Wadau kama mnakumbuka miezi michache iliyopita suala la yatima lilizungumziwa sana hasa katika blogs mbalimbali, kiukweli mpaka wakati huo nilikuwa sikuwahi kupata mzigo juu ya ibada hiyo ya yatima, yaani nilikuwa najua kuna yatima lakini sikuwahi kuumia sana kwa habari ya kufanya kitu juu yao zaidi ya wale walionizunguka mfano ndugu, nao sio kihivyo zaidi yakuchukulia km ndugu wasiokuwa na uwezo, Sikuwahi kujiuliza hawa watu km yatima wanatakiwa kuhudumiwa vipi, maumivu wanayoyapa, wanatofauti gani katika jamii na mambo km hayo, na cha ajabu zaidi hata katika kusoma kwangu maandiko nilifungwa kabisa ufahamu juu ya hili, nilikuwa nasoma tuuuu km gazeti lkn utendaji sikuwaHI kuupata.......
Nashukuru Mungu kupitia muda huo ambapo nahisi ndio ulikuwa wakati wa ufahamu wangu kufunguka kupitia blogS hizo. Ndipo nilijigundua mimi ni nani? na tofauti iliyopo kati yangu na yatima, na ninatakiwa kufanya nini juu yao japo kwa sehem fulani. Kwa kweli nilijikuta nina mzigo mkubwa sana kuna kipindi nilikuwa nasoma mpaka ninalia mwenyewe, nashukuru MUNGU niliweza kushiriki kwa namna moja ama nyingine.Cha ajabu haikuishia hapo nilijikuta nikiwaza sana juu ya hili, kuna wakati hata nilikuwa nawaangalia wanangu wakinirukia ,kunichezea na kunifanyia lolote ambalo litafanya tufurahi km familia, kitu kilinikumbusha kuna mtoto yupo mahali fulani hajawahi kuona hata jino moja la mzazi tena hajui furaha ni nini ktk maisha yake. Kwa kweli inaumiza wapenzi.............
Jamani nikitaka kuzungumzia how i feel!!!!!! kwa kweli ukurasa hautaishia.Mwezi uliopita nashukuru Mungu nilifanikiwa kuja bongo japo nilikuja kwa majozi yakumpoteza baba mkwe wangu( REST IN PEACE MY FATHER) Lakini nilijifunza kitu jamani,!!!!!!!!! nikiwa bado akiri yangu haijatulia juu ya yatima nilikuwa tayari kuna kitu ambayo tulikuwa tunasave km familia, Tulianza kufanya research ni wapi ambapo panastahili sisi tufanye kitu na hatukutaka kwenda vituo ambavyo viko popular coz tulijua hivyo huwa mara kwa mara vinapata kitu japo bado niwahitaji.ndugu zangu kunastory huko uuuuwiiiiiii!!!!!!!
Mmmh hivi km kweli hakuna dhambi kubwa wala ndogo jamani......HII NI LAANAAAA kweli unafungua kituo misaada unayopata haifikii walengwa!!!?????? pesa unatumia kwa mahitaji yako unaacha viumbe na njaa!!!???? vyakula vinaletwa walezi mnapeleka majumbani mwenu na viumbe vinateseka na njaa!!! ???????yaani we binadamu wa dizaini hii uuuuwwiiiiii!!!!!!! ndugu yangu kweli kweli umeamua kuwafanyia biashara viumbe hawa?????? kweli najua kuhukumu na kulaani si kwangu ila naomba utambue hukumu ipo na laana ipo na lazima ioneka kwa macho, malipo ni hapa hapa ndugu yangu, Kweli hakuna mkamilifu chini ya jua lakini.................we haya.
MTAZAMO
Kwa ndugu wote ambao mnaguswa na yatima na mnaguswa kufanya jambo kwa ajiri yao msikurupuke tuuu kwa sababu nikituo kwani unaweza kujikuta hujafikisha lengo, japo kuwa kule kuwaza tu, kwaajiri ya yatima nakufanya kitu halafu watu wenye mikono mirefu wakakwamisha lengo MUNGU akubariki sana.PIA tukumbuke"WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA" Haisaidii km unatoa huku unajua kuna utapeli utafanyika,Yaani chunguza sana kwa kweli ikiwezekana omba Mungu akuonyeshe ni wapi unatakiwa kwenda ukiingia kichwa kichwa wanahadithi ndefu sana hao,NAWAOGOPA SANA KWA KWELI SIJUI UJASIRI WANAPATA WAPI???????? hata km maisha magumu mmmmhhhhh!!!! hii kwa wale ambao wanajikongoja km kinasie uwezo wakuwakusanya au kuchukua hata mmoja kukaa nao wenyewe kwa sasa hatuna ILA, kwa wewe mwenzetu uliojariwa hata kumchuka mmoja au zaidi na unauhakika utaweza kwa kweli mchukue........ Hawa watu niwahitaji kwa kweli na pia jikaguo usije baada ukaingia tamaa na kufanya km hao tunaowazungumzia maana naamini wengine walianza kwa kupondeka hivi hivi lkn roho za tamaa badae zikawaingia.
ANGALIZO
1. Sijasema vituo vyote ni vya kitapeli, Kuna watu kweli Mungu awabariki sana kwa kazi mnayofanya kwa mda mfupi nimeona magumu mnayopitia lakini mmeweza kuthubutu, kweli ni roho yakipekee sana na Mungu anatambua hicho mnachokifanya msikate tamaa.
2.Sijapigia debe kituo chochote wala sijasema nilipoenda mimi ndio perfect or not. na popote nilipofika au kuulizia lakini sikufanya chochote sijasema ndo nyie wenye midomo mirefu hapana,km nilivyosema mwanzo kuhukumu si kwangu lkn ukidanganywa km uko makini utastuka tuuu.
3.KWA HILI SITAFUTI SIFA ILA KUNA WAKATI INABIDI TUAMBIZANE KUTUMIA MIFANO HALISI ILI TWENDE SAWA.( NATAMBUA UNAPOTOA SADAKA USITAKE MKONO WA PILI UTAMBUE UMETOA NINI) NA PIA JIULIZE, BILA MTU MMOJA KUSIMAMA NA KULIZUNGUMZIA HILI SUALA MIMI MAMA WAWILI UFAHAMU WANGU UNGEBAKI PALE PALE HATA LEO HUU MTAZAMO NISINGEANDIKA.
IN GOD WE TRUST