Haya wadau salam zangu za mwaka mpya...... bila shaka wote tumefull na mikakati ya mwaka maana ndio kwanza tunaanza............. leo nimeona nikumegee kidogo moja ya vitu ambavyo kwangu ni msingi wa yote tutakayojuzana kwa mwaka huu......... ukipenda chukua yasipo kufaa niachie mwenyewe au sio....
1. shukrani
1. Mshukuru Mungu kwa vile ulivyo na kwa mambo yote aliyokufanyia yawe yalikupendeza au la....... aliyaruhusu kwa sababu........
2.Samehe
majaribu ni kawaida ya mwanadam lkn Bwana anatuokoa nayo, ni kweli tunajeruhiwa sana na kukatishwa tamaa tena na watu wakaribu ambao wanaweka vidonda ndani ya mioyo yetu............ hiyo yote ni njia ya muovu ili ukae ukiangalia vidonda ulivyonavyo na kukucheleweshea safari ya ndoto zako........ nimejifunza na ninaendelea kujifunza kuachilia ili niiandae akili yangu kuwaza yale ya msingi.........kama Mungu wetu anatusamehe sisi ni nani????
3. kuutafuta uso wa Mungu kwa nguvu na kwa akili zote maana ndipo ilipo chemchem ya uzima.
jamani soma maandiko usingoje kumezeshwa kila kitu...... km tujuavyo siku hizi manabii ni wengi, wengine wataka vitu na wale wanaongozwa kwa roho mtakatifu, ni kazi kujua km husomi neno........... hapo chacha!! kunawengine watakumezesha sumu utaibebea ikujeruhi mwenyewe na wale utakaowashirikisha hahahaaaaa!!!! itakusaidia ukalisoma mwenyewe kwa kumuomba roho mtakatifu akusaidie ili hata km ukitokea umepewa sio lenyewe utajua tu km hilo changa au la ukweli.......... ( MTU HATAISHI KWA MKATE BALI KWA NENO LA MUNGU)
4.Panga mikakati yako na umkabidhi Mungu
.kama mimi mama wawili kila mwaka naandika list yangu ya mikakati ya mwaka ,Mungu ni mwaminifu aisee ( NJOONI NA TUSEMEZANE NIPENI HAJA ZENU ZA MOYO.....)
5. Imani
Je nijambo gani gumu ambalo Mungu wetu hawezi??? yeye aliyekausha Bahari ndio tumaini letu, aliyefanya maji kwenye jangwa ndio msaada wetu,yeye aliyempigania Daudi goliati akateketea ndiye msaidizi wetu,yeye aliesema atakuketisha na wakuu ndiye alikufanya uwe hapo ulipo............
Angalizo
haya yote tarajia ugumu wakati fulani lkn mwisho wa siku ushindi ni wako..........
HAPPY NEW YEAR WADAU
Happy new year too mama wawili na be blessed.
ReplyDeleteVero!
Kheri ya mwaka mpya kwako na familia pi....Asante kwa mazungumzo haya..MUNGU azidi kukufunulia na kukutumi...Neema ya Mungu iwe nawe Daima!!!!!!!!
ReplyDeleteDUUU UMENIGUSA MAMA WAWILI ILA NTAJITAHIDI KUYAFANYIA KAZI NA KUYATAFAKARI THANKS HAPPY NEW YEAR
ReplyDeleteubarikiwe sana mama wawili and keep kumtegemea Mungu mana wenyewe hatuwezi kitu kabisa,sio juhudi zetu ni neema tu
ReplyDelete