Pages

Ads 468x60px

Monday, September 29, 2014

ONESIES DAY.....................

a.k.a mnyelamumo  kama wewe wakusini huko unalielewa eti eeh??? ha! ha! ha! ha! siku yetu yakivivu vivu nimichezo tuu ndani ya nyumba na left over kwenye friji ..............

Duuu ila jamani watoto wana pumzi mwee!!! wananipigishaje kwata yaani huu mwili unahitaji mazoezi aisee sina pumzi!!!
 Haya ndo mniambie naenda kujiandikisha gym  maana ni hatari nachoka haraka mnoooo.......... haya  ndo mniambie mazoezi gani nikafanye ya afya  nimesma ya afya  masharti hutu tunyama tubaki kama tulivyo au tuongezeke kidoooogo!!!!Sasa tukiisha itakuwaje???? mweee!!!

Wanangu jamani wakimuona Mama yao na hili gwanda wanafurahije na wao mbio kwenda kuvaa maana wanajua its Mumy & them time...........



 bora mradi tuu siku iendee

 hayo mapaint yao walitoka nayo kwenye birthday jana tukiingia kuoga hata hatushughuiki nayo tunajimwagia tuu maji kwi! kwi! kwi!




priceless.............

Tunawapenda

THE LOOK....................


Nani huyu???
Muke ya Slay
Nawapenda

Saturday, September 27, 2014

MREJESHO............

Wapendwa nilisema  ntawaambia kwa nini huu mwezi nimewachomesha mahindi sana japo, ni kawaida yangu kutokana na hali halisi ya kimaisha,  lakini kwa mwezi huu naona imekuwa too much.... Wengine mmeni inbox kutaka kujua kulikoni Mbarikiwe mnoo. 

Haya ngoja niwape mrejesho............

 Kama baadhi yenu mjuavyo maisha yangu ya siku za kazi ndo haya (pichani) ............Kwa mwezi huu ubusy umeongezeka  sana kwa sababu nimeona nifunge kaofisi kidogo kwa ajili ya Binti yenu Careen si mnajua ndo tunasherekea miaka sita???? basi kama familia tumeona tupate sababu  yakusahau mambo mengine yoooote ili tuwe na muda wa kubond zaidi kama familia.

Ninachomshukuru Mungu Biashara yangu kwa sasa haiangaiki kupata wateja......... yaani ninawateja ambao kila siku ya Mungu lazima wanipe kazi ,Ni nguvu zangu tuu mwenyewe( JINA LA BWANA LIBARIKIWE)........ Kiukweli ni mwendo wa toa gari ,Ingiza gari na  mara nyingine inanibidi nikatae kazi za wateja wa kawaida, maana nakuwa nimezidiwa mnooo ......Hasa ukizingatia huku kwetu kupata nguvu kazi ya haraka haraka ni kazi mnooo na hata ukipata sometimes unaona bora ukomae mwenyewe..........(Hapa ndo nawakumbukaga mateja wa Bongo duu!!!! ningewapaje ajira nakuwapiga neno huku nikiji Ray C foundation humo humo Kwi! kwi! kwi! Tatizo visa duuu!!!!) 

Anyway,

 ili kuiweka biashara kwenye mazingira mazuri  ya kipesa na kuwafanya wateja wangu  wasihangaike sana kwa kipindi ambacho sitakuwepo, aiseee!!! imebidi tupige double mzigo( Thanks to the team)....... yaani ni mzigo haswa leo nimekamilisha mahesabu ndo nasikia mwili hauna kazi ni choka mbaya............

Naamini kwa kipindi ambacho sipo kuna $$$ nyingi nimeziacha ziende lakini  nahitaji haka kabreak mwee!!! halafu ni vile tuu hatujui jamani....... break ni njia nyingine yakurudisha shukrani kwa Mungu kwa jinsi alivyokuwezesha .................

Nimetamani sana, hii break ningekuja Bongo mweee!!! kwa kweli nimewamiss mnoooo.......... miaka miwili na kitu sasa  mguu haujatua Bongo!!!!! tatizo moja tu....... Mungu anisaidie nipate mtu wakumwamini kumwachia Biashara yangu mweee!!!  Hii kazi inahitaji mtu mwenye moyo wa kazi sio tu kwa sababu anataka pesa yakujikimu, inahitaji mtu atakae ifanya kama biashara yake,mwaminifu, anayemthamini mteja na kujishusha ikibidi, anayeamini huduma anayoitoa leo itajitangaza yenyewe kwa kipindi kirefu, asikwambie mtu kwa wale wafanya biashara wooote kama utashindwa kumuhudumia mteja pale anapoondoka akaridhika na huduma yako, Ndugu utajaza matangazo kwenye ma Instagram, Blogs,maredio na tv mwisho wasiku utapoteza $$ na nguvu zako bure........... tena hasa huku tulipo utajutaaa!!!............ Acha mteja akutangaze mwenyewe yes, utapata ambao kwa namna moja ama nyingine hawakuridhika  huwa hawakosekani lakini, mwisho wa siku asilimia kubwa ya kile unachokitoa ndo kinajitangaza.........( Bila kusahau kuachilia upako kwi! kwi! kwi!)

Kwa kusema hivyo basi Wapendwa wangu Bongo bado ngumu mnooo!!!Lakini namwamini Mungu hili litafanikiwa tuuu.......yaani nahitaji @list mwezi.........si mnajua tena lazima twende mashambani  kina Mbeyela, kina Mwinuka, kina Sanga, Wapendwa,Mashoger,Zenji,Mwanza,Arusha is a must go, mpaka ni kwa Be you Fans duu!!! hata mwezi hautoshi..........





Haya ndo Maisha ya Mama wawili...........

NAWAPENDAAAAA!!!

Thursday, September 25, 2014

NIKUSHIRIKISHE...........


Wandugu mwenzenu pamoja na uchovu, huwa lazima nipitie NENO........ niko tayari kuwasahau humu ndani lakini japo dakika tano tuuu nijiongeze kwa Neno.Wapendwa wangu hebu jengeni haka kautaratibu,HUTAJUTAA............ Halafu unajua nini huhitaji kusoma kama gazeti mpango nikuelewa sio kukariri au kumaliza ukurasa. 

Tafadhali usifanye kwa sababu Mama wawili amesema..... Weka nia Muombe Mungu akupe Masikio ya rohoni yaani kuna siku unaweza ukasoma mstari mmoja tuuu na roho yako ikapona.


Leo nilikuwa na 1Wakorintho1 nilipofika hapa nimeshindwa kuvumilia nimeona niingie tuu kukushirikisha


26. Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za binadamu; wengi hawakuwa wenye nguvu au watu wa tabaka ya juu. 27 Ndiyo kusema, Mungu aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni upumbavu, ili awaaibishe wenye hekima; na aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni dhaifu, ili awaaibishe wenye nguvu. 28 Mungu ameyachagua yale ambayo kwa fikira za dunia ni mambo yaliyo duni na yanayodharauliwa, mambo ambayo hata hayakuwako, ili kwa hayo ayafutilie mbali yale ambayo kwa fikira za binadamu ni mambo ya maana. 29 Basi, hakuna mtu awezaye kujivunia chochote mbele ya Mungu. 30 Mungu mwenyewe ndiye aliyewaunganisha ninyi na Kristo Yesu. Mungu amemfanya Kristo awe hekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwa na Mungu, tunakuwa watu wake Mungu na kukombolewa. 31 Basi, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Mwenye kutaka kujivuna, basi, na ajivunie kazi ya Bwana."


nawapendaaaaa!!!!

Monday, September 22, 2014

GUESS WHAT?????

SHE IS 6YRS OLD...................

SIFA NA UTUKUFU ZIMRUDIE YEYE ALIYE KWELI NA AMINA, ANAYEZIANGALIA AHADI ZAKE ILI APATE KUZITIMIZA,ALIYESEMA HATANIACHA WALA KUNIPUNGUKIA........ NIMEMUONA KWA NAMNA YA AJABU, NIMESHUHUDIA MPAKA WAKATI MWINGINE SIJIAMINI, SIO KWAMBA SIMUAMINI YEYE BALI NI VILE NINAVYOJICHUNGUZA NAKUTAFAKARI UPENDELEO HUU ALIYONIPA!!!!!!!! KIUKWELI SIKUSTAHILI!!!

 YAWEZEKANA USINIELEWE, MIMI NDIO NINAYEJIELEWA KAMA SI NEEMA YA UKOMBOZI YAWEZEKANA MAMA WAWILI UNAEMUONA LEO INGEKUWA HABARI NYINGINI..............

AHSANTE MUNGU,BABA WA MABABA,MFALME WA WAFALME,SIMBA WA YUDA HAKUNA KAMA WEWE NA HATATOKEA DUNIA KOOTE.

halafu nyie eti siniliwambia mwenzenu nimeacha kulia lia bila sababu ila kwenye hili eneo sijaelewa bado yaani nikianza kutafakari kwa habari ya kitu changu binafsi  labda tuseme mtihani wa maisha niliofaulu,ndoa na mara nyingine nikawaangalia wanangu wenyewe wanasmile labda badala yakurudisha ile smile machozi yanaanza kunitoka,  yaani tuvitu tuuu na asilimia kubwa naweza kusema 100% yote ni vitu ambavyo na takiwa kufurahi. ninaposhindwa kabisa nikimalizia ahsante Mungu weee!!!!

imenitokea hata leo asubuhi nimeamka kwa furaha nije nidoborishe mwenzenu nimekuza nini na nini kama Mama yoyote yule Duuu!!! yaani hayo maandishi hapo juu niliyoandika imebidi nizabe kibao kwanza(joke) nitulize akili ndo nijipange kwa utulivu hata hivyo nilivyofika hapo kati nimejikuta tena nimeanza anyway..................

HAPPY BIRTHDAY  TOTO YA MIMI
Nimekapa maneno yake leo katajijua mi naamini sikio limesikia, akili itamkumbusha tuu huko mbeleni na Neema ya Bwana itamtangulia..................
Kaone kwanza hiyo shughuli mpaka kametulia hapo mkononi ni balaa!!! nimekambia kunyanyuliwa na Mama yake kwake iwe old fashion duu!!  na kwa taarifa nilizonazo kutoka kwa mwalimu wake yeye ndo tallest wa darasa na wa pili kwa uzito...... usishangae Mama yake hana mwili dogo kashajisevia mapema......

 Lets see Baba,Mama na Cristabell wamekuandalia nini Toto zuriiiiii..........


Sunday, September 21, 2014

MMENIMISS EEH!!!

Haya ntawambia kwa nini wiki mbili hizi ubusy umekuwa ubusy haswaa.............mnivumilie....
muonekano wa jumapili

miondoko
 topic yetu naikumbuka itaendeleaaaa
nawapendaje sasa!!!

Monday, September 15, 2014

TAFAKARI...............


Hii ya leo nimeshindwa kuipotezea kabisa!!!!!na hata ile sauti inayonishawi mara nyingi kwamba na hitaji muda imebadilika kuwa msisitizo, muda unavyozidi kwenda na kila ninalolifanya lazima kuwe na dakika kadhaa najikuta natafakari sana hili, napata masumbuko. Nimejitahidi  kwa akili za kawaida kulipotezea kwa kuhofia labda ntashindwa kulileta na kueleweka nimeshindwa.................

 Napengine nimehisi labda nimejazwa ujinga kama tujuavyo wote,  Mtu akisifiwa kuna namna fulani unaifeel ambayo, mwisho wake ukajikuta unaharibu, Lakini pia nimejiuliza pamoja na ile sifa je ???sijajifunza kitu, sijajikumbusha kitu, kwa nini napata masumbuko siku nzima basi???? vyovyote ilivyo ngoja nijitendee haki labda masumbuko yangu yatakwisha na kujiwekea kumbukumbu.

Ni mmoja wa wateja wangu wakubwa, Binafsi huwa namchukulia kama Baba ( Kibongo bongo hasa ukizingatia mtoto wake wa kwanza ni umri wangu) Lakini, ulimwengu huu niliyoko na namna tunavyodeal naye,naweza sema amekuwa kama rafiki na wakati mwingine mshauri hasa kwenye mambo fulani, Sijawahi kumfuata kwa ajili ya ushauri bali kila ninapokutana nae mara nyingi tutaongea, tutaulizana maswali mwisho wa siku mimi ntaondoka na kitu........... sijui kwa upande wake ila ninahisi ndivyo ilivyo hata kwake ( nimesema NINAHISI) yuko kwenye ulimwengu wa biashara almost miaka 20................

Na wakati huo huo ndani ya mahusiano yetu ya kibishara kuna huyu mtu watatu ambaye ni MCHUNGAJI  nlikuwa nahisi nima rafiki wakushibana japo huyu mwingine kwenye ulimwengu huu hayupo sana...........lakini leo nimejikuta natafakari tofauti...........(naomba nisizungumzie sana hapa nisije nikashindwa!!!! nimeileta ili ninavyoendelea ukanielewe ninachokitafakari ili kama umekusudiwa basi, sote tukajiongeze kwa kadiri kila mmoja wetu atakavyoongozwa..........

Leo sasa,
 Ndani ya dakiki kama 15 aliniswalika maswali mazito kwa habari hii ya wokovu na hata sijui ujasiri na mimi ulitoka wapi??? sijui mistari yakumuweka sawa ilitoka wapi?? maana wanasema maarifa bila daftari ni kazi bure..........Ahsante Bwana Yesu, maana  badae nikajiuliza hivi angeniuliza hilo neno linapatika kitabu gani sasa hata simu yakugoogle nilikuwa sina kwi! kwi! kwi! ila nina uhakika na neno limeandikwa, halafu !!!!basi tuu kujistukia kwani huyu Mungu aliyenipa hiyo mistari lazima angenikumbusha na mistari inapopatika km ilihitajika.............(binadam sisi bwana mmmmh!!!) 

Ninachomshangaa Mungu zaidi, kulikuwa kuna ile connection yakuelewana, yaani unaona kabisa huyu mtu haya maswali ndio yaliyomfanya abaki kuwa mwamini( asemavyo yeye naamini lakini  system nzima ya watumishi(wachungaji) haijanishawishi kuingia kanisani japo utotoni nilipelekwa kanisani na pia naamini Biblia lakini sisomi)

Ntakudokezea tena kidogo..........Miezi kadhaa iliyopita ametoka kuachana na mkewe wa pili  huo ni upande wake mwingine  wa maisha yake,ambao alinishirikisha lakini sikuwahi kuingiza maneno yangu ya wokovu km nilivyosema hapo  juuna yeye  (NAHISI a.k.a Mawazo yangu, mtazamo wangu)  mpaka leo tena nilivyokuja kutafakari nakuwaza...... Hivi unajua huwa tunajisahau hasa mtu anapokuwa na pesa, sijui huwa inakuwaje tunaamini wamejitosheleza sijui, hatudhani km kuna kitu zaidi ya pesa wanakihitaji, labda ni namna walivyojiweka au sisi ndio sababu..........labda ni ubinafsi, au haya tumesahau imeandikwa atakayenionea haya.................

Maswali yake ya leo yamenikumbusha hayo, nimetafakari sana kwa habari ya ubalozi imenifanya nikumbuke miezi kama sita iliyopita tukiwa watatu yaani mimi, yeye, na Mtumishi kuna kitu niliingizia ndani ya maongezi yetu ya kawaida katika kumshawishi huyu mteja  pamoja na lugha zetu za biashara na maisha ya kawaida ni vipi kama hata pande hii tukawa pamoja???,majibu aliyotoa kumlenga Mtumishi hasa mimi nikiheshimu ile nafasi ya Mtumishi ,ilinifanya nijisikie vibaya kwa nini nilianzisha .....................Kilichonifanya nipotezee ni ile respond ya Mtumishi ambayo mwishoni nikajua mazoea na urafiki ukizidi sana heshima nayo inaweza ikawa kigugumizi hivyo nikapotezea kabisa na kusahau.........  ukizingatia Biblia yangu inasema ni MARUFUKU KUWANYOOSHEA VIDOLE WATUMISHI weeee.... nduki sikutaka hata kujiuliza kulikoni hadi leo tena nilipojikuta kwenye tafakari

Nimewambia nimejazwa ujinga eeeh???? ujinga wenyewe ndo huu ,Baada ya Maswali mengi na maelezo mengi mwisho wa maelezo ameniambia Nahisi wewe ungepewa hiyo nafasi ungetusaidia wengi, nimekutana na wewe mwaka sasa na maongezi yetu ya leo umeanza kunirudisha kwenye mstari (amesema NIMEANZA hajaseme YUKO TAYARI SASA KUINGIA KWENYE MSTARI) hapo chacha!!!!

 Kabla ya hizo sifa swali lake la mwisho aliniuliza Je???? unasemaje kwa Habari ya mtu fulani (Mtumishi)  swali gumu sana kwangu ambalo hata yeye aliona amenipata .akasema kama ulivyonijibu maswali yote nikaridhika na bila wasiwasi ndani yako hata hili naamini utalitendea haki.japo nimekuona umestuka ............Kwi! kwi! kwi!

 Nilimjibu hivi, hata mimi sijui kwa nini nilijibu hivi,

Unajua wokovu ni wa mtu binafsi, na Mungu anaweza mtumia mtu yeyote yule kwa ajili ya ufalme wake, hata wewe kuna nafasi yawezekana Mungu anakutumia pahala(which is true ana moyo wakusaidia sanaaaa)  lakini haimaanishi ufalme wa Mungu ni wako. yawezekana hapa nimetumika tuu kukupa majibu yaliyokupa amani lakini bado mimi sio mkamilifu................... akanikatisha No!!wewe ni mkamilifu na km huamini nakuhakikishia hilo , AKANIVURUGA nikaona sasa tunapakana mafuta kwa mgongo wa chupa nikaanza kufunguka no sometimes i argue with my huby, i get mad, sometimes nimeshindwa kuwa balozi mzuri,yaani nikaanz kukumbuka na maugomvi gomvi niiyosabisha kwenye jamii, ninavyoishi na jamii.................. yaani nilifunguka kama vile naungama maana sikukumbuka lolote nzuri nililolifanya bali ni makosa tuu( Ahsante Yesu maana kwakupigwa kwako nimesamehewa) mpaka hapo aliponikatisha akasema huo wote ni ubinadam na kama mtu akifanya hivyo ninamuelewa kabisa, lakini naamini wewe huwezi ukapanga mbinu zakumdhuru mtu!!!!!!!! mmmmh!!!

 hapo ndipo MASUMBUKO YALIPOANZA, NILIJIFUNZA KITU.


 NILIPOACHANA NAYE NIKAJIKUTA KUNA MAANDIKO HUWA HATUYAELEWI, TUNAYABEBA NA KUYAPA SURA TOFAUTI
mfano. Nabii hakubaliki kwao naTusichangamane

Tukutane kesho kwenye Tafakari 2 nikushirikishe mwenzio Nabii hakubariki kwao na Tusichangamane limekaaje sasa mukichwa.......

Thursday, September 11, 2014

THE LOOK........

 Yaani mkiona siku nyingine napiga deshi huwa nataka kuja kuzungumza ila sasa muda kila nikiubana unakataa mwenzenu............ sometimes mpaka point zinapotea naamua kupotezea sijui shetani ndo anakuwa anakomaa nisishare au ni akili zangu zinalazimisha kumbe sio wakati wake.......

 haya basi tupate ngoja nirushe the look tusiwe kimya sanaaaa

 nahisi Camera ilikuwa na mark fulani zimereflect kwenye gauni...



spotted



NAWAPENDA

Tuesday, September 9, 2014

Monday, September 8, 2014

SIVUMI LAKINI NIMO KWI! KWI! KWI!!!!

Haya wandugu  mwanamke kujiongeza kidogo eti  eeeh.........sawa tunapiga goti naamini kabisa bila goti Haiwezekani  we kama mbishi haya...........  haya mengine ni nyongeza tuuu.   Haya mwenzenu  ilikuwa Father's day huku kwetu kwa kweli sikuwaza kuwafanyia chochote wanangu kwa ajili ya Baba yao, walikuwa na vizawadi vyao wenyewe mashuleni huko nilikuwa nawasaidia tuu kuvificha Baba yao asivione mpaka siku ifike.......... Ukizingatia a night before tulikuwa na couple's day out mtu mzima nikajua ntampa maneno matamu huko,  basi inatosha, Na asubuhi mwanamke ntaenda kuwaamsha wanake waje wamsuprise Baba yao chumbani............ Duu!!!!  hapana chezea Mwanamke nimestuka saa kumi na mbili sio kawaida ujue???? akili hainipi, natamani kufanya zaidi na nilichopanga ( Chezea kupenda nyie!!!) na mara nyingi siku kama hizi yeye ndo huwa anatupa offer yakututengenezea Breakfast , Sikuhitaji kabisa hii offer kwa siku hii. Mwanamke nilinyata asinisikie jikoni tafuta kilichopo Mama mtu nikasababisha maandazi ya fasta, maini roast, chai tangawizi,.............. weeee!!! mtaniweza nyie??? (ha! ha! ha! ha!) kabla ya alarm yake kumuamsha Mama mtu mbio kwenda kuwamsha watoto na  zawadi zao  na mplate wangu wa haja........twendeni wanangu na wenyewe wanavyopenda masuprise  yaliyoendelea ndo hayo mjionee wenyewe...............

 meona eeh!!! bado mtu anashanga shanga usingizini....

 Haya na zawadi za shule hizo


 jamani mahanjumati yangu kama yameshasahaulika vile eti??? kweli mtu wanawe.......


Angalizo... dont try this kama  mnuno ulikuwepo ,ambao unatakiwa kumalizwa  yaani ushughulikiwe kwanza kabla ya mahanjumati yako .......aiseee usije mwagiwa chai yako ya tangawizi usoni ukajuuuutaaaa!!! Matatizo yanatatuliwa hayafunikwi,funikwi ukipenda kuyafunika mwisho wa siku lazima uwe fake kwa mwenzio.................


 Kumbuka hakuna mkamilifu ila Ahsante Mungu kwa neema yake kutulinda na kutuwezesha........

Wednesday, September 3, 2014

MAMA WAWILI

Jamani picha za leo nimewashirikisha tuu lakini ni special kwa mwanangu mie..........Nimemuita haya njoo umpige mumy picha, sasa hilo dori ndo limeingia nyumbani mwetu ni sheeeder!!!! ili usikilizwe lazima hilo dori ulitambue uwepo wake. Huyo kaja  na masharti km unataka nikupige picha unatakiwa upige nae........ Mama mtu huyo nikajua ntapiga nae mbili tatu kumridhisha then ntaendelea na yangu....... duu asikwambie mtu tulianza michezo hapo, nakufundishwa mapozi mwisho wa siku nikasahau lengo!!!! 

mtu mzima akionyesha pengo ujue ameshindwa kabisa kuizuia furaha aliyo nayo eti????

nikaambiwa nimrushe rushe ili acheke.......

nikaambiwa just pretend she is crying........................(in Her voice)


Swali nililopigwa hapa mmmh!!!!!ushawahi pigwa swali la namna fulani watoto wanapatikanaje halafu hutaki ajue kwa sasa na pia hupendi kumdanganya  halafu kiinglish cha kihehe ni majangazi...............wakati huo km tayari ana idea fulani kutoka mashuleni mweeeee!!! usiombe ukukute huo wakati aiseee!!!

Mwanangu mie kweli alinipa rahaaaaaa.......

Monday, September 1, 2014

LA FAMILIA.............................

Kama kawa kijiwe chetu , tukitokaga tuliko toka hapa ndo kwakumalizia story na kucheza cheza bora mradi tumalize siku................

Mama na Baba yao ............
spotted!
kuna mtu wivu umeanza kumshika nyuma  yetu mnamuona eeh????enzi zetu ukishaona Baba na Mama wanafanya yao husogei labda uitwa ila Watoto wa dot com mmmh!! hawabanduki!!!
na Dada mkubwa na vinywele vyake mwee!! tunavyotoka najitahidi kuvibana jamani duu by the time tunarudi  ndo kama mnavyoviona...... lakini zinaota.
 Ha!ha!haaa!! mwanangu anachukia kuambiwa ana kitambi sasa sijui ilikuwaje, Baba yake kamwambia mbona pozi lako unatanguliza tumbo??? mweee!!!! mwanangu kaona isiwe shida eti anabinya lisitokeze na kamkono ki! ki! ki!
 na Dada Dogo.....
mwe ningejua ningebeba Camera ningeomba tupigwe picha ya wote mtu nne..... tatizo wazo limenijia nilivyorudi basi tena
Nisemaje zaidi yakuwambia tunawapenda mnoooo..........

KAMA SIO NEEMA YA MUNGU  MMMMMMMHHHH!!!!!