Pages

Ads 468x60px

Friday, May 8, 2015

MSAADA WA KIROHO.................



Eti wadau sote tunajua kwamba Mungu anamtumia mtu yeyote , Mara nyingine huhitaji kuwa mtakatifu ili utumike yaani Bwana anakutumia vile vile  yaani unatumika haswa na Bwana anajitwalia utukufu................... Tena unajua nini mara nyingi anatutumia kina sie ambao tunajua kweli ila kuna vipengelea  tumejihalalishia,  na tunatumia nafasi hizo tulizonazo labda kuvuruga wale wadogo wanaoanza kukua kiroho waone ni kawaida........ mbaya zaidi km ni uko kwenye mamlaka fulani labda niseme nimchungaji kwa mfano ...... na kwa sababu Mungu anakutumia sana kwenye madhabahu  yaani ni ukitulia madhabahuni moto unaotoka pale ni hatariiiiii basi kupitia hicho alichoweka Mungu ndani yako, tumejikuta waumini tunakuamini sana sasa kumbuka tuliokaribu na wewe ndo tunajua mapungufu yako behind the scene binafsi huwa sioni km ni tatizo maana sisi sote hatujakamilika tatizo linapokuja ni pale sasa unapotaka kuhalalisha/kulazimisha yale mapungufu yako  sisi tuliowakaribu labda tukuunge mkono au tushirikiane na wewe kwa namna fulani........ labda niseme bodi ya kanisa imeona kabisa hilo pungufu halimpi Mungu utukufu na pia sio sheria iliyoweka ili ifuate (maana imeandika tiini mamlaka na sheria zilizowekwa) ni kapepo tuu kamejiingiza huko  na sisi wapendwa tulivyowanyenyekevu sasa na umepewa kanafasi kaushemasi basi lolote utakaloambiwa na huyo mchungaji utafanya tuuu...........

Naomba nieleweke sipo kumnyooshea kidole mtumishi yeyote yule............ nawaheshimu mnoo hasa kwa nafasi wanayoitumikia sio ya kila mtu aisee, binafsi huwa nasema ni nafasi ngumu kuliko zote ila km umepandwa kweli hujaingia kwa akili zako Bwana lazima akutetee........... tatizo langu ni hako kapepo sasa kanavyoambukiza .......

 Mara nyingine niliwahi kuwaza ili ukue kiroho labda uwe muumini wa kawaida tuu ujue kuingia na kutoka .......lakini, ni nani atakaye jenga nyumba ya Bwana??siamini km una utakuwa kiroho hapo. Maana ni bora uyajue hayo mapungufu na ukabiliane nayo ili ujipime kiwango chako na Mungu ujue ni kweli unamuamini Mungu anayemtumia huyo mchungaji au unamuamini mtu???

Kinachonipa tafakari zaidi mara nyingi watu wanaomzunguka mtumishi wa dizaini hiyo huwa ana nafasi zaidi kimwili na kiroho..... ninaposema kimwili nina maana ya kwamba labda kuna kahela fulani kakujikimu kanapatika, au labda kuna namna fulani kwenye safari yako ya maisha alisimama na wewe, na mengineyo na ninavyosema kiroho ni vile anavyotumika madhabahuni basi hii roho nayo inajiingiza kwa siri watu tunasahau kusudi...................mbaya zaidi hizi roho za dizaini hizi zikituingia tunajisahau kabisa.......... unaweza ukajikuta hata madhabahuni tunazileta kwa namna fulani hivi....... ngoja nikupe mfano 

Huku kwenye nchi za wenzetu vitu km boyfriend & girlfriend  vimehalalishwa hadi makanisani yaani watu wamezoana huko wanakuja wanashikana shikana na watu tunawabariki tuu...... hakuna cha  engagement  wala nini jana alikuwa peke yake leo amekuja na binti wanashikana shikana tuu  mbaya zaidi wanaweza wakakukalia mbele yako ili uwaone vizuri ha!ha!ha!  umekaa nyuma unasikiliza mahubiri watu mbele yako wanashikana shikana tuu mbaya zaidi utaambiwa watoto wa wachungaji sijui nini na nini..... kuna hiyo moja niliwahi kuishuhudia  nilikuwa kwenye ibada moja tuliambiwa tufurahi na hao watoto wamefanikisha mwaka mmoja pamoja  aiseekumbuka kuna waumini ambao walishindwa kuvumilia kwani wana watoto wa umri ambao walikuwa wanaona hayo wasingependa watoto wao waige na kwa sababu kanisa lilichukulia kawaidi baadhi ya waumini waliona bora wahame tuu (kondoo wa Bwana walipotea usitake kujua imani yao ilikuwaje baada ya hapo je hawakuona umuhimu tena wakubaki kwenye kusudi au??? Yes sad story after...... ........ lakini pia huhitaji kukurupuka tuu nakusema neno kuna hekima inatakiwa na kutubu kwa ajili ya kanisa........baada ya mda hao watoto wakaachana ha!ha!ha!  guess what nikaitwa kushiriki kuomba heee!!! kwa lipi sasa  jamani bora ungekuwa uchumba ningemuomba Mungu atusaidie macho ya rohoni tujue labda ule uchumba haukuwa kwa kusudi la Mungu sasa niombe uzinzi ???uliobarikiwa badala yakufurahia sasa pepo la uzinzi halitakuwa lina niblock mbele yangu nikiwa kanisani!!!! duu ikatokea sasa wameingia kwenye kumi nane zangu ikabidi niulize kwani nyie wezangu hili swala lote mnalichukuliaje?? tulielezana mengi ila jibu nililopewa mwisho  niliambiwa hivi, kuna wakati unatakiwa kujua km mwanao anapanda mlima  au hapandi ....upo hapo?? nikamjibu sasa kwa sisi waumini muongozo wetu uko wapi? si kwenye biblia? na biblia inasemaje juu ya hili?? .......................

Ninachotaka kusema ni hivi sasa kwa mfano huu utaona kabisa watu tuhalalisha vitu ambavyo sasa mwisho wa siku vinatuhamisha kwenye kusudi........ na kwa kusema hivi jamani nimetoka huko yaani wokovu wangu umenikuta tayari niko huko kwenye dimbwi la takataka thank God mara baada yakujua kweli juu ya hilo nilipanga mikakati mizito yakumshinda Shetani kwenye eneo hilo na nilimuona Mungu akinitetea. Sasa ninapoona mtu tayari anaijua kweli nakuhalalisha bila kuweka mikakati !!!!mbaya zaidi anataka na mimi nishiriki kwa namna moja ama nyingine duuu!! hapo ndo nahitaji kujua nafasi yangu iko wapi??? Ninachojua mimi wokovu wangu umegaramiwa aisee ........ sijiweki kwenye nafasi hii miaka kadhaa ijayo wanangu watakapo fika umri huu lakini ninachojua mimi kweli ndio wanayotakiwa kuijua  macho yangu hayakotayari kushuhudia na wala moyo wangu haupo tayari kubariki wao wamezaliwa kwenye kweli na kweli ndio itakayowaweka huru. haijalishi Mama yao neema ya wokovu ilinikuta wapi wanachotakiwa kujua wao wamezaliwa ndani ya wokovu na Mungu atawasaidia kuyashinda...... nakubariana na wewe kuna wakati inaweza tokea lakini jukumu langu ni nini??? kamsome Heri utanielewa nasema nini.............halafu mbona imeandikwa (Waebrania 10:26 Maana, tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kufahamu ukweli, hakuna dhabihu iwezayo kutolewa tena kwa ajili ya kuondoa dhambi.)


Wengi mtaniambia ni hekima kukaa kimya nakuangalia ,ngoja niwambie kajiupeo kangu kadogo kakusoma soma biblia namuona Yesu alipotakiwa kusema alisema, nikweli hakutaka kujiboost boost kujionesha yeye ni nani  ila alihakikisha kila alilolisema halibadilishi maana kama Yeye ni Mwana wa Mungu, namwangalia Daudi alijificha sana mbele ya macho ya Sauli lakini kila walipokutana uso kwa uso Daudi alimpiga la uso Sauli kwakumwambia ukweli.... Huyo huyo  Daudi kwani hujamsikia alimpiga neno mfilisti jitu kubwa??? Kwani Bwana alimuacha?? ha!ha!ha!  utaniambia Yohani kajifanya kampa ukweli mfalme mwisho wa siku kichwa chake kikakatwa Ha!Ha!Ha! unajua haikuwa rahisi kihivyo yaani Muda mrefu ulipita yaani mpaka hilo tendo likatendeka hapo kati Yohani aliendelea kupiga injili km kawa binafsi huwa nasema hivyo ndivyo ilivyoruhusiwa iwe ili mimi na wewe tujifunze kitu ni bora ufe kwa sababu ya kulitetea kusudu au uhame kusudi?? halafu unajua nini Muda wa kufa ni ule ule yaani..................

Tujiulize sasa nafasi zetu ziko wapi?? wewe ndo unajua ile kweli kwa jinsi na namna uliyookolewa je bado uko pale pale au kusudi limebadilishwa kwa siri bila kujijua labda leo Mama wawili nimekukumbusha??

 Kwakusema hivi nikiwa niko kwenye hili tafakari nimeingia mitandaoni nimeona kuna hii freedom of speech ndugu zangu mnataka kunyang'anywa nimeenda kuisoma hiyo bill ama sijui ndo sheria wapendwa kwa maoni yangu yaani hii kitu inatakiwa IREKEBISHWE  yaani imekaa kukukandamiza sana wewe uliyebarikiwa  sauti ila nafasi huna($$$ ze cheo huna,  ha!ha!ha! kumbuka wewe ni nchi na nchi ni wewe .... nimeshangaa sana nimepita kwa wapendwa wengi hatujasema lolote juu ya hili ..............  sijaelewa au ndo tumejifungia kuomba mavyumbani au???binafsi jamani km juzi kati hapo nilijikuta kabisa kuna haja kuwe kuna sheria mitandaoni........ lakini tena nilivyoipitia hivyo vipengele duu aisee marekebisho ni muhimu ama sivyo ibaki tuu kama ilivyokuwa maana huko ndo tunaenda kuharibu kabisaaa nazungumzia kimwili hapa ha!ha!ha!ha!huu ni mda wa kusema nini maoni yako ikishapita mpendwa hauna choice nilazima uifuate........Nyie haya mwenzenu nawasikilizia nikiona vipi fasta nabadili gamba from kijani to........ ha!ha!ha!ha!


Siwangalii usoni leo maana wengi wenu nimewavuruga ha!ha!ha! nawapenda lakini.





No comments:

Post a Comment