Namshangaa Mungu jinsi anavyoruhusu jambo na jinsi anavyoweza kukutoa, kama tujuavyo hakuna mteremko kama kuna mtu anaweza kunithibitishia hakuna ups and down in either way sijui huyo ni mwanadam wa aina gani............. naongea km mwanadam wa kawaida ambaye kuna wakati napita haswa mpaka nahisi hakuna mlango wa kutokea LAKINI, Mungu hajawahi kuniacha ktk kila jambo nimemuona akiniinua nakunitetea nakunipa ushindi nisioutarajia........moja ya Mambo yaliyotokea ndani ya mwezi huu ambayo nimeona nikushirikishe mdau labda inaweza kukuinua kwa namna moja ama nyingine hasa pale unapopoteza tumaini.......
ilikuwa ni siku ya tarehe 11/04 siku ambayo ni birthday ya mwanangu mdogo Cristabell ( 3yrs old) na siku inayofuata 12/04 ni birthday ya mume wangu na nisiku niliyotakiwa kupanda pipa kwa ajili ya Vacation ya 5th anniversary ...... unaweza ukaelewa ni jinsi gani hiyo week ilikuwa special ndani ya familia yangu kwi! kwi!kwi! kwi! adui (Shetani)naye hajalala bwana akuache tuu wewe ule good time kwa lipi unalomfurahisha???????
nikiwa na kawaida yakufanya kitu kwa ajiri ya hiyo vyote ( birthdays) this time niliamua iwe yakifamilia na ilikuwa ni one of the week days Baba watoto yuko mzigoni nikawaza ngoja nifanye suprise fulani kwa ajili ya mtoto na Baba yake, wakati huo huo jana yake nilijikuta nataka kujua afya ya Mama yangu kabla sijaenda vacation kwa hiyo nilifanya appointment na Doctor wangu ambayo nilipewa siku ya tar. 11/4....... plan ilikuwa ni kumpeleka mama then kuwanunulia zawadi wahusika , kumalizia mikakati ya suprise ambayo nikuwa sijui nitaiandaaje.......
Mama yangu niliambiwa anakisukari lkn hakuwahi kupimwa kuthibitisha, na alipofika kwangu alikula chochote ice cream everyday nawajukuu zake, chocolate ze coca cola,na vitu km hivyo bila tatizo lolote mpaka tukaamini ule ulikuwa uzushi japo maji alikuwa anakunywa sana nilichoamini ni kwa sababu ya joto, kwa hiyo nilivyomuona doctor maelezo yangu ya kwanza yalikuwa Mama yangu anakunywa sana maji na pia nataka afanyiwe general check up. Doctor alianza na kipimo cha sukari kwa nini mi sijui na wala sikumwambia km tunahisi anakisukari ile kumpima tuu Doctor anatetemeka nakusema anatakiwa kupelekwa emergency department huku akiangaika na simu kuwapigia simu kuna mgonjwa analetwa mda huo anatakiwa kushughulikiwa mapema heeee!!! nimebaki nashangaa kumwambia mama ameshastuka lakini haelewi kulikoni ze kingeleza ze issue ha!ha!ha1haaaa!!! i love my Mumy............. mmmh! ikabidi nimwambie alichosema mi siumwi huyu doctor ana matatizo, hata km naumwa mwambie mi nauwezo wa kusubiri mpaka nyie mrudi ndo tuje tuendelee na matibabu, nilijikuta nacheka huyo mgonjwa na maneno yake...... Doctor aliniambia hichi kiwango sijawahi kukutana nacho( sukari ilikuwa 30) na anashangaa ni jinsi gani bado kachangamka nikamueleza Doctor idea ya Mumy aliniambia nikikuruhusu urudi ya huyu mgonjwa nyumbani mimi nafungwa hapo ndipo nilipogundua km hiyo ni serious issue
hapa ndipo tulipoishia .....
natafakari namba za shetani???? ni kweli ameamua kuchukua furaha yangu kuwa huzuni???? ni kweli Mama yangu kipenzi ni mgonjwa kiasi hiki na angalia hayo mamipira waliyomchomeka mmmh!!!,no birthday imegeuka kuwa huzuni, Doctor kaniambia mama atakuwa hospital for 4night kwa hiyo in any means i cant make my vacation kwa nini Mungu uliruhusu gharama na unajua sitaweza kurudishiwa zaidi ya ticket ambayo ningerudishiwa asilimia fulani baada ya kutoa taarifa in 24 hrs kitu ambacho mpaka sasa hakitawezekana hiyo walokole tuna sema chuma ulete kwi kwi kwi! ..... na hata km mama akitoka bado sidhani km ntakuwa na amani kumwacha mama nyumbani pekee yake,.na tena nilimuuliza Mungu hata km nimekukosea hivi ndivyo ulivyoamua kuniadhibu???? ni wapi nilipokukosea ktkt hii furaha niliyokuwanayo mpaka ukaamua kubadili kuwa huzuni??? kwa kweli niliwaza duuu
wakati huo huo sikutaka kumuonyesha mwanangu kipi kinaendelea siku yake yakuzaliwa japo alimstukia Bibi na hiyo mipira aliyoweka akawa anamuogopa halafu ni ma best hatari akiwa amekaa hapo ananikumbusha mumy is it my Birthday or Careen's birthday?????? let's go buy a present Mumy....... km Mama unanielewa ni jinsi gani utajisikia kwa mazingira hayo....... Bibi naye amekazana mpe mtoto haki yake mimi nipo kwenye uangalizi hapa mchukue mtoto mkafanye km mlivyopanga na safari usiahirishe mwambie doctor wanipe dawa za kunywa kwa kipindi hicho ambacho hampo you can imagine akili yangu ilivyokuwa na mvutano Bibi alikuwa anajitahidi asitoe ile furaha tuliyonayo HOW????? NINGEWEZAJE KUFURAHI HUKU MAMA YANGU YUPO KITANDANI MGONJWA????.na mengine meengi yaliendelea hapo LAKINI, Mungu sio kibuyu wala mwanadamu, Hawezi kukuacha ukaangamia,anauwezo wakuruhusu jaribu na mlango wakutokea lazima atakupa, kama mwanadamu utajeruhika sana lakini, huo ndio mtaji wakukuinua kiimani..........Madokta ri waliendelea na utaratibu wao wakutumika tumelala haturuhusiwi kulala ila niliruhusiwa kwa sababu yakutafsiri lugha hivyo nilibahatika kuona na kujua kila kilichoendelea.Asubuhi sasa taarifa niliyopewa wanashangaa wamefanikiwa kuishusha na kuicontrol vizuri itabidi tulale one more night kwa ajiri ya uangalizi tuu just in case....... Doctor alinipa barua yakuthibitisha kuchelewa ndege kwa sababu ya emergency na book in next two days ambayo nilikubaliwa, taratibu zote za hotelini na sehemu tulizotakiwa kutembelewa zote zilifanikiwa na wakati huo huo nilipata simu 2 weeks before kuna Dada mmoja aliniomba aje akae kwangu anatakiwa kuja chuo kumalizia unit yake hana pa kukaa huyo Dada jamani sijui kwa nini nilimruhusu simjui kihivyo, niMzimbabwe nilimjua kupitia Dada mmoja kanisani ninachokumbuka siku ya kwanza kuonana naye aliniangalia vibaya mpaka nikajiuliza nimemfanyia nini kumbe alikuwa mjamzito, siku ananipigia simu kunieleza shida yake na ananiambia anamtoto mchanga waje ndani mwangu Bado najiuliza ilikuwaje moyo wangu haukuangalia hayo zaidi yakumkubalia, kumbuka hata habari ya Mama atakuwa anaumwa sina au kipindi hicho ntaondoka sina.........siku anayokuja yeye ndo anaingia jamani ameishi na mama yangu na watoto vizuri sikutegemea!!!!! tumeshakuwa km ndugu anaishi mbali km 4-5hrs driving. it is amazing Mungu anavyofanya njia na mama mzimaaaa sukari imerudi normal ila tuu ameambiwa acontrol diet yake. na vacation tulienda simmejionea wenyewe shetani alivyokuwa na wivu alijua hilo bata lake kwi! kwi! kwi! na mwanangu baada ya taarifa tuliyopata ilibidi tufanye kitu humo humo Hospital ...........
my Angel
hide n seek hiyo wanatafuta simu hiyo hata hawaioni mwee
Cristabell alifanikiwa Simu Careen alifanikiwa funguo
hapo chacha
Slay's girls
she is cute hey
poor Dady
tukajikatia keki ALL IN ALL SHETANI ALICHEMKA ALITUPOTEZEA MUDA LAKINI USHINDI TULITOKA NAO
WATAPIGANA NA SISI LAKINI HAWATA TUSHINDA