MAANA UMESHAFIKA KWENYE MLANGO WA JARIBU LAKO NA SASA UNAENDA KUTOKA,,,, ILA UWAPENDE WALIOKUSEMA VIBAYA NA USIWE NA KISASI JUU YAO,,, NAKUTIA MOYO SADAKA ZAKO HAZIJAPOTEA ZINASEMA MBELE ZA MUNGU NA SASA NI WAKATI WAKO WAKWENDA KUPOKEA..... MUNGU ANAENDA KUKUINUA MPAKA TUTASHANGAA... WANADAMU TUNAKUONA UMECHOKA ILA MUNGU ANAKUONA UNANGUVU,,,,, WANADAMU TUNAKUONA MASKINI NA UMEFULIA,,, MUNGU ANAKUONA TAJIRI NA UMEKAUKA..... PIGA MOYO KONDE,,, MWAMINI BWANA SAA YAJA NA SASA IMESHAKUWA........ KWA USHUHUDA HUU WA MAISHA YANGU WA KWELI NA KUTIA MOYO SONGA MBELE,,,,, NA USIACHE KUJA KWENYE MAOMBI TAREHE 1 PALE USTAWI WA JAMII TUOMBE ILI KIELEWEKE MWAKA UNAOKUJA.... BARIKIWA





Thursday, December 19, 2013

THEY MADE IT.................

CONGRATULATIONs MR & MRS A. TWALANGETI

GORGEOUS VICK
mmependeza mnooo

shemeji yangu naomba vazi la suti lisiishie hapo Ha! ha! ha!ha


Wednesday, December 18, 2013

MMMMMH!!!

 watumishi mtufungue hapa , Tatizo ni mwili  wake?? au kwa sababu ya nafasi yake anayotumika haipasi kuvaa hivi? haya mfunguke........ 


”Yes, you are a beautiful, curvy woman…but No ma’am 
you are singing the
gospel of Jesus Christ,” wrote pastor Stacey Woods on American
Preacher. We compel men to come through our love for Jesus, but when
we wear things that are distracting, the message is somehow lost and it
becomes about us and not about Him,

 HAPO CHACHA na mama wawili nikakutana na hii comment  kwenye page yangu facebook kwenye picha hii lakini nafikiri mtumishi alifanya utani tuu akihusianisha  na story ya  bidada hapo juu...............
nimeicopy na kupaste
  • "Yaani kwa hapo lazima watakuzuia kuingia kanisani" mwisho wakunukuu
 haya tufunguke wengine tupone mama wawili hapa sifunguki ng"ooo  nakuwamsomaji na kuachilia comment.

tumalizie na wololo 

Tuesday, December 17, 2013

MAMA WAWILI


Ninachoweza kusema namshukuru sana MUNGU kwa ajili yenu wadau wangu..... Humu ndani kuna vichwa vyenye hekima mpaka namshangaa Mungu, mbarikiwe mnooooo..........kwa kweli hasa kwenye ile topic  kwa kweli mpaka nimeshindwa niongeze nini maana kila kitu mmegusa......... mnisamehe kwa wale ambao sijaachilia comment zetu nyingi zenu zilikuwa wazi sana kiasi kwamba kama muhusika anasoma atajua kabisa huyu ni mke wangu kaandika ha!ha!haaa! naogopa kuleta majanga kwenye ndoa za watu........ na nyingine Lugha  iliyotumika  mmmh!!.

kwa zile comment chache bila shaka muhusika umeilewa nini tatizo na wapi pakurekebisha. LANGU LAKUONGEZA  NI HILI

jamani huu utaratibu wakunirudisha kwa wazazi wakanifundishe mie siuelewi kabisa kwanza naona hata aibu..... mwenzeko wazazi mpaka wakanikabidhi kwako inamaana kiwango chao ndo kilipoishia hayo mengine ndio maana tuliapa katika raha na shida.......... sasa mwenzangu situyamalize wenyewe NDOA ni ya kwetu  ngoja basi tuwape na hao wazazi break wandugu...... ndio maana  maandiko yanasema WANAUME KAENI KWA AKILI NA WAKE ZENU, NA WANAWAKE WATIINI WAUME ZENU. kila mtu asimame kwa nafasi yake tukiona ndivyo sivyo ndugu maombi ndo msaada pekee kutufanya tupondeke na kurudi kwenye mstari...........wapi paliposema mrudishe mkeo kwa wazazi????? labda mimi  sielewi!!!  

Haya tumalizie na muonekano

IGNORE HAKO KAMKANDA KEUPE MKONONI MWENZIO HIYO ILIKUWA TICKET YA NILIKOTOKA
HERSELF

Monday, December 16, 2013

NAFUNGUKA!!!!

Wandugu nimepita pita huko vijiweni naona kama tunajazana ujinga kiaina sina uhakika lakini ni maono yangu tuuu................Wanasema mwanamke  kujiamini mwanaume asikubabaishe hata kidogo tena kama unakazi yako na unajeuri yakulea mwanako/wanao  MBONA watatukoma!!!! Binafsi naona huu ni umaskini wa kufikiri uliojawa na ubinafsi............ UPENDO kwetu umeondoka kwa kiburi na jeuri  tumesahau nini maana kamili ya ubavu wa mwenzio ,Tumesahau kiapo tulichoapa  akili zetu zimekaa kuwaza baya litokee all the time na zaidi tunafikiri tunawapenda hawa viumbe wa viuno vyetu asikwambie mtu nenda kamuulize yoyote aliye lelewa na single parent, au muulize mzazi anayelea mtoto bila mzazi mwenzie kama mkweli atakwambia........ wachache sana wanayomudu hayo maisha na mwisho wa siku wanaishia kuwa  wazinzi( nini kwani hao ni wanadam aisee......... na mbaya zaidi walishawahi kuonja asali)  nenda kasome  na kuelewe neno linalotuambia tuwahurumie wajane.......... ndo utaelewa ni maana ya Baba na Mama........ asikudanganye mtu.HOFU YA MUNGU INAPOTEA watu tunafikiri tunaweza kubadilisha uhalisia TUNAJIDANGANYA



Naongea na kina sie ambao mpaka sasa hivi Tunamshukuru Mungu tunazimudu ndoa zetu.....na badala yakuendelea kumuomba Mungu atupe Hekima zaidi kwenye ndoa zetu, tumekaa mkao wakuwaza hayo.... kinachonikasirisha zaidi tunawashauri wenzetu wafanye hayo....... ni kweli wanapitia lakini kuna namna fulani ya hekima inayotupasa kuifanya na sio kumpa jeuri na kiburi kuharibu zaidi............................Pamoja na kuwa ndoa zetu zina amani na upendo lakini bado kuna vi ups and down vingi tuu  ambavyo hatuvileti kwenye mitandao   na unavimudu....... yawezekana huyu mtu alivyolileta kwako ameshindwa kulifikisha sawa sawa na wewe ukalichukulia kubwa kumbe ni zaidi ya lile ulilolizoea......... ni jinsi tu yakulichulia na unavyofikishiwa.

kwa kuongea hivi naelewa kuna watu wanapitia....... ni bora kunyamaza nakumuombea huyo mtu kuliko kushinikiza afanye uhalifu zaidi ya hilo analopitia...... na katu usifananishe ndoa yako na mwenzio. Huyo ni mtu na ubavu wake kama tungekuwa wamoja  basi kusingekuwa  na tofauti kwetu.

MSINIPIGE MAWE HAYO NI MAWAZO YA MAMA WAWILI  NA YALE YALIKUWA YENU  HIVYO NIJUKUMU LA MLENGWA KUELEWA NINI AFANYE.

MUHUBIRI 7

5Afadhali kusikia karipio la mtu mwenye
hekima,
kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu.
6Kama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya
sufuria,
ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu.
Hili nalo pia ni ubatili.
7Dhuluma humfanya mtu mwenye hekima
mpumbavu,
rushwa huuharibu moyo.
8Mwisho wa jambo ni bora kuliko mwanzo
wake,
uvumilivu ni bora kuliko kiburi.
9Usiwe mwepesi kukasirika rohoni mwako,
kwa kuwa hasira hukaa kifuani mwa
wapumbavu.
10Usisema, ‘‘Kwa nini siku za kale zilikuwa bora
kuliko siku hizi?’’
Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama
hayo.

11Hekima, kama ulivyo urithi, ni kitu chema
na huwafaidia wale walionao jua................


kwa pamoja na umoja Mungu anatupa neema yakuwafanya na furaha zaidi kuwafundisha nini maana ya upendo


maombi yangu kwa all single parents MUNGU AWAPE FARAJA YA ROHONI
na huyu ndo Christabell
Anaitwa Careen




Sunday, December 15, 2013

MUONEKANO..........

THE JOY OF THE LORD IS MY STRENGTH................. Hiyo ndio siri kubwa ya mama wawili, si kwa akili zangu wala uweza bali ni kwa ajili ya huyu aliyenifia msalabani............... anipaye amani na furaha, aponyaye majeraha yangu aniketishae na wakuu, aiseee!!!!! ni ninamengi mnoo yakumrudishia Mungu utukufu
 Angalizo: unapoandaa vita na mimi usiangalie hako kamwili aisee....... ki ukweli mi hata kukunja ngumi siwezi kwanza huwa na kimbia nikijua kuna kipondo cha mwili  mbona utanihurumia!!!some of you mnanielewa kwi! kwi! kwi!........ila neno moja tuu nalijua VITA NILIVYONAVYO NI VYA MUNGU........
 BE YOURSELF NDO MPANGO ili upate kutimiza kusudi na mpango wa MUNGU
MBARIKIWE WANDUGU..........TUSISAHAU KUCHANGIA HIYO TOPIC ILIYOPITA WAPENDWA NA ROHO ZETU TUPONE. MI NTAZUNGUMZA YANGU KWENYE TOPIC YATUZUNGUMZE

Saturday, December 14, 2013

HAYA WAKE WEMA MPOO??????

PLEASE PLEASE TUSIPITE KIMYA KIMYA....... HATA WAUME WEMA MNAOPITA HUMU MTUSAIDIE, HUYU NI MKE FANYA KAMA NI WAKO,  UBAVU WAKO UNATARAJIA NINI AFANYE ILI NDOA ZETU ZIWE KATIKA KUSUDI LA MUNGU????  BABA WATOTO UKINISOMA PLEASE SEMA NENO NA MIMI NIPONE............WAPI WATUMISHI WA MUNGU TUMEAMBIWA MWANAMKE MPUMBAVU HUBOMOA NYUMBA KWA MIKONO YAKE MWENYEWE LAKINI HATA NYIE MMEAMBIWE MUISHI KWA AKILI NA WAKE ZETU..................... Tufunguke wandugu lugha za hekima zitumike hata mtoto mdogo akisoma  ajifunze hekima ya ndoa .........yangu ntafunguka mwisho baada ya wadau. MBARIKIWE

Rose dada yangu,

sijui nianzie wapi lakini huwa napita bloguni kwako nikaona umesema kama tuna issue tuitupie wadau wasaidie.Naomba na wewe mwenyewe pia unijibu.

Mimi nina shida jamani mwenzenu, wanawake wacha Mungu nisaidieni mnakuwaje wake wema kwa waume zenu?Ndoa yangu inakaribia five years imebarikiwa watoto.Mume wangu ni mtu mzuri sana.Tatizo tunapogombana ananiambia mimi nina kiburi am too proud na nina dharau.Eti hakuna mwanaume anayeweza vumilia dharau zangu.

 Hayo yote yanaanzia wapi sasa uliza,Kweli tkikorofishana yeye anaamua kunichunia kama vile kunikomesha sijui sasa na mimi huwa siwezi kwenda kuanza kubembeleza.Wandugu yaani siwezi njiona kama najichoresha.Kama juzi na hairstyle nilibadilishawatu wakanisifia sana Mume hakusema hata neon kama hajaniona.Iliniuma sana.basi na mimi huwa nakaa kimya naendelea na maish kama kazini naenda kama mahitaji ya nyumbani yan=mepungua eg nyama maziwa nanunua bila kusema neon. Hapo ndo ntaambiwa najifanya superwoman etc.Yaanimwenzenu sielewi nauo=mia mnoo hata tukiwa tumechuniana nalia mno kimya kimya nikiwa peke yangu.Mbele yake hata machi=ozi hayatoki maana najifeel kujicchoresha.

Jingine ambalo naadmit mimi ni mkali kwa maana y a sauti yangu.Iko juu..kwahiyo huwa naepeuka discussions nae anponikwaza maana ansema namgombeza wakati mm ndivo nilivo.Maongezi yetu inabidi yafanyike usiku wa ma manane maana ni majibizano hasa.

Kwakifupi nifanyeje mwenzenu naaombiwa siko humble am too proud.Wenzangu mnafanyaje jamani. Hapa nilipo  karibu mashtaka yanapelekwa kwa wazazi wangu eti nikakae nyumbni nijifunze kuwa mke.I am so offended mwenzenu..Hata nikinunua vitu tu vya watototo naambiwa najifanya nna hela.Kamamkuna hata wakaka wa imani mnasoma huku hebu nisaidieni .Au sikuumbwa kuwa mke?

Asante
Mke mwema mtarajiwa

Friday, December 13, 2013

BASI SAWA NGOJA TUIMBE..............................


Nimejikuta leo nipo busy na huyu bidada huwa ananifurahisha sana hasa nikiwa najisikia kucheka huku na msifu Bwana.................. anahuduma fulani hivi lazima uwe umekomaa kumuelewa


kama ingekuwa Topic yatuzungumze huu wimbo umejitosheleza wapendwa........  mi napenda kuambiwa kinamna hii bila kuzungusha zungusha ujumbe na maneno yakubembelezwa yasiyonisaidia  maana by the nakuja  kujua maana too late....................
 kweli duniani hakuna wembamba jamani duu


hapa ndo kanimaliza kabisa  mpaka nimejicheka wapendwa hii video ikitoka naomba niione aisee maana siipatii picha...............

 nimemalizia na huyu Mama hapa Mama wakuabudu
muwe na week njema wapendwa

Thursday, December 12, 2013

LABDA HATUKUELEWANA...............


 Wandugu niliposema TUJIFUNZE KUCHUKULIANA nahisi labda sikueleweka vizuri kwa baadhi yetu na mbarikiwe wote tulioenda sawa, baada yakupokea inbox nyingi kuhusiana na topic yetu ya tuzungumze iliyopita kuna kitu nimeona nikazie..........

 Dunia yetu ya sasa  hatujui tunaishi na nani, tunakula na nani, Tunamshukuru huyu Mungu aliyetuachia huyu ROHO MTAKATIFU anayetupa mafunuo ya yanayoendelea na kutupigania tusivyoweza kutambua, japo kuwa, kama tujuavyo  hakuna aliye mkamilifu na kwa sababu hiyo kuna wakati tunamzimisha huyu Roho mtakatifu  na kuwa kimwili zaidi na hapo ndipo adui anapopata nafasi yakuingia................ 

TUNAPOSEMA  TUCHUKULIANE kuna hekima ya ziada inatakiwa itumike usije ukajikuta unachukuliana na pepo.... na kazi ya pepo nikutumika (mawazo yangu). Pepo anaweza kutumika kupitia mpendwa mwenzio, ndugu, rafiki,jirani kama wasemavyo kikulacho ki nguoni mwako............ ukitaka kunielewa zaidi kamsome Abel na Kaini, nenda kakazie kidogo kwenye habari ya Yusufu iliyompelekea kuuzwa, Ili upate nyamanyama zaidi kasome habari ya Daudi na mwanae utanielewa.....................

 Naongea  kwa kutumia kajiuzoefu kadogo, ambako Mungu aliwahi kuniruhusu nipitie, ilinitesa sana, nilijikuta nakosa ujasiri  wa kila japo, naweza kusema sikuwa mimi Muda mwingi nilikuwa fake bora mradi nilihifadhi hili neno TUCHUKULIANE.  hili neno lilinifanya niwe mjinga naweza sema, nilikosa ufahamu na kuna wakati nakumbuka nilifanya maombi special  na kwa sababu ya kutokufahamu nilimpa Mungu mipaka  anijibu vile  nilivyotaka mimi.......... (mtageuka kuume au kushoto, masikio yenu yatasikia sauti nyuma yenu, ikisema, “Hii ndiyo njia, ifuateni.’’) hii sauti niliisikia lakini sikuipa nafasi... nilijisumbukia mno.

nilikumbatia watu ambao naamini  hawakutakiwa kuwa wangu kwa kipindi hicho, nililazimisha mahusiano chakushangasha kila niliposhughulikia hilo ndo niliharibu kabisa....... kuna watu mnanielewa hapa kuna kipindi unakwenda kukutana na watu unajianda hadi maneno utakayozungumza maana unaogopa usije ukajeruhi mioyo ya watu,  na kuharibu mahusiano,lakini bado baada ya siku hiyo kupita utakutana na wale watu ulio thubutu kugandisha akili yako ili kuwafurahisha,we unajichekesha mwenzio  amekununia  amelivuta hilo domo  mbona utajuata!!!!  unajiuliza kulikoni  badae  utaambiwa ulimjeruhi mtu,  utajitahidi kutafuta suluhu wapi itajirudia rudia mwisho yanakuwa km mazoea, Na hivyo wakina sie tunamalizwa na kauli zao zile YULE ANAJIFANYA MLOKOLE MNAFIKI, ANA MAMBO YAKE ANATUMIA KIVULI ( kwi! kwi! kwi!)  leo nacheka lakini kiukweli nilikuwa nalia mnoo  mbaya zaidi unaambiwa na anavyojifanya analia lia atatukoma nyie we acha tuu sehemu zingine ambazo Mungu alikupitisha ukizikumbuka unaweza kujicheka aiseee.........nilipoteza muda mwingi kwa ajili ya hili na hata muda ambao nilikuwa natakiwa kutumia na familia yangu  nilijikuta naingiza hayo ilinipata wakati mgumu mnoo, asikwambie mtu hata amani na familia yangu ilikuwa inakosekana Baba wawili nae alishachoka kunifuta machozi duuu!!!! kweli kale kapepo kalitumika aisee mpaka nilikuwa naona Mungu hana msaada kwa hili...........

Kumbe nilitakiwa niruhusu uweza wa Mungu na mamlaka  zaidi  kuomba bila kumpa mipaka Mungu.  Hadi hapo nilipojikuta nimefanya hilo. ........TUCHUKULIANE kwangu kwa sasa lazima liambatane na amani, furaha, nakutokuwa fake( uhalisia wangu)  naweza kusema hapa ndipo nilipotoka na 
BEYOU.Na hapo ndipo nilipofunguliwa kuna mambo huwa yanafanyika katika ulimwengu fulani ambao wewe hujui na vita vyake si vya kitoto ukikuta watu wamekununia bila sababu ya Msingi  ambayo hata ukijikagua utafute wapi hapakuenda sawa hupaoni ujuwe MOTO unawaka somewhere....... na wala usiulize ulize kwa nini na chanzo chake nini we mshukuru Mungu kwa ushindi maana naamini hajataka kukuonyesha maana huwezi kustahimili ( VITA TULIVYONAVYO NI VYA MUNGU) ila ukitaka kumsaidia mwisho wa siku utapitia niliyopitia mwenzio na usiombe aisee...........

Ni marufuku kuchukuliana na mtu ambaye anataka kuzima ndoto zako, mtu anakwambia haiwezekani  wakati tumeambiwa TUNAYAWEZA YOTE KATIKA YEYE ATUTIAYE NGUVU,mtu aisyeweza hata kukutia moyo,mtu anaependa kukuona huna furaha, mtu anayetaka kila siku ukalie njaa kwake asikupe mbinu yakujisaidia mwenyewe ( hakuna mteremko), mtu ambaye ukiinuliwa kidogo ye kanuna, mtu ambaye  haoni zuri kwako. yaani ye ni hasi mwanzo mwisho kwa ajili ya maisha yako no chanya hata kidogo mmmh! mpendwa hapo stuka  CHUNGUZA SAWASAWA maana na uelewa wako wa neno TUCHUKULIANE...................

Angalizo
nimeongea kama mwanadamu ......Nikikubali japo kuwa na hayo yote bado hata mimi kuna wakati nilikuwa na mapungufu ambayo yawezekana nilizidi kumpa nafasi adui akae sawasawa...... na kwa kuandika hivi sijania kukumbusha au kutibua vidonda vilivyopo au kwa namna moja ama nyingine yawezekana unaenisoma haka kapepo kalikuwa kanashughulika ndani yangu na wewe  Mpendwa take it easy. Tukubali tulitumika ili tuzisaidia roho fulani fulani zilizoandaliwa kupitia mfano wetu...........
nimekutana nayo nimeipenda nimeona niwachafulie ka hali ya hewa kidogo 

MBARIKIWE

Wednesday, December 11, 2013

MAMA NA MWANAE LEO

usinikanyage ................
kitaani
nilivyorudi hiyo rangi ya raba imekuwa sio.........huyu bidada niliyeongozana nae leo bila kunikanyaga siku yake naona isingeenda sawa...............

bidada mwenyewe  huyo!!!  kameniambia mumy those are cool shoes in her voice.......... 

Tuesday, December 10, 2013

KITAANI LEO



mimi mwenyewe

mama wawili

ahsante kwa kunitia moyo maana nilijua nimeharibu mnoo...........

Monday, December 9, 2013

WAWILI TIME


Their moment @ CHURCH......................

kama si neema ya MUNGU!!!!
IN THE POSSIBILITY ROOM
with her friend

the greatest gift parents can give children is to be in the house of GOD.... my opinion
 na kama hunielewi nenda kamsome Ana sio kwamba alitambua tuu kumpata Samweli ni Neema bali alithamini nakuelewa umuhimu mkubwa wa nyumba ya Mungu................ nielewe vizuri haikuwa kumpeleka tuu, kuna nafasi kama Mama aliwajibika  MAOMBI KWA AJILI YA UZAO WA KIUNO CHAKE.
kamekuwa wapendwa

toto za mie

anapenda picha huyu kama mama yake......

Saturday, December 7, 2013

TEAM SHORT HAIR

I 'VE BEEN WANTING THIS LOOK BUT NEVER DARE IT.................... Last night nilikuwa natakiwa kwenda kwenye mnuso my hair was all messy and i had two choices only head wrap or chop chop  my hair kulingana na muda uliopo...............nafikiri this was a right choice  hey!! just for a change wandugu
haya sasa naanza na nani hiki kipilipili ?????? kama kawa olive oil ndo mpango
ndani ya miezi mitatu mpaka sita kitaeleweka kama nywele zako zimegoma olive oil usijaribu aisee utajuta.... mama wawili na olive oil ni kama mapacha labda inigomee this time

i know was nothing wrong with my hair  mnuso wa haraka haraka umeniponza ukizingatia nimejiwekea BIG NO na mawigi kwi! kwi! kwi! kama ntaweza
kuna watu wamenuna hapa ha! ha! ha! msijari mtanizoea tuu.......

Thursday, December 5, 2013

HAPPY BELATED 8TH ANNIVERSARY MR & MRS KAKWAYA




 napenda kuwaita Mumy na Dad yangu........... kuna kajihistory hapa kananikumbusha tulikotoka (dar mpaka Moro ha! ha! ha!)
miaka 8 tayari mbona kama jana???? duuu soon mtaitwa vijana wa zamani

nawapenda mno ...................Mungu azidi kuwatetea na kuwapigania.

Wednesday, December 4, 2013

TUZUNGUMZE



Kwa uelewa wangu huu mdogo nyumba ya Mungu ni sehemu pekee tunapokuwa na Muda mzuri  wakutafakari, kujifunza, kujikumbusha, neno la Mungu  na pia kusifu na kuabudu kwa habari ya Matendo makuu ya Mungu. kwa mfano unapokuwa kazini akili yako nyingi unaitumia masuala yanayohusu hiyo kazi, na unapokuwa shuleni  muda mwingi uko bize na masuala ya shule japo kuna muda wakuvusha bado hauchukui muda  mwingi, ndivyo ilivyo pia harusini,msibani,na shughuli yeyote ile wanadamu tumekuwa tukiwajibika sawa sawa ........... nazungumza na yule anaenielewa japo kuwa ,bado tuna watu wako kinyume kwa kila kitu yupo darasani anawaza makumbi ya starehe,kanisani anawaza biashara yaani yeye ni Z-A sio A-Z huyu tumuache kwanza...........................


Kinachonishangaza inapofika kwenye suala la nyumba ya Mungu, wandugu tumekuwa wazito  mnoo, tunatafuta sababu sana ,sijui hili pepo limetokea wapi?????? wengi wetu  tunaamini lakini ikifika suala la nyumba ya Mungu linapewa nafasi ya mwisho kabisa. imefikia hatua tunakwenda nyumba ya Mungu kwa bahati mbaya na sio bahati mbaya kukosa kuingia nyumbani mwa  Mungu.Nijuavyo mimi ile tuu kwenda kwenye nyumba ya Mungu ni ishara ya Shukrani, unyenyekevu,kuthamini ile nafasi aliyokupa Mungu hapa Duniani bila kujari unapitia nini na una hali gani ile pumzi tu, inatosha kupondeka na kumrudishia Mungu utukufu.


Wengi wetu tumenyoosheana sana vidole kupata sababu tusiende kanisani tunadai kwa sasa hakuna kanisa la kweli sijui unasoma kitabu gani basi hata kama ndo hivyo nenda basi ukabadilishe hali ya hewa ( siumesoma Mungu anajibu maombi ya mwenye haki?? kupitia wewe kanisa la kweli litapatikana kama ukisimama kwa nafasi yako) wengine wamedai wanakwazika kupitia waumini wengine( kwani huja soma tuchukuliane sisi kwa sisi mbona ukialikwa maharusini,na shughuli zozote zinazofanana ukifika unawakuta wenyewe wamekuandalia na taarabu na miili yao sasa, we mwenzangu na mimi mwili kama wa Mama wawili hapa na hata hizo nyimbo zenyewe huzijui lakini bado utachukuliana nao tena utahudhuria mpaka mataa yazimwe, sasa kwenye nyumba ya Mungu kinakushinda nini tena unadeal na watu wa imani moja?????? asikwambie mtu hakuna kitu kizuri kama kudeal na mtu wa imani moja na hofu ya Mungu ikiwa ndani yenu.

wengi wetu tumedai makanisa ni Biashara  kila ukienda kinachozungumzia ni sadaka ,kwani we mwenzangu unasoma kitabu kipi  ambacho hujakutana na  fungu la kumi,sadaka za shukrani, ahadi,malimbuko,kawaida,mavuno,upatanisho, dhambi na zinginezo??? huyo unaesema mfanya biashara yeye anakufundisha kweli ikupasayo kufanya huku anajilia taratibu fungu la kumi na kulijenga kanisa,hata hivyo  ni haki yake wandugu msimchungulie sana!!! na hata kama haitendei sawa sawa wewe haikuhusu fanya kama neno linavyokwambia hayo mengine atajuana na Mungu wake........ tufikie hatua tukomae wandugu .......... ninachosikitika sana hapa hata madhabahuni hofu imeingia kulisemea hili tumekuwa tukiambiwa habari za kupokea  bila kuhusianisha na kutoa, kwa akili zangu hizi ndogo somo la kupokea linamahusiano makubwa  nakutoa, kupokea  bila kutoa ni danganya toto wandugu...............

Nawengine tumejiwekea kautaratibu kabisa eti badala yakutoa fungu la kumi kanisani bora nikampe muhitaji, ndugu kila sadaka inautaratibu wake sadaka ya muhitaji na fungu la kumi ni sadaka mbili tofauti labda mimi ndo sielewi lakini kama wote tunasoma kitabu kimoja turudi tena darasani na roho wa Mungu akatuongoze kulipambanua hili (watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa)
 na hizi zote  ni mbinu za muovu kutaka kutuchanganya KWELI ITABAKI KUWA KWELI.

Na wakati mwingine mi naona roho za ubinafsi umetuingia tunakwepa majukumu, kanisani hebu tutafakari utawajibika wapi kufanya kazi ya Mungu????? kama tupo bize mitaani??? nikisoma wenzetu waliweka manukato kwenye madhabahu, wakina Suleimani walijenga kanisa kwa Dhahabu,wakina Daudi walibeba sanduku kucheza mpaka nguo kutoka leo hii hata kwenda kushiriki  kupanga meza,kusafisha kanisani hatuwezi  na bado tunalalamika hatumuoni Mungu maishani mwetu ...... tujiulize wewe na mimi tumefanya nini nyumbani mwa Mungu hata tukatikisa madhabahu ya moto ikashuka kujibu maombi yetu.tufanye kwa nafasi zetu na yeye Mungu wetu atafanya nafasi yake tusitegeane wapendwa.

wanadamu tumekuwa na sababu mnoo wandugu, haya kwa sisi watafutaji sasa utakuta jumapili pesa inakuchungulia mnoo ,wenye shift nao za double pay, na mimi mama wawili hapa jumapili utakuta na magari kama matatu yakuosha yenye thamani si chini ya $800, hapo mimi na Baba wawili kama sio kanisani mbona tunakomaa tunapiga bila garama zakumlipa mfanyakazi......... wakunielewa na anielewe mwisho wa siku pesa ni makaratasi mpango nikujiongeza kwa huyu yeye anayeweza kukupa hayo makaratasi.....................



Wandugu sijakamilika hata mimi bado sana nahitaji neema ya Mungu kumjua zaidi ila kwa hili la kwenda kwenye Nyumba ya Mungu lisitafutiwe sababu tena litufanye kuwa na shauku ......yaani kama mimi Mama wawili hunipangui kabisa kwenye Muda wa kwenda kanisani wanaonifahamu wanalijua hilo na wengine wameniita mnafiki naenda kufichia maovu yangu huko ( waache wajinga na ujinga wao kasome mithali 14:7-9) ukizingatia naupata kwa masaa mawili asubuhi na jioni mawili hapo nimesifu,nimeabudu, nimepata neno na kunyweshwa chai,  tofauti na hapo milango imefungwa kama unaingia lazima uaminike kupewa funguo yakuingia mara  kwa mara  hata hivyo hairuhusiwi(chezea nchi za watu) nawaonea wivu sana mnaopata muda masaa 24 nyumbani kwa Bwana aisee.


NIMEMALIZA NA MBARIKIWE




Yohana 15:18-20

18 “Kama ulimwengu ukiwachukia, fahamuni kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa watu wa ulim wengu huu, ulimwengu ungeliwapenda. Ulimwengu unawachukia kwa sababu ninyi si wa ulimwengu huu na mimi nimewachagua kutoka katika ulimwengu.

Tuesday, December 3, 2013

ONJA


 Leo onjeni tuu muonekano yaliyoendelea naona ya kwangu na Baba wawili ushahidi wa Camera hatuutaki.....................

lady in red..........

Monday, December 2, 2013

FRIENDS OF AFRICA DAY


HEADING..................

Thanks to SUBIRA WAHURE for Dressing ............... ilinifaa mnoo nilijiona kweli nimeitendea haki shughuli.

guess  nani mshindi wa Prize for best dressed couple?????


hata kipofu angehisi hili, wamependezaje???? perfect for the event, wifi yetu naye eti katunalia khanga DUNIA NI MAARIFA namuuliza unajua maana  alivyoitafsiri sasa plus accent alinivunjaje mbavu zangu????
the smile says it all............



beautiful faces  spotted
 herself with her cute baby.......
 nilikuwa busy mpaka nikasahau camera nakuja kukumbuka siku imeisha.