Nimemaliza sehemu ya kwanza ya kitabu, Pamoja na yote kuna hili nimeona niwashirikishe.............
Anasema, kuna siku walikuwa na Dada yake mahali fulani, waliamua kwenda kujificha kwa muda baada ya muda mrefu wa maisha kuwatenganisha(umbali na majukumu). Moja ya maongezi yao ndani ya siku hiyo ilikuwa nikukumbushia jinsi walivyokuwa walivyolelewa,nani aliwafanyia nini,na vitu km hivyo............
Maongezi yao namapokeo yalikuwa yanagongana kidogo ,hasa pale mmoja wao alipokuwa anakumbuka mambo yalioyomuhuzunisha,nani alimdharau,nani aliyemwambia maneno yanayomfanya ayakumbuke mpaka leo na kumjeruhi........Kitu ambacho kwa mdogo mtu(mtumishi) kilimpa wakati mgumu kila alipojaribu kufanya ushirikiano na Dada yake kwa wakati huo, ilikuwa bahati mbaya maana hakuweza kukumbuka na kama akikumbuka anashindwa kulielezea lilianzaje nakuishiaje hivyo ilimbidi awe anamuuliza Dada mtu, Hivi alivyosema vile ilikuwaje?alianzaje,Ulimfanyia nini, na mengineyo ili tuu, ajaribu kufanya ushirikiano........... Haikuwa kama alivyotegemea zaidi alimfanya Dada mtu akasirike nakumuona anaigiza mwisho wa siku alijitahidi kujitetea.............. Dada mtu akamwambia UNAJIFANYA UMESAHAU SAWA NDIO MAANA ULIKUWA UNAITWA PRINCESS...............PRINCESS ni jina alilokuwa anaitwa kama nick name akiwa mdogo lakini hakuwahi kulitumia kama jina. Mara baada ya Dada mtu kumkumbusha alijikuta ameingia kwenye tafakari ..................... Mwisho wa siku akatunga kitabu kinachoitwa PRINCESS.
Niliwahi kuzungumzia hapa kwa habari ya kubeba mizigo, maumivu,masimango,makunyanzi ambayo yametukwamisha sana katika kutimiza ndoto zetu.Tumesahau kwamba Imeandikwa
Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.
19 Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.
Wapendwa wangu kama tusipojifunza kuachilia........
Majibu ya ndoto yako yanaweza kuwa ni hadithi za kale,
Tunajifungia milango sisi wenyewe wakati mwingine
tunaamini Mungu amechelewa kutujibu ,kumbe ni sisi
wenyewe tumekaa mlangoni, tumejizuiya.
Wapenzi wangu kama nimidomo ya watu basi huwa nahisi
leo nisingali kuwa hapa, Kusudi la Mungu ndani yako
aliharibiwi na Mwanadamu awaye yoyote............. Niliwahi
kusema hapa Mama alivyokuja kuna vitu alikuwa
ananikumbusha tena hasa kwa wale ambao kwa sasa ndo
tuko karibu mnooo!!!! Kiukweli na mimi nilijikuta naingia
kwenye shida kama mtumishi hapo juu, (Namuelewa kama
mzazi ni jinsi gani aliumia hasa mtu alipomzungumzia
mwanao negative).
Ninachotaka kusema Damu ya Yesu imekusafisha huna
haja yakutafuta tafuta laana yako imetoka wapi
TAZAMA NITATENDA NENO JIPYA.
Tumia muda wako kumuuliza Mungu kwa habari ya kusudi la maisha yako.
HUJACHELEWA WAKATI NDIO HUU..........
NAWAPENDA
Hivi ni kweli Rose?
ReplyDeleteMi bado naambiwa laana yako yaweza kua ni toka vizazi vinne nyuma yako.
Mungu atusamehe