Haya wandugu hili nimeona nililete tujifunze kitu, binafsi huwa kuna maandiko huwa ninayasoma lakini huwa sijakutana nayo kwenye uhalisia ingawa huwa naamini yapo........... kupitia hili kuna neno nimefunguka nakuliona katika uhalisia , mtanisamehe siwezi kuliweka wazi hilo neno kwa maana, naweza kuwa natoka hukumu wakati sistahili kuhukumu au naweza kudhani nimeelewa kumbe nimejidanganya............... Kikubwa nikujifunza kitu........ kama ulitakiwa kuwa kwenye huu ujumbe utanielewa na unaweza kufunguka ni neno gani au unaweza ukawa hujaelewa kama nilivyoelewa mimi lakini na uhakika utajifunza kitu.
Angalizo
Muhusika yuko radhi kutumika kama shuhuda ili mimi na wewe tupone. kikubwa ni mimi mwandishi kuwa na hekima yakulileta ambalo halitania kumdhalilisha.(MUNGU ANISAIDIE)
Ni hivi, nilipata maombi ya kazi kwa mtu ambaye kwa kweli nilistuka , nilitaka kujua kwa nini? maana akili yangu haikutaka kukubali kama muhusika anataka kazi yangu hasa kulingana na sifa alizonazo. nilitaka urafiki wa karibu sijui kwa nini nilikuwa nahisi kabisa kuna kitu natakiwa nijifunze kupitia yeye siku iliyoruhusiwa ikawadia na hivi ndivyo alivyoniambia....
Nina umri wa miaka arobaini, nina watoto wanne na mke, ni msomi ( GEOLOGIST) nina experience ya kazi ya miaka kama kumi na miwili, nimefanya kazi na kampuni nyingi na kubwa. tangu nilipomaliza shule kila nilipoweka barua yangu ya maombi sikuwahi kukataliwa ,tena nilikuwa nachagua ipi niende ipi nisiende.Nimeishi maisha yakujivunia sana na Elimu yangu sikuwahi kuwaza kama kuna siku Elimu inaweza kuwa pambo naisinipeleke popote. Sikuwahi kuwaza kama kuna kitu zaidi ya Elimu kikakufanya kuwa mtu.
Mke wangu ni mtu ambaye huwa anajishughulisha sana na mambo yakanisa, Nisikudanganye kuna mengi yalichangia kuweka chuki ila zaidi lilikuwa ni hili sikuwahi kuamini kama Huyu Mungu ni zaidi ya Elimu yangu, nakumbuka ni mara nyingi nimewahi kumwambia Mke wangu kama huna Elimu ndio uhangaike na huyo Mungu, maisha yangu kwa sasa simuhitaji huyo maana hawezi kunipa mahitaji yangu, na maneno mengi yakejeli niliwahi kuongea, lakini siku isiyo najina,
Nakumbuka nilimtuma mke wangu akanunue bia pub ( japokuwa alikuwa kanisani lakini tulikuwa tuna kunywa wote,tunagombana kiukweli sikuwa naona ushuhuda anaoubeba wa mimi kunitoa kuamini tofauti na nilivyokuwa naamini zaidi yakuhudhulia ibada).
Alichelewa kidogo mimi nilihisi tofauti na kwa sababu nilikuwa nimelewa kidogo niliamua kumfuata. Nilimkuta pub na kumnasa kibao mbele za watu, nakurushiana maneno ambayo waliona hawakupendezewa. kama ujuavyo sheria za nchi hii, mwanamke hapigwi hata kama amekosea hiyo kesi itakugeukia.
Taarifa zilifika ofisini kwangu kwa namna ambayo hata mimi sikuilewa na bila kumlaumu mtu, nilijikuta nimefukuzwa kazi kwa kosa hilo, niliondoka kwa majigambo japokuwa nipo kwenye record yakumdalilisha mwanamke nilijipa moyo kwa sababu nahitajika sana na baadhi ya makampuni bado hawata fuatilia hiyo record .niliondoka kwa kiburi nikidhani haitachuka hata mwezi ntarudi kazini.
kwa mara ya kwanza niligundua Mwanadam anahitaji zaidi ya Elimu. kila nilipo peleka maombi nimekataliwa,hata wale waliokuwa wananihitaji nakunitoa kwenye kampuni niliyokuwa mwanzo kwa dau kubwa leo hawanitaki hata kwa dau dogo. Nimejikuta nimeuza hata magari leo natembea kwa miguu umbali ambao sikuwahi kuwaza kuna siku ntatembea, miezi kumi ya mateso najiona kama nimeishi maisha haya kwa miaka mingi sana. nakataliwa na kupewa kejeli kila ninapoingia nakutoka. najikuta ninaishi kwa ajili ya hela ambayo mke wangu anapata serikalini lakini hiyo hela imejaa masimango, chuki, sioni nafasi yangu kama Mume. na wakati mwingine ananiambia niondoke. kila ninapojaribu kuleta amani ndani ya nyumba nakuonyesha upendo ninachopata ni majeraha na zaidi kukumbushwa ule uovu nilioufanya miaka mingi ya nyuma.
Sijajua kwa nini umenikubali nikajihifadhi hapa, Kila siku nnavyoondoka hapa huwa nakutafakari sana.....najipa moyo nakuona kweli Mungu anakupa adhabu,nakukusamehe. nahisi huu unaweza kuwa mwanzo wa milango yangu kufunguka!!!!!! ( ahsante sana Dada, umenisitiri mnooo) unajua, Huyu Mungu anachotaka ni mwanadamu kujitambua kwamba pamoja na yote bila neema yake wewe si kitu. kinachonishangaza ni kwamba huyu Mungu ni wa wote uwe udhambi au sio ila isifike mahali ukamtukana kama nilivyofanya mimi. najishangaa baada yakugundua kwamba hii yote ni kazi ya Mungu nimefikia mahali nimekubali kuitumikia hii adhabu maana, inanistahili ila siachi kumsihi Mungu anipunguzie maumivu ya adhabu hii maana kuna wakati nashindwa kabisa nasioni mwisho wake................akifuta machozi
Pamoja na kwamba nimetambua uweza wa Mungu my sister, Bado sijapata shuhuda ni wapi naweza nikakaa nikamwabudu huyu Mungu , maana kila ninachokiona mbele yangu kuanzia Mke wangu na wengine ni maigizo tuu!!!!!! na tena kama leo nikipewa nafasi kushauri pamoja na haya yote, siwezi kumruhusu kijana wangu au yeyote KUOA. ninachokwambia my sister,Hii adhabu ninayoitumikia na hii ya ndoa nahisi nikifa leo ntaenda mbinguni moja kwa moja sidhani kama ntapata adhabu nyingine( Wanawake wenzangu mpo hapo?????)
TUTAENDELEA............
Angalizo yawezekana nimeongeza au nimepunguza nimejitahidi kujiweka kwenye ile nafasi kama alivyokuwa ananielezea na kuileta kwa kiswahili,hapo ndipo nilipofikia naamini ungemsikiliza mwenyewe ni zaidi ya hii aisee.
Wacha nitafakari kwanza,nitarudi baadae! Maana haya ni mazito
ReplyDeleteDah nimekosa comment zaidi ya kuhisi uchun gu. Imeniuma sana.
ReplyDeleteNi kweli mengi nimejifunza kwa hili mmh
ReplyDelete1. Kumtii na kumheshimu Mungu bila kujali cheo au dhamana uliyonayo
2. Kutokua vuguvugu, kanisani upo lakini pia kwa mzee wa kiza upo
3."Kusamehe"wengi tunaliona neno hili lakini ni wagumu kuliishi
4. Kutambua kosa, kujutia kosa, kuhitaji msamaha na upendo wa kweli.
Haijalishi hadithi ya upande wa pili ikoje kubwa ni kusameheana na kuwa na upendo wa kweli.
Kuna lile neno mama wawili. Upendo hauhesabu mambo mabaya,..............tafadhali nikumbushe liko kitabu gani
Uwii, ni kweli binadamu huwa tunajisahau sana, ni bora umeweka huu ujumbe tujifunze kitu, ubarikiwe sana dada.
ReplyDeleteUwii, ni kweli binadamu huwa tunajisahau sana, ni bora umeweka huu ujumbe tujifunze kitu, ubarikiwe sana dada.
ReplyDelete