haya wandugu ngoja na mimi nizungumzie kwa kajiupeo kangu kwa habari ya mavazi hasa suruali kama mdau alivyosema......
Binafsi naona kama tunatumia nguvu nyingi sana kutaka kubadilisha watu, hasa kwenye kipengele cha mavazi badala ya kuwapa neno linaloweza kumfungua .Pia tunasahau kwamba Mungu ndie anayebadilisha mtu na sio Nguvu zetu na mara nyingi tunapotumia nguvu tunapelekea kuwafanya watu wakaficha uhalisia wake na kuvaa fake, kwa sababu anataka kufanya kwa sababu ya ile nguvu inayotumika........ nikichukua mfano kwa mdau alivyomuona mchungaji na kujistukia na kutafuta khanga, hapa mdau alikuwa anafanya kwa sababu ya mchungaji lakini ndani yake haoni kama ni Tatizo, nikimsoma zaidi ameniambia kwamba amejadili hilo yeye na mtumishi ambaye amemwambia hakuna kwenye Biblia palipoandikwa usivae suruali, hata mimi naunga mkono ila papo palipoandikwa tusivae mavazi ya kiume........... ( hapo chacha) mavazi yakiume ni yapi?? kwa kaakili kangu kadogo kipindi hicho kanzu ndo zilivaliwa na wanaume na baadaye tukatengenezewa suruali za kike na kiume................naomba nisikwambie vaa au usivae nenda kasome neno naulielewe na maamuzi yako yoyote yakakupe amani.
Tukitoka kuyaelewa maandiko sasa tunakitu kinaitwa mazingira, mfano wangu mwenyewe nimezaliwa kwenye familia ambayo khanga na wewe, kitenge na wewe, mpaka ninavyokwambia sasa hivi Tanzania nina kabati nimejaziwa vitenge na khanga nikifika tuu nikufunikwa mwanzo mwisho mda mwingine napigiwa na simu kuna kitenge kipya tumekununulia, utaratibu huu umenifanya hata nikiwa kwangu huku nikijua ninakishughuli fulani wageni watakuja nguo ya kwanza ntakayowaza ni nguo pana au kujitupia khanga juu lakini huyu Mama wawili maisha yake mengi amekulia shule na si nyumbani na kama mjuavyo mashuleni suruali ndo mpango na hata walezi wangu walikuwa wanalijua hilo kikubwa nilichokuwa nasisitizwa kwenye pochi yangu mwanamke lazima kuwe na khanga na nikiwa nyumbani kama nipo sebuleni kwenye mazungumzo na mwanaume mfano Baba, Mjomba, Bamdogo mazungumzo yanayohitaji tension na yanakuchukua mda fulani, khanga ni lazima...........
lakini mazingira hayo hayo ninamarafiki zangu huku hasa wazimbabwe huwa wananishangaa sana na viroba vyangu vya vitenge na wanavitamani mnoo, hapo mwanzo sikuelewa mpaka walipofunguka wakidhani nimetoka familia yakitajiri, kwani huko kwao vitenge ni gharama mnoo kuliko jeans na tops hivyo wengi wao hawakuwa na uwezo wakuvaa na kujikuta suruali na top ndo vazi kubwa na hii imepelekea wengi wao hakuna vazi linalowafanya wawe comfy zaidi ya suruali........ nina huyo rafiki yangu ukimuona amevaa gauni au skirt hata kanisani utamuona anavyohangaika yaani utamuhurumia anavyotembea kwa kujikanyaga kanyaga.
na pia huku kwa wenzetu kunamisimu ya hali ya hewa hivyo utajikuta jeans ni mkombozi kwa hali ya hewa fulani kiasi kwamba inachukuliwa kawaida sana kwani ni vazi ambalo halimfanyi mtu kuwaza tofauti nikimaanisha limezoeleka sana yaani imekuwa kama moja ya tamaduni yao na wakati kule kwetu hili vazi limekuja baadae na bado halijazoeleka kwenye jamii fulani, hivyo unahitaji hekima fulani ukiniangalia kabla ya hii post nimetoa post mbili mwanzo nikiwa nimetoka kanisani na moja nikiwa kwenye kajimtoko kangu fulani so utaona tofauti huwezi ukanikuta nimevaa ile high waist kanisani hata kama hali ya hewa inaniruhusu..............bado nataka kusisitiza hata kama umepewa amani ya jibu uvae au usivae bado kuna vitu vyakuzingatia.........
Namalizia na kipengele alichosema mdau Mume wake hapendi avae kanisani lakini hilo limekuja mara baada ya hawa watu kujitambua nakuanza kwenda kanisani japo kuwa ni vazi ambalo mumewe alimkuta nalo...... Ngoja ni kupe kajimfano Kwi! Kwi! Kwi! nimecheka kwanza maana kuna watu mapovu yatawatokaje sasa???? anyway chamsingi nieleweke kwa yule anayetaka kupona. Haka nikama kajiutaratibu fulani ka Baba watoto wangu, hata siku kadhaa zilizopita kametokea tulikuwa tunatakiwa kwenda mahali fulani ambapo Mimi nilijiandaa vizuri na vazi lilienda sawa ambalo huwa analipenda lakini hajawahi kuniambia why analipenda, nasijawahi vaa kwenye tukio la dizaini hilo ila kwa jinsi lilivyonikaa( kila ...... na mbuyu wake) Taratibu namsikia Baba watoto, Mama umependeza lakini hilo vazi lipo............ akafunguka kimtindo, Mama watoto nikajiongeza kimtindo nisije nikapoteza concetration huko tunako kwenda........ nikarejea na kwa nini nilifundishwa kuvaa khanga sebuleni nikiwa kwenye mazungumzo,na pia nilizidi kujifunza pia umbo la mtu pia linachangia nguo inaweza kuwa kawaida lakini nikivaa mimi nakuwa kama mti umevalishwa gauni hapo hata nikiingia kwenye maombi sitakuwa kwazo la mtu kuvusha na kuamisha akili yake, lakini ukivaa wewe mdau duu Mume mwema anaweza akasahau kama yuko kwenye maombi anavusha tuu anachowaza kurudu nyumbani............sorry haka kajipengele kawa kubwa tuu lakini ndo hivyo tufanyaje sasa tunataka tupone.
na mwisho namalizia hivi, suala la mavazi ni la muda, na kwa kadiri muda na vile uelewa unavyokuwa kuna namna fulani ya kiroho na kupondeka vitu huwa vinaisha vyenyewe na kuvifanya tena vinakunyima amani kabisa.... mfano wangu binafsi kipindi fulani ulikwa hunikuti nimevaa knee length yaani nilikuwa nikivaa ni very short na kama ndefu basi ni ndefu haswa imepambwa na mpasuo huo.hakuna aliewahi kunishurutisha niache au mimi mwenyewe kujistukia kwa kigezo kwamba watu wananiita mlokole kwa hiyo natakiwa ni act kama walokole ...... hilo jamani nililikataa sipendi kufanya kitu kwa sababu ya vazi ambalo watu wananichukulia, huwa napenda kuwa real then roho mtakatifu ananibadilishe nakunipa amani bila kumuogopa mwanadam yeyote, huwezi ukaamini siku hizi kuna picha huwa naziangalia nimevaa kidude hicho najiuliza sasa huu ulikuwa ulimbukeni, utoto, au????? juzi juzi nilitakiwa kwenda kwenye shughuli kulikuwa na rangi husika tulitakiwa tuvae nilisaka hiyo rangi muda ulikuwa mfupi, nilifanikiwa kupata iliyokuwa juu kidogo ya magoti huwezi amani sikuwa na amani na haikuwa mbaya na shughuli yenyewe ilikuwa ya wanawake ,sema tu ile hali nimetokea kuanza kuzichukia nguo fupi na sikutaka kuharibu shughuli ya muhusika. nikisema hivyo wandugu kuna mtu naweza kumuona amevaa nguo fupi kwa eneo linalohusu nikaona amependeza haswa lakini sitamani kujiweka hapo naona sio mimi zina wenyewe. kwa hiyo usinielewe tofauti sichukii wewe uvae ila mimi mwenyewe najiona siko sawa ILA nikogo sensitive na mazingira kidogo yaani utakuta mtu amekuvalia kitu kituko sehemu isiyo sahihi mpaka naanza kuona aibu mimi wakati sijavaa mimi na hata kumwambia siwezi (hayanihusu)ila na baki kujisemea tuu huyu na yeye kale kajihekima nilikokapata mimi kakujiona limbukeni,kupania,kutokujua,................ naomba kamkute duu!!! fujo
Asante wenye kupona watapona,wengine pia watapindisha shingo, ni mtu na nafsi yake na kile anacho kiamin.
ReplyDeleteAsante kwa somo zuri hata mm swala la mavazi huwa linanisumbua japo nakuwaga mkaid na bd navaa suruali hadi ss.Kitu kingine nilikuwa naomba utoe funzo tunapoamua kufunga na kuomba lets say unaombea kazi au Mume mwema kutoka kwa Mungu au unombea Nchi yko na viongozi ni unasimamaje kuomba hilo mbele za Mungu?je unaomba huku ukifanya ref na mistar ya bible yenye ahadi izo au?pia naomba utupe mwongozo ukifunga lets say masaa kumi na 12 yaani katika hayo masaa inabidi ujikabidhije kwa Mungu?labda asubuhi uombeje.then mchana mpaka itakapo fikia muda wa kufungua.Au twambie ww huwa unafanyaje ufungapo kwa maombi.
ReplyDelete