Huku kwetu tumeanza hivi hatua chache kutoka kutoka hapa nyumbani kuna hicho kama park Mama mtu ndo nlienda kuficha Easter eggs asubuhi asubuhi nikarudi kuwavalisha twende tuka hunt ha!ha!ha1 ni aina tuu ya kuwa na family bond .... Kulikuwa navimanyunyu lakini tulikuwa wabishi ha1ha!ha!
Haya napita basi mnione bila shaka wote mko gado makamanda wangu........ kikubwa acha kulalamika just go with the flow kikubwa omba amani na Mungu ili kuthibitisha hivyo ndivyo alivyoruhusu iwe......
nimejirekodi kakitu ila sasa sijui ni ushamba wa you tube au yenyewe tuu imegoma naendelea kuishughulikia nikiwa na mda . matumaini yangu itakubali otherwise itabidi nijipange upya ha1ha!ha!
that serious face speaks everything ha!ha!ha!
kwa kweli nafikiri tunahitaji kumrudisha gardener wetu ha1ha!ha! maana duu!! sio kihivi yaani msitu umekubari hatariiiii.
Bwana Yesu ananiandaa mahali fulani......... Nakungoja Bwana sihangaiki na wajuzi wa Dunia bali kwa kunyenyekea mbele za bwana......
Wapenzi wangu kumekuwa kimya sana...... kikubwa kwa sababu ya mda ambao nimejiona km ikitokea kupost basi cha haraka ni mapicha kitu ambacho sina uhakika km ndio kusudi kubwa la blog yetu.......
Lengo kubwa la blog yetu ilikuwa nikumrudishia Mungu utukufu kwa yale aliyotenda anayotenda na atakayoendelea kutenda, nikimaanisha kimwili na kiroho, uelewa wa mambo na jinsi unavyoweza kukabiliana nayo.........Hivyo utakubaliana na mimi topic za Tuzungumze ndo kubwa zinazobeba ujumbe wa blog. Mapicha ilikuwa ni kajisehemu tuu kakuchangamshia genge.
Kutokana na kubanwa kidogo (jina la Bwana libadilikiwe ananiinua viwango kwenda viwango) lakini bado kuna hii kalama ambayo naamini nisiiache ikapotea...... naamini kuna wengi mnabarikiwa ha!ha!ha! badala yakukaa masaa matatu mpaka manne chini kuandika kufuta yaani too much nimejikuta nimekaa baada ya kutoka kanisani nawaza hayo masaa yakuandika yaani naweza sema huu ndo muda wangu mwenyewe hasa baba wawili akiwa hayupo nawatoto wako busy na movie zao baada ya kanisani............nikajikuta nimewaza kumuita mtoto anichukue video ya dk 10 kusave masaa yakuandika nilichotaka kuandika ha!ha!ha! yaani nizungumza kwa sauti hahaha!! nianze kujirekodi halafu niwarushie kitu ambacho naamini hakita chukua muda na labda kwenye kuzungumza sitatumia nguvu mnoo na akili ya kuchambua ili ujumbe ufike ha!ha!ha!
halafu ndo tuendelee na mapicha....
nimejikuta nasutwa sana kurusha mapicha tuu bila kusimamia kusudi ambalo hapo mwanzo lilikuwa kiukweli nimejikuta nateseka tuu km mkinisoma nimekuwa mvivu sana kuyapost huku ila ukinifuata facebook na instagram narusha rusha tuu.......
haya kwa udhamini wa Careen ingia kwenye link
ukajue nimezungumza nini.... hatukujipanga jamani imetokea tuu kiswangishi kiko humo ni noumaaa ha!ha!ha! na dogo kweli kunichukua kwa dakika 8-9 aisee...... nilimuahidi chocolate ha!ha!ha! wanaruhusiwa chocolate moja kwa siku so nimemwambia akitulia ya pili anapata ha!ha!ha! utaona mikono mara sijui kafanyaje lakini kwa ujumla ujumbe umefika......