Pages

Ads 468x60px

Wednesday, June 25, 2014

TOTO ZA MIE..............

Jana mwenzenu wanangu wameniongezea kitu aiseee, namshukuru Mungu hawa viumbe kila siku wananiongezea kitu ambacho najikuta namtukuza Mungu sana kwa nafasi aliyonipa, Ni vitu vya kawaida sana!!!lakini kwangu huwa vinanibariki mnooo.yaani vinanipeleka kwenye ulimwengu mwingine kabisa............... ....hata kama niko kwenye hali gani yakimawazo, ninapoamua niwape dakika tano tuuu za muda wangu huwa wananirudisha na kunisahaulisha vingi nakujiona nimebarikiwaaaaaaaaaaaaaaa.................

 mfano jana shuleni kwa Careen walikuwa wanashindana kukimbia, sikuwepo wakati wa tukio lakini nilipigiwa simu kamekuwa ka kwanza kwa wasichana darasani( kipaji cha riadha hicho kwi! kwi! kwi!) nikaomba niongee nako............ jamani !!!!katoto kalikuwa kana furaha ya ajabu, sio kwa sababu kameshinda, bali kwa sababu kanajua her mumy will be happy for her.... ungekasikia kwenye simu jamani!!!! maneno meeengi ila msisitizo ulikuwa, Mumy are you proud of me??  nilijikuta natokwa na machozi ni jinsi gani watoto wasivyopenda ku disappoint wazazi ,ila, huwa inatokea na hawana jinsi........... nimeiona sana hii kwa wanangu....... kwa kweli nilishindwa kuvumilia jamani nilijikuta natengeneza mazingira nifunge tuu ofisi maana kazi haziendi, sikutaka kuhesabu ni sh. ngapi itapotea ofcourse siku haikuingiza some $$$$ ...... nilichokuwa nahitaji kwa muda huo nikumkumbatia ,mabusu na kupiga story na wanangu. 
Wakati huo huo nilitakiwa pia mwisho wa siku kumpeleka mdogo wake kupata sindano ya kinga, hii nayo ilikuwa inanipa mawazo mnooo sipendi sindano!!!!!! so nikaanza kumuanda kimawazo ajue tuu nini kitaendelea, huku nikichukua mfano wa Dada mtu alivyonifurahisha , nikamwambia  i hope na wewe hautaniangusha,naelewa inauma lakini itakuwa pale unavyochoma. kakaniambia Mumy, i promise you am gonna be brave (in her voice). Tulivyofika nilikuwa naiona ile hofu ndani yake ila kwa sababu anataka kuitunza ile promise aliyompa Mama aiseeeee!!! nilimshangaa mtoto hakulia zaidi ya ule mshtuko wa kwanza inavyoingia sindani kitu ambacho sikutegemea kabisa!!!!!!!!

 AM BLESSED!!!!

Nimrudishie nini Mungu kwa zawadi hii????

muda mwingine ambao hawaelewi ni jinsi gani mama yao anajisikia raha ni huu wanaopeana makiss na mahug na kusimliana vihadithi ambapo hawaelewe kama Mama yuko pembeni anafanya yake lakini mind yake yote inawasikiliza na kuwaangalia nyie!!!! ( naelewa kwa nini ufalme wa mbingu umelinganishwa na mtoto mdogo aiseeee!!!!)pure love!!!

Wawili


spotted!!!

3 comments:

  1. Mungu aendelee kukubariki na matendo mazuri ya binti zako.

    Wapendane wao kwa wao na wawapende wazazi pia

    ReplyDelete
  2. Ehh hivi yule aliyejipunguza nywele umefanyaje Rose

    unajua alinikumbusha enzi hizo nikiwa mtoto nikiwa nimefumua nywele ili nisukwe umeme ulikua umekatika akili za utoto nikabeba kibatari kichwani nikitoka nje kuoga upepo si ukadakisha nywele moto nami kwa kuona mwanga najoto limeongezeka nikaanza kukimbia kumbe ndo naukoleza .

    nywele zote za kati zikaungua, uziona lazima ucheke.mama akaona ni vema ninyoe nami kunyoa sitaki.

    Basi ilibidi niwe nasuka tano kichwa hadi zile za kati nazo zikaota

    ReplyDelete
  3. Kweli hukutumalizia stori yaalie jipunguza nywele jamani

    ReplyDelete