Pages

Ads 468x60px

Thursday, January 30, 2014

TUZUNGUMZE

Haya ndugu zangu leo nilitaka tuzungumzie habari ya maombi ya kufunga kama mdau alivyotaka tulizungumzie, tupeane mawili matata juu ya maombi haya kwa jinsi Mungu atakavyotuongoza. lakini nimepokea e mail tena kwa mdau mwingine anaomba tuzungumzie ni namna gani tunaweza kuachilia hasa tunapokuwa tumebeba mizigo ya makwazo na kujeruhiliwa ndani ya mioyo yetu.................Nimeona bora tuanze na hili la kuachilia maana maombi ya mfungo bila kuachilia bado ni kazi bure, tukijua jinsi ya kuachilia inatupa wepesi tunavyoingia kwenye mafungo yetu.......


 Kwa uelewa wangu huu mdogo wandugu kwangu kuachilia ilikuwa ngumu mno kama nisingezingatia haya  machache nitakayosema hapa chini, na zaidi ya yote  kuomba neema  ya ujasiri  kwa namna yoyote itakayonifanya nikabiliane na hilo suala baada ya kuachilia, nilikuja kugundua kusema nimesamehe ilikuwa nirahisi kwangu lakini nilitaka lile jambo lisijirudie, na kwa sabubu shetani hajalala kila siku alitaka kunikwaza na kunikosesha raha hivyo nikajikuta lile kwazo linakuja mara kwa mara  na sa nyingine kwa namna tofauti  nilijikuta naishia kusema   ( "JAMANI NILIMSAMEHE LILE NA LILE NA HILI TENA??") ilinibidi nitulie nakutafuta njia mbadala yakutokumpa shetani nafasi ( narudia tena NEEMA ya Mungu yakukuwezesha inahitajika sana baada ya kuamua hili) niliamua kujifunza KUSAHAU ,Aisee hii kitu imenisaidia sana yaani ukiona nimelikumbuka nimeligeuza kama utani fulani mfano niliwahi kuandikiwa ujumbe fulani mwishoni uliomaliziwa na ("CHAT YOU LATER NILIKUWA NAKUPA HI TU..") kwa akili ya kibinadam ukiniuliza ntakwambia  ule ujumbe ulijaa makwazo na majeraha ambayo siyakumbuki vizuri ila haka kaneno naweza nikawa na Mume wangu tukaongea utani fulani nikamalizia na hako ka msemo.Hii aimaanishi nimebeba machungu ya ujumbe ila ninamna yakujisahaulisha nakugeza kuwa kama joke fulani na kukusaidia kupotezea. nilizidi kujigundua hili pia mara Mama yangu alipokuja huku kuna mtu nilitakiwa kufanya kitu  sasa nimekaa na Mama tunapanga mikakati nilifanyaje  nasikia ( hivi huyu mtu anakumbuka alivyokufanyia hivi na hivi,anakumbuka....... anakumbuka ......) kila anakumbuka ilikuwa ni machungu na mizigo ambayo kibinadam haibebeki all you can think ni jinsi gani yakumlipa kwa mabaya kama alivyokufanyia, kilichoshangaza siku ile nilianza kumuuliza hivi nakumbuka kama hilo neno lilitokea lakini sikumbuki ilikuwaje???? alianzaje sasa kunitafuta kunirudisha nikumbuke????mpaka alikasirika nakuniambia unajifanya hukumbuki unanienjoy eeeeh!!! ( in my mumy's voice)ha! ha! ha!  i love my Mumy aisee nimeongea mpaka nimemmiss gafla....... anyway tuliishia kubadilisha topic  maana hakukua na maelewano yeye kanibebea mizigo ambayo mimi hata siikumbuki. Nina mifano mingi mnoo kupitia hili lakini nafikiri mpaka hapo tumepata kamuelekeo kidogo.

Namna nyingine niliojifunza jinsi ya kuachilia ni kujipa muda juu ya jaribu lolote  linalonipata  hili ni muhimu mno....... rejea kwenye mfano wangu mimi mwenyewe.......  kama msomaji utanielewa kwazo lilipo nipata sikujipa hata sekunde  ubinadamu ulichukua nafasi kubwa, nilijikuta nimechoka, sikutaka kuruhusu hekima ya kiMungu  Dont you worry hizo zote ni mbinu za shetani aisee baada ya nusu saa ndo akili ya Mama wawili  inakaa sawa nakujiona mkosefu, nimekuwa mjinga nakumpa shetani nafasi . mbaya zaidi  nimepublish kitu ambacho impact yake inaweza kuwa sio nzuri kwa jamii fulani  na nakuwadissapoint. na usione ajabu kwani kupitia ule ujinga  na japokuwa nimeshaachilia na kutubu  bado  zile dakika thelathini zinaweza kuwa kwazo mbeleni kama tuu sitazingatia  hiyo nafasi ya kwanza( kutafuta namna yakujisahaulisha)

kupitia hili pia  hapo mwanzo nilishindwa kuelewa Neno liliponambia  OMBEA ADUI YAKO........  Nilijiuliza nitawezaje kumsamehe nakupiga goti kumuombea tena???? iliniumiza kichwa mpaka hapo nilipopata amani ya jibu hili......... unapopata kwazo jaribu kumuanagalia aliyekukwaza na namna alivyokukwaza, utakachokiona ni majuto,majeraha,kushindwa,wivu,kutokutumia vizuri nafasi aliyopewa,  kutokujitambua na pengine hata kutokujithamini na mwisho anakosa hekima ya namna yakusawazisha hayo anageuka kuwa kwazo kwa kila kitu  na pengine hata kwangu ambako kunanipelekea tuwe maadui. hili limenisaidia sana maana baada yakumwangalia yeye mwisho wake utajikuta kwanza unamuhurumia na kumuhurumia kutakufanya umsamehe  na kumsamehe utajikuta unamaliza na kumuombea tuu bila kutaja lile kwanzo. ambayo moja kwa moja itakuleta kwenye kuachilia.nafikiri mnanielewa vizuri hapa.

Bila kuendelea kuwachosha labda nimalizie na hili  nilijifunza kutokukaa ndani ya tatizo,makwazo kwa namna ambayo haitavuruga mahusiano ikitokea imevuruga basi hivyo ndivyo ilivyotakiwa kuwa........  nikimaanisha  hivi kama kila ninapokutana na wewe lazima tukwazane kwa namna moja ama nyingine ambayo inatutengenezea uadui nitajitahidi kwa namna yoyote yale makutano yasiyo ya lazima yasiwepo 
haimaanishi nakuchukia au nina jambo na wewe NO!  bado nakuthamini, nakupenda  nakukuombea kama unavyofanya wewe ( niaminivyo mimi) yawezekana sisi tunajitahidi kuondoa tofauti zetu lakini shetani yuko kazini kututumia pasipo wenyewe kujielewa  kwa hiyo tunapopeana nafasi inaleta uthamani fulani kati yangu na muhusika kama sisi sote tuko kwenye same page. ukiona hii mbinu haijafanikiwa zaidi yakuletea makwazo tena ujue huo uhusiano haukua wa muhimu kwako na sina haja yakujaza huo mzigo ndani yangu zaidi ya kuachilia kusamehe na kusonga mbele bila makunyanzi........


angalizo

nimeongea kwa namna nionavyo mimi inaweza ikakusaidia au isikusaidia kikubwa upate NEEMA YA KWELI NA IKAKUONGOZE. Na pia hili nimelizungumza kwa mtu yeyote yule iwe ndugu,rafiki,au jamii yoyote ambayo wewe kwako imekupa kwazo linalokufanya ushindwe kuachilia.

TAFADHALI USITUMIE HIZI MBINU KWA MUME AU MKE NO! NO! NO!
 ninamtazamo tofauti juu ya hawa watu wawili.

UTOTO RAHA NYIE ..............

Basi tuu, kuna mda huwa nikikaa na wanangu kuna vitu fulani huwa vinafanyika mpaka huwa najiuliza hivi na mimi nilikuwa hivi..... yaani hawa wenzetu ni malaika aiseee, huhitaji nguvu  kuwapa furaha.... kama Mama unanielewa we chukua kaji mda kaa na mwanao  kuna vitu vya kipekee vipo ndani yao hasa mnavyofanya mazungumzo, wakitaka kujua kitu wanavyokuuliza hicho kiswali, wakiwa wanataka kitu halafu wewe mzazi hutaki kwa kumaanisha labda hakiwafai kwa muda huo na vitu kama hivi.............

 Leo nimewawaza sana wanangu, kama kawaida mishe mishe za shopping kujiandaa na shule week ijayo, wote tukoje na furahaje sasa....... my Christabell anaanza Kindy na Careen Pre primary duu!!!! kama sio kweli vile Jana tuu vilikuwa vinanyonya mweeee.....(AHSANTE BWANA YESU)
 basi katika hizo shopping Muda wakununua Viatu vya shule umefika mtu kagoma (MUMY I DONT WANT NEW SHOES CAUSE I WANNA WEAR MY PINK SLIPPERS AT SCHOOL in Careen's Voice)  Nikakumbuka juzi naye Christabell alipokuwa analala alisisitiza mtu asitoe slippers zake alipoziweka ile asubuhi  naingia chumbani kwake kumuangalia mtoto kastuka MUMY WHERE ARE MY SLIPPERS??? in Christabell's voice) yaani inanichukua muda sana kuelewa mpango mzima wa hizo slippers  umekaaje, cha ajabu nilishawahi kuwanunulia huko nyuma hakuna aliyezipenda mpaka sasa hazikuvaliwa sana na haziwatoshi tena..... juzi kati baba yao aliwanunulia tu ili aone km this time watazielewa.... mbona zimekuwa gumzo ndani mwetu kila anapoenda huwezi ukawapa story nyingine zaidi ya malapa................ ni hayo tuu yaliyonifanya nitafaaaakaaaariiii   na kujiuliza kulikoni na kujikuta natamani na mimi nirudi utotoni.............

 KITAA NA DAD YAO about to go..........

wandugu hizo nywele za kisharo  kwa Christabell msinipige mawe  anayetoka  nao ndo kataka.

nawapenda mnooo hawa watu mwenzenu mwee
wanavyoondokaga utafikiri, hawa watu kuwaona mpaka jua lizame kwi! kwi! kWi!  kiboko yao niwe nao Mama Shughuli ntawatembezaje kitaa sasa.

 wamerudi nakutafuta vishughuli
The end

Tuesday, January 28, 2014

CHEKA NA MIMI..............

Jamani huu DADA ni nouma duu kila mtu na kipaji chake aisee.............. 



pamoja na vituko vyote lakini bado kuna kitu tunajifunza .

HUTOKEA KWA SABABU................

Haya ndugu zangu nisameheni bure......  ni kweli nimejiona mjinga narudia tena kwa hili nimejiona mjinga ............ nimetaka kupigana vita visivyo vyangu nimejiuliza sana kilichonikwaza sio kwamba ni mara ya kwanza kukisikia, nilisikia mpaka nikakizoea lakini sijui kwa nini last sunday nilichoka kujizuia, mpaka aliyetukanwa ameniuliza kwa ni mara ya kwanza kusikia hilo???? akili yangu ikaanza kukaa sawa nikajiona kabisa adui kapata mlango..... anyway wandugu na mnielewe mimi ni mwanadamu najua wengi wenu hamkutarajia hili na bado mnajiuliza, limetokea ili  mjue mapungufu yangu ili mniombee na pia hili litawathibitishia hata mimi nawahitaji mnoo na sio nyie pekee mnaonihitaji mimi. najifunza kutoka kwenu na nyie mnajifunza kutoka kwangu ili jukwaa letu lisonge mbele kwa ajili ya utukufu wa BWANA........

 Kwa kusema hivi, nimemshangaa Mungu kwa jinsi alivyosema na mimi juu ya hili, kama kawaida yangu kila siku lazima nisome chochote hata kama nimechoka hii ni ratiba yangu, gafla najikuta nimefunua  haya maandiko jana wapendwa......  kwanza niliogopa kabisa mpaka nilivyokaa sawa  nikasoma tena kwa umakini,imebidi niyatafsiri kiswahili ili wote twende sawa( ahsante Google)  nimemshangaa mungu anavyoweza kusema na mtu tena mimi nilikuwa nasikia sauti ya ukari kabisa nilivyokuwa nasoma sa sijui na nyie wenzangu itawakuta hivyo au mimi tuu kwa mazingira niliyonayo.

Snakes and spiders terrify a lot of people. Not a big surprise, is it? Not when you consider their habit for biting people with life-threatening poison and all... People can bite too. Not with their teeth (we hope) but definitely with their words. But we're not called to fear people. The Bible says, 'We can say with confidence, "The Lord is my helper, so I will have no fear. What can mere people do to me?"' (Hebrews 13:6 NLT) If you've had words spoken over you that hurt, bring them to your Dad in Heaven. If they go against what God says about you, reject them.
God says, 'Stop being bitter and angry and mad at others.' If God says stop, you can be sure He won't give you that command unless He'll also give you the grace to help you. Words can bite and, just like venom, get into our system. Then bitterness, rather than love for God and for others, can pump through our veins. Focus on who God's called you to be, so you can move forward in the opposite spirit. Take a contrary attitude to bitterness! Pray for the people who hurt you to be blessed instead and watch God flourish your life. Have peace that 'in all things God works for the good of those who love Him.' (Romans 8:28 NIV)
God cares about justice. Free yourself and let Him judge.

Nyoka na buibui kuwatisha mengi ya watu. Si mshangao mkubwa , ni? Si wakati wewe kufikiria tabia zao kwa kuuma watu na kutishia maisha sumu na wote ... Watu wanaweza bite pia . Si kwa meno yao ( sisi matumaini) lakini dhahiri kwa maneno yao. Lakini sisi siyo kuitwa hofu watu . Biblia inasema , 'Hatuwezi kusema kwa kujiamini , "Bwana ni msaada wangu, hivyo mimi sina hofu . Nini watu tu wanaweza kufanya ili mimi?" ' (Waebrania 13:06 NLT) Kama umeshapata maneno yaliyosemwa juu ya kwamba madhara, kuwaleta baba yako Mbinguni. Kama wao kwenda kinyume na kile Mungu anasema kuhusu wewe, kukataa kwao.

Mungu anasema, 'Stop kuwa machungu na hasira na wazimu kwa wengine . Kama Mungu anasema kuacha, unaweza kuwa na uhakika Yeye si kutoa amri kuwa kama Yeye itabidi pia kukupa neema ya kukusaidia. Maneno yanaweza kuuma na , kama sumu , kupata ndani ya mfumo wetu. Kisha uchungu, badala ya kuleta upendo kwa Mungu na kwa wengine, wanaweza kusukuma kupitia mishipa yetu. Kuzingatia ambao Mungu amekuita kuwa , hivyo unaweza kusonga mbele katika roho kinyume. Kuchukua tabia kinyume na uchungu ! Kuomba kwa ajili ya watu ambao kukuumiza kubarikiwa badala yake na kuangalia Mungu kustawi maisha yako. Na amani kwamba ' katika mambo yote Mungu hufanya kazi kwa manufaa ya wale wampendao . (Warumi 8:28 NIV)

Mungu wasiwasi juu ya haki. Bure mwenyewe na kumruhusu kuhukumu.

nimeingia facebook nimekutana na Mdau kanitumia hiii nayo nimeitafsiri kwa chini

A GENTLE ANSWER TURNS AWAY WRATH, BUT A
HARSH WORD STIRS UP ANGER. ( PROVERBS 15:1* NIV ) Dear .......... We all become angry sometimes with the words or actions of another. When we do it is important that we do not respond to them with words of anger. For it is written; HE WHO GUARDS HIS MOUTH AND HIS TONGUE KEEPS HIMSELF FROM CALAMITY, and oh how true that is indeed! ( PROVERBS 21:23 ) The Apostle Paul wrote; DO NOT LET ANY UNWHOLESOME TALK COME OUT OF YOUR MOUTHS, BUT ONLY WHAT IS HELPFUL FOR BUILDING OTHERS UP ACCORDING TO THEIR NEEDS, THAT IT MAY BENEFIT THOSE WHO LISTEN. ( EPHESIANS 4:29 ) Further, James the half brother of Jesus' wrote; OUT OF THE SAME MOUTH COME PRAISE AND CURSING. MY BROTHERS, THIS SHOULD NOT BE. ( JAMES 3:10 ) After all; PLEASANT WORDS ARE A HONEYCOMB, SWEET TO THE SOUL AND HEALING TO THE BONES. ( PROVERBS 16:24 ) So ......... keep your words soft, sweet and pleasing to our Heavenly Father. After all He hears every word that we say! So just as King David did, remember these words when someone angers you. Then next time before your anger can take control, recite them in your mind. "MAY THE WORDS OF MY MOUTH AND THE MEDITATION OF MY HEART BE PLEASING IN YOUR SIGHT, O LORD, MY ROCK AND MY REDEEMER. Amen. ( PSALM 19:14 )


Jibu mpole jiepusha hasira yake, bali A    HARSH NENO huchochea hasira.                          ( METHALI 15:01 * NIV)    Ndugu ..........        Sisi wote kuwa na hasira wakati mwingine kwa maneno au    matendo ya mwingine. Wakati sisi kufanya hivyo ni muhimu kwamba sisi    wala kujibu kwa maneno ya hasira. Kwa maana ni    iliyoandikwa; Yeye alindaye kinywa chake na WAKE    TONGUE anaendelea mwenyewe kutokana na msiba , na oh    jinsi ya kweli kwamba ni kweli! ( METHALI 21:23)        Mtume Paulo aliandika ;    Usiruhusu yoyote TALK usiofaa kuja OUT    Ya vinywa vyenu , lakini ni yale tu kusaidia    YA Kuwajenga wengine kulingana na wao    Mahitaji, ili faida kwa wale ambao kusikiliza.    (Waefeso 4:29 ) Zaidi ya hayo, James nusu ndugu wa    Yesu aliandika, Katika kinywa kile kile kuja SIFA    Na laana. Ndugu zangu, hii haipaswi .    (JAMES 3:10)       Baada ya yote ; Maneno yapendezayo ni asali,    Ni tamu nafsini na uponyaji kwa mifupa .    ( METHALI 16:24) Hivyo ......... kuweka maneno yako    laini , tamu na kumpendeza Baba yetu wa Mbinguni . baada ya    wote Yeye ni Mwenye kusikia kila neno sisi kusema!        Hivyo tu kama King Daudi alivyofanya, kumbuka maneno haya wakati    mtu uhasama wewe. Basi wakati mwingine kabla ya hasira yako    unaweza kuchukua udhibiti , soma yao katika akili yako. " MAY THE    Maneno ya kinywa changu na mawazo ya MY    Moyo ufanywe ilivyokupendeza , Bwana, MY    ROCK na mkombozi wangu . Amina. (ZABURI 19:14)



Mbarikiwe wadau mlionijali nakunithamini hapa ndipo nilipogundua kwa nini nawahitaji................. huu ni moja ya chat na mdau wangu .


TUSONGE MBELE NDUGU ZANGU NA TUSAMEHANE

natumai haujambo my dear
I love yor blog for so many reason, ila zaidi najua na kuamini pia watu wengi sana wanasoma blog hiii, nimeamua kukuandikia hivi kwakuwa sipendi kuona watu wanavyotaka kugeuza blog uwanja wa malumbano. Katika biblia kuna mahali kumeandikwa kuwa KUNYAMAZA NI HEKIMA ILIYOZIDI ZOTE.
my personal opinion ni hivi sio kila jambo unaloambiawa au kisikia unalijibu wkati mwingien shetani hujipenyeza mahali bila hata wewe kujua kuwa hapo sasa amekutumia na hufurahi nakujona mshindi na pia zaidi wale waliotumia na shetani kukufanay na wewe uwe njia ya shetani kupita kujidhihirisha wanafurahi sana.
Nakuomab sana mimi naamini blog yako ni mahali ambapo mnugu napatumia kwa mambo mengi sana wewe kibinadamu unaweza usilione hilo kabisa ila impact yake kwa jamii hasa ya wadada ambao wanfamilia they REAL LOOK AT YOU, i know most ofmy friends does
Please nisamehe kama nitakwu animekukwaza.
Nimeshamaliza ...... and am all good Mimi ni mwanadam kmalivyo mwingine naumizwa nachoka ni vingi ambavyo huwa siviachilii ukiona numeachia nikwamba watu wanielewe natokea wapi........ But anyway nimesha publish siwezi kubadilisha mapokeo kila mtu atachukua anavyoona. Naamini nimedisapoint for some people km hawajanielewa things work for a reason am so sorry maana hata mimi nimejiona mjinga badae
Mungu akupe uvumilivu na hekima zaidi ya uliyonayo sasa. Tuombe amani na upendo katiyetu sote. You will be in my prayers. Ubarikiwe Mpendwa
Bless you
about an hour ago

Sunday, January 26, 2014

NIGHT OUT WITH LADIES


About to go...........
here we are.........
happy gurlz....

ooh yes!! we ate, drink, share and laugh...........
Mama wawili, Portia,Edna, Stacey,Heleni,Shamy,Mercy,Angeli &Asena
Stacey & angeli
Asena & Heleni

really it was  fab. time to hang out with these gurlz......
THE END.........

AM BLESSED

 Wandugu nimerudi nitokako mpango ulikuwa   kupost muonekano kama muonevyo........
  herself


  sasa katika kuingia humu nikakutana na pumba za mwanamke asiyejielewa kabisa maishani mwake ikabidi nitoe na picha zifuatavyo
Hivi ni mwanamke gani asiyeweza kumshukuru Mungu kwa ajili ya familia yake hasa anapoona yanayofanyika kwenye familia kama si neema za Mungu asingaliweza???????

Mwanamke gani mpumbavu asiyefurahia kuona Mumewe ni kichwa cha familia anayejali na kuthamini familia yake?????

Mwanamke gani asiyependa kupendwa????? tutakupeleka milembe sio bure.....






  khaa!!! sa nyingine kweli inatubidi tucheke tuu maana tunakuonea huruma povu linavyokutoka huko gizani uliko


Naomba niongee sasa baada ya taarifa.

Mwanamke mwenzako tukusaidiaje sijui, maana naamini kwa mpango huu hata kale kaelimu kachekechekea mwalimu wako alisalimu amri, maana una akili mgando!!!! ulijanzwa mimaagano tangu utotoni tunajitahidi kukusaidia hata upate ukombozi bado hujielewi, tunakupa na mistari ya biblia basi ukasome mwenyewe kichwa kigumu huwezi kujiongeza, haya basi tumekupa hata exposure basi  kakuingia kwenye mitandao ujue wanawake wenzako wanafanya nini? wanawaza nini ufunguke bado unajifungia minyororo namakufuri ya chuma, maisha yako  yamejaa hasi......hutaki kuachilia chuki  na makunyanzi ya wivu ndo chakula chako, tumesema na wewe kiupole na hekima   mwanamke bado umejaa kichefuchefu cha labour...................... haya basi tumeshindwa sie  sasa hautuhusu tumeamua kukupotezea, basi sasa fanya kama na sisi hatukuhusu, najiuliza  hivi umekutana na mama wawili,hivi hayo maneno yako yakimkuta mwanadam aliyekata tamaa ambaye anahitaji mtu kumuinua hivi wewe siutammaliza kabisa??? wewe umekubali haiwezekani sawa we si mjinga basi acha wenzio tunaoamini inawezekana tusonge mbele .................na tunasonga mbele kweli we mwenyewe  unakubali kama nakuona unavyosema na giza maana hujui mwanga.(MWANAMKE  MCHAWI NA AFE) sio mimi ni maandiko, simuonee huruma hata kidogo maana ni bora hilo kuliko zile roho zitakazo anguka kwa ajili yako. Mwanamke usiependa mwenzako afanikiwe, ainuliwe kila siku unatafuta baya mazuri huyaoni???? na hata ukiyaona mazuri lazima uzilinganishe na imani zako mara mwanga, nimekuona kwenye paa sasa siunitungue basi kama umeniona  na wewe mjanja wakuona??? au umepewa uwezo wakuona kwa macho tuu huku mimi naendelea kukukandamiza kwi! kwi! kwi!unasubiri nini au nimekuzidi????? utasubiri sana na hivyo nimejaliwa likitanda likubwaaaa halafu nikamalizia na neno NITALALA KAMA MTOTO MCHANGA WALA HAKUNA CHAKUNITISHA............... weweeeee!! hapana chezea mwana ya mfalme... utasubiri sana mbona....... yaani na unabahati mimi ningekuwa wewe ndo nakuona hivyo huo usiku utanisomea kuanzia kitabu cha mwanzo mpaka ufunuo,utaimba nyimbo za mwimbieni Bwana kuanzia wa kwanza mpaka mwisho tunamaliza na sala ya Toba kwa lazima.

 kiukweli huwa naumia sana na watu wenye roho zakukatisha tamaa. wewe ukalilishwa kuwa ndoa ni jehanamu la moto na umebaki hapo unaugulia basi acha wenzio tunaotiana moyo ndoa ni full upendo na amani  na inawezekana kuwa hivyo pamoja na  misukosuko ambayo ipo kila kona kwenye biashara, makazini lakini bado tunafocus..................

namalizia kwa kusema wanawake hebu tuombeane wandugu kwenye ndoa zetu, malalamiko, wivu na maneno yakukatisha tamaa hayatusaidii. hebu umia basi kama we ndoa yako niyamaumivu basi usiruhusu na mwingine  na mwingine apitie tambua lile kosa na elimisha mwanamke mwenzio ili asipitie hapo. na uonapo wanandoa wamefunikwa na upendo hebu saidia kumshukuru Mungu kwa ajili yao eti na muombe Mungu awazidishie huku na wewe ukiweka hitaji lako kupitia hilo. MWANAMKE MPUMBAVU HUBOMOA NDOA KWA MIKONO YAKE MWENYEWE. 

 kilio changu huyu mwanamke wa dizaini hii akikutana na mwanamke anayehitaji msaada wa kuinuliwa itakuwaje??? kama anaweza kuniandikia mimi ambaye anajua kabisa ntakacho kifanya ni kum SCROLL,SELECT,DELETE  hii ndo kanuni yangu kubwa yakuishi na watu wasiojielewa. sasa kwa hao ambao wahitaji ITAKUWAJEEEEE??????

 jana nilialikwa  sehemu fulani  ilikuwa ni wanawake katika kupeana hili na lile hasa kwa habari ya ndoa niliwambia hivi, Ndoa ni serikali ambayo ina idara zake na kamwe usitake kuleta sheria za serikali ya Mugabe  ziwe za Kikwete. kikubwa ni unalipokeaje nakulitatiuaje???????


Wednesday, January 22, 2014

MTU CHAKE BWANA.....,.......

Wandugu mwenzenu nimekaa kwenye kajisehemu kangu kakupumzikia all i can see in front of me ni Baba watoto busy  busy tuuu nikajikuta nimetumbukia kwenye dimbwi la mawazo mnooo, nimewaza nakuwazua mara nikajikuta nimeingia ndani nakuanza kumpiga picha nipate kumbukumbu kwi! kwi! kwi! all i can say i thank God kwa kumfanya huu mwanaume kuwa ubavu wangu.................. AM BLESSED!!! sio kwamba tunaishi kama malaika   hakuna purukushani zipo sana tuu ila tunamshukuru Mungu tunajua  kuzimaliza na kusahau..................... nimeona nishare japo kwa Picha tuu 

 I love this Man here aiseeeee!!!! 

 perfect for Mama wawili



 Yote hiyo ilikuwa to make his kids happy...............

TUZUNGUMZE



 haya wandugu ngoja na  mimi nizungumzie kwa kajiupeo kangu kwa habari ya mavazi  hasa suruali kama mdau alivyosema......

 Binafsi naona kama tunatumia nguvu nyingi sana kutaka kubadilisha watu,  hasa kwenye kipengele cha mavazi  badala ya kuwapa neno linaloweza kumfungua .Pia tunasahau kwamba Mungu ndie anayebadilisha mtu na sio Nguvu zetu  na mara nyingi tunapotumia nguvu tunapelekea kuwafanya watu wakaficha uhalisia wake na kuvaa fake, kwa sababu anataka kufanya kwa sababu ya ile nguvu inayotumika........ nikichukua mfano kwa mdau alivyomuona mchungaji na kujistukia na  kutafuta khanga, hapa mdau alikuwa anafanya kwa sababu ya mchungaji lakini ndani yake haoni kama ni Tatizo,  nikimsoma zaidi ameniambia kwamba amejadili hilo yeye  na mtumishi ambaye amemwambia hakuna kwenye Biblia palipoandikwa usivae suruali, hata mimi naunga mkono ila papo palipoandikwa tusivae mavazi ya kiume........... ( hapo chacha)  mavazi yakiume ni yapi?? kwa kaakili kangu kadogo kipindi hicho kanzu ndo zilivaliwa na wanaume na baadaye tukatengenezewa suruali  za kike na kiume................naomba nisikwambie vaa au usivae nenda kasome neno naulielewe na maamuzi yako yoyote yakakupe amani.

Tukitoka kuyaelewa maandiko  sasa tunakitu kinaitwa mazingira, mfano wangu mwenyewe nimezaliwa kwenye familia ambayo khanga na wewe, kitenge na wewe, mpaka ninavyokwambia sasa hivi Tanzania nina kabati nimejaziwa vitenge na khanga nikifika tuu nikufunikwa mwanzo mwisho mda mwingine napigiwa na simu  kuna kitenge kipya tumekununulia,  utaratibu huu umenifanya hata nikiwa kwangu huku nikijua ninakishughuli fulani wageni watakuja nguo ya kwanza ntakayowaza ni nguo pana au kujitupia khanga juu  lakini huyu Mama wawili maisha yake mengi amekulia shule na si nyumbani na kama mjuavyo mashuleni suruali ndo mpango na hata walezi wangu walikuwa wanalijua hilo kikubwa nilichokuwa nasisitizwa kwenye pochi yangu mwanamke lazima kuwe na khanga na nikiwa nyumbani kama nipo sebuleni kwenye mazungumzo  na mwanaume mfano Baba, Mjomba, Bamdogo  mazungumzo yanayohitaji tension  na yanakuchukua mda fulani,  khanga ni lazima...........  

lakini mazingira hayo hayo ninamarafiki zangu huku hasa wazimbabwe huwa wananishangaa sana na viroba vyangu vya vitenge na wanavitamani mnoo,  hapo mwanzo sikuelewa mpaka walipofunguka wakidhani nimetoka familia yakitajiri, kwani huko kwao vitenge ni gharama mnoo kuliko jeans na tops hivyo wengi wao hawakuwa na uwezo wakuvaa  na kujikuta suruali na top ndo vazi kubwa na hii imepelekea wengi wao hakuna vazi linalowafanya wawe comfy zaidi ya suruali........ nina huyo rafiki yangu ukimuona amevaa gauni au skirt hata kanisani utamuona anavyohangaika  yaani utamuhurumia anavyotembea kwa kujikanyaga kanyaga.

 na pia huku kwa wenzetu kunamisimu ya hali ya hewa hivyo utajikuta jeans ni mkombozi kwa hali ya hewa  fulani kiasi kwamba  inachukuliwa kawaida sana kwani ni vazi ambalo halimfanyi mtu kuwaza tofauti nikimaanisha limezoeleka sana yaani imekuwa kama moja ya tamaduni yao  na wakati kule kwetu hili vazi limekuja baadae  na bado halijazoeleka kwenye jamii fulani, hivyo unahitaji hekima  fulani ukiniangalia kabla ya hii post nimetoa post mbili mwanzo nikiwa nimetoka kanisani na moja nikiwa kwenye kajimtoko  kangu fulani so utaona tofauti huwezi ukanikuta nimevaa ile high waist kanisani  hata kama hali ya hewa inaniruhusu..............bado nataka kusisitiza hata kama umepewa amani ya jibu uvae au usivae bado kuna  vitu vyakuzingatia.........


 Namalizia na kipengele alichosema mdau Mume wake hapendi avae kanisani lakini hilo limekuja mara baada ya hawa watu kujitambua nakuanza kwenda kanisani japo kuwa ni vazi ambalo mumewe alimkuta nalo...... Ngoja ni kupe kajimfano Kwi! Kwi! Kwi! nimecheka kwanza maana kuna watu mapovu yatawatokaje sasa???? anyway chamsingi nieleweke kwa yule anayetaka kupona.  Haka nikama kajiutaratibu fulani ka Baba watoto wangu, hata siku kadhaa zilizopita kametokea tulikuwa tunatakiwa kwenda mahali fulani ambapo  Mimi nilijiandaa vizuri na vazi lilienda sawa ambalo huwa analipenda lakini hajawahi kuniambia why analipenda,  nasijawahi vaa kwenye tukio la dizaini hilo ila kwa jinsi lilivyonikaa( kila ...... na mbuyu wake) Taratibu namsikia Baba watoto, Mama umependeza lakini hilo vazi lipo............ akafunguka kimtindo, Mama watoto nikajiongeza kimtindo  nisije nikapoteza concetration  huko tunako kwenda........ nikarejea na kwa nini nilifundishwa kuvaa khanga sebuleni nikiwa kwenye mazungumzo,na pia nilizidi kujifunza pia  umbo la mtu pia linachangia nguo inaweza kuwa kawaida lakini nikivaa mimi nakuwa kama mti umevalishwa gauni hapo hata nikiingia kwenye maombi sitakuwa kwazo la mtu kuvusha  na kuamisha akili yake, lakini ukivaa wewe mdau duu Mume mwema anaweza akasahau kama yuko kwenye maombi anavusha tuu anachowaza kurudu nyumbani............sorry haka kajipengele kawa kubwa tuu lakini ndo hivyo tufanyaje sasa tunataka tupone.

 na mwisho namalizia hivi, suala la mavazi ni la muda, na  kwa kadiri muda na vile uelewa unavyokuwa kuna namna fulani ya  kiroho  na kupondeka  vitu huwa vinaisha vyenyewe na kuvifanya tena vinakunyima amani kabisa.... mfano wangu binafsi kipindi fulani ulikwa hunikuti nimevaa knee length yaani nilikuwa nikivaa ni very short na kama ndefu basi   ni ndefu haswa   imepambwa na mpasuo huo.hakuna aliewahi kunishurutisha niache au mimi mwenyewe kujistukia kwa kigezo kwamba watu wananiita mlokole kwa hiyo natakiwa ni act kama walokole ...... hilo  jamani nililikataa sipendi kufanya kitu kwa sababu ya vazi ambalo watu wananichukulia, huwa napenda kuwa real then   roho mtakatifu ananibadilishe nakunipa amani bila kumuogopa mwanadam yeyote, huwezi ukaamini siku hizi kuna picha huwa naziangalia nimevaa kidude hicho najiuliza sasa huu ulikuwa ulimbukeni, utoto, au?????  juzi juzi nilitakiwa kwenda kwenye shughuli kulikuwa na rangi husika tulitakiwa tuvae nilisaka hiyo rangi muda ulikuwa mfupi, nilifanikiwa  kupata iliyokuwa juu kidogo ya magoti huwezi amani sikuwa na amani na haikuwa mbaya  na shughuli yenyewe ilikuwa ya wanawake ,sema tu ile hali nimetokea kuanza kuzichukia nguo fupi  na sikutaka kuharibu shughuli ya muhusika.   nikisema hivyo wandugu kuna mtu naweza kumuona amevaa nguo fupi kwa eneo linalohusu nikaona amependeza haswa lakini sitamani kujiweka hapo naona sio mimi zina wenyewe. kwa hiyo usinielewe tofauti sichukii wewe uvae ila mimi mwenyewe najiona siko sawa ILA nikogo sensitive na mazingira kidogo yaani utakuta mtu amekuvalia kitu kituko sehemu isiyo sahihi mpaka naanza kuona aibu mimi wakati sijavaa mimi na hata kumwambia siwezi (hayanihusu)ila na baki kujisemea tuu huyu na yeye kale kajihekima nilikokapata mimi kakujiona limbukeni,kupania,kutokujua,................ naomba kamkute duu!!! fujo

Sunday, January 19, 2014

THE LOOK


 Nsajikuta najipenda tuu  i might keep this  natural look for sometime wandugu........ inanirahisishia  sana hasa kulingana na hili joto na shughuli zangu ................ ila ndo zinakuwa na  unyunyu wa olive oil balaa



 vikilo vimeondoka tena kidogo mweeeee mi naona nijisahaulishe tuu maana kila ninavyopania ndo naharibu kabisa  bado najipenda lakini  huko kungine huwa na  mimi natamani tu nione kunakuwaje kama na nyie mliojaliwa mkiamua kuongezeka haya, kupungua haya yaani kote kote mnaweza. 

 fashion hazitupiti au sio wapendwa......ila tunazitengeneza kidogo maana huu mvao wengi wao lazima tumbo lionekane lakini mimi kama mnijuavyo ( ushamba mzigo) nimejitahidi kuziba kale kaeneo  kama sijakwambia huwezi elewa..... ....... kwa wavaa mawigi makubwa  na mliojaliwa mkono ivalie kata mikono utapendeza zaidi but again inategemea unaenda wapi  hilo ndo la msingi kuliko yoooote.
  my self..............
 nenda kajipatie na wewe high wilst just make sure kakuzibia eneo la tumbo hakatofautiana colour na suruali /skirt yako ili kasiweke tofauti.

Saturday, January 18, 2014

SUNDAY LOOK.....


Niende wapi mie kama sio hemani mwa Bwana?????
 ni choice tuu wapo waliochagua kuamka na hang over, wapo waliochagua kuisahau kabisa siku kama ya leo unaweza ukamkuta mtu anauliza hivi leo juma ngapi viloe??? lakini ju8matatu mpaka ijumaa anaikumbuka ni siku ya kwenda kazini na  wengine wanaitambua na kuipuuzi kwani hawaoni umuhimu na wengine siku kama hii ni siku wasio taka kuikumbuka kabisa kwa walijeruhiwa mpaka wamefikia kuona wote tuwanafiki mbele za Mungu....................

ngoja nikwambie mwisho wa siku hesabu ni yako wewe na kile unachoamini,na kile unachokifanya ukiona hakikupi amani wala furaha zaidi yakuigiza ni muda  wa kujitambua , hujachelewa bado.... tulikuwepo huko na sisi Ahsante kwa ajili ya NEEMA ya ukombozi aiseee ..............yaani kama nakuona  rafiki ulivyovuta limdomo maana huamini kama inawezekana kwa sababu ya UGUMU WA MIOYO YETU......Alijisemea na YESU ( Musa aliruhusu taraka klwa sababu ya mioyo yenu migumu lakini tangu hapo Mwanzo........................marko 10:5........) yanayofuata ni akili mkichwa tusikariri sanaaa..... na hivyo ndivyo ilivyo katika kufanya maamuzi
Tafakari ujuwe mamlaka na uweza ulio ndani yako katu usikubali kuburuzwa.
Happy sunday wandugu

Friday, January 17, 2014

KUTOKA KWA MDAU.........

 HAYA WAPENDWA WE UNAONAJE, UNALICHUKULIAJE HILI?? SEMA NA SISI TUPONE MI NAOMBA NIZUNGUMZE BAADA YENU MAANA NIKIZUNGUMZA HAPA WATU TUTACHOKA KUSOMA ..... YANGU NITAIFANYA TOPIC KABISA NA JINSI NILIONAVYO NAKULICHUKULIA KAMA MTAZAMO WANGU BINAFSI.

(MSISAHAU KALE KABAJETI KETU WANDUGU)



Asante sana mama wawili'nafurahi kujibiwa ila jitahidi mpenzi hata kutupa neno tu au hata ushuhuda wako huwa unatufanya tuseme tunaweza pale tunapoona tumeshindwa na nikushuhudie tu;kupitia wewe Rose umenifanya niwe namtegemea Mungu sana yani imani yangu imepanda maradufu na namuomba sana Mungu anisaidie niwe mke mwema kama wewe ulivyo kwa mumeo;nikimaanisha nisiwe mama wa manung'uniko;Ila mama wawili naomba unieleweshe kuhuhu hili tene ikibibidi iwe topic kwenye kile kiwanja chetu.

Mimi nilikuwa ni mvaaji sana wa suruali lakini mume wangu alikuwa hapendi ila hakuwa na jinsi coz me ndo mavazi yangu;ila siku moja tukapata neema ya Mungu na kuingia kwenye wokovu nilifurahi sana;coz kuna vitu nina ushuhuda navyo'nilikuwa mnywaji pombe na sasa sinywi tena'mvaaji mavazi ya wanaume na sasa sivai tena(suruali)yani kwa kifupi naona nimebadilika hata mwenendo wangu'Sasa shuhuda yeneywe inaanzia hapa kwenye mavazi mpenzi'baada ya kuokolewa tukaanza kuhudhuria ibada kila nikienda kwenye ibada utakuta mtumishi wa Mungu anaongolea kuhusu suruali ila kwa ukaidi tu ikawa naikataa ile sauti kwamba kuvaa mavazi ya kiume sio dhambi;na huwezi amini sikuwa hata na sketi ikifika siku ya ibada ni shughuli mapenzi coz Mchungaji wetu anakataza kabisa kwa hiyo mimi nikawa na mavazi mawili nikienda kanisani sketi nikwa kwenye mambo yangu suruali ila Mr.alikuwa ananiambia sasa mama mke suruali mume suruali na watoto suruali huoni kama haipendezi kwa kweli alikuwa akinikwaza sana ila nilikuwa siachi kuvaa;sasa siku moja kanisni kulukuwa na semina kwa hiyo tulialika mtumishi wa Mungu kutoka sehemu nyingine ila nikashangaa sana ujumbe ule kama niliandaliwa mimi nao ni kuhusa mavazi;baada ya semina mume wangu akaniambia sasa unaonaje leo tukichoma zile suruali zako we nikamwambia jaribu;akaniambia au nikununulie pakti nzima ya kiberiti nilikataa kabisa japo ujumbe uliniingia mnoooooo.

Ikafika siku ya mihangaiko asubuhi nikatoa suruali yangu najiandaa sasa lakini mtumishi wa Mungu huwezi amini kila nikijaribisha roho ya Mungu inanikataza kabisa nikajikuta kwa mara ya kwanza nimeend kuhangaika nikiwa nimevaa suruali;sasa siku ya pili nikashindwa nkikavaa suruali yangu kama kawa vile nafika kituoni tu nakutana na Mchungaji kwa kweli nilifadhaika sana nikatoa kitenge changu nikajifunga lakini nafsi ikaniambia gf mana unamwogopa Mchungaji kulliko neno la Mungu lililotoka madhabahuni?nilijifariji lakini moyo ulikataa kabisa kwamba sipaswi kuvaa suruali na kwa kupitia neno hili KUMBKUMBU LA TORATI (22:5)Amini nilipona hiyo sehemu na sijisifu bali kwa neema tu.

Sasa mwaka jana mwezi kama wa nane nilikutana na Mtumishi wa Mungu akiwa na mke wake wao ni wenyeji wa THAILAND'sasayule mama na mume wake wamealikwa kutua neno j'pili moja kanisa fulani na yule mama akaniuliza naweza kwenda madhabahuni nikwa nimevaa hivi?nikimaanisha alikuwa amevaa suruali we acha niongee hapana mama ukipanda pale watu hawatakuelewakabisa nafikiri mama wawili nikisema hivyo unanielewa'nikamwambia kwanza ni dhambi nikampa na ufunuo kabisa;Basi yule baba akamchukua mewe ikabidi akamnunulie nguo amabazo sio suruali alivaa kiafrika kwa kweli alipendeza sana tofauti na alivyokuwa amevaa suruali'lakini nikashangaa yule baba walivyorudi kwenye ibada siku nyingine akaniita akaniambia wapi imeandikwa mwanamke asivae suruali? we nikamfunilia fasta coz huwa natembea na bible'akaniambia imeandikwa asifae mavazi ya kiume hayakutajwa ni mavazi gani kwa hiyo kuvaa suruali sio kosa nilibisha sana na kumbuka nilikuwa naongea na mtu mkubwa mnoo coz amesoma sana elimu ya dunia na mbinguni.

Nikamwambia hebu nitasfirie hili nene linamaanisha nini?mwisho akaniambia unajua kule kwetu kuna baridi sana na upepo kwa hiyo ukivaa sketi upepo ukija inapanda juu ndio mana watu kule wanavaa suruali na pia kuna baridi sana kwa hiyo ukivaa sketi unaweza ukaganda;hapo nikamwelewa mno kwamba wanavaa hivyo kutokana na mazingira waliyopo.Lakini akaniambia pia mtu anaweza asivae suruali lakini akawa na matendo ya ajabu na mwingine akavaa suruali lakini akawa na hofu na Mungu hapo napo nikamwelewa mnoooooooooo
ila nafsi yangu inakataa kabisa kuhusu hili vazi'na mume wangu sasa anafurahi kuniona niko tofauti si mvaaji tena wa hilo vazi na kuna mtu mmoja nilimshuhudia na yeye ametoka huko nilikokuwa mimi;back to you mama mawili amini ukikutana na neno zaidi ya mara tano linaongelea tu kitu kimoja Mungu anakuwa na mpango na wewe na anakubadilisha kabisa hata wewe ipo siku utakuja kusema mdau kweli ulisema yani inatikea tu kila ukitaka kuvaa roho wa Mungu anakushuhudia au nafsi inakataa kabisa tena unajiona ukivaa suruali hupendezi yan hata sijui nieleze vp.

Swali kwako mpendwa mwenzangu'wewe unavaa hilo vazi kutokana na mazingira uliyopo au  ndio kama kina sie tunaosema Mungu haangalii mavazi bali anaangalia moyo wa mtu?naomba ujibu kwenye blog ili tulio wengi tufunguliwe;au mimi ndo natumia biblia vibaya hasa kwa ufunuo kama huu Kumbkumb (22:5)Barikwa mama na zaidi ya yote kasome  Zaburi (35).nakupenda.

Thursday, January 16, 2014

BAJETI.......





Haya wapendwa wangu  mshindi wetu amenijia na budget hii ili aweze kujikwamua kimaisha, kama tulivyo msoma  unaweza ukamuelewa.............. 

 kwa yeyote aliyeguswa naomba tuwasiliane ( slayros@yahoo.com) panda mbegu kwa Bwana  kwa namna hii......  nakuhakikishia kama utatoa katika roho ya kweli nakupata kibari mbele za Bwana, Mungu atakukumbuka, itamkie neno kwa imani huku ukitarajia muujiza wako........ Ngoja nikupe siri  kiukweli mimi  sijajitosheleza  wandugu, mimi nimetoka kwenye familia ya kawaida sana  yaani ukiniuliza hata $1 huwa nikifumba macho huwa namuona mtu kwenye familia yangu anaihitaji ............. usinione hivi ....nina   majukumu mengi tuu Mungu pekee ndo anayenijua lakini kwenye suala la utoaji na Baraka za Mungu huwa naliweka kwa namna tofauti kabisa..... Naelewa kumsaidia ndugu ni kama kawajibu fulani,  ingawa siwezi kuwatimizia kila kitu, ninapo mpa ndugu kuna kale ka roho kana sema  huyu ni Mama yangu, huyu ni Dada, mkwe,  yaani kunakauthamani kidogo ndani yake, sadaka ya Mjane,yatima hizo ni sadaka ambazo tumeagizwa  wandugu nenda kasome maandiko yaani hizo nazo  bado huwa tunatoa kwa sababu .

 Nakuja kwenye hii sadaka ambayo yaani unatoa unataka mtu ainuke,  humjui hakujui hutoi kwa sababu yakuonekana ila unashuhudiwa rohoni kwa namna fulani utoe sadaka binafsi huwa naziita mbegu...........  Pia huwa nikiwa nauhitaji fulani ambao yawezekana  kiasi nilichonacho kwa muda huo hakitoshelezi hata nijikusanye vipi, huwa naamua kupanda mbegu huku nikimwamini Mungu hiyo mbegu itakuwa na kuvunwa........... huwa navimsemo vyangu ni kwa neema tuu mara nyingi hapo ujuwe kuna kupanda mbegu, kunamaombi yamefanyika, kuna namna fulani ambayo kibinadamu mtu hawezi kukuelewa,  kwa maana nyingine ( muujiza) ,asikwambie mtu kipindi hicho huwa nakuwaga na list ya matatizo mnoo, nakumbuka niliwahi pata lawama fulani baada yakujulikana  nimefanya kitu fulani ,huwezi amini nilishindwa kujitetea maana swala la imani bwana mapokea huwa yanakuwa tofauti na mara nyingi ukijitetea sana utamkosea na Mungu wako................


HEBU SHIRIKIANA NA MIMI TUPANDE MBEGU CHOCHOTE ULICHOGUSWA, 

 niaminivyo mimi huyu Dada anauwezo wa kujiangaikia akala yeye na mwanae  japo kwa taabu mnoo,lakini amechoka na hii hali ni mpaka lini, anatamani ainuke, anataka awe mahali fulani ambapo labda wewe umeshapafikia  au unangoja, hebu turuhusu muujiza wake na yeye ukamilike wapenzi. tuungane tuwe sababu ya muujiza wake.

Mbarikiwe sana sana sana .......tupeane Muda mpaka mwisho wa wiki ijayo kutoa ahadi then tutaanza kuzikusanya kitakacho patika ndicho Mungu alichokiruhusu.

MUNGU ATUWEZESHE NA KUTUONGOZA KATIKA HILI 

MBARIKIWE

BAJETI

USED PHOTOCOPY MACHINE
 1,000,000
Description: Macintosh HD:Users:suleimanmbeyela:Library:Caches:TemporaryItems:msoclip:0:clip_image001.png
COMPUTER

PRINTER

LAMINATION MACHINE

BINDING MACHINE
 1,000,000
CUTTING MACHINE

B. CARD CUTTING MACHINE

OTHERS

STATIONARIES &OTHERS
 500,000
REN PER YEAR
 1,200,000
UKARABATI AND SHELFS
 300,000
TOTAL AMOUNT
 4,000,000