Pages

Ads 468x60px

Thursday, October 3, 2013

TUZUNGUMZE


Ahimidiwe huyu Mungu aliyetupa hii neema ya ukombozi na kuishi maisha ya toba,Na kwa uelewa wangu huu mdogo, wengi wetu tumetolewa katika shimo haswa hatukuwa hivi tulivyo leo kabisa!!!!...... tumezaliwa katika mazingira ya dhambi, tumekulia ndani ya mazingira ya dhambi na hata tulivyoletewa hii neema ya ukombozi    mazingira bado yalibaki kuwa kama yalivyo ila ule umimi uliondani yangu ndio uliobadilishwa na kufanyika kiumbe kipya na kuweza kukabiliana na hayo mazingira yaliyonizunguka.................Namshukuru huyu Mungu aliyeruhusu nikapita huko kote na wakati mwingine huwa najiuliza kama nisingelipita huko nahisi wokovu wangu leo ungekuwa mgumu hasa kwa mazingira haya tulionayo nyakati za leoyaliyozungukwa na vishawishi vingi, ( hayo ni mawazo tuu ya Mama wawili na kusema hivyo kama Mama nasugua goti kila leo kumuomba Mungu asiruhusu Mwanangu apitie hata njia moja ya upotovu niliyoipitia) lakini kwangu mimi history imenifanya niwe jasiri  na kutokushawishika kwani nilikuwepo kwenye mazingira  hayo nakutolewa faster!!!! ni neema kwa kweli na ninafasi ya upendeleo JINA LA BWANA LIBARIKIWE................


Baada ya Gazeti hilo hapo juu ngoja nifunguke sasa...........

wandugu tumekuwa na kajimtihani fulani hasa ukitangaza wewe uko pande hii ( yakipendwa) utakuta mtu hayuko pande hii labda kwa sababu fulani fulani anataka kuingia bado hajiamini, anakuja kwako kwa msaada zaidi ila anavyokuja haji kivile na kumbuka huyu ni mwanachama wa Baba wa uovu na hayuko tayari kumpoteza mwanachama wake na wakati huo huo mama wawili hapa( mfano) ninaishi kwa toba lakini ile asili bado inaninyemelea km nilivyoeleza hapo juu..... hapo ndipo mazungumzo yatakuwa kati ya Baba wa uovu na ile asili niliyonayo  na matokeo yake,  mwenzangu ataondoka  na ile kauli hawa ndo walokole, na hivi ndivyo wanavyofanya, na maneno mengi yakukatishwa tamaa...... huyu mtu ataondoka  na majeraha yakukosa msaada na pia itanichukua muda au huo mda  usipatikane kabisa kumrudisha kwenye mstari kwani Baba wa uovu atahakikisha amemfungia na mageti kabisa asitoke na wala kunipa nafasi ya mimi kuingia kusawazisha lile nililogundua nimekosea....... labda neema ya Mungu tena ifanyike kwa namna nyingine............

wakati huo huo mimi mama wawili sasa nimejistukia ile neema ya toba ikanijilia nikatubu na kukumbushwa ( ole wangu nimkoseshae mtu ufalme wa mbingu) nikaugua kwa hili lakini kila namna nilivyotafuta nirudi kusawazisha nimekutana na geti sina hata pakuanzia na mara nyingi nakutana na kejeli ambayo itanipelekea kutenda dhambiya maudhi tena ninachoamua nikuachilia  nakuendelea kutengeneza na Mungu wangu.........................

Ninachotaka kusema ni hivi ndugu zangu

 1. Hii safari ni ya mtu binafsi inakutaka ufanye uamuzi binafsi bila kuangalia nani anafanya nini, na imekuwaje.......

2. ukisha ingia usikubali kunyweshwa maziwa kila siku kubali kukua nakukomaa kwa kujisomea neno nakulitafakari.... ni kweli tunahitaji muongozo katika kila jambo lakini bado kuna muda wa kukua na kujikomaza ( nawapenda wale wanitafutao kwa bidii ..........) huku kuendelea kubebwa bebwa ndio kunakotupelekea kuto kusonga mbele na majuto.... akili zetu zinakuwa zinamtegemea sana mwanadamu( aliyezaliwa na kukulia kwenye mazingira ya dhambi) kuliko yeye aliyetuokoa.

 hii imekuwa changamoto mnoo hata kwenye madhabau watu tumekuwa mashabiki wa watu na tumekuwa tukinyooshea sana vidole watumishi wa Mungu ........ukweli ni kwamba mtumishi akisimama  kwenye madhabahu akiwa anafundisha neno la Mungu ambalo hata wewe unalisoma, wandugu anastahili heshima tena funga domo lako kukosoa kosoa unajitafutia laana za bure.........na unatakiwa uelewe atakapomaliza pale madhabahuni huyu ni mtu km ulivyo wewe, anapitia tena mara nyingine zaidi yako,tofauti ni kwamba yeye amechaguliwa kutumika katika ile nafasi............... wanahitaji maombi yako ili kulinda nafasi.........


nimetiririka sio kama tunajitetea kiroho safi nimeona nifunguke maana watu tunapotea sana na ki ukweli haini bariki mimi kuwa chanzo cha kukupoteza................kunakipindi tunaita dry seasons ni nouma shetani huwa anatutumia haswa lakini mwisho wa siku TUNAYE SIMBA WA YUDA YEYE ALIYEUSHINDA ULIMWENGU...........


MAMA WAWILI


1 comments:

  1. UNAPENDEZA SANA MDADA KAMA KASICHANA IVI....go girl you rock

    ReplyDelete