Pages

Ads 468x60px

Wednesday, September 30, 2015

HAMICY & FATMA DAY..................


Wandugu hebu niwaonjeshe na nyie khaa!!! mwenzenu nimetumiwa na shemeji yangu hizi picha zake za big day  all the way from London(harusi imefanyikia Bongo)........... ameamua kunikomesha ha!ha!ha! maana ilikuwa tukikutana tuu kwenye maongezi or chatting zozote lazima niulize lini sasa???? maana tunangoja sana watu tunataka wake wenza ha!ha!ha!   

Ahsante kwa kunikomesha........ Kumbe ile Shemu, we tulia mambo yanaiva habari ndo hii???? Nimenyoooka ha!ha!ha! kweli huongopi Fatma mama we ni mrembo.........!!!!

Wow!!

mkalitunze hilo tabasamu wandugu na Mungu akawapiganie ya walimwengu.....

Raha sana yaani......

Achana na urembo pia ulipendeza mnoo ulijitendea haki.....

Nimependa hizo colour mix




 duu!! naona ntakuonea Londona soon mamii ha!ha!ha! 
Ahsanteni tumekoma..........Mmependeza mnooo!!

Karibuni kwenye ulimwengu wa ndoa.

Monday, September 28, 2015

CAREEN'S 7TH BIRTHDAY PARTY..................

Wandugu mapicha ni mengi aisee ngojeni muonje tuu ila ki ukweli mwanenu siku yake kweli alienjoy............ na Mama mtu sasa akili imejiridhisha kwamba nina mtoto wa miaka saba ha!ha!ha! sijui hii miaka imekimbiaje!!!! ila kikubwa Sifa na utukufu namrudishia Mungu.

khaa!!  nimejizalia mwenyewe huyu wapenzi.........


na zawadi yake imekuwa revealed ha!ha!ha!(quad bike) mjiandae sasa mapicha yakuride around the beach maporini huko (nature)  we go mean business
roho yangu namwangalia simmalizi aisee

 mmh!! shida mnao mbona ha!ha!ha!

game room nikatoa makororo yote nikafanya ndo sehemu yao yakulia ha!ha!ha! ubunifu kipaji ....

Wawili wangu 

sweet corner nayo ilikuwepo
roho zangu yaani nilikuwa sipati view nzuri kwa kamera ila kajieneo haka kwa macho kalikuwa katamu.... mama misifa kujisifia ha!ha!ha!

princesses....
am blessed!
too cute....

kazi hizi zote wandugu ni za mikono yangu kwa usaidizi mkubwa wa Baba wawili nilifanya kuhire tu vitu ..... 
nalalamika tena kamera haikunitendea haki...... hii view kwa macho ilikuwa nzuri imeingia mpaka kule jikoni ,upande wa pili view ya swimming pool kupitia dirishani ilikuwa balaa then dirisha la upande wa pili ulikuwa unachukua view ya nje aisee palinoga mnoo.........

nilikuwa nawatoto ishirini......
haya garage yangu ya magari ndo nikadizaini uwe ukumbi wa disco..... disco disco haswa yaani mataa  yalireflect vizuri sana............(chezea kupania wewe ubunifu lazima) nilikumbuka enzi zileeee ha!ha!ha!ha!

ila sema ndo nilikuwa nakazi mara watoto wengine wako vyumbani, mara nyuma ya nyumba,mara...............yaani security mwenyewe,mtumbuizaji mwenyewe,.........,........,........, Baba wawili msaidizi ndo maana niligoma kupika nilihakikisha vinywaji vya kutosha, nika order pizza na macdonald mchezo ukaisha ha!ha!ha!

basi tena akafungua na zawadi zake ambazo alizifurahia mnooo.........

tunawapenda

Wednesday, September 23, 2015

TUZUNGUMZE..........


Shughulini kama kawa ha!ha!ha! Eti wadau, hivi mmegundua kila nikipost picha za mialiko nakuwa na team tofauti tofauti??? haya basi, Kiukweli sina sina team ila nimezungukwa na watu na team zao...... I treat kila mtu sawa yaani.... sina mwandani wala so called rafiki msiri. I can guarantee  when i go out there kuna watu wanaweza kuwa wamejazwa ujinga unaonihusu and sometimes they all got it wrong...... But hey! i will never ever give them my air time kuniambia au to prove them wrong or right aisee......... kuna mahali utaona tuu ile introduction km watu wanategemea more than just a simple intro, yaani walikuwa wana hamu wakuone kiuhalisia ha!ha!ha! Dont get me wrong sometime huwa wana good news ambazo wanatamani kunisikia mwenyewe but hey, i think we should respect  muda wa kusocial..... who wants to hear who is who, what she is doing,and................... jamani mi kila siku nasema facebook acha iwe facebook, mabox yaishie maboxini, yawapendwa nayo yawe yakipendwa ha!ha!ha! japo injili inatakiwa ienezwe ila hekima muhimu aise huwezi ukaenda shughulini ukakuta watu wamenogewa na Mwana ya Alikiba gafla ukawastopisha nakuanza kunena ha!ha!ha! Duu!! bwana wee...... sio mbaya kuwepo ila roho mtakatifu havami vamia ovyo kha!!we cheza mwana ila maintain ile kitu ya ndani uliyonayo maana hiyo ndo muhimu .............so km kuna umuhimu i always carry my business card au km unanihitaji kwa mambo yakwaida nitakupa my personal mobile, km uko serious tutatafutana.

Napenda kusocial baada ya mabox......... yaani humu ndani mwangu nikiwanunia huwa wananifukuza hawachelewi kuniambia kwani huna mwaliko ha!ha!ha! maana wanajua huo ndo muda wao wenyewe kufanya yao na hata nikirudi nimesahau kila kitu naanza kuwapa mastory yaliyojili ha!ha!ha!.............  thank God team zote(zilizo nyingi nisijifagilie kha!) wakiwa wanavishughuli they count on me ha!ha!ha!  ila nikigundua km nakuja  kwenye shughuli itakayokuwa  kuna kuonyeshana vidole sijui nini na nini,  au mtu lazima ujistukie kila sentesi utakayotoa kisa watu wataichukulia tofauti....... aisee huko hamnioni yaani, ntapata tuu sababu ambayo itahakikisha haijamkwanza aliyenialika basi..........Jamani achana tuu na wokovu tumezeeka sasa kha!!!  why wasting time kwenda kutafuta madrama ambayo  ulikuwa na nafasi yakuyazuia.........

 By saying this wapenzi i dont hate, yaani mi ninatatizo moja yakusahau makwazo...... kuna wakati hata nikitaka kujikumbusha why sikumbuki hata moja ha!ha!ha! Mweee nimekumbuka siku moja bwana, miaka hiyooo niliwekwa mtu kati aisee nilisutwaje sasa.....kha!!! maana wenzangu wanakumbuka A-Z mama wawili hola najitahidi kujieleza mwenzao wanielewe duuu!!! niliishia kulia mweee!! walinisondaje sasa eti najifanya kulia!!!! kikikiiii(true story)

 So kwa sababu ya mapungufu hayo niliyonayo, huwa mzuri sana wakuchukua pre caution. napenda kuwa na distance relation na watu wa dizaini fulani fulani, huwa naamini hakuna aliyemkamilifu sote tuna mapungufu, na pia kuna watu ambao its hard kuwa na meeting nao za mara kwa mara. few hours after months or year/s zinatosha just to maintain ile respect na kutokumruhusu shetani kutumia yale mapungu yenu mliyonayo................

Yaani kuna watu i must admit my heart is crying for them yaani, nawapenda mnoooo, yaani hata nikisika kuna kitu kimewapata aisee muulize Baba wawili i can even try to help @ my best  bila wao kujua.... huku najua the fact kwamba, them people hawaelewi how i feel na labda they think am one of their worse enemies.............yaani hata ikitokea tumekutana thank God i can fit and tolerate mazingira ambayo i know one of us can fake just to keep up na hayo masaa machache yaliyotulazimu tuwe pamoja, though nikirudi nyumbani huwa naumia sana why we had to do so???? mwisho wa siku Mungu ndo anaembadilisha mtu its either mimi mwenyewe ndio tatizo,mwenzangu au sote. na Binadamu tunatofauti.

hee eti leo nimeandika hahahaa hata sikutegemea eti imebidi nibadilishe hata tittle iwe tuzungumze sasa.

  onjeni tuu km kawa wale wa facebook mshaona tukio eti eeh?



unywele unachachamaa tuu.... no makorombwezo wala nini . Ni kuoga, paka mafuta yakupikia chana zikiwa mbichi mbichi zikiwa kavu zinaumaa so km na haraka nachukua kitaulo kibichi kidogo navuruga zinakuwa km dreads ready to go.



Nawapenda

Monday, September 21, 2015

HAPPY 7TH BIRTHDAY TO MY PRECIOUS DAUGHTER........

Haya wandugu mwenzenu ndo nshaitwa mama wa binti wa miaka saba!!! Jina la Bwana libarikiwe............... weekend tuliona  ngoja tumfanyie ka family pre birthday kabla ya birthday party yake coming weekend. haikuwa special sana lengo ni kwenda kujificha anapenda sana maficho aisee km Mama yake ila sio kila maficho ha!ha!ha! kana taste za hatariiiiiii............ha!ha!ha! tulikapatia ila mwisho kalilamika why we didnt let her use most of the hotel facilities.... muda haukutosha alitakiwa leo aingie darasana.

onjeni machache yaliyojili......


kamekuwa jamani mweeee......


humu ndani ndo ilikuwa home picha niliyopigia hapo haikutenda haki tochi ilihusika so nimeamua kuiba kwenye website yao kuileta ha!ha!ha!ha! 
nani yule kule spotted????

na hawa unawafahamu kawatag basi ha!ha!ha!

roho zake Mama wawili

spotted watching TV in a room

my fav spot in the room, Amazing view..........


haya nimewatangazia na biashara sijui watanilipa??? kawatag basi ha!ha!ha!
twenzetuni kitaa wanangu, sameheni hizo kauka nikuvae jamani zimevamiwa ha!ha!ha!


she got her wheels............ to be revealed on her birthday party ha!ha!ha! natafuta masponsor kwanza.

Tunawapenda

Friday, September 18, 2015

SIJAANZA LEO MJUE????............



Hahahahaaa leo mwenzenu nimetumiwa hizi picha yaani hata sikumbuki matukio ila dah!!! kweli amenikumbusha mengi mnoooo basi tuuu.......

 Mapicha sijaanza leo mjue???  lets flash back


bagi swags are for real kikikikiiiiiii

jamani najipendaje sasa kha!!!

Wednesday, September 16, 2015

MAMA WAWILI..............


Wiki ijayo mwenzenu ntakuwa Mama wa binti wa miaka saba ha!ha!ha! kweli miaka inaenda before you know uzee huo hahahaaa! sasa huyo birthday girl anavyonishughulisha mweee........


na ubora wangu



sijui hata nilikuwa nafanyaje hapa khaa!! ila ndo nimejisikia kupost

niko busy na birthday girl msinitafute kikikikiiii

Monday, September 14, 2015

ONJENI........

Mkiona picha hazieleweki mjue nilialikwa mimi na camera yangu............... Dakika za mwishooo ndo huwa najikumbuka ha!ha!ha! mbaya zaidi huwa mchelewaji hata muda wakujipiga ze look kabla kuondoka huwa sina....... basi sasa ndo mnionje kihivi............Wale marafiki zangu facebook bila shaka mmeliona tukio ha!ha!ha!

na chizi langu mwenyewe lakizambia........




maelekizo yakushika Camera ..........maelekezo yenyewe yakizungu kha!! Mama wawili lazima mikono nayo inisaidie  ki!ki!ki!kii

Nawapenda