Haya wandugu nimejizuia hili, maana niliona kama halitakuwa msaada kwenu, lakini tangu jana nimekosa amani kwa nini ni siliseme?? na kama lilikuwa msaada kwangu kwa kunifungua upeo zaidi kwa nini isiwe msaada pia kwa mdau wangu??????? Basi ngoja nifunguke wapendwa......
Namshukuru Mungu mnoo kwa namna anavyotenda ndani ya maisha yangu, nimemuona , nakumshangaa zaidi kuna wakati najifinya finya kujithibitisha kama ni mimi au ??? na mara nyingine natoa namachozi ,maana vitu vingine kwangu niliwahi kuamini ni ndoto isiyoweza kutimilika, na ahimidiwe huyu Mungu anayetupa neema(mithali 3:33-35) kasome utanielewa hauhitaji kuwa mkamilifu ili upate neema ni unyenyekevu tuu( kutambua,kuthamini,na kukubali kuwa bila yeye wewe si kitu),
Natokea jinsi nilivyoimaliza week iliyopita hadi leo, kila ilipoitwa leo nilikuwa na kitu cha pekee chakumshukuru Mungu mojawapo ni hili....... nikiongozwa na neno NITAKUKETISHA NA WAKUU
Nilijikuta nimekaa na mtu mmoja ana mahela aisee mweee!!!! anacontract yakujenga Nyumba 200 kwa mwaka huu, yeye mwenyewe anamiliki nyumba 40 za kwake binafsi, amenitajia ana investment hizo, Mama watoto ndo anadeal nazo hata hajuagi zinaendaje ila anachojua zinaingia $$$ za uhakika, anyway tuliongea mengi, ila hili ndilo linalonisumbua niwambie.......
huyu mtu ana hofu ya Mungu kuliko maelezo ..... ana mistari yake alikuwa ananiambia nakuleta kwenye uhalisia wa maisha yake akasema, kuna vitu mtu anatakiwa kuvijua, nakuwa msingi mkubwa wa mafanikio yake, ambavyo ni, kukua kibiashara, kukua kimahusiano,na kukua kiroho.
Alisema utajiri wake usingelifika hapo alipo kama alisahau familia yake na maisha yake yakiroho . Pale alipo anasema ni lazima ahakikishe anabalance vyote sawa sawa, hataki mali imuzoee kiasi kwamba apoteze familia yake, na nimarufuku kwake nafasi yakiroho ikamezwa na utajiri wake. anasema anaheshimu sana mipaka ya hivi vitatu.
Akaendelea akasema kuna group la watu watatu katika maisha group la maskini, saizi ya kati, na matajiri.... ukitaka kujua wewe uko wapi jichunguze juu ya hili.
ukiona asilimia kubwa ya maongezi yako na fikira zako ni kwa habari ya watu, mfano fulani kanifanyia hivi, fulani kamtenda huyu, fulani, fulani , fulani ujue wewe uko kwenye group la maskini.
Ukiona asilimia kubwa ya fikira zako ni kwa habari ya gari, tv, nyumba,nguo, viatu yani ni vitu, vitu, vitu, vitu hata kama hauna wewe uko kwenye group la saizi ya kati.
Na ukiona wewe fikira zako ni idea hata kama bado hujafanikisha ile idea wewe ni tajiri. akamalizia na kusema hata uumbaji ulianza na idea. kama asingelijua hii mbinu yeye hapo alipo asingelikuwapo.
Mngeniona Mama wawili ninavyotundika maswali ungenihurumia!!! huku nikijiambatanisha yale maombi yetu yakipendwa aliyonifundisha Mama mchungaji wangu Bongo ,BWANA YESU NAJIAMBATANISHA NA HUYU MTU, KUANZIA UELEWA WA HUYU MTU MPAKA URITHI, AHSANTE BWANA YESU MAANA SISI TUWARITHI, AHSANTE BWANA YESU MAANA UMESEMA MIMI NI KICHWA, NAJIAMBATANISHA,NAJIAMBATANISHA,............ yaani nilikuwa nimekaa lakini ndani yangu nilikuwa naruka ruka na maombi weeee nyie acheni tuu. Hivi ushawahi kukutana na mtu hupendi haondoke wala mmalize maongezi basi ndo siku hiyo. akaniambia sasa hivi ndo nataka kuangalia biashara yangu imeendaje maana nimetoka vacation nchi mbali mbali na familia yangu.Alniimaliza kabisa mie mpenda vacation kwi! kwi! kwi! kiukweli maongezi yalinoga mno... nahisi nimeshindwa kufikisha ujumbe sawa sawa ungemsikiliza mwenyewe nakimombo chake duuuu!!!
Ni hayo tuu wapendwa ninachotaka kukutia moyo wewe uli nje ya nchi, tuliozungukwa na urangi, ndugu mimi sasa hivi ukiniambia kuna urangi nakukatalia........ kwa jinsi ninavyokutana na watu ambao nisingetegemea hata ushauri kutoka kwao, kama kuna huyu mwingine ndo huwa simuelewe kabisa amekuwa kama ndugu wa hiyari!!!! anakupa ma idea mpaka unachanganyikiwa. Nilichogundua ukabila uko kwa kina sie wa level ya chini kabisa yaani vibaraka wa mabig boss, lakini hawa mabig Boss wenyewe hawana shida, wanathamini kuliko maelezo. press on ndugu zangu kwa msaada wa Mungu tutashinda.