Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 9, 2013

KIATU CHANGU


Hii ni kwa wale mlioniuliza ninawezaje kumudu familia na majukumu...... nimeona nikitoa ratiba yangu sidhani km itasaidia hasa ukizingatia tunatofautiana mnoo, ukipendacho wewe mimi sikipendi unachokipa kipaumbele wewe kwangu ni cha mwisho, na pia mazingira na nafasi za utekelezaji  bado ni tofauti, lakini nimeona nitoe kitu chakufikirika ambacho kitakufanya ujitathimini nakujigundua ukitumiaje kiatu chako.......

Mama wawili naamini maisha yangu ya duniani kwa sasa yamezungukwa na watu watatu japo kuwa nina wazazi, ndugu na marafiki.lakini hawa watatu kila ninachokifanya au kabla yakufanya hawa watu watatu lazima wawe kwenye mipaka yangu,  zaidi nikuangalia hicho ninachotaka kufanya au ninachofanya kinawaathirije???? na je kuna umuhimu?????

Mtu atamwaacha Baba yake na Mama yake naye ataambatana na mkewe nao hao wawili watakua mwili mmoja ( waefeso 5 ndo mpango mzima km msomaji kaisome)  
Kwa maana hiyo Basi mimi  Mama wawili kuamka asubuhi, kumuona mume wangu akienda kazini, kuwaandaa watoto kuwapeleka shule na mimi kwenda kubeba mabox au kulea wazee, kurudi kuwachukuwa watoto, kurudi nakuandaa chakula cha familia, kumsubiri Baba watoto ambaye yeye anachelewa kidogo kuliko sisi, akirudi anapenda kujitengenezea chocolate/milo drink anywe na wanae, acheze kidogo na wanae huku mama watoto nikianda meza tukae tule pamoja , baada ya hapo tupeane matukio ya siku, tusali,Baba watoto  au mimi  tukawalaze watoto huku tukiwasomea hadithi NI KITU  AMBACHO SIPO TAYARI KUUZA KWA FEDHA WALA DHAHABU............  nitakwambia kwa mifano halisi ( mwelevu atanielewa  mpumbavu atabadilisha maana, tumeambiwa acheni magugu na ngano yakuwe pamoja...........)

Niko kwenye nafasi nzuri  yakuweza kufanya biashara ya btn 30m-50m ( ha!ha!haaa!! hazipo mfukoni wandugu kwani hata mikopo si ipo? cha msingi nielewe) ambayo na mimi ningeweza kuonekana mwanamke wa mjini usiku na mchana nipo kwenye mapipa kubeba mizigo yaani bora mradi tuu kuleta heshima mjini na mimi nionekane, nimefanya utafiti wa hizo aina ya biashara nimejikuta naweza pata faida km 3m mpaka 4m kwa mwezi  sasa basi  ukinisoma vizuri hapo juu pamoja na ratiba zote bado hayo mabox yananipa 4m kwa mwezi na sina stress zakupata hasara au faida.. nikitoka mlango wa ofisi kila kitu nakiacha huko akili yangu ni Mume wangu na watoto......... sasa basi nina sababu gani yakuruka ruka barabarani kuiacha familia??  nini faida yake?????kuna umuhimu gani wa kuleta heshima mjini wakati nyumba yangu siitendei haki?????mi ninachoamini umaarufu ni wa muda na hakuna cha maana na mwanamke yeyote anayeishi kwa kutaka kuleta heshima mjini, au kufanya kwa sababu mama wawili amefanya, yaani kwa maana nyingine kufanya kitu bila kujitathimini nafasi ya kiatu chako uliyonayo we kwangu NI MPUMBAVU japokuwa  naamini 70% ya wanawake mtakaonisoma hapa mtaniona  mimi ndo mpumbavu haina shida mbele kwa mbele...............

uhalisia mwingine, nipo kwenye nafasi ambayo ningeweza kuishi city na wanangu, Baba watoto angefanya fly in fly out siku kadhaa nyumbani siku kadhaa mine site ( lets say Shinyanga na  Dar)lakini  kuna haja gani mi nawanangu tukala bata mjini kutwa kwenye high way tunaenjoy hela za mwenzetu ambaye yuko site, anakula mavyakula ya kopo yasiyo na radha wakati mwingine anahitaji mtu wakumtia moyo kwa kazi ngumu aliyoifanya, inashindikana kisa nataka kuwa mwanamke fulani fulani ujinga mtupu...........(MWANAMKE MPUMBAVU HUBOMOA NYUMBAYAKE KWA MIKONO YAKE)

nafikiri mpaka hapa baadhi ya watu tumeelewana,TUSIKURUPUKE,TUSIWE NA HARAKA,KUIGA KWETU KUWE KWA MANUFAA KIKUBWA NIKUJIANGALIA KIATU UNACHO KIVAA NA KUTUMIA NAFASI ILIYOPO ILI  AMANI, FURAHA NA UPENDO UKATAWALE MIOYONI MWETU.

Angalizo
sijasema mwanamke kushughulika ni dhambi, au kumruhusu mumeo afanye fly in out ni dhambi kuna watu wengine hivyo ndivyo inavyotakiwa iwe na wako sawa na mpango wa Mungu upo mbele yao 
na.....

hicho hapo juu ni kiatu cha mama wawili na hivyo ndivo anavyokitumia , binadamu tunatofautiana yawezekana wewe chako hakina nafasi km hizo zangu lakini kuna namna fulani kupitia kiatu changu unaweza kujiongeza nakujitambua zaidi,JICHUNGUZE

7 comments:

  1. umenigusa sana my Rose, watu wengi sana hawaelewi, na sisi proffesional women tuna kazi kubwa sana jamani kila siku mikutano, safari, huku una watoto, you really need to balance both and mostly your relationship to God, i thank GOD i have a very understanding family, highly caring husband and although i cant cook and clean daily like you ( wouldnt mind to ) still i manage to be there for every important activity, i love our quality time together and cherish each opportunity i have, you know being a director comes with a price, so we pay a high price for the lifestlye we chose, mimi ni mama, mke, mjasiriamali, mtaalamu mshauri, mfanyakazi, mwanakikundi kanisani....where do you really stop and care for your family and mostly important care for YOU...maana usipojiangalia wewe mwenyewe, huwezi kuwaangalia waliokuzunguka, so kwakweli japo yote nayafanya, ila ni kwa urefu wa kamba yangu, nikipata safari nafurahi kuwa nitalala bila stress nyingi za moooom !! si kuna wakati you need a breather ???

    ReplyDelete
  2. Rose umejibu swali langu vyema sana. Barikiwa mno mpendwa. Mimi ni graduate since 2008. Aisee nilipoacha kazi, nilipitia magumu sana. Lakini yote ni kwa ajili ya watoto wangu ninaowapenda sana. Japokua niko tanzania, yes naamini MUNGU atafungua macho na akili yangu. Naamini wewe ni mwana maombi, tafadhali sana nikumbuke kwenye maombi yako au hata kama una kikundi. Siku moja nitakuja kutoa ushuhuda hapa. Barikiwa sana.

    ReplyDelete
  3. Nimesoma jana na leo pia nikarudia kusoma... NIngependa kusema tu, Kila mtu ana maisha yake na maamuzi yake lakini ustawi wa familia ni jambo la muhimu sana kuliuko yote...kwa hivyo baasi wale ambao ni kama mimi na wengineo tulifunga ndoa katika makanisa tulifanay mafundisho ya NDOA tunafhamu kabisa anachokisema Rose hapa.

    Ningependa kukumbusha wewe msomaji na Rose pia kama Vile ambavyo watu tutumiwa na shetani bila kujua...Basi namomba niseme hivi Mungu alimpa hekima ya kujibu swali hili na kwa manufaa ya wengine pia hasa walioko nje na ndani ya Tanzania kujua somo hili sio jepesi tu kama ambavyo limeandikwa tafakari zaidi kwa upeo wa kimungu utaelewa.

    Mbarikiwe sawa na Bwana anoymous hapo juu Mungu hata kuacha kwakuwa wakati anakuumba alijua wewe utakuwa nani basi naomab nikuhakikishie kuwa anaujua mwisho basi usivunjike moyo na kuwa na imani ukimtumainai yeye, Je wamjua Yosefu aliyeuzwa na ndugu zake kama waijua habari hiyo utaelwa ninalo sema.

    Qr.

    ReplyDelete
  4. Amina unknown hapo juu. jambo la ajabu ni kwamba juzi nilikua nimefungua chanel fulani ya dini mida ya saa kumi na mbili jioni hua kuna katuni kwa ajili ya watoto. nilikua busy kuandaa juice lakini nilifanikiwa kuona katuni ya joseph alivyouzwa misri, ndoto aliyoiota halafu mwisho wa siku akapitia majaribu. leo tena mdau wa 3:14 am umerudia somo la moses. MUNGU ni wa ajabu, unaweza kumuomba jambo halafu akajibu kwa njia ambayo hukutarajia. this is more than a coincidence na naona ni muujiza. mbarikiwe sana. This blog is something. Barikiwa Rose, na wadau wote.

    ReplyDelete
  5. jaman nimelipenda hilo somo maana limekuja kwa wakati mzuri, maisha bila kubalance nalo ni tatizo hasa tulio kuwa kwenye maisha ya ndoa..








    ReplyDelete
  6. Vick nimeguswa ulivyoelezea ila hakika wewe ni mfanyakazi hodari na hauna mashauzi yakijinga.. ila angekuwa mwingine kwa position yako na taaluma yako sijui ingekuwaje.. ur my role model my dada.
    XOXO

    ReplyDelete
  7. thanks love.... anonymous wa 7:59 ubarikiwe sana

    ReplyDelete