Pages

Ads 468x60px

Tuesday, March 11, 2014

SEMA NENO..........


 Haya wapendwa tafadhali sema neno tupone. Kama tujuavyo matokeo  ya kidato cha nne  yameshatoka. na matokeo ndiyo hivyo yalivyo kuna wale walifanikiwa na wale ambao kwa kweli hawakufanya vizuri. Sijui ni mimi au wote huwa naamini kabisa mtu huwa anahitaji second chance, huwasipendi kuuliza uliza sana ilikuwaje ,  najikumbuka mwenyewe kama nisingelipewa second chance sijui ingekuwaje???  hasa kwenye haya mambo ya shule na katika level hii. Utakubaliana na mimi asilimia kubwa kwenye hii level tulivuruga mnoooo. na wengi sio kwamba  walikuwa hawana uwezo wakufanya vizuri ila huwa kunakajipepo fulani kanadanganya  wengi kwenye umri huu nakusahau nini likupasalo kufanya, tena wengi ni ule umri unakuwa hutaki kuambiwa  unataka ujifundishe mwenyewe, ni neema sana kwa kipindi hiki kupata mtu wakutokata tamaa na kukubeba kwa namna yoyote ili uwe kwenye mstari..... nimejikuta nimetokwa hadi chozi  nilivyoandika NI NEEMA..... wapendwa naongea kwa uzoefu maana nimepitia hichi kipindi.

Nakumbuka mara baada ya matokeo nilijikuta nimerudi kwenye akili zangu nakujiona kabisa nimecheza pata potea. mbaya zaidi watu walishakata tamaa hawana mahesabu na wewe sasa nikipindi cha wewe kuwabembeleza ( dont take me wrong walikuwa wana timiza wajibu wao) na mbaya zaidi kipindi wewe unabembelezwa uwezekano wakufanyiwa chochote unachotaka upo ila hutaki kufanyiwa. kipindi kinapokuja  wewe ndo unabembeleza hata uwezo hao watu hawana  ila watajitahidi watakapo ishia......... piga picha  unapambana kurudi kwenye mstari kwa mazingira kama hayo na bado hakuna anaye amini you can make it!!!

 Naibarikiwe ile siku niliyopewa hiyo second chance aisee, ama kwa hakika ilibadilisha historia ya maisha yangu!!!!!( wengi huwa hawachezei second chance labda awe hajajitambua na hata kama haikuja kama alivyotegemea bado itatia matumaini fulani) . Mimi hapa ndo huwa najiuliza  maswali  kwa yeyote ambaye kwa namna moja ama nyingine natakiwa kumpa chance ya tatu. mara nyingi huwa natumia vigezo  vya second chance kama nitumike tena au nimpotezee.

 Baada ya kujieleza sana  nakuwatia moyo ni jinsi gani mtu anahitaji second chance tusaidiane hili

 Unataka kumsaidia Binti ambaye ametoka na zero.
 unaanzia wapi,  kumbuka  ni binti ambaye unataka kumvusha hili eneo  baada ya hapo hujui kama utaendelea au sio itategemea na Mungu atakapo kujalia. na jinsi atakapoitumia hiyo second chance.

 huyu binti ni yatima mwenye ndugu kama wewe,mimi na wengineo  ambao tutasaidiana hata kimawazo, yuko tayari hata kurudia form 2 ajipe mda mzuri. 

 Swali langu kama ni shule ni shule ipi huko Tanzania itamfaa, tunaipataje?? kutokana na mazingira ikiwezekana iwe bording. na kama una idea nyingine ni ipi? chukulia kama wewe ndo mtoa msaada kwa kuzingatia vigezo hivyo.Kama kwa namna moja ama nyingine una mtu wa dizaini hii mmemsadiaje????

MBARIKIWE

2 comments:

  1. yaani umentoa mpaka machozi we mdada,ckujui ila uminigusa sana nimetengeneza hadi picha ya sauti yako akilini kwangu naimagne tuko pamoja tunaongelea hili na mie yalinitokea mwenzio nikapewa na third chance,sasa leo zamu yangu harafu wazazi hawapo na wao wako wawil (twins)woote wana zero uwezo wangu wenyewe dah yaani basi tu maisha haya mwacheni mungu aitwe mungu

    ReplyDelete