Pages

Ads 468x60px

Wednesday, March 11, 2015

HAKUNA JIPYA CHINI YA JUA............................

Imeandikwa mtu hataishi kwa mkate bali kwa neno la Mungu.......... We mwenzangu unalielewaje hili neno??  Umejaribu kila unaposoma neno na kulileta kwenye uhalisia??? Je ukitafakari hupati picha halisi ya yale yanayotendeka leo??? Nimejikuta na waza sana aisee?? 

Basi mwenzio leo nilikuwa namtafakari mtu mmoja tuu kwenye biblia  nikajikuta nimemleta kwenye uhalisia wa sasa.  Ngoja nikushirikishe........

YOHANA 12

Basi, Maria alichukua chupa ya marashi ya nardo safi ya thamani kubwa, akampaka Yesu miguu na kuipangusa kwa nywele zake. Nyumba yote ikajaa harufu ya marashi. 4 Basi, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema, 5 Kwa nini marashi hayo hayakuuzwa kwa fedha dinari mia tatu, wakapewa maskini? 6 Alisema hivyo, si kwa kuwa alijali chochote juu ya maskini, bali kwa sababu alikuwa mweka hazina, na kwa kuwa alikuwa mwizi, mara kwa mara aliiba kutoka katika hiyo hazina. 7 Lakini Yesu akasema, "Msimsumbue huyu mama! Mwacheni ayaweke kwa ajili ya siku ya mazishi yangu. 8 Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini hamtakuwa nami siku zote."

 Namzungumzia Yuda Iskarioti na Maria.... Hawa watu wawili kuna mmoja amesimama kwenye nafasi yake na mwingine mdogo mdogo ameanza kuchomoka kwenye nafasi yake  ( Kumbuka ni mmoja wa wanafunzi waliotembea na Yesu, waliokula na Yesu,  kwa maana nyingi ni mmoja wa watu wakaribu mnoo wa Yesu si eti eeh???)......... 

 Ukisoma kuanzia mwanzo wa hiyo sura tunaambiwa Maria alikuwa akihudumia tuu, Nilivyotafakari mimi nahisi alihudumu kikamilifu, mpaka kuamsha kale karoho kachafu kalikojificha ndani ya Yuda kalikosa uvumili  Ha!ha!ha! halafu unajua nini, Shetani anavyotumika mahali mara nyingi huwa anakujaga na kadizaini fulani hivi , usipo kuwa makini unaweza shawishika, nakuona ni busara   kumbe kuna uovu ndani yake.......... HAKUNA JIPYA..........

5 Kwa nini marashi hayo hayakuuzwa kwa fedha dinari mia tatu, wakapewa maskini? 

Wow! busara si ndio hii  au we unaonaje????  Ha!ha!ha!

tuendelee

6 Alisema hivyo, si kwa kuwa alijali chochote juu ya maskini, bali kwa sababu alikuwa mweka hazina, na kwa kuwa alikuwa mwizi, mara kwa mara aliiba kutoka katika hiyo hazina.

 Hapo chacha........HAKUNA JIPYA...........

Kuna mambo mengi yakujifunza kutoka kwakwe, Kuna muda alikuwa anajistukia nakuuliza maswali ambayo ana majibu maana yeye ndo muhusika mkuu, ila alitaka ajue km amestukiwa, na mwisho wa siku  tamaa ilimzidi kabisa  nafasi ya uwanafunzi hakuithamini tena, utunza hazina hakuumtosha tena nahisi mbinu za wizi zilimwisha  (mi nami kwakuongeza chumvi duuu!!!ha!ha!ha!ha!)  jamaa akaona ajitose mzima mzima  Amuuze kabisaaaa Yesu  Ametisha eti eh!!!   HAKUNA JIPYA...............

Kuna kitu kingine nimetoka nacho hapa wakati Yuda hajielewi, Yesu alikuwa anajua anadeal na mtu gani.......... Alideal naye kihekima maana andiko lilikuwa lazima litimie......Kuna wakati alifadhaika (27 Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: Baba, usiruhusu saa hii inifikie? Lakini ndiyo maana nimekuja--ili nipite katika saa hii)  

Sikia nikwambie mpendwa  NDOTO yako ni nini???  Je wajua unauwezo wa kuizika au kuifufua?? Wa Kina Yuda hawajaanza kwako, walikuwepo na wataendelea kuwepo. Wamewekwa kwa Makusudi  na makusudi hayo ili ndoto yako ikamilike..............

Ntakuwa mchoyo kama sitasema na Yuda wa sasa ........ Tumeambiwa mwisho wa siku Yuda hakuona thamani ya chochote pesa alirudisha nakuamua kujipoteza kabisa. HAKUNA JIPYA  huwa wanaishia kuwa maloser

Habari njema ni kwamba hii nafasi ya Yuda nayo  sio ya lazima uibebe mpenzi, Huwa inakuja kidogo kidogo ila mmmh!! ukishakuwa level ya juu aisee kukutoa kazi .......  Chezea shetani akishakuwa amejipigia chata yake??? Ha!ha!ha! Jamani Imeandikwa walio wangu na wajua........ 

 Kajiushauri 

kabla hujalala we jipe nafasi hata ya Dakika mbili ujue siku yako iliendaje yaani lazima utakumbuka na utajitambua tuu km ulivyofanya  ulitumika au sio hapa pia panahitaji na uelewa na jinsi yakuchanganua mambo.... Ha!ha!ha!  mi  natabia yakupiga story na Baba watoto bwana kiukweli mi mwenzenu siri ndo sina ukitaka iwe siri basi Baba watoto awe anaijua ha!ha!ha! yaani km kuna kitu niliwahi lkumficha  mmmh!!!  kama ni dhambi basi  nahitaji maombi yenu ki!ki!ki!ki! sasa sometimes huwa nampa story, ili kunogesha najikuta naongeza na chumvi ha!ha!ha! sasa  nikishaanza kujitathimini mwisho wa siku naanza kusumbuka yaani utanisikia best ujue pale mwenzio niliongeza na chumvi ilikuwa hivi ila mi niliielewa hivi ha!ha!ha! ntajitetea hapo bora mradi nibaki na amani ki!ki!ki!

 So ni hivyo ndugu ukijitengenezea kamda kakujithamini sio rahisi ukafikia hatua mbaya yakukutoa kabisa na kukusahaulisha kusudi lako.

Halafu unajua nini ndugu zangu Mungu wetu ni Mungu wa rehema yaani anasamehe!!! anachotaka ni wewe tuu kujitambua baasiiii.......


Nawapenda mnoo

4 comments:

  1. Ni kweli kuna adui wa aina hizo, marafikiadui mi huwaita hivyo, wazee wa kusugarcot uovu, tuombe hekima kuwatambua na namna ya kuishi nao.
    Asantee kwa neno binafsi nimeguswa!!

    ReplyDelete
  2. Ni kweli Mungu an asame he mdd

    ReplyDelete
  3. AMINA mama wawili mungu akupe miaka elfu uendelee kutupa chakula hiki.

    ReplyDelete
  4. AMINA mama wawili mungu akupe miaka elfu uendelee kutupa chakula hiki.

    ReplyDelete