Mi mwenzenu ndo nishaimaliza.......... Kiukweli being a mother is a greatest privilege of all!!!!! hata sijui nisemaje??? mbarikiwe all mothers out there. Tukumbushane tuu Wamama wote hili ni Jukumu aiseee, Leo tunaitwa kina Mama kwa sababu kuna waMama waliokubari kutumika kutuandaa hivi tulivyo, Mungu atusaidie na sisi kuwaanda wa Mama wajao haijalishi una watoto wa jinsia gani ( kuna huu msemo unasema mtoto wa mwenzio ni wako) .........Jamani huwa sielewi kabisa Mama anayemfanya katuni ,nakumchambua mtoto wa mwenzie tena malaika hata asiyeelewa chochote aiseeeee!!!!Hasira za wazazi unazipeleka kwa mtoto weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!! Narudia tena Mama ni jukumu na hilo ndio lililokufanya leo uwe special.Tuangalie sana kile tunachotamka kwa mtoto wa mwanamke mwenzetu hasa hawa wasioelewa kitu wandugu. oooh!!! Sorry wandugu nimehama gafla ha! ha! ha! haaaa.Hisia zimenijia unajua tena UMAMA.........
Wapendwa wangu woote mnaowish siku moja kuwa waMama, Mungu akaikumbuke haja ya moyo wenu Amini ipo siku na wewe utaitwa Mama. Sawa, Doctor amekwambia haiwezekani hizo ni sauti tuu za wanadam zinazokuthibitishia Wanadamu wanakikomo,usitegemee akili za mwanadamu yupo Mungu aliyesema hakuna Tasa,Neno lake huwa halijipingi yaani ni kweli na amina.Achana na historia tuingie kwenye uhalisia. naelewa ni neema kuhamisha akili na kuamini haya ninayokwambia maana hata Sarah alisema Alicheka na kusema LITAWEZEKANAJE JAMBO HILI???? nimeshudia watu waliambiwa Haiwezekani na ikawezekana. Wanadamu hii ndo asili yetu maana nakumbuka hata baba wa Yusufu alipopelekewa lile gwanda la mwanae alichoamini ni kile alichoambiwa, sidhani kama hata alikumbuka kwenda zaidi ya pale, hata kutaka kujua eneo la tukio ili japo akaone hata mfupa, basi hata nywele iliyodondoka ili kuthibitisha kile alichoambiwa na kuona.alichoishia ni kuomboleza na sidhani kama aliamini Bwana ameruhusu kwa ajili ya utukufu wake.................Hebu tuombe neema itakayotuwezesha ku AMINI,AMINI,AMINI INAWEZEKANA . ondoa hicho kipingamizi kinachozuia kutokuamini kwako ili uruhusu ile Nguvu na mamlaka itende kazi. Wandugu haya mambo yakiroho yanategemea sana nakuamini kwako.
HAYA BASI NAWAPENDA MNOOOO.
lunch @Nandoz.............kijiwe chetu mara nyingi siku za jumapili mchana
About to go......
Mama wawili.
Jamani My Christabell ujanja woote huwa hawezi kunyosha kidole gumba kama baba yake hapo ukimstukizia atahangaika dakika kadhaa. ndicho kilichomfanya Mama wawili acheke mpaka Pengo lionekane.
ukimzingua sana anakasirika ha! ha! ha! Dad anasema mwache afanye mwenyewe Mama huruma tena ha! ha1 ha! ha! uMama tena.........
Mtoto mkubwa amewakilisha kikweli ukweli aiseee.Alijitahidi mnoo kuwapanga wanawe na kufanya vitu vilivyonifanya kweli nijivunie kuwa Mama.AM VERY VERY VERY PROUD OF HIM. Yaani hii week nzima wanake wanavyorudi na vizawadi vya Mother's day (sijui wenzangu na nyie yamewakuta???mimi mwenzenu nimeletewa michoro miingi kuanzia jumatatu hata mingine siielewe zaidi ya pale walivyoandika Happy Mothers Day na kiss kiss tuu meeengiiiii.......Walimu nao walikuwa na shughuli kweli kweli duuu!!!!) sasa Baba yao anavyojitahidi kuwaelimisha waelewe nini maaana ya siku. Asubuhi mwenzangu kawahi kuamka na wanake mi naamka watu wameshajiandaa na kunisuprise tuuu. NIMRUDISHIE NINI HUYU MUNGU KWA WEMA NA FADHILI ZAKE?????
Mutu na Mama ya watoto yake..........
The End.........
Barikiwa dada, nimependa staili ya nywele ya watoto.
ReplyDeletependeza sanaaaaaaa
ReplyDelete