nimefanya kucopy na kupaste maana yamenigusa mnoo............ ushuhuda unajenga, ushuhuda unainua, hasa tukiwa tunapata kwa watuNtofauti tofauti na jinsi walivyopitia..................INAWEZEKANA KIKUBWA NI KUKAA KWENYE MSTARI NAKUJITAMBUA
KUNAKOPINDI WAKATI NAPITA MAPITO MAGUMU,, AMBAYO SINTASAHAU,,, WAKATI NATOKA KARIAKOO NA MIGUU NAKUJA MPAKA MAGOMENI NDIPO NAPANDA DALADALA ZA KUJA SINZA MAANA MFUKONI NINA MIAMBILI TU,,, NA KUANZIA MAGOMENI MPAKA MWENGE ,, WAKATI MWINGINE DALADALA HUWA MIA MBILI KABLA NAULI HAZIJA PANDA... WAKATI MWINGINE NILITEMBEA KUTOKA MORROCO HADI SINZA KWA MIGUU NA JUA KALI LIKINIPIGA,,,,, MARAFIKI WENGI WA KARIBU WALINISEMA VIBAYA SANA MANENO YALIYONIFANYA KILA SIKU NILIKUWA NAOMBA MAOMBI YA UCHUNGU SANA NA KULIA TU... KILA MMOJA ALISEMA LAKE,, OOH WAMBURA CHOKA MBAYA,,, WAMBURA KAFULIA,,,, YULE MWIMBAJI KWISHAA,, NIMEMKUTA ANAOMBA NIMNUNULIE CHAKULA.... NA NIKWELI NILIFIKIA HAPO PA WATU KUNISAIDIA ILA BAADHI WALIONISAIDIA WALINISEMA TENA KWA WATU,,,,,, HUWEZI AMINI WAMBURA KANIOMBA BUKU NAULI WANGU,,,,, HAHAAA,, NI KWELI SIKUWA NA UJANJA,, MAPITO YALIKUWA MAKALI MNO,,,,, NA KUMBUKA MUNGU ALIKUWA AMENIAMBIA NIITOE GARI YANGU NIMPE MTUMISHI FLANI NA NILIKUWA NAYO HIYOHIYO NA NILIFANYA HIVYO KWA MACHOZI MENGI NA ILIKUWA NI BENZI.... KUTOKEA HAPO HALI ILIKUWA NGUMU SANA ,,, NIKAWA NIKIMUULIZA MUNGU KWANINI NIKITOA NDIO MAMBO YANAGEUKA KUWA MAGUMU TENA ISAKA WANGU YAANI GARI LANGU MOJA ,, HILOHILO TU NILIKUWA NALO,,,, NIKAWA MTU WA KUPANDA DALADALA NA MWISHOWE NIKAWA MTU HATA WA KUKOSA NAULI NA KUTEMBEA KWA MIGUU NA MWISHOWE NIKAWA NIKIPEWA CHAKULA NA RAFIKI ZANGU KAMA,,, IMASON MWANA ZAMBE NA CHRIS'S MWASOTA WALIOJITAHIDI KUFICHA SIRI ZANGU MNO ZA MAPITO YANGU,,,, HAWA WALIUSIKA SANA KATIKA MAPITO YANGU NA KUNILIPIA NAULI KILA NIKIALIKWA KUIMBA NA HUKO NILIPOALIKWA NILIKUWA SIPEWI CHOCHOTA HIVYO ILIWALAZIMU KUNILIPIA TENA NAULI KURUDI HOME NA KUNINUNULIA CHAKULA........ NDUGUZANGU ILIFIKIA MAHALI NILIONA BORA NIFE,,, NILIKATA TAMAA YA KUISHI MAANA NILIKUWA MWAMINIFU KATIKA ZAKA NA SADAKA NATENA NILIFANYA NA ZAIDI,,, ILA MUNGU HAKUWA KIMYA BALI ALIKUWA AKINIRANDA........ NAWASHUKURU SANA IMASONI, CHRIS'S NA HATA WALE WALIONISAIDIA WAKANISEMA ,, WOTE ILIKUWA NI MPANGO WA MUNGU ILI LEO NIFIKIE MAHALI NACHAGUA GARI LA KUTOKA NALO ,,,,,,, NI NEEMA TU ,,, NEEEMA,, NDUGU.... LAKINI KWA USHUHUDA HUU NATAKA NIKWAMBIE WEWE ULIYEKATA TAMAA,, AU WEWE ULIYEDHARAULIWA AU WEWE UNAEPITIA MAGUMU NA UNAONA AFADHALI UFE,,, NAKUTABIRIA HUTAKUFA NA UTUKUFU WAKO WA MWISHO UTAKUWA MKUU KULIKO WA KWANZA,,, VUMILIA MAANA UMESHAFIKA KWENYE MLANGO WA JARIBU LAKO NA SASA UNAENDA KUTOKA,,,, ILA UWAPENDE WALIOKUSEMA VIBAYA NA USIWE NA KISASI JUU YAO,,, NAKUTIA MOYO SADAKA ZAKO HAZIJAPOTEA ZINASEMA MBELE ZA MUNGU NA SASA NI WAKATI WAKO WAKWENDA KUPOKEA..... MUNGU ANAENDA KUKUINUA MPAKA TUTASHANGAA... WANADAMU TUNAKUONA UMECHOKA ILA MUNGU ANAKUONA UNANGUVU,,,,, WANADAMU TUNAKUONA MASKINI NA UMEFULIA,,, MUNGU ANAKUONA TAJIRI NA UMEKAUKA..... PIGA MOYO KONDE,,, MWAMINI BWANA SAA YAJA NA SASA IMESHAKUWA........ KWA USHUHUDA HUU WA MAISHA YANGU WA KWELI NA KUTIA MOYO SONGA MBELE,,,,, NA USIACHE KUJA KWENYE MAOMBI TAREHE 1 PALE USTAWI WA JAMII TUOMBE ILI KIELEWEKE MWAKA UNAOKUJA.... BARIKIWA