Pages

Ads 468x60px

Tuesday, December 30, 2014

LATE POST..........

Jamani siku zinakimbia duuu!!! sitaki kuamini tumebakiza masaa eti????? Kwa kweli ni kwa neema!!!!

 Haya naona matukio mengine yatakuwa so 2014 tuyapotezee tuu ngoja tulimalizie hili......... Sasa basi wenzenu sijui ndo ushamba au ndo sio watu wakujipanga hata hatujielewi.... Tulikuwa tuna sehemu kadhaa ambazo tulijisemea Mungu akitujalia tutaenda kusherekea Christmas huko .... so hata mialiko tuliyokuwa tunaipata miezi miwili kabla ya wenzetu ambao huwa wanataka kujua nani mgeni atakuwepo ilibidi tuwambie hatuta kuwepo...........

 Tukaendelea na mabox kama kawa, wiki mbili kabla ndo tukaanza kujua ni wapi kati ya kule tulikotegemea kwenda  na tuna uwezo nako maana sehemu ni nyingi  mshiko nao lazima uhusike ha!ha!ha!ha! so kabajeti kakawa kanaruhusu sehemu fulani .... heee ile kupiga simu ni full kujaa tena unaambia till next year duuu!!!!

 Isiwe shida!!! tukaona tutajiachia humu humu ndani kwetu ila kivipi??? Ha!ha!ha! ile mialiko ya too late tukaanza kuipokea sasa wee ilituwekaje busy??? sasa kuna Mualiko mmoja tulikuja kubebwa kwenye basi kwenda kuzunguka  kuangalia watu wlivyopamba nyumba zao Christmas lights duuu!!! nyie kuna watu wanajua kusherekea aiseee!!!! 

Hapo ndo makelele yalipoanza ndani mwangu........... Mum&Dad why dont we have a christmas tree in our house??? ni why?why?why? mpaka mzazi unaanza kujistukia ha!ha!ha!Hapo ndo tulipopata idea  nini chakuwafanyia ili wajione hata nyumbani kwao kulikuwa na christmas.

So siku mbili kabla ya christmas nikaenda nao duka moja tuu ambalo nilijua ntapata kila kila kitu watakavyopenda, nikawambia lets make a list just incase Santa anakuja nyumbani kwetu tumuombe atununulie nini.......... Walichaguaje sasa hivyo vikololo?? nikabahatika kupata na haka kacheap Christmas tree .............. hao Tukarudi zetu nyumbani.

Shughuli kesho yake Mama mtu nikaenda kuvinunua nikarudi kuvificha. Siku ya christmas tumerudi tulikotoka usiku mweee !!! ikabidi tuwambie guys mnatakiwa mkalale saa hizi, ili tuwahi kuamka kesho ndo Siku ya Santa kuja (BOXING DAY) Ha!ha!ha! 

Shughuli ndo tulikuwa nayo sasa na Baba mtu tumekesha kufunga hivyo vizawadi, kuja kustuka  saa nane usiku,nilisahau kununua Christmas light duuu!! na maduka ndo washafunga. Ha!ha!ha!

 Basi sasa sisi hao kulala kumbuka masaa 4-5 kuna watu wataamka huko kumuwahi Santa Duuu!!! aisee nahisi ndo nilikuwa naanza kupata usingizi Mara Makelele hayo yanakuja chumbani kwangu Mum &dad,Mum & Dad  amkeni, njooni muone Santa ametuletea............(in English though ) yaani!!! unatamani upotezeae sema ndo hivyo inabidi uwajibike ha!ha!ha! 


 Yes walifurahi mnooo........ ila mwisho wa siku niliambiwa Mum i think santa forget to put the Light ha!ha!ha! Nikawambia nafikiri ameacha ili Mum & dad wanunue. So maduka yalipofunguliwa Baba yao alienda nao kununua hizo taa zakizushi zimeshukaje bei sasa????? na vijipambo kidogo . wakaja nyumbani na wao wakijisikiaje raha kuupamba mti Ha!ha!ha!

 JAMANI WATOTO WANAENJOY VITU VIDOGO MNOO ............. SA NYINGINE HATA HUWEZI KUVURUGA BAJETI YAKO............KIKUBWA NA WEWE JIWEKE WEKE KITOTO TOTO HIVYO HIVYO HASA KIPINDI KAMA HICHI 




ndo mjue story ya camping ilipoanzia......

 Wamesema Santa amewapendelaje sasa kila walichoweka kwenye list amewanunulia ha!ha!ha!


 hivi kwani miavuli humu ndani hamna hao ndo watoto bwana ????


Kweli Santa is the Best Ha!ha!ha!ha!

 Baba wawili katisha eti na mimi mpenda Nandoz zawadi zangu ndo hizo ha!ha!ha!ha!

Tunawapenda

No comments:

Post a Comment