Hivi imewahi kukutokea??? labda umekuwa ukitafakari juu ya kufikia mipango fulani au ndoto. Wakati mwingine unajua kabisa ili kuifikia ndoto hiyo kuna namna nyingi ambazo labda ni lazima uzipitie,Simnajua kuna ile yakufanya kwa nafasi yako then the rest unamuachia muweza wa yote .........maana amesema twende mbele zake tuhojiane na tumpe haja za mioyo.............
Sasa katika ile kutafakari au kujiandaa na ile nafasi yako yenye mipango mingiiiiii.......... Gafla anakuja mtu, anaongea na wewe, kwa macho ya kawaida unaweza ukadhani labda mjamaa anajua zaidi yako ha!ha!ha! lakini ukitulia kuitafakari ile sauti ya muhusika, namna alivyokuwa akielezea na mengineyo yote bora mradi kukupa majibu ya ndoto yako aisee kuna namna fulani yakipekee, ambayo unaanza kujiuliza hivi huyu ndo ananiambia mimi au??Basi, hii siku kwangu ilikuwa kihivyo yaani Bwana alisema na mimi kupitia kinywa cha mtu!!! we km hunielewi kasome
Yohana10:27 Kondoo wangu husikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata; 28 nami ninawapa uzima wa milele. Hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka katika mikono yangu. 29 Baba yangu ambaye amenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa hawa kutoka katika mikono yake. 30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.”
haikuishia hapo nikajikuta nimefunuliwa hili neno
Yoshua11
Ikawa Yabini mfalme wa Hazori
aliposikia habari za mambo haya
akatuma ujumbe kwa Yobabu mfalme wa
Madoni, na kwa mfalme wa Shimroni na kwa
mfalme wa Akshafu, 2pia kwa wafalme wa
upande wa kaskazini wale waliokuwa milimani,
katika Araba upande wa kusini mwa Kinerothi,
nchi chini ya vilima upande wa magharibi na
katika miinuko ya Nafoth-Dori upande wa
magharibi, 3kwa Wakaanani upande wa
mashariki na magharibi, kwa Waamori, Wahiti,
Waperizi na Wayebusi, katika nchi ya vilima na
kwa Wahivi chini ya Hermoni katika nchi ya
Mispa. 4Wakaja na vikosi vyao vyote na hesabu
kubwa ya magari ya kuvutwa na farasi, jeshi
kubwa, kama wingi wa mchanga ulio pwani ya
bahari. 5Wafalme hao wote wakaunganisha
majeshi yao na kupiga kambi pamoja penye Maji
ya Meromu, ili kupigana dhidi ya Israeli.
6BWANA akamwambia Yoshua, “Usiwaogope, kwa sababu kesho saa kama hii
nitawatia wote mkononi mwa Israeli, wakiwa
wameuawa. Utakata mishipa ya nyuma ya
miguu ya farasi wao na kuyachoma moto magari
yao.”
unajua nini Hapa nimesoma km adui lakini nilijikuta neno adui nimelipa jina ya mipango mirefu inayoniumiza kichwa ili kufikia ndoto yangu.Naamini Yoshua aliamini kuwa ushindi ni wake maana ni dhahili kuwa Neno la Mungu halijifungi,Ahadi zake ni lazima zitimie............ kwa macho ya kawaida Yoshua lazima aliumiza kichwa. kikubwa alikaa mkao wakungoja kusikia Bwana anasema nini juu ya hilo?Hebu jiulize ndani ya masaa 24 sio kwa vita hivyo vyakuungana majeshi mengi kha!!
Halafu unajua nini sauti ya Bwana inakujaga km kwakutekenya fulani hivi, kubembeleza fulani hivi, halafu tena inakujaga na option ukijisikia kusikiliza na kuamini au upotezee ha!ha!ha!ha!
NIMEMUONA SIMBA WA YUDA.......... SIFA NA UTUKUFU UMRUDIE YEYE MWENYEWE MAANA SIO KWA AKILI HIZI ZANGU BALI NI NEEEMA!!!
mapicha time
mtandio umegeuka nanilii chezea fashion wewe.......
nawapenda