Jamani hapa ndo judge nilipofikia.......
naomba lidhaa yakuwasiliana na muhusika halafu ntakuja na kitu.
mbarikiwe
naomba lidhaa yakuwasiliana na muhusika halafu ntakuja na kitu.
mbarikiwe
Nimejifunza
mengi sana kupitia wewe ikiwemo, uaminifu kwa Mungu, Upendo, Shukrani, Msamaha,
Ibada, Mafanikio na mengine mengi.
Kwanza
kabisa nimejifunza kwamba unapopanga jambo lazima umshirikishe Mungu ili
akuongoze bila kufuata njia zako mwenyewe. Nimeona post kadhaa umeweka kwamba
kuna wakati ulienda kinyume kufuata jinsi unavyotaka na si Mungu akikuongoza na
mambo yakawa hayaendi sawa lakini ukimfuata Mungu basi mambo yalienda vizuri.
Pili
nilijifunza kwamba kuwa mlokole sio kwamba wewe ni mkamilifu moja kwa moja
sababu we ni binadamu tofauti na walokole wengine huku mtaani utasikia mimi
nimeokoka siwezi kukosea hata kidogo na kuamini kwamba kama umeokoka basi
umkamilika. Kuna post umekua ukiweka na kuomba samahani pale unapokosea kwakuwa
sote ni binadamu. Kwaiyo nimejifunza kitu hapo.
Tatu
Mavazi: kwakweli hili lilikua linanichanganya sana. Mavazi yako niliona kama
hayako kilokole nikajifunza kwamba tusiangalie mavazi ya mtu jamani ndio tuseme
ameokoka bali tuangalie na roho yako na matendo yake ni jinsi gani yanaleta
ushuhuda kwa Mungu.
Kingine
nimejifunza upendo kupendana sisi kwa sisi na kuombeana mema: kupitia familia
yako nimejifunza mengi. Upendo na uaminifu kwa Mume kunamfanya ajisikie mwenye
furaha katika ndoa bila kujali anacho au hana. Upendo kwa watoto bila kubagua
utakuta kuna wazazi wengine wanabagua watoto wao ila kwako nimejifunza mengi
mnooo. Kuombeana mema hapa dunia na kupendana sisi kwa sisi basi tutazidi
kubarikiwa mana ukimuombea mwenzako limpate baya basi huwa lina kurudi bali
ukimuombea mema nawe utafanikiwa.
CHAKUONGEZA
·
Binafsi nitapenda sana kama utakuwa unatuwekea historia ya
waimbaji wa injili walikotoka na walipo
hili litazidi kuongeza ushuhuda na utukufu kwa Mungu.
·
Neno la Weekend uwe unatuachia neno kutoka kwenye biblia tuwe
tunaita neno la wiki
Mwisho
dada yangu Rose, Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa kiume ambaye baba yake
tuliachana mtoto akiwa na miezi sita na mpaka leo hamfahamu baba yake na wala hatuna mawasiliano yoyote na
mzazi mwenzangu. Nimelea mtoto mwenyewe katika hali ngumu mara sina kazi kwa
ajili hata msichana wa kazi kupata ilikuwa ngumu, hata nikiwa na kazi mshahara
mdogo sana. Kweli mpaka sasa mshahara wote ninaopokea unaishia kwenye matumizi
kama unavyojua mishahara huku kwetu Tanzania hasa sisi tunaofanya kazi na
wahindi ni mdogo sana. Nimejitahidi
kukusanya kidogo na nimefanikiwa japo hakitoshi kuanzisha biashara yangu
mwenyewe. Hivyo kwa sababu mimi nimesomea mambo ya secretarial na ninaweza
kufanya hizo kazi nimepangilia na kwa uwezo wa Mungu nianzishe stationaries
& secretarial services ili niweze kujiajiri na kuachana na kazi za
kuajiriwa. Kama nikibahatiaka kupata hii zawadi nitaiingiza kuongezea mtaji.
Asante
sana na Mungu awabariki
ReplyDeleteThis is so touching.....kulea mtoto bila mwenza nadhani ni tabu sana na |Mungu amsaidie mdau, Ila Rose nadhani pia sasa ifikie wakati humu tuweze kuwatuna changia kidogo kutimiza ndoto za watu kama ya huyu dada sadaka si lazimam ikajenge kanisa au iende kanisani nadhani kufanya hivyo tutakuwa tumeyoa sadaka ya dhati na itamsaidia huyu dada.
Huu ni mtizamo wangu binafsi.
QR.