Pages

Ads 468x60px

Monday, June 30, 2014

MAMA WAWILI..........



Kuna wakati unajitoa akili kidogoooo unataka kujifanya na wewe katoto kumbe uzee unakunyemelea kwi! kwi! kwi!


someone needs to be remainded,  she is no longer a teeneger!!!!........... She is Mama wawili,Muke ya mtu, 30 yrs old................... lakini hivyo ndivyo anavyojisika kufanya kwa muda huo  kwi! kwi! kwi!  who wants to be old anyway....Tunakomaaa
Haya Nawapenda

Thursday, June 26, 2014

MY MUNCHKINS..........................

Leo si ndio ile siku yetu ya TBT???? nimekutana na hizi picha  za wanangu zilipigwa wiki ileee......... nimeona nizitendee haki kuzidobolisha ha! ha!ha! haaaa


Spotted.....


 mdau uliyeuliza nywele zilizokatwa imekuwaje. Bado ndugu yangu tunajitahidi kufunika funika  ila ndo  ziko rough vibaya!!!!! ukimsuka zile zilizokatwa hazishikiki, ukimbana zinakuwa kama zimevurugwa vile .... hivyo hivyo tunakomaaa mpaka ziote..........

 sura yakikazi

ukimuomba pozi ndo umeharibu kabisa............

 na hiyo ndo TBT yetu ya leo

Wednesday, June 25, 2014

TOTO ZA MIE..............

Jana mwenzenu wanangu wameniongezea kitu aiseee, namshukuru Mungu hawa viumbe kila siku wananiongezea kitu ambacho najikuta namtukuza Mungu sana kwa nafasi aliyonipa, Ni vitu vya kawaida sana!!!lakini kwangu huwa vinanibariki mnooo.yaani vinanipeleka kwenye ulimwengu mwingine kabisa............... ....hata kama niko kwenye hali gani yakimawazo, ninapoamua niwape dakika tano tuuu za muda wangu huwa wananirudisha na kunisahaulisha vingi nakujiona nimebarikiwaaaaaaaaaaaaaaa.................

 mfano jana shuleni kwa Careen walikuwa wanashindana kukimbia, sikuwepo wakati wa tukio lakini nilipigiwa simu kamekuwa ka kwanza kwa wasichana darasani( kipaji cha riadha hicho kwi! kwi! kwi!) nikaomba niongee nako............ jamani !!!!katoto kalikuwa kana furaha ya ajabu, sio kwa sababu kameshinda, bali kwa sababu kanajua her mumy will be happy for her.... ungekasikia kwenye simu jamani!!!! maneno meeengi ila msisitizo ulikuwa, Mumy are you proud of me??  nilijikuta natokwa na machozi ni jinsi gani watoto wasivyopenda ku disappoint wazazi ,ila, huwa inatokea na hawana jinsi........... nimeiona sana hii kwa wanangu....... kwa kweli nilishindwa kuvumilia jamani nilijikuta natengeneza mazingira nifunge tuu ofisi maana kazi haziendi, sikutaka kuhesabu ni sh. ngapi itapotea ofcourse siku haikuingiza some $$$$ ...... nilichokuwa nahitaji kwa muda huo nikumkumbatia ,mabusu na kupiga story na wanangu. 
Wakati huo huo nilitakiwa pia mwisho wa siku kumpeleka mdogo wake kupata sindano ya kinga, hii nayo ilikuwa inanipa mawazo mnooo sipendi sindano!!!!!! so nikaanza kumuanda kimawazo ajue tuu nini kitaendelea, huku nikichukua mfano wa Dada mtu alivyonifurahisha , nikamwambia  i hope na wewe hautaniangusha,naelewa inauma lakini itakuwa pale unavyochoma. kakaniambia Mumy, i promise you am gonna be brave (in her voice). Tulivyofika nilikuwa naiona ile hofu ndani yake ila kwa sababu anataka kuitunza ile promise aliyompa Mama aiseeeee!!! nilimshangaa mtoto hakulia zaidi ya ule mshtuko wa kwanza inavyoingia sindani kitu ambacho sikutegemea kabisa!!!!!!!!

 AM BLESSED!!!!

Nimrudishie nini Mungu kwa zawadi hii????

muda mwingine ambao hawaelewi ni jinsi gani mama yao anajisikia raha ni huu wanaopeana makiss na mahug na kusimliana vihadithi ambapo hawaelewe kama Mama yuko pembeni anafanya yake lakini mind yake yote inawasikiliza na kuwaangalia nyie!!!! ( naelewa kwa nini ufalme wa mbingu umelinganishwa na mtoto mdogo aiseeee!!!!)pure love!!!

Wawili


spotted!!!

Monday, June 23, 2014

MY WEEKEND................................

Wandugu weekend yangu kwa kweli ilikuwa nzuri mnooooo, nimemshangaa Mungu aisee.......................ilikuwa ni moja ya weekend  ambayo kwa kweli moyo wangu ulikuwa mzito kuiruhusu ifike haraka, maana kulikuwa kuna baadhi ya events kama ningeziruhusu zingeweza  kunivuruga kabisa na pengine kunipotezea uwepo..... hii yote nilihisi kwa akili yakibinadam  labda niseme kujistukia kutokana na historia.................... haya Tutazungumza hili kama tukiruhusiwa

Pata moja ya muonekano wangu wa weekend.

shoe game
about to go
Muke ya Slay

dobolilo





Friday, June 20, 2014

TUZUNGUMZE..........


Ngoja nikwambie mpendwa wangu, Mwana wa Mungu huwa ni wakipekee, Majaribu na mafanikio yake huwa hayafikiriki kwa namna ya kikawaida, Wakati anapopitia jambo fulani kwa bahati mbaya au nzuri jamii fulani ikalipokea asilimia kubwa ya hilo jambo litapewa sura tofauti na mara nyingi hupoteza uhalisia wa jambo husika.Maumivu na misukosuko yanayoelezwa na ile jamii mara nyingi huwa ni mazito na kukatisha tamaa kuliko muhusika mwenyewe anavyolichukulia ............Na hata kama ni kweli kama wanavyodhani jamii hii huwa wamepigwa upofu wasiione ile amani na tumaini aliyokuwa nayo muhusika. Na hapa ndipo wanapotokeaga na manabii wa uongo (kwi!kwi!kwi!) maana nabii wa uongo huwa lazima awe na chakuanzia halafu yeye anamalizia,Si tulisema sisi, maskini hivi itakuwaje, sasa itabidi wafanye hivi, yaani maneno meengi yafujo fujo............  na wengi wao huwa hawasogei kwa muhusika kuupata uhalisia wa jambo. Ni heri hata yule basi, anayethubutu kusogea kwa muhusika ili apate uhalisia lakini, bado nao lazima kuwe kuna lugha moja ( Mwana wa Mungu) ambayo itafanya muelewane.  Ikiwa sio lugha moja mara nyingi huwa wanafungwa uelewa kwa namna yoyote utakayojieleza wewe wao watakuwa wamekuja na majibu na hayo ndio wanayotegemea uwambie , mara nyingi hawa watu wametengwa na kweli.  Kama hunielewi nenda kamsome Ayubu alipopitia na ashukuriwe huyu Mungu aliyemtoa mwanae wa pekee pale msalabani maana haitatokea pito kama la Ayubu. Na hii ndo tofauti iliyopo kati ya mwana wa Mungu na wa Mataifa.


 Unapokuja kwa habari ya mafanikio. Namna Mwana wa Mungu anapotoka kwenye utukufu mmoja kwenda mwingine. Mara nyingi huwa kuna vitu vinafanyika hapo katikati ambavyo jamii kubwa huwa haielewi na kama jamii imelewe basi  haiko tayari kufanya, kwa sababu labda sio chaguo la wengi anaowaona yeye ( nikimaanisha Mungu ana watu weeengi kuliko unavyodhani wewe ila unachokiona ni kile unachokiona wewe kwa maana ndio mazingira uliyojiweka na kupigwa upofu usione).Mara nyingi huwa kuna namna yakipekee, mfano, Mwana wa Mungu ataamka saa sita za usiku kuomba kwa ajili jambo fulani, Jamii isiyoelewa haitapokea kama ni kawaida, lakini ataona kawaida kwa anayekesha kwenye makumbi ya starehe kwa maana hayo ndo mazingira aliyojiweka nakuamini ndivyo inavyotakiwa iwe, Ukija makazini mara nyingi ukiona mwana wa Mungu ameketishwa na wakuu au yupo kwenye nafasi kubwa kubwa ,mara nyingi sehemu aliyotokea mpaka akafike kwenye hiyo ngazi huwa ya kipekee na hata alipofika, jamii huwa haitaki kuamini au kukubali kama huyo muhusika ndie yeye aliyekaa hapo....... kwa sababu haikufanyika kama ilivyo kawaida ya wengi mfano rushwa,kumfahamu fulani,................... Na ukija kwewnye ulimwengu wa kuwekeza, jicho unaloliona mwana wa Mungu juu ya milango iliyo mbele yako wengi wao hawalioni na kama wameiona hawako tayari kutoa kipaumbele maana hawapendi tofauti, na wengine wanataka short cut, ( Usishangae kuona sasa hivi walio wengi wanatafuta kila namna yakukutana na maboss wa sembe ili na wao wabebeshwe (wawe punda). wakati wewe mwingine unakesha ukiomba hili janga liishe, na usishangae unapokuwa kwenye hatua fulani ukapewa majina fulani fulani mfano mchawi,Sembe,......... kama kweli wewe ni mwana wa Mungu na kweli unayo wewe Hii ndio tofauti na upekee ulionao wewe ( mwana wa Mungu)............Hebu nenda kasome Daniel 1-3 ikiwezekana kasome zaidi kuna vitu vingi sana vya kujifunza kuhusiana na hii topic ya leo na labda utanielewa zaidi.


Ninachotaka kukumbusha ni hivi mpendwa, kama hivi ndivyo ilivyo kwako, UPEKEE HUO ndio unaoleta UTUKUFU KWA BWANA, ndio unakufanya upondeke  maana kila lililotendeka kwako ni NEEMA.Ukisoma Daniel utanielewa pamoja na yote aliyowezeshwa na Mungu kufanya hata siku moja hakuwahi kujinadi, alirudisha utukufu kwa Bwana hata pale mfalme alipotaka  kumkuza Daniel kama Daniel ,bado Daniel alimkumbusha mfalme kwamba, hayo yote sio yeye bali kuna mtu zaidi ya yeye.Na hata alipowekwa mahali pa juu hakulewa na ile nafasi maana aliamini yule aliyemuweka pale si mwanadam.  Hana sababu yakumnyenyekea mwanadam ambaye yeye anatumika tuu kutoa tamko la kuketi mahali pa juu lakini anayemketisha ni yule anayemtumikia................... kasome Daniel mlango wa 4 utanielewa.

UPEKEE HUU unakufanya ufanye vitu visivyoeleweka kwa wengi, nimemsoma Daniel wakati mfalme amekusudia kuwalisha vyakula vinono vya kifalme ili watoke wamenona,Daniel yeye hakuamini kwamba hicho chakula  ndicho kitakacho timiza lengo zaidi yakujitia unajisi ,yeye aliomba mtama na maji (kasome mazungumzo yake na yule mlinzi) lakini mwisho wa siku yeye na wenzake ndio waliotimiza lengo, kuliko chaguo la walio wengi.(anyway haikuwa chaguo maana ilikuwa kama kajiamri fulani lakini kulikuwa kuna hitaji upekee ili kujinasua hapo)

 Nikimsoma zaidi kuna kitu nimejifunza pia wakati Daniel na wenzie wanaomba kwa habari ya Mungu ampe ufunuo wa ndoto ili wajinasue kwenye adhabu ya kifo, CHAKUSHANGAZA!! kumbe huo ndo mlango wa kwenda kuketishwa na wakuu, utanielewa hapa niliposema hapo juu kwa jinsi Mungu anavyokuinua kutoka chini kwenda juuuuu......... kwa kweli niyakipekee na kwa namna yoyote ile utarudisha utukufu kwa Mungu.

HII YOTE NINATAKA KUKWAMBIA HIVI......

MWANA WA MUNGU NI JASIRI, ANAJUA ANACHOKIFANYA,HASHUGHULIKI NA KAWAIDA ZA WENGI,ANALO TUMAINI  NA PALE UVUMI (UONGO AU HABARI ISIYO YA UHAKIKA)  INAPOJADILIWA SANA NA WATU KUHUSU YEYE HUWA HANA MUDA WA KUJITETEA MAANA ANAAMINI HIVI NDIVYO JAMBO LINAVYOTAKIWA KUVALISHWA SURA HIYO ILI MAMBO MENGINE YAENDELEE NYUMA YA PAZIA KWA AJILI YA UTUKUFU  WA BWANA.


HIYO NDIO SIRI YA MWANA WA MUNGU HIYO.........................

Angalizo mtazamo wangu ukinisoma kwa makini nimesema walio wengi, japo kuna walio wachache(baadhi) ambao yawezekana mimi na wewe hatujui wako (tuko)wapi, ama labda ni vuguvugu, na ama labda ni vyovyote vile.... Mama wawili sijaruhusiwa kusema chochote juu ya hilo labda ipo siku nitaruhusiwa kutoa yangu au isiwepo kabisa.

NAWAPENDA

Wednesday, June 18, 2014

RAFIKI BALL 2014

Rafiki Surgical Missions is a non-profit charity that sends teams of qualified surgeons, anaesthetists, nurses and allied therapists to Tanzania to provide free surgical treatment and medical training.

The organisation raises funds in Australia and Tanzania to support professional surgical teams who travel to Tanzania from Australia. The teams and other volunteers work in collaboration with Tanzanian Hospitals, Governments and other stakeholders to provide surgical treatment and surgical teaching.

Rafiki works with Tanzania’s Ministry of Health, and senior medical and training officials to facilitate the delivery of the Rafiki programs.

 Haya wandugu na sisi tulisupport kwa namna hii, kiukweli ilipendeza na tulifurahi  mnoooooo!!! kikubwa zaidi tumetumika kuleta smile kwa mtu huko nyumbani.


Wandugu waliniimbia (Mungu afanye nini ili wanadamu tujue anatupenda??????) Mama wawili nilishindwa kujizuia kusimama........

 Raha eeeh?? ku fundraising nakupendeza na masmile...... .......

 Tulikuwepo

$190 tu! imeongeza furaha kwa jamii yetu nyumbani.... Mbarikiwe wote mliochangia kwa namna moja ama nyingine. Tufanyeni zaidi na zaidi  mbona tunaweza!!!!( Baba mwenyekiti chonde chonde Baba na wasaidizi wako TUNAWEZA)
 Olga & Huby ( mtaelewa kwa  nini kijana alikuja kupiga hodi nyumbani khaa!!! Olga we ni mrembo bwana duu!!!)
 na shemeji yangu mimi

The boss him self & wifi yetu
my Dada Doti & a friend
Mahede & Wife(Katibu wa Watanzania Western Australia)
 yeyoooooo ni shiiiida, nisemaje sasa bwana ???? picha yenyewe imejieleza. (Esther& Huby)
Hivi kuna mtu amewahi kumshuhudia shemeji yangu mie kanuna??? utakuwa umemfananisha bwana!!! halafu sasa ukiwa karibu naye lazima usahau shida anakuambukiza hayo ma smile ukikumbuka shida zako basi we umeshindikana...............
 Majembe yangu hayoooooo!!!! haya wadau na hawa ndo Kikwete & Salma   kwa ajili ya Watanzania waishio Western Australia. Kama ulimpiga kura  ni amini  kura yako haikupotea aisee na hata kama ndio yako haikuwa kwao lakini imekuwa kama ilivyo please let us support  them............. mi nawakubali mno I mean majembe kweli kweli
 shiiiiiiida nyingine iko hapa sasa duuu!! haya wandugu wa ni marafiki tuuu ( wameniambia wenyewe)

Lily na Sally( Mama mwenye kigoda)
nahisi hili swali huwa hunijibu vizuri!!!!! hivi ni kweli hii Damu yakichaga na kisukuma?????



  Hapa chacha Jesca wangu tunakumiss sana unajua kwenye huu ulimwengu wa networking??? hatujakuzoea Bwana turudishie hii cute face,body,.......,.......,...... Muna  wee unajua nakupenda eeeh!!! umejisemea mwenyewe Toto la Mujini haya bwana mimi ngoja niendelee kuchunga mbuzi zangu huku kijijini.
Mama Africa (Lemmy) ulipendezaje sasa ++++ vile vigeregere vyetu sasa Ahsanteeeeeee!
Diane nimechoka kukusifia ujue??? (Lily,Diane,&Lemmy)
Mona &Diane
Mona,Lily&Diane
Happy Ladies (Mariam,Doti & a friend)


Mwenyewe amesema hebu waite kaka zangu mie nipige nao picha!!! haya Mama Mutu na Kaka zake

Boys
happy boys

Huyo hapo & a friend

Happy Ladies

Mutu na Dada Yake.......( amejisemea mwenyewe the boss "mimi mu......... niko ulaya nakuraaa raha" in his voice)
walikuwepo wengiiiiiiiiiiiii nimechoka mwenzenu kupost picha zoooote

 The woman behind the Camera

 dakika  za mwisho na mie nimejikumbuka hizo ndo hasara zakuwa mpiga picha.

The END.........

Monday, June 16, 2014

LA FAMILIA

unajua nini hata mimi nimewamiss sana tuuuu...............  haya sisi hapa tunawapenda mnooooooooo!!!
unahisi ni nani na nani yake hawa?????
Baba na Mama yao
us

Tunachoweza kusema inawezekana ukiamini, cha msingi,jitambue na kujielewa bila hofu ya umezungukwa na nini,  unapogundua kila unachokiona mbele yako ni mlima ambao haukupi matumaini yakuupanda,hujiongezi jinsi gani utapata njia mbadala yakuupanda, jua mafanikio kwako ni historia,  ndoto yako kamwe haitakuja kwenye uhalisia............. Hebu jaribu kulipa hilo jambo sura na mtazamo tofauti then fanya kwa bidii na kwa uaminifu nafasi yako,iliyobaki muachia Mungu  huku ukiamini HAKUNA KINACHOSHINDIKA KWAKE!!!!!HUTAJUTA RAFIKI!!!