Pages

Ads 468x60px

Monday, September 15, 2014

TAFAKARI...............


Hii ya leo nimeshindwa kuipotezea kabisa!!!!!na hata ile sauti inayonishawi mara nyingi kwamba na hitaji muda imebadilika kuwa msisitizo, muda unavyozidi kwenda na kila ninalolifanya lazima kuwe na dakika kadhaa najikuta natafakari sana hili, napata masumbuko. Nimejitahidi  kwa akili za kawaida kulipotezea kwa kuhofia labda ntashindwa kulileta na kueleweka nimeshindwa.................

 Napengine nimehisi labda nimejazwa ujinga kama tujuavyo wote,  Mtu akisifiwa kuna namna fulani unaifeel ambayo, mwisho wake ukajikuta unaharibu, Lakini pia nimejiuliza pamoja na ile sifa je ???sijajifunza kitu, sijajikumbusha kitu, kwa nini napata masumbuko siku nzima basi???? vyovyote ilivyo ngoja nijitendee haki labda masumbuko yangu yatakwisha na kujiwekea kumbukumbu.

Ni mmoja wa wateja wangu wakubwa, Binafsi huwa namchukulia kama Baba ( Kibongo bongo hasa ukizingatia mtoto wake wa kwanza ni umri wangu) Lakini, ulimwengu huu niliyoko na namna tunavyodeal naye,naweza sema amekuwa kama rafiki na wakati mwingine mshauri hasa kwenye mambo fulani, Sijawahi kumfuata kwa ajili ya ushauri bali kila ninapokutana nae mara nyingi tutaongea, tutaulizana maswali mwisho wa siku mimi ntaondoka na kitu........... sijui kwa upande wake ila ninahisi ndivyo ilivyo hata kwake ( nimesema NINAHISI) yuko kwenye ulimwengu wa biashara almost miaka 20................

Na wakati huo huo ndani ya mahusiano yetu ya kibishara kuna huyu mtu watatu ambaye ni MCHUNGAJI  nlikuwa nahisi nima rafiki wakushibana japo huyu mwingine kwenye ulimwengu huu hayupo sana...........lakini leo nimejikuta natafakari tofauti...........(naomba nisizungumzie sana hapa nisije nikashindwa!!!! nimeileta ili ninavyoendelea ukanielewe ninachokitafakari ili kama umekusudiwa basi, sote tukajiongeze kwa kadiri kila mmoja wetu atakavyoongozwa..........

Leo sasa,
 Ndani ya dakiki kama 15 aliniswalika maswali mazito kwa habari hii ya wokovu na hata sijui ujasiri na mimi ulitoka wapi??? sijui mistari yakumuweka sawa ilitoka wapi?? maana wanasema maarifa bila daftari ni kazi bure..........Ahsante Bwana Yesu, maana  badae nikajiuliza hivi angeniuliza hilo neno linapatika kitabu gani sasa hata simu yakugoogle nilikuwa sina kwi! kwi! kwi! ila nina uhakika na neno limeandikwa, halafu !!!!basi tuu kujistukia kwani huyu Mungu aliyenipa hiyo mistari lazima angenikumbusha na mistari inapopatika km ilihitajika.............(binadam sisi bwana mmmmh!!!) 

Ninachomshangaa Mungu zaidi, kulikuwa kuna ile connection yakuelewana, yaani unaona kabisa huyu mtu haya maswali ndio yaliyomfanya abaki kuwa mwamini( asemavyo yeye naamini lakini  system nzima ya watumishi(wachungaji) haijanishawishi kuingia kanisani japo utotoni nilipelekwa kanisani na pia naamini Biblia lakini sisomi)

Ntakudokezea tena kidogo..........Miezi kadhaa iliyopita ametoka kuachana na mkewe wa pili  huo ni upande wake mwingine  wa maisha yake,ambao alinishirikisha lakini sikuwahi kuingiza maneno yangu ya wokovu km nilivyosema hapo  juuna yeye  (NAHISI a.k.a Mawazo yangu, mtazamo wangu)  mpaka leo tena nilivyokuja kutafakari nakuwaza...... Hivi unajua huwa tunajisahau hasa mtu anapokuwa na pesa, sijui huwa inakuwaje tunaamini wamejitosheleza sijui, hatudhani km kuna kitu zaidi ya pesa wanakihitaji, labda ni namna walivyojiweka au sisi ndio sababu..........labda ni ubinafsi, au haya tumesahau imeandikwa atakayenionea haya.................

Maswali yake ya leo yamenikumbusha hayo, nimetafakari sana kwa habari ya ubalozi imenifanya nikumbuke miezi kama sita iliyopita tukiwa watatu yaani mimi, yeye, na Mtumishi kuna kitu niliingizia ndani ya maongezi yetu ya kawaida katika kumshawishi huyu mteja  pamoja na lugha zetu za biashara na maisha ya kawaida ni vipi kama hata pande hii tukawa pamoja???,majibu aliyotoa kumlenga Mtumishi hasa mimi nikiheshimu ile nafasi ya Mtumishi ,ilinifanya nijisikie vibaya kwa nini nilianzisha .....................Kilichonifanya nipotezee ni ile respond ya Mtumishi ambayo mwishoni nikajua mazoea na urafiki ukizidi sana heshima nayo inaweza ikawa kigugumizi hivyo nikapotezea kabisa na kusahau.........  ukizingatia Biblia yangu inasema ni MARUFUKU KUWANYOOSHEA VIDOLE WATUMISHI weeee.... nduki sikutaka hata kujiuliza kulikoni hadi leo tena nilipojikuta kwenye tafakari

Nimewambia nimejazwa ujinga eeeh???? ujinga wenyewe ndo huu ,Baada ya Maswali mengi na maelezo mengi mwisho wa maelezo ameniambia Nahisi wewe ungepewa hiyo nafasi ungetusaidia wengi, nimekutana na wewe mwaka sasa na maongezi yetu ya leo umeanza kunirudisha kwenye mstari (amesema NIMEANZA hajaseme YUKO TAYARI SASA KUINGIA KWENYE MSTARI) hapo chacha!!!!

 Kabla ya hizo sifa swali lake la mwisho aliniuliza Je???? unasemaje kwa Habari ya mtu fulani (Mtumishi)  swali gumu sana kwangu ambalo hata yeye aliona amenipata .akasema kama ulivyonijibu maswali yote nikaridhika na bila wasiwasi ndani yako hata hili naamini utalitendea haki.japo nimekuona umestuka ............Kwi! kwi! kwi!

 Nilimjibu hivi, hata mimi sijui kwa nini nilijibu hivi,

Unajua wokovu ni wa mtu binafsi, na Mungu anaweza mtumia mtu yeyote yule kwa ajili ya ufalme wake, hata wewe kuna nafasi yawezekana Mungu anakutumia pahala(which is true ana moyo wakusaidia sanaaaa)  lakini haimaanishi ufalme wa Mungu ni wako. yawezekana hapa nimetumika tuu kukupa majibu yaliyokupa amani lakini bado mimi sio mkamilifu................... akanikatisha No!!wewe ni mkamilifu na km huamini nakuhakikishia hilo , AKANIVURUGA nikaona sasa tunapakana mafuta kwa mgongo wa chupa nikaanza kufunguka no sometimes i argue with my huby, i get mad, sometimes nimeshindwa kuwa balozi mzuri,yaani nikaanz kukumbuka na maugomvi gomvi niiyosabisha kwenye jamii, ninavyoishi na jamii.................. yaani nilifunguka kama vile naungama maana sikukumbuka lolote nzuri nililolifanya bali ni makosa tuu( Ahsante Yesu maana kwakupigwa kwako nimesamehewa) mpaka hapo aliponikatisha akasema huo wote ni ubinadam na kama mtu akifanya hivyo ninamuelewa kabisa, lakini naamini wewe huwezi ukapanga mbinu zakumdhuru mtu!!!!!!!! mmmmh!!!

 hapo ndipo MASUMBUKO YALIPOANZA, NILIJIFUNZA KITU.


 NILIPOACHANA NAYE NIKAJIKUTA KUNA MAANDIKO HUWA HATUYAELEWI, TUNAYABEBA NA KUYAPA SURA TOFAUTI
mfano. Nabii hakubaliki kwao naTusichangamane

Tukutane kesho kwenye Tafakari 2 nikushirikishe mwenzio Nabii hakubariki kwao na Tusichangamane limekaaje sasa mukichwa.......

1 comments: