Leo naomba nizungumzie hili, mimi sio mzuri sana wa madhabahu, na nina amini hili likimkuta mwenye kalama ya madhabahu angelizungumzia vizuri sana, lakini hivi ndivyo ilivyo, sijui kwa nini niwe mimi leo, nimejitahidi sana kujizuia nikidhani sio fani yangu nimejikuta nakosa amani. Ngoja nilitendee haki hili sumbuko la moyo wapendwa........
Mwanadam hajakamilika kila siku ntasema, hakuna aliyemkamilifu hata maandiko yanasema, ashukuriwe huyu Mungu anayetupa msamaha. Yeye pekee ndiye anayesamehe na kusahau bila kuangalia ukubwa wa matatizo yetu (HATA KAMA DHAMBI ZENU NI NYEKUNDU KAMA DAMU ISAYA 1:18), sijui kwa nini watu tumefungwa hili eneo,nitakupa kajimfano unielewe natokea wapi,
Ni hivi nimeona wengi kwa namna fulani na mazingira ambayo hayakutegemewa tumejikuta tumefanya agano, na hata mara baada ya kugundua badala ya kurekebisha tunaona ni bora tuendelee kuitetea ile dhambi kwa kudhani, kama tutarudi kwenye mstari jamii haitamuelewa. kwa mfano,
Wengi wetu tumejikuta kwenye mazingira yakumsengenya mtu, na wakati mwingine hata kushiriki dhambi ya uzushi kwa ajili ya mtu fulani. kuna kitu nimegundua kwenye ulimwengu wa roho mara nyingi kuna yule ambaye anatumika kamili na anajua anafanya nini, na kuna wewe mwenzangu na mimi hujui kama mwenzio yuko kikazi,analeta story ambayo kwa namna moja ama nyingine utajikuta na wewe umetia neno ( ipo hiyo sana tuu kama mwanadam wa kawaida)..... kinachonifanya niseme ni baada ya hilo tukio na kugundua ulikosea.
Labda kwa sababu ya nguvu fulani iliyotumika muda huo, au ni ubinadamu tuu wa kawaidi ukajikuta umeingia kwenye hilo agano......... wengi wetu hapa huwa hatuwezi kutoka!!!!! kila unapowaza kujifungua kwenye hilo agano unawaza mahusiano ya wewe na yule aliyekusababisha ukaingia kwenye hilo agano( bila kujua mwenzio yuko kazini), na wakati mwingine hatuko tayari ile dhambi ikawa wazi hasa tunapoamua kutengeneza, unahisi mwenzio ataamua kuweka ile dhambi wazi na jamii, au yule muhusika mliyempikia jungu kugundua yaliyojili gizani. Mara nyingi watu wa dizaini hii huwa tunakosa maamuzi binafsi. tunaanza kuishi maisha ambayo kiuhalisia tusingependa, kifungo kimebadilisha uhalisia wetu. na tena mara nyingi yule aliye kikazi kuwa anakuwa msemaji mkuu wetu. usipo jielewa hii hali inatesa mnooo.
Leo nimeona tukumbushane wandugu msamaha upo....... hakuna namna yoyote ya dhambi iliyopita kukufanya upoteze uhalisia wako kama wewe mwenyewe hujaruhusu,ukifanya amuzi la kutengeza Mungu lazima atakupa na hekima yakuikabili aibu, na masimango ambayo hauko tayari kuyapokea kwa sasa.
Nakubaliana na wewe maagano mengine ni mazito mfano labda ulijikuta umetoa siri ya Mumeo, mkwe, mawifi ambao unahisi endapo mumeo atasikia hilo nyumba itawaka moto. ( naongea with experience hapa)..........Nasema hivi kulibeba hilo agano sio msaada zaidi yakupoteza uhalisia nakujikuta unaongeza agano juu ya agano.
KUBARI KUJITENGUA, OMBA MUNGU AKUPE HEKIMA JINSI YA KUTENGENEZA.
KIKUBWA AMINI MUNGU ANASAMEHE HATA KAMA WANADAMU WAMEKUWA WAGUMU ATAFANYA WEPESI WA JAMBO .
No comments:
Post a Comment