Jiwe linatupwa gizani hata mimi linawezakunipata kiaina fulani lakini ndo hivyo tunajitambua taratibu na kile tulichokitambua tunajitahidi kushirikisha na ndugu zetu........... Nimegundua sisi wanawake tatizo sio lonya zetu tatizo hatujui tuzivalie wapi na wakati gani????? tunajikuta nguo ambayo tulitakiwa tuvae Kanisani tunaivaa kitaa,tuliyotakiwa tuvae usiku tunavaa play ground tena na michuchumio mara nyingine unaweza ukakutana na mtu kituko alichovaa mchana halafu ukakutana naye usiku tena unajiuliza sasa hii si bora angevaa mchana halafu hii usiku.zote ni nzuri lakini wapi na mahali gani zivaliwe ndio majangaz......
Nilichozidi kugundua kutokujua nini kivaliwe wapi na kwa mda gani kumetufanya tubadilishe kabisa zile nafasi tulizonazo kama zakuitwa Mama, Mke, Dada na zinginezo ........jamii inaweza isituambie na muda mwingine kutusifia kutujaza ujinga lakini kiukweli tunajishushia nafasi tulizo nazo...............
kuna kina sie ambao tumeonja na tamaduni za hawa wenzetu mwee tunafujo balaa yaani tunaiga na visivyoigwa mpaka wenyewe wanatushangaa tulivyowehuka..... hawa wenzetu wanavaa vikaptula hata kanisa hasa wale wenye umri kati ya miaka 18 kushuka chini, utakuta na sisi na rangi zetu na maumbo yetu hao tumevaa makanisani tena wengine ni wake za watu mwee...... haya basi tumeamua kuvaa ovyo kweli ukavae kigauni kifupi kinaangaza na jua hilo play ground????? yawezekana baada ya hapo unatakiwa kwenda sehemu nyingine panapokupelekea uvae hiyo nguo lakini kuna namna fulani tunayoweza kujistyle na bado kote tukaonekana na hatujachafua mazingira...........kila kitu kina umri,mahali na muda wa kuvaa haijalishi kina thamani gani.............
msisistizo nilikuwa na safari tatu bila kurudi nyumbani lakini naamini bado nilirock kila mahala sio saaaaana lakini, bado ilinitunzia kajinaafasi kangu nilikokuwanako bila mimi mwenyewe kujistukia........ hivi unajua kuna nguo tunaweza kuvaa wewe mwenyewe huna amani na mara nyingine utajikuta umeganda kwenye kiti hata mkojo ukubane hunyanyuki unaona aibu kupita kwa watu????? ishawahi kunikuta hii wandugu ni noooumaaa???? sasa sijui ulimvalia mtu, au ulitaka tuu uonekane na wewe umo?? au ndo ulishamuona fulani amevaa basi unataka kumuonesha km na wewe unayo bila kujali nafasi yako, umri, na umbo lako..........
mnisamehe km nimejeruhi hisia za mtu ningenyamaza nisingeitendea haki nafsi yangu.......
nimepiga picha nyumbani kabla ya safari baada ya picha visivyotakiwa kuvaliwa kwa mda muafaka vilibaki ndani ya gari.........
hapa nikiwa kwenye safari zangu zilizoniruhu kuvaa hivi
na hapa nikwa tayari kuelekea play ground kukutana familia yangu
na hii kuelekea kupata chochote na familia yangu baada ya siku kuwa ndefu Mama wawili hajaingia jikoni kabisa na huku nikizingatia hali ya hewa ( kajikoti) kamening"arisha kidogo .
Angalizo
kuvaa uchi sio kupendeza wala ujanja wakati mwingine kunaonyesha ulimbukeni nakujishushia hadhi yako.
hili nimelitambua mwenzenu na nimeanza kujistukia hata Baba wawili anisifie nimependeza na jua hii ni love blind tuu mwanamke kuchanganya akili yako na yakupewa..........
mbarikwe wadau
ookay..umependeza mwayego!; haya mambo ya mavazi ni mapana mnooo...cha msingi wewe mvaaji uwe comfortable tu na ulichokivaa;
ReplyDeleteumenena hakika tujitambue kina mama
ReplyDelete