Siku tatu kabla hajatoka masasi girls ambako alikuwa amemaliza shule,Upendo Andrew alitumbukia kwenye shimo lililokuwa likiwaka moto wa majani makavu ya mwembe,alizama hadi kufikia karibu na kiuno, moto ulikuwa km umechokolewa na kijiti alipotumbukia,alipelekwa mkomaindo, baadaye miguu yake yote miwili ilikatwa, wazazi wake wote wawili walifariki kabla hajamaliza shule. baada ya hapo alikuwa analelewa na babu yake,naye alikuja kufariki...... alikosa msaada kabisa akaamua kuja dar kuanza kuomba omba maeneo ya imalaseko na maeneo mengine katikati ya mji.........alibahatika kumpata mtu wakumsomesha compyuta , akapata kazi, bahati mbaya sana alishindwa kuifanya hiyo kazi kwa sababu machozi yalikuwa yakimtoka sana, alimuona doctor akaambiwa inasababishwa na mshipa umefail kichwani ndo unashababisha kutokwa na machozi.... hivyo kuamua kuendeleza kazi yake ya kuomba omba..............
Tukumbuke kwamba Upendo ni binadam aliyepata hayo majaribu akiwa bado ana umri fulani ambao pamoja na majaribu anayopitia ni rahisi kurubuniwa au kushawishika kwa namna fulani........Upendo alijikuta amezaa na mfanyakazi wa kazi za ndani kwa wahindi ambaye nae ana mke na watoto wawili na Upendo akiwa na mtoto wa miezi kadhaa kwa sasa..........mmmmh!!! naomba niishie hapa please
UPENDO ANAPATIKANA KWA NAMBA HII 0715271201 umeguswa, unata kakufanya kitu, una elfu moja,laki,million, mtafute au mrushie m pesa jamani hata mia tano.......au chakula , mavazi,ikiwezeka mtafute uongee nae labda unaweza msaidia kimawazo au kumfariji, chochote fanya kwa vile ulivyoguswa na Mungu wa mbinguni atakukumbuka...........
Dada Upendo
AKIWA NA MWANAE
TUZUNGUMZE
1.najiuliza tuu huyu dada hana miguu ambayo hata angeweza kufanya kazi ya mabox,wazee, usafi na zinginezo km za kina sie..... akajivunia kwa pesa anayojitafutia mwenyewe ameishia kuombaomba barabarani.......hapo zamani nilijua wanaomba omba ni wavivu lakini nikisoma hapo juu huyu dada hii ndo only option aliyonayo..........
2.na bado huyu dada ana ujuzi wa compyuta kwa sababu ya huo mshipa wamachozi hakuna atakaye mpa kazi labda mpaka pale atakapo saidiwa kufungua biashara yake mwenyewe....maisha yangekuwaje km angesema akuuu!! mi ninaujuzi wangu wa compyuta hivyo naisubiri mpaka niipate.... marufuku kuombaomba hahahahaaa!!!! nimecheka tuu wadau ni jinsi gani naumizwa.......hivi?????mmmmmh!!!
3.tuheshimiane,tuthaminiane,tumia kila nafasi uliopewa kwa jinsi ulivyojaliwa,dharau, dharau iwe mwiko kwako, lia na anaelia, cheka na anaye cheka.........hujui kesho yako wewe.... laiti km Upendo angejua asingepita karibu na ule moto uliobadilisha picha nzima ya maisha yake japo kuwa alishakuwa kwenye jaribu lakufiwa.......
week end njema wadau.......saturday & sunday ni siku ya Baba wawili na wawili wangu........sipost chochote zaidi yakuachia comment.........
MBARIKIWE!!!