Pages

Ads 468x60px

Wednesday, October 29, 2014

NIMEPENDEZA EEH!!!!

Ha!ha!ha!  nyie hata msiponisifia mimi ndo nishajisifia ............. Do you want the look?????  go follow akailatailors  on Instagram............ hutajuta  popote ulipo atakutimizia hitaji lako simmeona wenyewe??? nimefanya kumtumia vipimo tuu hajafanya kosa kitu kimekaa mahala pake....... Wachache sana aisee kama hawa kama huniamini uliza wapenzi wakushona nguo watakwambia fundi nguo ni nomaaa..............
 mimi huwa namwita kiranja mkuu  huko kwenye kijiwe chetu......
Mama umetisha!!! Ahsante mnoo Am a happy happy customer............Pongezi nyingi kutoka kwa Baba watoto pia



kwenye Matukio ya picha huwa hawakosekani ha!ha!ha!

Tunawapenda.

Monday, October 27, 2014

CAMERA IMENIVURUGAAAAAA......................

Mnajua nini Hii Camera yenu ina wivu na nyie ,au ina pepo inahitaji ikemeweeeee?????  Ha!ha!ha! sijui nimechezea nini basi inanitoleaje madudu na mazekingereza yakicamera mi bwana siyaelewi  kha!!!

Basi sasa nmatukio ya hii siku ndo mmekosa fanyeni kuonja tuu.........

Aisee si nikaenda mwenzenu kwenye event, watu walitakiwa hayo makofia wayatengeneze yaani hata kama umenunua basi uweke weke mavitu ionekane kama umeitengeneza mwenyewe ........ Mi mkinga hayo mambo bwana sinaga......... nikalibandika km nilivyo nunua.......  ofcourse sifa nilipewa mnooo, ila nafasi ya ushindi sikuitegemea kabisa na nilikuwa muwazi jamani sina nilichofanya hapa zaidi yakubandika kichwani........... Duu hapo ndo nasemaga yaani km ndio ni ndio tuu.Kibari cha Bwana hakinaga wewe ni nani?umetoka wapi?au nini na nini........ Mara kidogo nikaitwa eti mie ndo Winner nikajaribu kujitetea wandugu mi sijatengeneza hii kitu......... nilichosikia ni 95% ya waliokuwepo wakipaza sauti Haijalishiiii!!!(ha!ha!ha! nimeongeza chumvi mweee waliongea kiinglish lakini)

Anyway Sifa na utukufu zimrudie yeye aliye juu.......... kiukweli ukiona umezungukwa na rangi nyeupe zaidi ya mia moja halafu nyeusi ziwe hata kumi hazijafika na Bado ukatambulika na kuheshimika aisee usiichukulie poua!!!!Ni NEEMA!!! Wanao ishi nchi za watu mnanielewa hapa eti eeeh...........

Haya basi mfanye kuonja huo muonekano.........
Mmeniona eeh???

Kha!! mi mweusi lakini hapa Camera imeongeza chumvi mweee!!





with my Friend


in our own world........

love you all...

Friday, October 24, 2014

MIMI HAPA........

Tufanye kumaliza wiki yetu kihivi basi, Wandugu tusisahau kwenda kwenye mikusanyiko ya ibada. Muombe Mungu akusaidia usiwe tu ni mmoja wa mkusanyiko bali Akusaidie masikio ya rohoni usikie na kutambua kile alichoandaa kwa ajili yako. Wengine tumesahau hata mlango wa Kanisa labda kwa sababu tuliumizwa, Ngoja nikwambie Mungu aliruhusu hilo ili aone imani yako. Ulimpenda wewe kama wewe au ulimpenda kupitia aliyekuumiza, Ama labda unaona ni usanii tu yawezekana yule anayekuhubiria ulikutana nae kona fulani isiyompa Mungu utukufu (uwe na uhakika acha mambo mbofu mbofu yakuambiwa nakuhisi)  Sikia mpendwa wangu, Mungu wetu anatumia mtu yoyote yule ili kujenga ufalme wake.............. kikubwa heshimu madhabahu, ule muda na saa aliosimama madhabahuni nakukufundisha neno ambalo hata wewe mwenyewe unaamini ni neno la Mungu Eti ???kwani kusoma siunajua au?? hilo ndo la msingi mengineo achaga watu watumike na wewe ufanye yako.......

Haya  basi ndo mnionage nilivyojitumbukiza kwenye manguo makubwaaaaa Chezea fashion wewe???
nani huyu???
ndani ya tinted wee lazima unipende
nakununa kunaruhusiwa mjue.....

Nawapenda

Wednesday, October 22, 2014

MAMA WAWILI.......

Nani huyu???




eti nimeringa kwi!kwi!kwi!





jamani nyie imejileta bahati mbaya...... Ha!Ha!Ha! danganya toto nimeiachia makusudiiii

PENDA NYIEEE

Monday, October 20, 2014

BACK TO REALITY..................

 Thank God, Am loving & Enjoying where God put me @ the moment.................. Get my Hands dirtyyyyy  is the thiiing!!!!

 To all my Kalgoorlie people, why waste you precious time queuing in the car wash line??? Drop it to Stevo's detailing and you car will get my personal(lil Boss lady kwi!kwi!kwi!) attention.................. OhYes!! you can't beat that!!!

Whatever the reason,Our Full Detail Service will make you want to get in and go for drive.

kwenye maswala ya $$$ kakidhungu huwa kanapanda Ha!ha!ha!ha!
nikiwambia niko busy hamnielewi tuu???

niliwambia mpango NI nini unampa mteja no longolongo 


mwisho wa siku hata nikipata faida mara mia kwani we unaumia nini Bwana ???? acha uvivu wakuchunguliana shika jembe!!!!!


Thanks to my team........... they did justice to the exterior

 got my hands here!!! meeeiiin!! 


Glory & Honor be to God

Deuteronomy 30:9 
Then the Lord your God will make you most prosperous in all the work of your hands and in the fruit of your womb, the young of your livestock and the crops of your land. The Lord will again delight in you and make you prosperous, just as he delighted in your ancestors,

Wednesday, October 15, 2014

IMEBAKI KUMBUKUMBU TUU.............

Siku yetu ya mwisho tukasema sasa leo ni kukaa hotelini tuu huku tukikusanya vilago vyetu.......


 ila kwa kweli hii hotel nimewapa 99% hasa kwa watoto mzazi hutojuta.....  yaani kama bajet yako ya hotel tuu hutaki kwenda sehemu nyingine bado mtaenjoy humo humo ndani...... games za watoto kibao....... bila kuwasahau wazazi wana 4hrs free yakufanya yao ma bby sitter wapo humo humo ni wewe tuu kuwapata taarifa km utahitaji huo muda or not........


kwenye suala zima la maji ni shiiiida!!!


 Mara nikasikia tuendeni basi hata baharini tukapate upepo!!! maji tena ya humo ndani sijui haya radha mi sijui..........

Hapo chacha maji hayakuwa sana huo mchanga  sasa tulichimba,chora,andika............


msindikizaji nilikuwepo

kikweli  we had lots of fun!!!  haya sasa tumerudi kubeba mabox kama kawa huo ubusy wake sasa !!!!

Haya tunawapendeni nyinyi  wooote

Monday, October 13, 2014

NA MENGINEYO.............


 Humu ndani tulijionea jinsi movie inavyotengenezwa

 na sisi hao tunatengeneza kamovie ketu ha!ha!ha!

spotted 
Mama wawili in action chezea mimi nyie??? na vazi langu sasa!!
humu ndo ilikuwa hatari ............kujieleza nashindwa bwana!!! nyie angalieni picha tuuu kwi!kwi!kwi!


mweeeeee!!!


sinikajua moto kweli na ushamba wangu weee!!! nilipiga kelele nahisi wote walijua mpori pori kavamia jiji.........

Story ya huyu Scooby nini sijui..........sina hamu
Bwana sinikajua ride ya kawaida kumbe inakonipeleka ni roller coaster iko ndani kwa ndani..... humo ndani giza kujitoa huwezi yaani ni lazima  safari uimalize weee niliita majina yote humo ndani ungemsikia mwanangu anavyonihurumia mwee........ mumy we r going to finish soon, mumy dont cry, Mumy .......,Mumy ......... mtu mzima nalia mwanangu mbona hukuniambia km ndo hivyo,Slay weweeee....... Slay mwenyewe hayupo anatusubiri nje na Cristabell. Cristabell haruhusiwi so tukafanya zamu zamu huku Careen akitusindikiza....... Sirudii tenaaaaa!!!!

mbaya zaidi hayo madudu sasa yalikuwa yanakuja usoni kabisa kunitisha duu!!!!
mimi eti ukanibingilishe humo juu khaaa!!!


mwenzangu huyu Bwana ikifika kwenye hayo madude napewa la uso ,Mama we kama hutaki kaa pembeni  tutaonana nikimaliza.........kwi!kwi!kwi!

 Hapa mwenzenu nilizidi kujifunza hawa watoto wa dot com nikukazana kuwafunika kwa damu ya Yesu basi .................
 Unajua nini??Wanangu hawaangalii haya mavitu nyumbani kwangu nawanalijua hilo. kuna zile ambazo nimezipitisha na nyingine nimarufuku, sasa tulivyoingia humu ndani madude yote wanayojua wao nimarufuku kuangalia yalikuwepo ......... mmoja akanipiga swali la kizushi Mama mbona leo umetuleta tuangalie wakati nyumbani ni No??? nikawajibu leo mnaangalia kwa sababu sio video ni live na mko na Mumy & Dad. wee Baada ya hapo watoto walianza kutaja majina ya hayo madude kama wanashindana nani anajua zaidi...........Mie na Baba mtu tukatoleana macho na kuulizana haya mambo wamejulia wapi?saa ngapi?na lini?    Mwisho wa siku utaumiza kichwa ........fanya uwezalo kama mzazi then mkabidhi Mungu akusaidie yagizani usioweza kuyaona aiseeee...........mbaya zaidi ya gizani huwa wanayafanyia bidii kuyajua kuliko................



Kwa pamoja tunawapenda.........

Friday, October 10, 2014

KIJIWE KINGINE..........


The view
 ndo tukapanda huto tudude  mi hata sijui vinaitwa vinatutembeza huko juu tunaangalia yanayoendelea chini

 tumezoea kuona movie hapo ndo tukajionea live nakupanda tukapanda.............

 wabishi kila kitu lazima tuvamie

Dereva wetu alikuwa huyu
chezea Dereva kila kiendesho lazima aendeshe..........

sisi waleeeee

na mafarasi nayo tumo

Wanangu walifurahiaje sasa


weekend njema wapendwa wetu............