Pages

Ads 468x60px

Wednesday, October 1, 2014

MITHALI 31

Haya wapendwa wangu, Mwenzenu huu mlango wa MITHALI 31 hasa mstari 10-31 nausoma sana nakuupenda ila kuna mstari mmoja huwa natamani niuruke au ni ubadili (Sema tuu NENO LA MUNGU LIMEJITOSHELEZA haliongezi wa kupunguza its either a deal or not)yaani kila nikiusoma sijielewi, naunukuu "Tena huamka, kabla haujaisha usiku, Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula, na wajakazi wake sehemu zao" (Soma kuanzia 10 utanielewa)
Hili neno gumu mnoo kwangu ntalala hata saa kumi usiku wapendwa ukweli muda wa kuamka naamkia njaa tuu a.k.a natakiwa kwenda mzigoni simnajua ninavyopenda hela??? na hivyo siku hizi najiboss mwenyewe duu kwa ujumla mi sio mtu wa alfajiri.......

 Basi sasa hizi siku mbili nimejikuta nimekosa amani sana,hata sijui imekuwaje imekuja tuu bila hata kushurutishwa tena kama familia yangu naona wamelizoea mpaka hawajui kama ni tatizo............. nimejikuta kama sijakamilika kabisa!!! kuna kitu sijitendee haki kabisa , halafu mimi nimchelewaji  kwa hilo najulikana nahisi kwa watu wote walionizunguka halina ubishi........ nimewaamlia sasa we ngoja ha! ha! ha!

Sasa katika kujistukia leo tulikuwa tunatakiwa airport ( yes! tuko mafichoni tunasherekea birthday ya bidada).......

Mwanamke kwa mara ya kwanza au labda kwa muda mreefu sana nimeamka mapema andaaje familia huku nikijua nusu saa mpaka dakika ishirini kabla natakiwa niwe hapo....... kama wengi wetu tulivyojua maana huu mkasa umetupata wengi leo.

Njiani najisifuje jamani mwenzenu leo naona nimetendea haki huu mstari nina amani mnoo
duu!!! kufika tuu naambiwa tumechelewa option ni $480 na kupewa ndege ya masaa 4-5 yajayo. 

MIPANGO YOOTE YA SIKU IMEHARIBIKA ........... tuliishiwaje nguvu??? lakini kikubwa tuliamini ndivyo ilivyotakiwa kuwa na tulichukulia ile kawaida mara nyingi  huwa tunaenda tumechelewa (Africa time) lakini kabla ndege haijaondoka na tunaingia,  nakujiona kabisa nimefanya kauzembe somewhere.......

nilijitia moyo zaidi maana 
 Kuna watu kibao tumeachwa, nafikiri wahusika(compuni husika ya ndege) leo kuna kitu kinaendelea.............. kuna hii familia ya mtoto hapo chini wanasema wao kama kuchelewa basi ni dakika 2-3 badala yake wameambia walitakiwa wawe saa moja kabla anyway...........

Unajua kwa nini nasema ndivyo ilivyotakiwa iwe??? katika kufahamiana na kutiana moyo na wahanga wa tukio duuu!!! kuna mmoja amefunguka kitu ambacho kilikuwa kichwani mwangu lakini kwa namna nyingine ...........lakini yeye alivyokitoa bila kujua sisi tunakiwaziaje Jamani amenipa majibu ya mawazo yangu yaani sijui nisemaje!!! naamini Mungu aliliruhusu hilo kwa sababu na nikiliangalia sana kwa mapana na marefu kila kitu ni mpango.......................

Kumbuka nilianza kwa masumbuko ya moyo,nikafanya nia, nikaamini inawezekana...........................
na kabla yakujua mpango halisi ulikuwa nini, kumbuka nikakatishwa tamaa na kulambwa vidola vyangu ambavyo vilinipa uchungu wa Muda........ hasa nikijua nimefanya nafasi yangu kwa namna fulani,.........Guess what??? nilipoelewa kusudi nzima na labda mengine aliyoniepushia Mungu ambayo hayajanifunulia.

 NASEMA HIVI SIJAJUTA NA HATA HAYO MAUMIVU YA KIAKIBA CHANGU YAMEBAKI HISTORIA.............lakini lile nilipowe ndo kwanza niko excited kulifanyia kazi na nina amini ni daraja lakunipeleka kwenye moja ya ndoto zangu kama Mungu atakavyoruhusu.........

Haya basi huko juu kote ni longolongo zangu zakukuleta hapo kwenye kumbuka bila shaka kuna mtu atanielewa otherwise tuendeleze longolongo.........

Unajua nini tuligoma sasa hakuna kuondoka nikuzunguka humo airport mpaka hayo masaa 4-5 yafike, Simnazijua toto zenu dakika 5 kwao nyingi mnoo sembuse masaa, wakakutana na hiyo namba nyingine ndo balaaa
Camera yangu iliwakuta hapo wandugu ( sijui kwenu watoto wa mujini........ ila si wa shamba tunaamini mtoto ili asiuguwe  mweke kwenye mavumbi vumbi immune zake zizooe shida, Mzazi analima dogo kalazwa pembeni ya shamba.......... ila Toto za mujini mzazi akiona hivi fasta check up ya afya yake ha! ha! ha!


Vione visura vyao............. kujitetea kwingiiii

Finally we are here!!! (mashauzi +++ ushamba shurti kizungu eti eeh!!!) Nachangamsha genge mwenzenu  Maandishi mekundu ndo mpango

ugonjwa wa Mama wawili mweee!!!

 Nawapenda

JAMANI ILE TAFAKARI 2 MBONA NAKUWA MZITO KUILETA??? haya basi niambieni nyinyi mmejifunza nini juu ya ile topic ukiweza email halafu na mimi ntachanganya na haka kaufahamu kangu niitoe post au comment kwenye ile topic @list nijue naogopa kupoteza kondoo mwenzenu sambi sangu sinanitosha ha!ha!ha!


No comments:

Post a Comment