Pages

Ads 468x60px

Monday, July 14, 2014

ULOKOLE NA MAMA WAWILI..................


 Haya wandugu ngoja nifunguke kwa haka kaji ufahamu nilikonako kwa habari ya nini maana ya ulokole .

Nijuavyo mimi mlokole ni Binadam kama alivyo binadamu yeyote aliyepo dunia.................. moja ya sifa inayomtofautisha na mwanadamu mwingine yeye anaamini NENO LA MUNGU, KWELI nikimaanisha BIBLIA. na hiyo haina ubishi BIBLIA imebeba maandiko matakatifu ya MUNGU.Kama hukubali hili kuendelea kunisoma huku chini unapoteza muda.

 Kama umekubaliana na mimi hapo , basi nielewe kuwa Mlokole ni mtoto mzuri, mtoto mzuri siku zote ana muongozo, pamoja na kwamba hapakosekani makosa ambayo kwa namna moja ama nyingine makosa hayo yanamsaidia kukua na kukomaa zaidi, kutambua lipi lililo jema na lipi baya. Na ndio maana imeandika TUKISEMA HATUNA DHAMBI KWELI HAIPO NDANI YETU...............Lakini, hili neno halimpi msamaha wakufanya dhambi za kukusudia..Niongeze kwa kusema Ulokole  ni mtu na uhalisia wake (BE YOURSELF) Usifanye kama kilemba chakufichia maovu maana siku ya umbuko lako inakuja........... ni bora ukaonyesha uhalisia wako ili uweze kukosolewa..........Asikwambie mtu ulokole pia una hatua za ukuaji , unatoka kwenye utufu kwenda kwenye utukufu zaidi..............Sifa moja ambayo huwa naipenda Mtu akinishangaa!!!! kwa kuniuliza hivi kweli Rose ndo wewe???!!!!! Sikutegemea kama Rose wewe wa miaka ile utaniambia Hivi, halafu unaambiwa kwa mazingira ambayo hujategemea....... yaani huna wazo kama kuna kilemba cha ulokole, lakini ndani yako una ufaham wa muongozo yaani we unafanya tuuu.............na hata anapokwambia hata wewe unastuka nakuanza kukumbuka miaka ile ilivyokuwa , Nielewe kuna vitu ambavyo Bado nilifanya nikiwa ndani ya ulokole ambavyo labda havikutoa picha kamili ya ulokole  lakini nilichotambua ni kwamba ulokole  sio kuwa fake,  Na leo hii ndo maana umekuwa shahidi kile ulichoshudia nilikifanya hata sasa sifanyi tena kwa maana niliingia mimi kama mimi nakuruhusu Neema ya kunitengeneza na kuniponda ponda ili niwe hivi nilivyo leo.................Inawezekana kabisa  bado niko kwenye kunolewa, safari ndo kwanza inaanza lakini, nina kila sababu yakumshukuru Mungu  kwa hapa nilipo, SIFA ZIMRUDIE YEYE ALINIWEZESHA.

Utaniambia kila mzazi ana muongozo wake hivyo na malezi yanatofautiana.... Sawa kwani siumekubaliana na mimi hapo juu???? BIBLIA inatuambia MUNGU NI BABA WA BABA  kwa mlokole huyo ndio mzazi wake na Muongozo unaanza hapa.................

Usiwe na miungu mingine ila mimi.

                        Usijifanyie sanamu ya kuchonga.

Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako.

Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

Waheshimu baba yako na mama yako

Usiue

Usizini

Usiibe.

 Usimshuhudie jirani yako uongo.

Usitamani…cho chote alicho nacho jirani yako.


Nielewavyo mimi huo muongozo hapo juu, mlolole yeyote wa kweli sio kilemba atakayejikuta amefanya lazima kutakuwa namaandalizi...... yaani kuna nafasi ambayo huwa inakupa muda wa kujiuliza ufanye au usifanye ........ Mlokole kweli naweza sema asilimia 90 itampa masumbuko ya moyo kabla yakufanya hilo tendo...........Masumbuko hayo hayatampa amani yakuyafanya hilo tendo na hata kama ikitokea amefanya mara baada ya tendo  roho ya toba humjia na wakati mwingine huwa anajikuta alichokifanya hakiwezi kusameheka, ana kuwa na moyo wakugua  mno, hawezi kuchukulia kawaida hata kidogo na hainaga marudio marudio hiyo ukiona  kuna marudio  marudio hata masukumbuko ya toba hayapo MMMMMH!!! kuna shida somewhere aisee. ukitaka kunielewa Msome Yuda msaliti unahisi kwa nini aliishia kujinyonga??? japo andiko lilitakiwa kutimia??? Acha turinge leo maana yote yalimalizwa msalabani !!!!!!!!Damu iliyomwagika pale msalabani ni ondoleo la dhambi zetu kama tukirudi  kwa moyo wakuugua na kupondeka vinginevyo tungekuwa tushaji Yuda sana tuuuuu!!!!( Ni shiida!!!)

Mlokole huyu sasa ambaye yuko sawa hapo juu, kama msomaje kasome Habari ya yule Tajiri aliyesema hayo yote nimeshayafanya tangu utoto wangu(Luka 18:18..............

  Unaweza kufanya yote lakini tuna mapungufu,Kuna vimapungufu vya papo kwa papo, yaani shetani analetaga tuu, labda kwa sababu ya mazingira tuliyonayo, au nafasi tulizo nazo, au vyovyote vile.........Yawezekana yule Tajiri angepewa muda angeweza kuwaza hivi,  huyu Mtu anayeniambia ndie mtoaji mwenyewe hivyo hata nisivyofanya atakavyo akitaka kuchukua atachukua tuu,Au labda angevuta picha ya Ayubu basi eeeh!!!( haya ni mawazo ya Mama Wawili),
 lakini iliruhusiwa iwe kama ilivyo ili tuwe na moyo wa unyenyekevu, japo kuwa wengi wamelelewa ndani ya muongozo ambao labda umekuwa kama sheria Ukisoma zaidi utakuta hata wanafunzi wameshtuka fulani (Ni nani basi awezaye kuokoka???? Yasiyowezekana kwa mwanadam...........)

Ninachosikitika ni kwamba kipengele hichi, Wengi wanatumia kama njia yakuwakatisha tamaa,Shetani huwa anatumia sana kupiga upofu watu nakuwanyima ufahamu kupitia kipengele hichi,kipengele hichi kimetoa sura tofauti ya ulokole labda niseme kwa sababu tumejipa unyonge sanaaaaa, nakushindwa kuelewesha .Lakini, mwisho wa siku ndugu naomba tuu uelewe Tatizo sio ulokole wangu ila kwa sababu umekaririshwa kwa habari ya ulokole na kupigwa upofu usione , usisome, wala usitambue sio rahisi ukanielewa..................Na kwakusema hivi Basi, sijasema kila anachofanya mlokole kiko sawa No! no! no! Tatizo ni vile wewe unavyokichukilia na kukitolea Hukumu.( Walokole wanafiki nyieeeeee!! Eti si ndio mnavyosemaga???Shushu kaimba Thamani ya ulokole wake anayejua muumba kama fake au sio  acha vijisababu endelea kutengeneza na Mungu wako..... hivi unajua wokovu ni wa mtu binafsi???? tutakusaidia kukuongoza toba ya kukiri na kukupa misingi ya neno la Mungu mwisho wa siku ni wewe na Mungu.)

Nikiendelea kusisitiza kwa habari ya huyu Mlokole Mimi na wewe tutakubaliana wanadamu tunatofautiana kuna wacheza sinema,wakulima,wafalme,mafashonista,......... yaani hizo zote ni nafasi za mtu ndivyo alivyo mlokole.Wengi tumekariri tunategemea kumuona mlokole masikini  (wa mali),hana hadhi,yaani hafanyi ilivyo kawaida zaidi ya unyonge...... Sikiliza nikwambie Tumeambiwa Tutakuwa vichwa na wala sio mikia, Tutaketishwa na wakuu, maana Bwana Atatupa kibali, ukisoma Biblia yako, utakutana na wafalme pia waliongoza kwa hekima, yaani kila nafasi iliyopo duniani iliyo halali ni haki ya mlokole kikubwa ni kwamba hiyo ndio nafasi uliyoruhusiwa kuwepo na mara nyingi huwa inakupa amani badala yakutafuta kuhurumiwa au kutukuzwa. (Naweza nisieleweke hapa Aliyekusudiwa atanielewa)

Na Mwisho naomba niseme hivi unaweza ukasema kama ni hivyo, basi wewe ni mtoto mzuri kwa maana upo kwenye kila kipengele hapo juu isipokuwa hujiiti mlokole ngoja ni kwambie

Tofauti ambayo ndo inakamilisha yooote hapo juu ni KUKIRI KUWA YESU NI MWOKOZI WA MAISHA YAKO KWA AKILI ZAKO TIMAMU  NA YEYE NDIO TUMAINI PEKEE.

kwani siumekubaliana na mimi unaamini maandiko, sasa maandiko hayo hayo siyamesema mtu haji kwa Baba kama hajapitia.......... ???????Na aminie na kubatizwa ...................????????? Na mtu akinikana mbele za watu ...........???? sasa unaogopa nini kumkiri?????? We ingia tuu mzima mzima bila kuwaza itakuwaje??? na ukubali kutengenezwa bila mipaka mambo mengi mwachie mwenyewe....Ha!Ha!Ha! nimekumbuka enzi hizo na Baba wawili Wangu Mweee!!!! Baada yakusahau mlango wa Kanisa kwa miaka miiingi!!!!hata hivyo  nilikuwa naenda kwa sheria, sasa basi!!! ile Siku Mungu alivyoamua kunivuruga  sasa duu!!!!! kwanza alinisahaulisha kama kuna Baba wawili ( enzi hizo Suleiman a.k.a Slay) Mara Baada ya kukiri ndo nikaanza kukumbuka sasa itakuwaje????? Halafu sasa ndo tulikuwa ndo malove yamechanganya mnoooo...... hatusikii wala kuambiwa Ha! ha! ha! mweeeeee!!!!! alikuwa kasafiri jioni Simu ya malove love lazima ipigwe kwi! kwi! kwi! unahisi niliipokeaje???? au ilikuwa wewe pepo kwa jiiiiina la Yesu toooooooka!!!!Nyie bwana acheni Mungu aitwe Mungu!!!!!Leo tupo hapa tulipo aisee acha niseme ni Neema!!!!!!!  ninaushahidi ujue???aiseee duuuu!!! we endelea kuniona chizi hivyo hivyo sauli sako, hiso ni sambi sako mwenyewe(in hehe accent)

halafu unajua nini laiti watu tungelijua safari ya ulokole is a sweetest journey ever!!!!!! haicomplicate aiseee,Lolote linalokupata unajua nina Tumaini yaani nina Baba wa MaBaba, Mshindi  wa Yote.HAKUNAGA KAMA YEYE

 Nyie ujue sipendi maswali??? ndo mi nishakupa nilichonacho.............. hivi tungekuwa tunaruhusu maswali madhabauni ingekuwaje kwi! kwi! kwi! ( joke)
 na mnikome hilo gazeti mmeliomba wenyeweeeeeee























No comments:

Post a Comment