Nimekaa nimewaza sana leo kwa vile jinsi neno HURUMA lilivyokuwa mzigo kwetu wanadam............... Nimejikuta nimewaza kipindi fulani nilipokuwa napitia jambo fulani neno huruma lilivyoongeza huzuni, idadi ya maadui na hata kupoteza muelekeo na hata pale nilipotakiwa kusema na Mungu wangu kwa habari ya lile ninalopitia. Ashukuriwe huyu roho mtakatifu anayejua kutuombea ipasavyo na lile jaribu likapata mlango. Kuna wakati tunaweza kujikuta tunaomba na kukemea kumbe tunapiga makelele mbele za Mungu, na kuna wakati tunafunga kumbe tumeshinda njaa................
Ninaposema hili neno lilinipa huzuni, nina maana hii, Akili yangu yote ilitegemea yoyote aliyesikia au kujua lile ninalopitia nilitarajia kumuona na huzuni kwa ajili yakunihurumia, nilishindwa kuelewa inakuwaje mimi na huzuni na kuna mtu haoni, na wala halipi uzito jambo langu. kuna mengi nilikuwa nawaza hapa mwisho wa siku nilijitengenezea maadui mimi mwenyewe.........sikuishia hapo nilijikuta nimewabeba kwenye maombi na asilimia kubwa ya yale maombi nilishughulikia hao maadui ambao leo naamini hawakuwa adui kama nilivyofikiria hivyo nilijikuta napiga makelele mbele za Mungu(nilijikuta maombi yangu yanataja taja tuu majina huku Mungu akisema huyo adui gani unaye unayemtaja taja maana hata kwenye list simuoni kwa maana nyingine hana hadi yakuitwa adui wa mtoto wa mfalme kwi! kwi! kwi! nimewaza tuuuuuu..........
Ninachotaka kusema wapendwa ni hichi, Unatakiwa kulijua jaribu lako, Tambua kama linahitaji kumshirikisha mtu(rafiki,ndugu) au unatakiwa kulishughulikia wewe mwenyewe, na kama kuna mtu anatakiwa kujua unatakiwa kuwa na hekima ya hali ya juu kujua ni mtu gani unapaswa kumshirikisha.
Nikiwa katika hali hii yakulitambua hili kama wote mjuavyo wiki mbili zilizopita kuna jambo ambalo nililipitia.Namshukuru Mungu lilinikuta wakati huu(kila jambo huja kwa wakati sahihi) maana lingenikuta wakati ule niliyo elezea hapo juu sijui leo ningekuwa wapi?????sijui ningelipokeaje????? yaani sijui kwa kweli!!!!! Hivi unaweza ukawa unapitia jambo ambalo akili haiwazi tena(imefika mwisho) badala yake hilo jambo halichukui nafasi kubwa ya Muda wako na wala akili yako kuwaza itakuwaje na imekuwaje????? kikubwa zaidi una amani na bila wasi wasi huku ukitarajia USHINDI MKUBWA????( kuna mtu hatanielewa hapa Mungu akupe masikio ya rohoni uelewe kama wewe umekusudiwa kuelewa hili)
Nimejikuta nimewachambua watu wawili kwa picha tofauti, nikajifunza kitu, unapomshirikisha mtu jambo kwa mfano unapokuwa uko kwenye level ya kuchezea sh.1000 gafla ukapoteza sh.200 ukamfata mtu ambaye unategemea akuhurumie, asimame na wewe katika hilo , lakini umesahau kwamba huyu mtu anchezea sh.50 ameishi maisha yakukutamani si kwa ubaya japo na yeye siku moja hata afike kwenye sh.500(kajifungia na hapo ndipo anapoamini mwisho wa mafanikio).
Kiukweli huyu mtu lazima kuwe kuna neema fulani ndani yake otherwise mapokeo ya mjaribu wako yatakuwa na maelezo mengi bila majibu na mwishowe kutengeneza maadui.
Atakwambia jamani hata hivyo mshukuru Mungu Bwana bado upo pazuri, una hichi, na hichi, na hichi yaani atakupa na mbinu zakutaka uridhike na kukubari amesahau lile neno nitakupandisha utukufu mmoja kwenda mwingine maana hakuna kushuka zaidi kuongezeka..............Usimlaumu huyu tena samehe kwa maana wewe ndo umemletea mjaribu, watu kama hawa wanatakiwa kushuhudiwa wajue uweza wa Mungu ni mkubwa kuliko wanavyodhani, usimfanye akaona hata hiyo ndoto yake haiwezekani, badala yake shughulikia hilo jaribu uje umshuhudie namna lilivyokuwa na namna ulivyodeal nalo. badala yakumchukia nakumfanya kuwa adui.na ikiwezekana badala ya kumtaka yeye asimame kwa ajili ya huo mjaribu wako hebu simama nae kwenye huo mjaribu wake huku ukimsihi Mungu aliyekuwezesha wewe kufika hapo ulipo amuwezeshe na yeye tena zaidi nakuhakikishia utaona wepesi wa mjaribu wako muda unaokuja kustuka tayari umeshapata majibu yako........
Picha ya pili ni ya huyu mtu ambaye yeye ni zaidi yako, labda tuseme anachezea sh.5000 na zaidi,huyu yeye anaamini kuongezeka na anaamini katika maongezeko kuna risks lazima ziwepo. Ni kawaida sana kwake kupoteza kabisa nusu ya kile alichonacho huku akitarajia kupata zaidi ya alichonacho sasa. wakati wewe umekazana kukumbatia kile ulichonacho kwa garama zozote kwa kudhani ukiruhusu kiondoke kidogo umekwisha!!! kumbe sivyo ni moja tuu ya challenge yakukupeleka zaidi. Huyu mtu ukimwambia hilo unalopitia naye lazima awe na neema fulani otherwise hutaona hata punje ya huruma zaidi ya kukuonyesha ni kawaida. Mpendwa kama huelewi utamuweka kwenye list ya maadui nakuona kwamba huyu mtu hataki ufike alipo, anataka yeye awe juu kila siku ila usimfikie.........................
Tambua jaribu lako, tafakari ni namna gani ikupasayo kufanya
Angalizo
kuna mtu unaweza ukamwambia bila kujari yeye yupo kwenye nafasi gani na bado akasimama na wewe ndio maana nikasema kuna neema fulani lazima iwepo.......... Na pia kuna watu hiyo ni karama zao kusimama kwa ajili ya mtu, mfano mwanamaombi au mtumishi lakini sio kila aliye kwenye maombi ni mwanamaombi.
Na pia sijasema Muda wa kutumia mamlaka ukifika usivunje,haribu ,na kusambaratisha maana tumepewa mamlaka.......... na sijasema tusiombe yeye autafutaye uso wa Bwana kwa bidii atamuona IMEANDIKWA
shiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!! nimesema siri usimwambie mtu.( mawazo yangu)
Kila ndugu ukimtafakali kwa namna uliyoielezea kiukweli huwezi kupata adui ,
ReplyDeleteMhh lakini yahitaji hekima ya kutosha.
Kiubinadamu ni ngumu kuwaelewa
Asante kwa tafakari hii 75% ya adui zangu kumbe c maadui
Mungu wa mbinguni aturehemu!
ReplyDeleteingekua enzi za Nyerere huyo mwalimu anastahili kuchapwa viboko 12 hadharani tena na mkewe akiona!
ivi na hao wazazi wanao watuza watoto hapo wanaakili kweli?????
ndo maana mungu akasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maaarifa........
Mama c