Pages

Ads 468x60px

Thursday, April 21, 2016

NYUMA YA PAZIA.................

Eeh bwana situkafanya boat cruise...... lengo kwenda tuu kuona wenzetu wanavyoishi.............  mi na Baba watoto wangu tumekutana yeye anapenda mnoo kucheza majini, yaani kunamichezo anachezaga mimi pembeni nahisi roho inatoka ha!ha!ha! lakini mi mkewe napenda view ya maji aisee ........ yaani ukinipeleka mafichoni  km ni eneo la maji maji naomba chumba kinachotazamana na  maji yaani kwa garama yoyote ntajitutumua (iwe ndani ya uwezo wangu lakini ha!ha!ha!) ila kuingia kwenye maji sasa ki!ki!kiii!

 Basi bwana tukafunga safari huko yaani nyumba zimejengwa  back yard mtu kapaki boat lake duuu!! we unafunga safari kwenda kuangalia dolfin mwenzio ndo nje kwake anapumzika ha!ha!ha!  tunajifungaga safari humu ndani kwenda fishing wenzetu wanafish nje ya nyumba ....... Duuu!!! ila kiukweli huku mafichoni ninakoendaga aisee kunanipaga mtazamo tofauti aisee..........

 na hii nimejikuta sina hela ila ndoto zangu zinakuwaga kubwa mpaka naogopa na pia imetusaidia sana kuona vitu kawaidaaa....... nakutokuwa na haraka zaidi kujipanga.... Yes inawezekana mbona nilivyokuwa umri fulani niliwahi kuaminishwa hapa nilipo  ningeweza kuona kwenye Tv pekee yake yaani ni ndoto kuwa !!! leo najiona ni zaidi ya ile ndoto basi na haya mengine yatawezekana Mungu atupe uzima nakuzidi kutuangazia neema yake.....


It is possible with Christ.........

nani hawa



Ndoto! andika ndoto yako.........
 Hapo Dolfin alipita ndo kumshangaaje sasa Ha!ha!ha!

 Yes  hii ndio ninayoizungumzia, Hizo nyumba za watu tuu kama mimi na wewe, tena nikuambiaje nilivyokuwa napewa historia niliambiwa wengi niwale walioretire ndo wamekuja na hela zako Bwana wewe why wait  mpaka huko kote????? Why why why...........


Tulivyokuwa wabishi mbona tuliwasiliana na wauzaji  ha!ha!ha! Mambo mengine yanatisha tuu kwa picha ila yanawezekana afanye akili yako iwaze tofauti............... na utakuwa tofauti

 Memory 


Tunawapenda

Wednesday, April 20, 2016

LA FAMILIA.............

Hamjambo humu kwetu??? kwetu  utukufu kwa Mungu kwa kweli, vyovyote ilivyo huwa tunaamini Mungu karuhusu   so we always go with the flow........ kama ni sad moment basi tunajitahidi sana kuomba amani ya Kristo ili turudi kwenye mstari na kama ni furaha time he!he!he! we always do our best to make memory...........

 Haya hizi picha za mafichoni kama kawa tukiwa mafichoni mapicha ya mtu nne hayakosekani ha!ha!ha! 

 haya twende kazi


Mama ake nani huyu???

Mapozi vepe


 na wawili wangu
 yaani hili pozi ni letu aisee mapicha huwa hayaishi km hatujafanya hivi ha!ha!ha!

 asikwambie mtu mtoto wa kike ni wa Baba yaani kikikikiii Jamani sijasema nataka maombi hapa kha!! hamchelewi kufunga na kuomba kwa ajili yangu ha!ha!ha! nikiwa tayari ntawambia msijitie kimbelembele  ha!ha!ha!

roho zangu



nani hawa etyi..........

kujibebisha vepe.........




Tunawapenda.............

Friday, April 15, 2016

DADA KUBWA NA UBORA WAKE.............

Mnuno vepe ha!ha!ha! showing mum business...........

he!he!he! she is only 7yrs old jamani ha!ha!ha! na hizi nywele ndo zimemfanye awe mkubwaaaaaa  najuta........ lengo ilikuwa Bad hair day shuleni............ sasa Mama mtu ndo nikaona ngoja nimtengeneze hivi halafu nimfunge mafundo fundo ha!ha!ha! lengo la siku lilitimia ila baada ya hapo bi dada kagoma kabisa kuzitoa ha!ha!ha!............ nimeamua nimpotezee for sometime 

 Blame my Mum (in her voice) ha!ha!ha!

ila jamani one thing ninachojitahidi kuwafundisha watoto wangu ni kuwa happy.......
yaani huwa nawambia huwezi ukatafuta furaha mahali popote km hautakifurahia kile ulichonacho na kukitumia kwa moyo wa shukrani.............nafikiri huu ndio msingi mkubwa wa nyumba yangu pesa zinatafutwa ila haziwezi kukupa furaha km akili yako yote itafocus huko.......... yaani you wont have enough............. lakini ukitanguliza furaha ndani yako kile utakachokipata utajua kuiridhisha furaha yako............. mitihani ya maisha ipo na huwezi kuizuia aiseee........... ila ukiamua kuitafuta furaha aisee yaani wewe  ni no stress zone.........Kila kitu kinaanza na mind set wapendwa.............

 Hapa mimi simo aisee ha!ha!ha! ila nilimuuliza ni nini maana na km hujui maana why doing ha!ha!ha! old school Mum

Tunawapenda

Wednesday, April 13, 2016

TUMEKUZA..............

Wapendwa humu ndani  hope mko poua yaani........... Ma wawili huku nyuma ya pazia full kumshukuru Mungu yaani...... aiseee  mwanenu ndo tayari ana miaka sita.... Duuu yaani kama jana kwa kweli Jina la Bwana libarikiwe halafu unajua nini naanza kuona uzee unagonga hodi aisee....... Imagine mtu akiniuliza namwambia my last born is 6yrs old ha!ha!ha!ha!
 Nyie Bwana mnisaidiage tuu kumshukuru Mungu yaani duu.... Ushawahi kuingia mbele za Mungu yaani kuomba huwezi, kushukuru huwezi yaani machozi tuu yanakutoka halafu huelewi why??? basi hili nalo mojawapo...............  Shuhuda zingine hazielezeki aiseee.


 nisiwachoshe mapicha mengi ilikuwa kumpiga moja ili nimuwish ila duu aliishia kunipa mapozi tofauti tofauti ambayo kila moja kwangu lina maana mnooo..........

 The joy of the Lord is my strength..........

 yaani nilivyokuwa nampiga picha huku akinipa mapozi na maongezi fulani duuu!!! priceless

  oh! my Cristabell!!!!!
 nahisi najua kila pozi lake anawaza nini au anamaanisha nini  aisee.......





 Amazing Grace, how sweet................  ...

Nawapenda

Friday, April 8, 2016

HAPPY ANNIVERSARY TO US

Haya basi muendelezo wa post iliyopita........ na kesho yake ndo ikawa ile siku iliyonisukuma ndani ya moyo kufanya nilivyofanya............

Wazee ndo tushapiga nane aisee.... Duu km jana yaani hii miaka inavyokimbia sasa....SIFA ZIMRUDIE YEYE ALIYETUWEZESHA yaani hapa ni mgomo tuu mpaka kifo not otherwise hata shetani habari anayo.............. 

Basi bwana hatukuwa na something special zaidi ya special prayer before my man kwenda kututafutia hela ya kula hahahaa mkewe nikaishia kuangalia picha zetu za kumbukumbu for sure zilinipa feelings tofauti tofauti aisee.... nililia nilicheka,nilishangaa,nikawaza yaani basi tuu


 kikubwa nilichokiwaza ni jinsi gani Mungu aliruhusu hili........... jamani hii harusi nilipewa mda wa wiki kuiandaa ninavyosema kuiandaa i mean niliandaa mwenyewe..........
in short taratibu za wazazi zote zilikuwa zimekamilika  hiyo wiki tulikuwa  tumeshajipangia wenyewe harusi itafanyika ndani ya miezi sita ijayo( mtajiju km ilikuwa kubariki ama ndoa ila ndo hivyo, Bwana alitusamehe  nakutufanya upya ha!ha!ha!)..... tukiwa sasa tunaanza kutoa taarifa mara Baba watoto akapata hiyo sponser yakuja huku iliyompa km siku 10 awe ameshakuja huku........(mipango mingine inakujaga na baraka zake aisee)

Aisee mchumba wakati huo(ha!ha!ha! hivi mchumba ni yule aliyefanya taratibu zote akisubiri harusi bila kukugusa ama yule...........Ahsante kwa ajili ya msalaba maana duu sijui nani angepona aisee nawaza tuu)
 Akiwa anaenda kupanda ndege kwenda kuresign kazi yake ameniacha mimi sijui ntaanzaje ninachokumbuka kauli yake hakikisha tumefunga ndoa kabla sijaondoka ha!ha!ha!ha!


aisee jinsi Mungu alivyofanya nimetafakari sana kumbuka ndoa inatakiwa itangazwe miezi mitatu kabla,kuupata ukumbi aisee ulikuwa maarufu sana enzi hizo uko posta, ulikuwa wawakubwa enzi hizo nimeusahau jina ndaini ulikuwaga gold.......,kumpata mc ambaye hakunidissapoint,band,music, mtu wa vyakula na cake kuwaleta ndugu kutoka mikoani, nakumbuka jinsi ilivyokuwa ngumu kuwashawishi wazee,wajomba kwamba hii kitu inaenda kufanyika ndani ya siku kadhaa not a week anymore maana, sikutaka kusema chochote kabla kibali hakijatoka serikali kumruhusu mchungaji kunifungisha ndoa.........kibali kilitoka jumatano harusi jumapili ha!ha!ha!,kuwafanyia shopping i dont remember anyone helping me with this.... ninachokumbuka kuwafuata walionisimamia kwenda kumtafuta fundi juma atutengenezee gauni ndani ya siku tatu maana nilikuwa mwembamba magauni dukani hayanitoshi ha!ha!ha! fundi juma aliomba poo aiseee wakati huo huo nikamwambia Mume wake akatafute suti zao ha!ha!ha! (sikumbuki km kulikuwa na muda wakutafuta slim fit ha!ha!ha!)Baba watoto anarudi 2night before almost kila kitu kiko mezani naona akaona anipongeze mke wake na hilo gari  na kuniweka Kilimanjaro siku hizi mnaita Kempist ha!ha!ha! halikuwa kwenye akili yangu kabisa..... alinisuprise aliondokea hotelini kwenda kupanda ndege hilo balaa lakujibu maswali yaliyotokea kwa wazee aliniachia mie ha!ha!ha!  na kakitchen part nilifanyiwa baadae mikoani hahaha! no send off you know ha!ha!ha! ka account sasa tulikokuwa tunajifichia vi hela vyetu kalikuwa keupeee  nani akuchangie ndani ya wiki?? kuna wale wakaribu waliojua kwakweli walijitahidi walivyoweza na huwezi kuwalaamu nakumbuka baada ya ndoa tulienda hotelini kupumzika kabla mda wa ukumbini na kadi zetu unapiga simu halo fulani , ndugu yangu nisamehe bwa mwenzio ndo nishafunga ndoa naomba uje hapa uchukue kadi ya ukumbini ha!ha!ha!
Mawazo jinsi yakuwarudisha watu mikoani vepeeeee ha!ha!ha! nani hatakuelewa maana umefanya fujo ya ndoa ha!ha!ha!duu nimekumbuka mengi mnooo aisee

Happy anniversary to us.



Mwisho wa siku  kila mtu alikuwa suprised yaani hata mimi mwenyewe mpaka leo ukiniuliza how i did it km sio Mungu basi mi jeuri wa shukrani......


 story of our wedding!!!


ila mimi Bwana nikirembwa aisee narembeka haswaaaaaa ha!ha!ha! km nawana wakina niniii huku walivyovuta mdomo ha!ha!ha! jamani nawapenda lakini


Bwana wee shetani hawezi kulala kihivi yaani ha!ha!ha! hata km anaumwa atajikongoja tuu ajaribu ha!ha!ha!ha! eti nimeaambiwa siku hizi wanaume hawatupigi hiyo forehead eti tunajaza sana ma make up by the time amemaliza mdomo wake unakuwa km wale coca cola addict ha!ha!ha!

 enzi hizo za photo point vepe ha!ha!ha!


nilikuwa mwembamba ila nahisi kilo zilipungua zaidi fundi Juma ilibidi anipime kila asubuhi kumake sure

kwa kweli kamati yangu haikuniangusha nilivyokuwa nawapa kazi niliwaambia sina kamati kwa hiyo mpambani we ndo mwanakamati,keki,mc,................... ha!ha!ha! they did their best aisee  kwa enzi hizo lakini,sikuwa nawakumlaumu hata mmoja hakuna aliyeamini km maandalizi yalikuwa ya siku chache.


 haya basi baada yakujikumbusha namapicha nikaona nimfanyie Baba watoto kitu cha tofauti ambacho huwa sikifanya.....

kiujumla humu ndani mwangu huwezi ukanikuta nafanya kazi za nje km garden,kusafisha pool, sijui kuosha magari tunayotumia wenyewe sio biashara, so nikaona ngoja nitoe moja ya toy yake nimuoshee.......... kama unavyojua hichi kitu kinaendeshwa kwenye vumbi,mchanga au tope.......  ilikuwa inamatope ya hatari mwanamke nikaing'arisha just to say Ahsante Baba watoto kwanikubali km nilivyo, nakunivumilia maada duu!!! mi mkewe majanga sometimes ha!ha!ha!

nafikiri nilimpata maana nikitu hadimu kutoka kwa mkewe ha!ha!ha! any way ataenda kuichezea tena kwenye matope ilikuwa inahitaji a good wash before..........

 nimeloga kihivyo yaani. wanasema ukipenda kitu kwa moyo ideas huwa zinakuja and it means a lot to a person.

 nawapenda

LATE POST........


Nimechoka kuwaomba msamaha kuingia humu......... yaani nyie mnisamehage tuu, ratiba yangu imekuwa tite mnoo aisee ..... Ila naamini ntarudi kuna mambo ngoja yakae sawa siwezi kuwapromise ni lini  ila tutarudi tena kwa style  nzuri mnooo........Hatufunguki sana siku hizi maana duu shetani nae ana style nyingi zakupata habari ha!ha!ha! na humu anaingiaga ujue kikikikiii!! Haimaanishi tunamuogopa ila sema nini ??hatupendi usumbufu bwana kipindi tunamsubiri Mungu amalize kazi yake................Ila aisee mwacheni Mungu aitwe Mungu.......

Je umewahi kuwaza why people wana maisha fulani lakini kwa hesabu zako za kichwani unaamini they deserve better yaani ..........then Mungu anaamua kukufulia  whats is behind the scene unabaki kutoa macho????



 Je umewahi kuona jambo ambalo wewe unahisi Mungu atamtumia fulani  for some reasons Mungu akakwambia mawazo yangu si yako, usinifundishe kazi wala usinichagulie nani atumike ha!ha!ha! am more than that Mwanangu.............. kaa kwenye mstari............ sio rahisi kujua nani atumike hasa ukiwa muhitaji ila, utajua nani ametumika mara baada ya jambo kufanyika.........Aiseee Namuogopa Mungu. 

 Ama imewahi kukukuta  ukidhani huu ndio utukufu ninao uendea kumbe!, Bwana kakuandalia utukufu mkubwa zaidi lakini kupitia ule utukufu ulioutazamia ndipo Bwana akakufunulia yale ya sirini???

Ninachotaka kusisitiza weka tumaini lako kwa Bwana, usitishwe na hekima  au wasomi wa dunia........ halafu ujue nini yani usipigane nao wala kuweka chuki ........wapende like never before ha!ha!ha! maana kupitia wao labda  Mungu asingekufungua halafu you know what?? you loose nothing yaani...........Huwa siamini eti kwa sababu ya fulani ndio imeshindika labda hukukaa eneo lako kiuaminifu......Mungu hafundishwi kazi aiseee na zaidi ya yote ni Mwaminifu.

Kwani hivi unafikiri Yesu hakujua nani atakuwa msaliti ha!ha!ha! ngoja nikwambia basi hata shetani nae alikuwa malaika mzuriii wa Mungu............ Mwisho wa siku kusudi lililokusudiwa  lazima litimie yaani nikimaanisha kusudu la Mungu sio la mwanadamu.......


 Naongea sana haya ha!ha!ha!........ 

Hii nayo ilikuwa siku wapenzi kama kawa nilijikuta na shughulika ha!ha!ha!

 Mmoja wa hao hapo niliyopiga nao picha namwitaga my Dada yaani  ha!ha!ha! kwenye vishughuli lazima aniite  sasa hii alikuwa na rafiki yake ambaye anakuja kumtembelea. Ambaye anamtoto alifunga mwaka akiwa kwenye ndege kuja kwenye kijiji chetu kumtembelea my Dada....... sasa Mama mtu akamuomba rafiki yake huyo anaemtembelea hapo chini, amuandalie japo kikeki akifika akate mtoto wake.....
 My Dada kama  kawa  akanifuata dizaini kama kumshauri au kuniambia km naweza ku team kiana fulani........ Yes anajua am a busy Mama......

 Then kimoyoni siku inayofuata ni anniversary yangu ....... Dogo nimesha team 8yrs hahahaaaa Mungu nimwaminifu aiseee....

 Basi sasa sikuwa na ratiba yoyote kutokana na Baba watoto yuko busy fulani...... sikutaka kumchosha  kimoyoni nikajisemea , hapa ndo muda wakujibebea mibaraka yangu kupitia huyu mtoto....... kupitia huyu mtoto nitamshukuru Mungu .......... ntafanya ntakachoweza bila kuwambia wahusika kwa nini nimeamua kulivalia njuga..... coz wao hawakuta kufanya sanaaa km nilivyo sema ilikuwa nikukata keki ila kwa namna gani ndo mama  shughuli nikatoka na idea ha!ha!ha!

 Siwajui,sijawahi kuwaona yaani ntawaonea kwenye hiyo event, nitawasuprise tuu wazazi ambao naamini kuna kitu kitatendeka ndani yao kwa ajili ya kumbukumbu ya mtoto wao ambao sidhani km hata walijua itakuwa hivyo........

  


 hichi ndicho nilichoishia kufanya i know labda in my life nimejeruhi sana mioyo ya watu......... lakini pia nimeweza kuweka tabasamu kwa mtu japo mmoja.......

Nimeshafuatwa sana kwenye hili eneo la kupamba na kuwapiga picha kwenye shughuli km hizi , huwa nawambia hivi sio kila huduma iliyopo ndani yako inatakiwa ikupe hela..... Huduma nyingine umepewa ili ufanye kwa mapenzi tuu...... hivi vitu huwa navifanya kwa kupenda aisee........ yaaani i love  doing it ......kunakuwaga na amani fulani unavyofanya yaani hasa pale bajeti inapokuwa hairusu lakini unahakikisha umefanya duuu!!! Amani yake hailezeki aiseee..

sisi hapa wakupendezaga tuu yaani ha!ha!ha!

sikutumia Camera yangu, nilimuona Baba mtu ana kamera yake hivyo  niliamini watakuwa na kumbukumbu yakutosha hizi nilitumia simu. na nisingependa kuwaweka humu coz siwajui as i said yaani tulimalizana usiku ule.

Nawapenda

Sunday, April 3, 2016

MAMA WAWILI......................

Siku nyingine tena na wakati mwingine Bwana amefanya nionekane ha!ha!ha!
 Binti wa Yesu katika ubora wake


 Sura ya kazi wito bwana  ha!ha!ha!




Nawapenda

Friday, April 1, 2016

MAMA NA WANAWE.......

Kama kawa wandugu late post yaani moja ya siku ndani ya week ha!ha!ha!

Mabinti wakubwa wa Slay na wapenda picha ha!ha!ha! ikifika muda wa picha huwa tunakimbiwa sometimes ha!ha!ha!

miondoko vepe

na kabinti kadogo picha ndo hakapendi siku hizi yaani nikukalazimisha tuu 


kasichana vepe? haa!ha!ha!ha!

Nawapenda